KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 30, 2010

Leadership & Human Behavior



Leadership & Human Behavior


As a leader, you need to interact with your followers, peers, seniors, and others; whose support you need in order to accomplish your goals. To gain their support, you must be able to understand and motivate them. To understand and motivate people, you




must know human nature. Human nature is the common qualities of all human beings. People behave according to certain principles of human nature.






Human needs are an important part of human nature. Values, beliefs, and customs differ from country to country and even within group to group, but in general, all people have a few basic needs. As a leader you must understand these needs because they can be powerful motivators.

Ruhsa Kumpiga Mkeo Lakini Usimtoe Alama


Mahakama ya sheria za kiislamu katika falme za kiarabu UAE imeamuru kuwa ni ruhsa mwanaume kumpiga mkewe na watoto wake ili mradi hatasababisha alama za vipigo kwenye miili yao.
Hatua hiyo ya mahakama hiyo inawapa haki za kisheria wanaume kuwaadhibu wake zao na watoto wao iwapo wataenda kinyume na matakwa yao.

Hukumu hiyo ilitolewa na mmoja wa majaji wakuu wa UAE, Falah al Hajeri, ambaye alikuwa akitoa hukumu ya mwanaume aliyepigwa faini sawa na Tsh. 160,000 kwa kumpiga kibao mkewe na kumpiga teke binti yake.

Mwanaume huyo alipatikana na hatia ya kumpiga mkewe kwa nguvu sana kiasi cha kusababisha apasuke mdomo wake na kuvunjika jino lake.

Mwanaume huyo pia alimpiga mateke binti yake mwenye umri wa miaka 23 kiasi cha kupelekea apate michuko na uvimbe kwenye mguu na mkono wake.

Mwanaume huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni, awali alidai alimpiga mkewe na mtoto wake kwa bahati mbaya lakini alipopatikana na hatia alikata rufaa akisema kuwa hata kama alimpiga mkewe na mtoto wake kwa makusudi, anayo haki kwa mujibu wa sheria za kiislamu kutumia nguvu dhidi yao iwapo njia zingine za kuwaadabisha zitakuwa zimefeli.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo, jaji Falah al Hajeri alisema: “Ingawa sheria zinaruhusu waume kuwapiga wake zao, lakini pia wanatakiwa wasivuke mipaka na kusawasababisha alama au makovu wake zao”.

“Kama mume atakiuka misingi ya sheria ya kumuadhibu mke au mtoto wake, basi lazima ahukumiwe kwa mujibu wa sheria”, alisema jaji Hajeri.

Jaji Hajeri alielezea kuwa njia rahisi ya kuangalia kama waume wavunja sheria ya kuwaadhibu wake zao ni kwa kuangalia alama za vipigo kwenye miili ya wake zao

Osama Bin Laden Agundulika Anapoishi


Kwa mujibu wa maafisa wa majeshi ya Nato, Osama bin Laden hajajificha mapangoni kama inavyojulikana bali anaishi maisha ya kifahari kwenye jumba moja la kifahari kaskazini mwa Pakistan.
Kiongozi wa Al Qaeda, Osama bin Laden hajakimbilia mafichoni kwenye mapango bali anaishi maisha ya kifahari kwenye makazi ya watu nchini Pakistan.

Msaidizi mkuu wa Osama, Ayman al-Zawahiri naye anaishi maisha ya kifahari katika nyumba nyingine iliyopo katika maeneo ambayo Osama bin Laden anadaiwa anaishi.

“Hakuna kiongozi yoyote wa Al Qaeda anayeishi kwenye mapango”, alisema afisa mmoja wa ngazi za juu wa Nato ambaye hakutaka kutaja jina lake kutokana na taarifa hizo kuwa nyeti sana.

Afisa huyo wa Nato alisema kuwa Osama bin Laden na al-Zawahiri wanalindwa na wakazi wa maeneo hayo ambao wanashirikiana vyema na majasusi wa Pakistan.

Baada ya mashambulizi ya 9/11 nchini Marekani, ilidaiwa kuwa Osama bin Laden na wadau wake wamejificha kwenye mapango ya Tora Bora yaliyopo kwenye milima iliyopo mpakani mwa Afghanistan.

Lakini sasa imedaiwa kuwa Osama amekuwa akiishi kwa kujificha katika nyumba ya kifahari iliyopo kwenye kitongoji cha Chitral kilichopo kaskazini mwa Afghanistan karibu na milima ya Tora Bora.

Taarifa ya Osama kuishi maisha ya kifahari nchini Pakistan huenda ikawaudhi maafisa wa Marekani ambao walitangaza kuwa mabomu yao yamemfanya Osama bin Laden ajichimbie kwenye mapango ya Tora Bora.

Rais wa Marekani, Barack Obama ameendelea kusisitiza kuwa wanamsaka kwa udi na uvumba Osama bin Laden ambaye amehusishwa na matukio mengi ya ugaidi katika maeneo mbalimbali duniani

Kaka Yake Obama Aoa Mwanafunzi Aliyemtorosha Kwao



Kaka wa kufikia wa rais wa Marekani, Barack Obama anayeishi nchini Kenya, Malik Obama mwenye umri wa miaka 52 ameongeza mke wa tatu ambaye ni mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka 19 aliyeacha shule na kukimbia kwao.
Kaka wa kufikia wa rais wa Marekani, Barack Obama anayeishi nchini Kenya, Malik Obama ambaye ana wake wawili ameongeza mke wa tatu ambaye ni mwanafunzi wa sekondari aliyekimbia masomo yake.

Mama wa msichana huyo mwenye umri wa miaka 52, alielezea hasira zake baada ya binti yake kuacha masomo ili aolewe na Malik ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 52.

Akiongea na televisheni ya NTV ya Kenya, mama wa msichana huyo anayeitwa Mary Aoko Ouma alisema kuwa binti yake awali alijaribu kufunga ndoa na Malik miaka miwili iliyopita lakini hakumruhusu.

Akiongea na televisheni ya NTV bila ya kujua kuwa anarekodiwa, Malik alithibitisha kufunga ndoa na msichana huyo ingawa hakusema ni lini harusi yao ilifanyika.

Sheria za Kenya zinaruhusu mtu kuoa mke zaidi ya mmoja iwapo vigezo vya kidini au kitamaduni vitatumika

Friday, October 29, 2010

Atengwa na nduguze baada ya kubadili dini


KIJANA mmoja aliyetambulika kwa jina la Christopher [31] mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam, amejikuta akiwa kwenye wakati mgumu kutokana na hali yake ya maradhi yanayomsumbua baada ya kutengwa na ndugu zake baada ya kubadili imani yake ya kidini.
Christopher hivi sasa anakabiliwa na maradhi ya tumbo na kupelekea kulazwa katika zahanati moja binafsi, amejikuta akikosa huduma za ndugu zake na kuhudumiwa na upande wa mke wake pekee hali inayomfanya akose amani .

Imedaiwa na mmoja wa ndugu wa mke wake kuwa, Christopher alichukua umauzi wa kubadilisha imani yake ya kidini ili aweze kufunga ndoa na mchumba wake hali hiyo ilipokelewa kwa mitazamo tofauti na kutoka ndani ya familia yake.

Ilidaiwa kuwa, kijana huyo baaddhi ya ndugu hawakuafiki kitendo hicho cha kubadili imani kwa kuwa ndugu hao walitaka mke wake aje katika imani ya ndugu yao na si ndugu yao kubadili imani.

Hivyo imendelea kudaiwa kuwa, mke wake huyo aligoma kubadili dini na kwa kuwa kijana huyo hakutaka amkose mchumba wake huyo aliamua abadili ili aweze kufunga nae ndoa.

Imedaiwa kuwa kijana huyo alifunga ndoa na mke wake huyo mwezi Februari, mwaka huu na kuhudhuriwa na baadhi ya ndugu na hivi sasa anakabiliwa na maraadhi ya tumbo na ndugu kumsusa kwa kutompa ushirikiano katika kumuuguza.

Imedaiwa kuwa kijana huyo anatakiwa apatiwe upasuaji

Kiharusi chaongoza Dar



IMEDAIWA kuwa wakazi waliowengi waishio jijini Dar es Salaam huongoza kwa kuugua ugonjwa wa kiharusi kuliko mikoa mingine nchini.


Hayo yamebainika katika utafiti uliofanywa na Taasisi ya aTaifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu [NIMR] na kutolewa tathimini hiyo jana.

Akizungumza na wanahabari jana katika sehemu ya kuadhimisha siku ya ugonjwa huo, Dk. Gerry Mshana alsiema, jiji la Dar es Salaam linongoza kwa wagonjwa hao.

Alisema katika utafiti uliofanyika umebaini kuwa kati ya watu laki moja watapatikana watu 316 wana ugonjwa huo katika jiji hilo.

Alisema utafiti huo umefanyika umebaini kuwa mabadiliko ya maisha ni chanzo cha kuongezeka kwa agonjwa hao ambao chanzo chake ni shinikizo la damu na kupelekea apaate maradhi hayo.

Alisema dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kupata ganzi ghafla mwilini na kuishiwa nguvu,kupata ugumu wa kuzungumza wa ghafla,kutoona vizuri kwa ghafla,kushindwa kutembea kwa ghafla ,kizunguzungu na kuumwa kichwa sana bila chanzo cha msingi.

Alisema idadi hiyo ya wagonjwa ni kubwa kuliko hata nchi zilizoendelea

Thursday, October 28, 2010

Kikwete kesho live.



MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Mrisho Kikwete kesho anatarajiwa kufanya mahojiano ya moja kwa moja, mdahalo utakaoanza majira ya saa 2 usiku katika ukiumbi wa Anatoglo na kurushwa na moja kwa moja na vyombo vya habari nchini.


Wananchi na waandishi wa habari watapata fursa ya kuuliza maswali kwa mgombea huyo na maswali hayo kujibiwa na mgombea huyo papohapo.

Fursa hiyo imetolewa na chama hicho kutoa nafasi ya kuulizwa maswali ya moja kwa moja kuhusiana na uchatguzi mkuuu kwa ujumla.

Meneja wa kampeni CCm, Kinana alifafanua kwua tayari Kikwete alishamaliza safari zake za kujinadi nchdi nzima na kusema ana nafasi nzuri ya ushindi kwa kuwa aliwaona wapiga kura wake ana kwa ana na kufafanuliwa kwamba katika kampeni zake alitumia jumla ya kilometa 48,000 kumaliza nchi nzima

Lipumba leo ITV



LEO kituo cha luninga cha ITV kinatarajia kurusha mdahalo wa moja kwa moja utakaofanya wananchi kuuliza maswali ya moja kwa moja kwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.
Mdahalo unatarajia kuwa wa masaa mawili ambapo utaanza majira ya saa 1 hadi saa 3 usiku na utarushwa moja kwa moja kutokea katika Hotel ya MovenPick ya jijini Dar es Salaam.

Mgombea huyo atapata fursa ya kumwaga sera zake aktika ungwe ya lala salama na wageni waalikwa walioko ukumbini hapo watapata fursa ya kuuliza maswali ya papo kwa hapo kuhusiana na uchaguzi mkuu.

Hivyo Lipumba atatumia nafasi hiyo kueleza sera zake na malengo yake kwa ujumla na endapo akipata ridhaa kupata urais atawafanyia nini watanzania na serikali yake.

Imedaiwa kuwa, Profesa Lipumba, atafunga kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani kesho, na atapata fursa ya kukutana na wananchi katika mkutano maalumu utakaofanyika leo kwenye Hoteli ya Landmark, Ubungo jijini hapa kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:30 mchana na baadae usiku atakwua MovenPick

Aliyemtukana Kikwete aachiwa kwa dhamana




MGOMBEA ubunge kupitia chama cha Demokrasia dna Maendeleo [CHADEMA] jimbo la Temeke Amos Dickson, ameachiwa kwa dhamana na jeshi la polisi baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa masaa kadhaa na jeshi hilo.


Aalifafanua kuwa, jeshi hilo lilimkamata mgombea huyo jana maeneo ya Temeke na kufanya naye mahojiano katika kituo kikuu cha polisi.

Alisema katika mahojianao hayo, mgombea huyo alipewa fursa ya kujitetea na aliwezwa kuachiwa kwa dhamana na upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea

CCM kuishtaki Chadema


CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), kimedhamiria kukishitaki Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na kutukanwa kwa mgombea urais wa chama hicho, Jakaya Kikwete juzi jijini Dar es Salaam wakati wa chama hicho kilipokuwa kikifanya mkutano wa
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Kampeni wa CCM, Kanali mstaafu Abdulrahiman Kinana, alipokuwa akizungumza na waandishi a habari katika ofisi ndogo za chama hicho.

Alisema CCM kinakusudia kuwasilisha malalamiko Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC] na katika ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa ktuokana na Chadema kutumia mkutano huo kumtukana mgombea wao hadharani pasipo na sababu za masingi.

Alisema kitendo kilichofanywa na Chadema mbele ya wananchi hadharani kwa kutukanwa matusi ya nguoni Kikwete matusi yaliyotoka kwenye kinywa cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia Chadema, Amos Dickson, ni udhalilishaji .

Alisema kutoa matusi katika mkutano wa hadhara ni kukiuka kanuni za uchaguzi hivyo ni lazima chama hicho kichukuliwe hatua.

Tsunami yaua watu wengi Indonesia



Zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine wengi hawajulikani walipo kufwatia tsunami iliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika pwani ya Sumatra nchini Indonesia.

Maafisa wanaoshugulika na misaada pia wanajaribu kukabiliana na athari za mlipuko wa volkeno katika Mlima Merapi Katikati mwa Java.




Nyumba kadhaa ziliharibiwa na mawimbi ya bahari karibu na visiwa vya Mentawai.

Maji yaliyofurika yaliharibu kabisa vijiji kumi kwenye visiwa hivyo, afisa mmoja anayeshughulika na uokoaji aliambia shirika la habari la AFP.






Baadhi ya watu walioachwa bila makao
Hali mbaya ya hewa na uharibifu imechelewesha juhudi za kufikia maeneo yaliyoathirika.




Hendri Dori Satoko,mjumbe katika visiwa vya Mentawai,aliambia kituo cha televisheni cha Metro: "takwimu zetu za hivi punde zinaonyesha kuwa watu 108 wameuawa na wengine 502 hawajulikani walipo."

Alisema baadhi ya wale ambapo hawajulikani walipo huenda walikimbilia maeneo salama ya juu na wanaogopa kurudi nyumbani kwao.

Maafisa wa wizara ya afya wanasema miili 113 imepatikana katika eneo hilo kufikia sasa,shirika la habari la Associated Press limeripoti.

Wakati huohuo maafisa wanasema zaidi ya watu elfu kumi na tatu wamehamishwa kutoka maeneo ya karibu na Mlima Merapi na kupelekwa katika kambi tangu mlipuko wa volkeno kutokea.

Lakini hali imeelezewa kuwa ngumu kutokana na idadi kubwa ya watu wanaotaka kuhama na kutafuta hifadhi katika maeneo salama.

Wakaazi wengi wa vijiji vilivyo karibu walipuuza onyo lililotolewa hapo awali na maafisa na hawakuwa tayari kuondoka na kuacha makao na mashamba yao

FIFA yatuma rambi rambi Kenya



Rais FIFA Sepp Blatter



Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema kuwa amesikitishwa na yale yaliyofanyika siku ya Jumamosi usiku katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo mjini Nairobi,tukio lililosababisha vifo vya watu saba na wengine wengi kujeruhiwa.

"Napenda nieleze kusikitishwa kwangu na napenda nitangulize rambi rambi zangu kwa mashabiki wa soka nchini Kenya,na zaidi kwa jamii na marafiki kufwatia vifo hivi," alisema Rais wa FIFA.

"Nafahamu kwamba uchunguzi umeanzishwa. Lazima juhudi zifanywe ili chanzo cha tukio hili baya kijulikane kwa nia ya kuzuia hali hii kutokea kwenye uwanja wa Nyayo tena."




Uwanja wa Nyayo



Ni hapo Jumatatu tu, ambapo FIFA ililitaka shirikisho la soka nchini Kenya FKL kuelezea mazingira, yaliyosababisha mkasa huo kutokea.

Shirikisho la FKL, limepiga marufuku mechi zozote kufanyika katika Uwanja wa Nyayo na ule wa City, hadi watimize masharti ya usalama kuambatana na kanuni za FIFA.

Mkasa huo wa Jumamosi ulitokea wakati mashabiki wa mahasimu wa jadi AFC Leopards na Gormahia waking'ang'ana kuingia uwanjani.

Ilikuwa ni katika pambano la ligi ya kitaifa

Tariq Aziz sasa ahukumiwa kifo



Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Iraq, Tariq Aziz amehukumiwa adhabu ya kunyongwa.

Mahakama ya juu zaidi nchini humo ilimpata Aziz na hatia ya kuwatesa wafuasi wa vyama vya Kishia.

Aziz ambaye pia alikuwa naibu waziri mkuu amekuwa jela tangu Marekani na nchi washirika kuivamia Iraq mwaka wa 2003.




Waziri huyo wa zamani ambaye ni mwumini wa dini ya Kikristo, alijasalimisha kwa majeshi ya Marekani wakati huo.

Mwezi wa Machi mwaka huu, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa kuhusika katika mauaji ya watu 40.





Kwa muda mrefu Aziz alipata umaarufu kimataifa akiiwakilisha serikali ya Iraq na mshauri wa karibu wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein.

Taarifa zaidi zinasema ambaye Aziz anaugua kiarusi, hali yake ya afya ni dhoofu.

Pweza mtabiri Paul amekufa



Pweza Paul amekufa


Pweza aliyepata umaarufu mkubwa wakati wa mashindano ya kuwania Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini amekufa.

Samaki huyo alibashiri matokeo ya mechi zote za Ujerumani nchini Afrika Kusini na baadaye ushindi wa Hispania.

Baada ya mashindano ya Kombe la Dunia pweza Paul alitokea kwenye video akiipigia debe Uingereza kuwa mwenyeji wa kombe la dunia ya 2018.

Kulingana na hifadhi ya Oberhausen nchini Ujerumani, kifo cha pweza huyo aliyepewa jina Paul ni cha kawaida.

Pweza Paul ambaye alikuwa maarufu sana katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa kutabiri sawasawa matokeo ya mechi za timu ya taifa ya Ujerumani nchini Afrika Kusini na pia mechi ya fainali, katika utabiri wake wa mwisho alikuwa akionesha England itakuwa na nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2018

Kipindupindu chaua zaidi ya 250 Haiti



Idadi ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa maradhi ya kipindupindu nchini Haiti imezidi 250.

Zaidi ya watu 3,000 wameambukizwa, alisema Gabriel Thimote, mkurugenzi mkuu wa Idara ya afya wa Haiti.





Watu watano waligundulika kuwa na kipindupindu katika mji mkuu Port-au-Prince, lakini maafisa wa Umoja wa Mataifa alisema wagonjwa waligundulika mapema na kutengwa.





Maafisa wanasema maradhi hayo ni tishio kubwa kwa watu milioni 1.3 waliosalimika tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Januari na ambao wanaishi kwenye mahema katika kambi zilizoko maeneo yanayouzunguka mji huu.




Hali itakuwa mbaya zaidi endapo tutakuwa na maelfu ya watu wakiwa wagonjwa kwa wakati mmoja," alisema rais wa chama cha madaktari wa Haiti, Claude Surena.






Lakini Bw Thimote alielezea matumaini yake kuwa mlipuko huyo utaweza kudhibitiwa

CCM kuishtaki Chadema

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), kimedhamiria kukishitaki Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na kutukanwa kwa mgombea urais wa chama hicho, Jakaya Kikwete juzi jijini Dar es Salaam wakati wa chama hicho kilipokuwa kikifanya mkutano wa
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Kampeni wa CCM, Kanali mstaafu Abdulrahiman Kinana, alipokuwa akizungumza na waandishi a habari katika ofisi ndogo za chama hicho.

Alisema CCM kinakusudia kuwasilisha malalamiko Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC] na katika ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa ktuokana na Chadema kutumia mkutano huo kumtukana mgombea wao hadharani pasipo na sababu za masingi.

Alisema kitendo kilichofanywa na Chadema mbele ya wananchi hadharani kwa kutukanwa matusi ya nguoni Kikwete matusi yaliyotoka kwenye kinywa cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia Chadema, Amos Dickson, ni udhalilishaji .

Alisema kutoa matusi katika mkutano wa hadhara ni kukiuka kanuni za uchaguzi hivyo ni lazima chama hicho kichukuliwe hatua

Mtoto ajeruhiwa kwa risasi na askari



MTOTO Juma Hamza (12) amejeruhiwa kwa kupigwa risasi maeneo ya tumboni, wakati askari walipokuwa wakijihami na wananchi.


Mtoto huyo alijeruhiwa na mmoja wa askari hao wa kituo cha polisi Chang’ombe wakati walipokuwa wakitoka kukamata waharifu.

Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Temeke, Kamishna wa Polisi, David Misime, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi Keko, karibu na ukumbi unaojulikana kwa jina la Jumba la Dhahabu.

Misime alisema, askari hao walipata taarifa kuwa kuna watu walipora kamera kutoka kwa mtu aliyekuwa akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa MWalimu Nyerere kwa kumtishia kwa panga muibia na kufanikiwa kupora kamera hiyo na kut oweka nayo..

Hivyo askari hao walifanikiwa kukamata waharifu hao na katika harakati za kupambana nao ndipo mtoto huyo alijeruhiwa maeneo yake ya tumboni kwa kuwa kulikuwa na mpambano mkali akti ya skari na waharifu hao kwa kufytua risasi kati yao

Hivyo katika harakati hiyo mtoto huyo aliweza kujeruhiwa na amechukuliwa na kukimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na hali yake kudaiwa inaendela vizuri.

Misime alisema, hakuna askari yeyote anayeshikiliwa katika tukio hilo kwa kuwa ajali hiyo imetokea kwa bahati mbaya

Nitaboresha kinywaji aina ya gongo- mgombea TLP



MGOMBEA wa urais kupitia Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Mutamwega Mgahywa amesema, akipewa ridhaa ya kuongoza nchi atabadilisha uchumi ikiwa ni pamoja na kujenga viwanda vitakavyomilikiwa na watanzania.
Mgombea huyo anayeomba ridhaa k wa wananchi alisema kuwa atafufua viwanda mama vilivyokufa kitambo na kuimarisha uchumi wa watanzania kwa viwanda hivyo.

Hivyo katika mkutano wake alisema hata kinyaji aina ya gongo kitakublika katika uongozi wka kuwa ataboresha kinywaji hiko katik ngazi za kimataifa kwa kuzalishwa kiwandani.

“Gongo itakuwa inazalishwa kiwandani, na si kama inavyofanyika sasa haina ubora ndio mana kinywaji hicho kinapigwa vita, hivyo itaboreshwa kwa kiwango vya hali ya juu” alisema

Hata hivyo baadhi ya wananchi walifurahi na kupiga makofi na kusikia ahadi hiyo ambayo baaadhi huwa wanaendesha uuzaji wa kinywaji hicho kwa shida kwa kuwa kinywaji hicho kinapigwa vita na serikali

Alisema, Tanzania haina viwanda vya uhakika jambo ambalo linachangia umasikini na vichache vilivyopo vinamilikiwa na watu kutoka nje.

Bado siku tano



KILA kona ya nchi, jiji na vitongoji vyake watanzania wamekuwa wakiisubiria kwa hamu siku ya Oktoba 31, ili waweze kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika kipindi cha miaka kumi na tano ijayo.
Hali hiyo imefanya watanzania wengi kuzungumzia siku hiyo huku kila mmoja akiwa na shauku kubwa ya kuingia katika chumba cha kura cha kumchagua kiongozi wake anayempenda amuongoze kwa kuridhika na utendaji wake ama sera zake.

Katika hali hiyo uchaguzi wa mwaka huu, umekuwa na upinzani huku wengine wakiusisha uchaguzi huu kutawaliwa na udini hali inayofanya watu kuisubiri siku hiyo ili waweze kumaliza mizozo na ubishani ambao umetawaliwa kwa rika zote.

Hivyo pia watanzania wametakiwa watembelee vituo vyao vya kupigia kura kukagua majina yao ili kuhakiki kama jina lake lipo katika kituo husika.

Wagombea nao wamekuwa wakimwaga sera zao zao katiika wiki la lala salama na kuendelea kumwaga ahadi kemkem katika kutafuta kura.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, UCHAGUZI UISHE KWA USALAMA, NA AMANI IENDELEE KUDUMU NDANI YA NCHI YETU

Msalaba Mwekundu kutoa huduma ya kwanza siku ya uchaguzi.



KATIKA hali ya kuonekana serikali imejipanga vizuri katika harakati za uchaguzi mkuu, Chama cha Msalaba Mwekundu[RedCross] kimeandaliwa kuhakikisha kinatoa huduma ya kwanza ya dharura kwa wapiga kura katika vituo vyote siku ya uchaguzi Oktoba 31,
Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Mayasa Mikidadi.

Mikidadi alisema kuwa, chama hicho kimejiandaa vya kutosha kutoa huduma ya kwanza ya dharura siku ya uchaguzi kwa wapiga kura katika vituo vyote kwa kuwa siku hiyo huwa na mlundikanao wa watu wengi mahala pamoja..

“Tutasaidia watu watakaokuwa wamezidiwa katika foleni, ambao wengine wana BP, na magonjwa mengine ambayo yatawafanya wakose amani, wagonjwa kuwasaidia”

Wajue Wagombea 7 Wa Urais Tanzania


Fahmi Dovutwa -Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha UPDP


Uchaguzi mkuu wa Tanzania utafanyika oktoba 31 jumapili ijayo, je unawajua wagombea wote saba wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Jumapili ijayo Watanzaniawaliojiandikisha kupiga kura watatumia kura zao kumchagua rais mpya wa muungano wa Tanzania.

Jumla ya wagombea saba toka vyama saba tofauti wanawania nafasi hiyo muhimu ya kuliongoza taifa la Tanzania.

Je unawajua wagombea wote saba wa Urais? Kama huwajui basi wagombea urais ni hawa wafuatao.


Muttamwega Mgahywa: TLP
Mbunge wa jimbo la Mwibara, Mkoa wa Mara toka mwaka 1995. Katika bunge lililopita alikuwa Waziri Kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri kivuli katika Ofisi ya Makamu wa Rais.

Fahmi Nasoro Dovutwa: UPDP
Fahmi Nasoro Dovutwa amekuwa mwenyekiti wa chama cha UPDP( United Peole Democratic Party) toka mwaka 2000. Ni mjasirimali mwanasiasa anayegombea urais kwa mara ya kwanza.

Peter Kuga Mziray :APPT-MAENDELEO
Mziray ni Mchumi wa Kilimo mwenye shahada ya uzamili aliyoipata Moscow, Urusi. Alikianzisha chama cha APPT Maendeleo mwaka 1990 baada ya kujiengua NCCR-Mageuzi. Mara yake ya kwanza kugombea urais.

Hashim Rungwe: NCCR-MAGEUZI
Bwana Rungwe ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Baraza la Wadhamini wa chama cha NCCR-Mageuzi. Hii ni Mara ya kwanza kwake kugombea urais.


Dokta Wilbrod Slaa: CHADEMA
Kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa, Dkt. Slaa alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kanisa Katoliki.
Amekuwa mbunge wa Karatu kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia mwaka 1995 hadi sasa. Alikuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA kati ya mwaka 1998 na 2002 na baadae aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa CHADEMA kuanzia mwaka 2002 hadi 2010. Hii ni mara yake ya kwanza kugombea urais.

Dokta Jakaya Mrisho Kikwete: CCM
Mgombea urais kupitia CCM. Anawania kuliongoza taifa la Tanzania kwa miaka mingine mitano baada ya muhula wake wa kwanza wa miaka mitano kuisha.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba: CUF
Kwa mara ya nne sasa Profesa Lipumba anagombea urais wa Tanzania tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania. Amewahi kuwa mwalimu wa vyuo vikuu vya Marekani na Tanzania na baadaye kuwa Mshauri wa uchumi wa Serikali ya Uganda kati ya miaka 1980 hadi 1990

JK atangaza kumaliza tatizo la maji umasaini




digg
Kizitto Noya, Simanjiro
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete jana aliendelea na kampeni katika Jimbo la Simanjaro ambako pamoja na mambo mengine, aliahidi kutafuta Sh30 bilioni kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji kwenye jamii hiyo ya wafugaji.

Akizungumza kwenye viwanja vya Orkesumet, makao makuu ya Wilaya ya Simanjiro, Kikwete alisema mbali na kumaliza tatizo hilo, serikali yake ijayo pia itatoa ruzuku ya dawa ya josho za ng’ombe kwa wafugaji.
“Jitihada za awali za tatizo la maji tayari zimeelezwa na mbunge wenu (Ole Sendeka) lakini serikali inajipanga kumaliza kabisa tatizo hilo," alisema Kikwete.


“Tunahitaji kuwa na Sh30 bilioni kwa ajili ya kuvuta maji kutoka Mto Ruvu na huu ni mradi mkubwa ambao mipango ya awali ya kuomba fedha imeshaanza.”
Kwa mujibu wa Kikwete, wakati serikali inaendelea kusubiri Sh30 bilioni, jitihada za awali zimeanza kwa kutenga Sh1.8 bilioni kwa ajili ya kuchimba visima virefu vya maji.

“Tutachimba visima hivyo kwa awamu. Tutaanza na vijiji 12 na baadaye vijiji vingine vilivyobaki,” alisema Kikwete ambaye pia alieleza kuwa lengo la serikali yake ijao ni kumaliza kabisa tatizo la maji nchini.
Kikwete alisema maelekezo ya CCM kwa serikali ijayo, ni kuhakikisha inatengeneza mipango ya kuendeleza sekta za maji, mifugo na kilimo na yeye kama msimamizi mkuu wa maelekezo hayo, amejipanga ipasavyo kuhakikisha hilo linafanikiwa.

“Tuchagueni tuendelee kustawisha nchi yetu. Tutahakikisha kila mfugaji anakuwa na maji yake katika kipindi chote cha mwaka ili kuondokana na tatizo la kuhamahama,” alisema
Awali kabla ya Kikwete kuanza kuhutubia, mbunge anayetetea nafasi yake kwa tiketi ya CCM jimboni humo, Christopher Ole Sendeka alimkabidhi rungu na mgolole kama ishara ya ushindi na uongozi.

Baadaye mbunge huyo mteule alisema CCM ni chama kinachostahili kuendelea kuongoza nchi kwani kimefanya mengi katika kipindi kifupi cha miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Kikwete.
“Katika kipindi hicho cha miaka mitano, makao makuu ya Simanjiro ya Orkesumet hayakuwa na umeme, lakini sasa tumefanikiwa kusambaza umeme,” alisema Ole Sendeka.

“Katika kipindi hicho pia tumechimba visima 55 virefu vya maji na kuongeza idadi ya wanafunzi wa sekondari kutoka 180 hadi 2,300. Tumeongeza pia shule kutoka tatu hadi 16 na kufanikiwa kutengeneza barabara ya Simanjiro hadi Arusha,” alisema
Rais Kikwete jana alifanya kampeni katika majimbo ya Kiteto, Simanjiro na Karatu kwa mpinzani wake wa urais, Dk Willibrod Slaa.

Tathimini inaonyesha kuwa Kikwete atapata kura nyingi zaidi kuliko wagombea wengine wa vyama vya upinzani katika jimbo la Simanjiro hasa baada ya ole Sendeka kupita bila kupingwa huku CCM ikipita pia bila kupingwa katika kata 16 kati ya kata 18 za jimbo hilo

CCM yataka wanachama wasitembee na visu Jumapili




digg
Ally Mkoreha na Sadick Mtulya, Zanzibar
CCM visiwani Zanzibar ,imewataka wanachama wake kutotembea na silaha ya aina yoyote katika siku ya kupiga kura. Pia kimewataka wasichokoze wala kuchokozeka na watu watakaojaribu kuwachokoza.

Kimesema kufanya hivyo, kutasaidia kuufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika kote nchini Jumapili ijayo, kuwa wa amani.

Wito huo ulitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM visiwani Zanzibar , Salehe Ramadhan Feruzi, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama hicho, uliofanyika katika Jimbo la Dole, Mjini Magharibi.

Mkutano huo ulihutubiwa na mgombea mwenza wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal.

“Ndugu zangu nachukua nafasi hii tuwekane sawa kuhusu siku ya kupiga kura. Tunaomba wanachama na wafuasi wa CCM siku hiyo wasitembee na okapi (visu) na wala tusivae sare au kutembea na kitu chochote chenye nembo ya chama chetu,” alisema Feruzi kabla ya kumkaribisha Dk Bilal kuhutubia.

Pia aliwataka wahimizane na kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupiga kura, ili kukiwezesha chama chao kuibuka na ushindi.

Kwa upande wake, mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha, alisema ushindi wa CCM ni wa lazima na kwamba hiyo inatokana na ukweli kwamba chama hicho kina sera zinazokubaliwa hata na wapinzani.

“Lakini pia matukio mawili ya hivi karibuni, pia yanaashiria ushindi mkubwa wa CCM. Viongozi wakubwa wawili wa CUF walikiagaa chama chao na kujiunga na CCM. Lakini pia kule Mwanakwerekwe watu wazima walilishana chakula hadharani. Hii ni ishara kubwa ya ushindi wa CCM,” alisema Nahodha ambaye pia ni Waziri Kiongozi anayemaliza muda wake katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .

Akizungumza katika mkutano huo, mgombea (Bilal), aliwataka wanachama wa CCM wajipange na kuhakikisha kuwa siku ya kupiga kura, wanawachagua Jakaya Kikwete kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk Ali Mohamed Shein, kuwa Rais wa Zanzibar .

“Mimi nimeshalala kwenye zaidi ya vitanda 63 nikiomba kura nchi nzima. Nanyi nakuombeni mtumie lugha laini hata kwa wapinzani wetu, kuomba kura, msiwaogope,” alisema Dk Bilal.

Alisema Kikwete na Shein, wamejipanga kuiletea Tanzania maendeleo na kuhakikisha kuwa amani ya nchi inaendelea kudumu.

“CCM tayari imeshajipanga kuwarithisha vijana amani kama ilivyowarithisha viongozi walioko madarakani ambao hawana hasira, chuki na ni watulivu,” alisisitiza Dk Bilal ambaye hata hivyo hakutumia muda mrefu kuhutubia.

Wafanyakazi TRL waipinga serikali kununua mitumba



Jackson Odoyo
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Reli (TRL) wanaupinga mpango wa serikali wa kununua mitambo chakavu ya mwekezaji kutoka India ambayo ilikodishwa kwa ajili ya kusaidia kupunguza tatizo la usafiri.

Kampuni ya Reli ya India (Rites), ambayo ni mwekezaji mwenye asilimia 51 za hisa za TRL, iliagiza mabehewa 23 na injini tano kutoka India kwa ajili ya kuyakodisha, lakini wafanyakazi walidai kuwa ni mitumba na yanaisababishia kampuni hasara kubwa. Akizungumza na wafanyakazi hao jana wakati wa kikao cha pamoja jijini Dar es Salaam, katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu), Sylvester Rwegasira alisema hawawezi kukubaliana na serikali katika suala hilo kwa sababu wao ndio wategemizi namba moja wa reli hiyo.

“Hatuwezi kukubaliana na uamuzi wa serikali wa kununua injini chakavu na mabehewa hayo kwa sababu havina ubora na havifai kwa matumizi ya nchi hii,” alisema Rwegasira. Alisema serikali ikishikilia msimamo huo wa kununua injini hizo pamoja na mabehewa, wafanyakazi hawatakuwa tayari kuzitumia na badala yake watalazimika kuacha kazi.

“Serikali inaendelea na mchakato huu na hadi hivi sasa kuna timu ya watu watatu kutoka Dar es Salaam, Morogoro na Tabora kwa ajili ya kukagua njini hizo,” alisema Rwegasira. “Ili kuona kama zitafaa kwa matumizi na hatimaye serikali ilipe fedha hizo wakati kuna tarifa mbalimbali zimeshatolewa kuhusu ubovu wa injini hizo pamoja na mabehewa lakini hazijafanyiwa kazi hadi hivi sasa,” alisema Fortunatus Chiliko.

Chiliko alisema Mamlaka Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra) ilisimamisha mabehewa hayo kwa sababu ya ubovu kabla ya Rites kuzuia matumizi yake ikidai ilipwe fedha zake za kukodishia injini na mabehewa hayo, leo hii Rites hiyo hiyo iko tayari kuuza kwa sababu wanatambua kuwa haviwezi kufanyakazi tena. Katika hatua nyingine Rwegasira alisema wafanyakazi pia wanaitaka serikali kuiondoa menejimenti iliyowekwa na Rites kwa sababu tayari kuna uongozi wa mpito ulio chini ya wazawa

Wanasayansi waunganisha nguvu kutokomeza Ukimwi



Neville Meena, Vienna – Austria

TAASISI kadhaa za kimataifa zinazojihusisha na utafiti wa dawa ya Ukimwi zimekubaliana kuunganisha nguvu zao ili kuharakisha upatikanaji wa tiba ya ugonjwa huo.

Tofauti na mwanzoni ambapo taasisi hizo zilikuwa zinafanya kazi kwa kujitegemea, sasa zimeamua kuungana ili kufanikisha lengo la kupatikana dawa ya kuponya au chanjo ya kinga ya ukimwi.

Wanasayansi hao sasa wanahaha kutafsiri matokeo ya tafiti mbalimbali zilizoonyesha mafanikio katika kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi ili zianze kuingia katika upatikanaji wa tiba na chanjo halisi za ugonjwa huo.

Katika mkutano wa Kimataifa wa Ukimwi unaofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Reed Messe Wien, mjini Vienna, wakuu wa taasisi zinazotafiti tiba ya ugonjwa huo wamekuwa wakitoa kauli zinazofanana kuhusu umuhimu wa kuuganishwa nguvu za utafiti na kuwepo kwa mfumo rasmi unaoziwezesha kubalishana matokeo ya tafiti husika.

Taasisi iitwayo The Global HIV Vaccine Enterprise ya nchini Marekani ndiyo imepewa jukumu la kuwakutanisha watafiti ambao sasa wanayafanyia kazi matokeo ya awali ya tafiti mbili ambayo yameonyesha kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa dawa na chanjo ya ukimwi, pamoja na utafiti uliowezesha kupatikana kwa dawa ambayo inadhibiti maambukizo ya ukimwi kwa wanawake.

Akizindua mpango wa unaoitwa ‘Njia ya kuelekea katika mafanikio ya kudhibiti Ukimwi’, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk Alan Bernstein alisema: “Kupatikana kwa chanjo salama na yenye uwezo wa kuzuia maambukizi ndiyo changamoto kubwa iliyo mbele ya wanasayansi hivi sasa”.

Kwa mujibu wa Dk Bernstein, mafanikio hayo yanatoa changamoto kwa wanasayansi na watafiti kuharakisha mchakato wa utafiti mwingine utakaowezesha dunia kupata chanjo au tiba salama na ya uhakika.

“Tumefungua ukurasa mpya wa kiutafiti wa chajo ya Ukimwi. Ipo ndani ya uwezo na kwa mtazamo wetu. Lakini ipo haja ya kujitoa mbali na rasilimali zinazohitajika, pia ujuzi wa kisanyansi wa hali ya juu na mwisho lazima tuwe na maono ya pamoja ya kiutafiti katika kulikabili janga la ukimwi,”alisema Dk Bernstein alipozungumza na Mwananchi baada ya kuzindua mpango huo.

Wiki iliyopita wanasayansi wa Marekani waligundua chembechembe yaani antibodies, zenye uwezo mkubwa wa kuzuia virusi wa Ukimwi (HIV) kuingia kwenye seli nyeupe za damu — kwa 90% — hivyo kusitisha mazaliano ya HIV.

Taarifa hizo zilitangazwa na wanasayansi wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaid) ya Marekani, wakisema tiba hiyo inaweza kuzuia virusi vya ugonjwa huo hatari kwa asilimia 90, kiwango kinachoiweka dawa hiyo kwenye uwezekano mkubwa wa kupitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kuanza kutumika rasmi.

Dawa hiyo huchochea mwili na kuuongoza katika kujitengenezea aina ya chembechembe za kinga zenye uwezo wa kukabili virusi vya ukimwi. Chembechembe hizo zimepewa jina la kitaalamu la VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuvikabili virusi vya Ukimwi kwa asilimia 90.

Juzi Kituo cha Utafiti wa magonjwa ya Ukimwi cha nchini Afrika ya Kusini (Caprisa)
kilitangaza kugundua dawa aina ya Tenofovir ambayo ni mafuta (gel) yanayopunguza uwezekano wa wanawake kuambukizwa virusi vya ukimwi wanapofanya tendo la ndoa na wanaume walioathirika.

Mafanikio ya Caprisa yalitanguliwa na mafanikio mengine ya taasisi ya nchini Marekani inayoshughulikia magonjwa ya kuambukiza na athari zake (NIAID) anbayo wiki mbili zilizopita ilitangaza kugundua chembechembe (antibodies) zenye uwezo wa kuvikabili virusi vya ukimwi kwa asilimia nyingi.

Mwaka jana wataalamu wa afya nchini Thailand kupitia mradi unaofadhiliwa na Jeshi la Marekani walibaini chembechembe katika mwili wa binadamu zenye uwezo wa kuvikabili virusi vya Ukimwi kwa asilimia 30, hatua ambayo iliwatia ‘wazimu’ watafiti wengine duniani kuanza harakati za kutafuta dawa ya tiba ya ugonjwa huo.

Utafiti wa Thailand ulibaini chembechembe za aina mbili zenye uwezo wakukabiliana na virusi vya ukimwi ambazo kitaalamu zinaitwa PG9 na PG16 ambapo katika matokeo mapya ya taasisi ya NIAID pia zimegunduliwa chembechembe mbili ambazio kitaamu zinaitwa VCR01 na VCR02.

Hata hivyo kwa mujibu wa taratibu za kitaalamu, lazima ziwepo tafiti nyingine za kuthibitisha matokeo ya tafiti za awali kabla ya bodi na mamlaka mbalimbali za udhibiti hazijaidhinisha kuanza kutengenezwa na baadaye kusambazwa kwa dawa husika.

Dk Bernstein alisema kazi iliyopo mbele ya wanasayansi na watafiti hivi sasa ni kubainisha maeneo au ajenda za utafiti kwa kuzingatia matokeo ya tafiti za awali pamoja na kuboresha miundombinu ya mawasiliano ili kuwezesha upatikanaji wa takwimu na taarifa nyingine za kiutafiti.

“Pia ni lazima turuhusu watafiti wapya wenye mawazo mapya ya kisayansi huku tukitafuta vyanzo vipya vya fedha kwa ajili ya kugharamia hatua hii mpya inayoweza kutupa majibuya uhakika kuhusu tiba ya Ukimwi,”alisema Dk Bernstein.

Kwa upande wa matokeo ya utafiti wa kisayansi wa nchini Marekani na Thailand, wataalamu wanalazimika kutafiti zaidi ili kufahamu jinsi chembechembe zilizobainika zinavyoweza kujenga kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi na matokeo ya tafiti hizo ndiyo yatakayowezesha kutafutwa kwa chanjo husika.

Mmoja wa viongozi na washauri waandamizi katika tafiti za tiba ya Ukimwi duniani Dk. José Esparza alisema: “Pamoja na matoke mazuri ya tafiti hizi, hatuwezi kusema tumekaribia kupata tiba kamili inayoweza kutumiwa na umma dunia nzima”.

Kwa mujibu wa Dk Esparza wajibu wa watafiti ni kuugana sasa na kuhakikisha inapatikana dawa baada ya kupitia katika hatua zote ili kukidhi matakwa ya kitaalamu.

Aliongeza: “Ili kufikia hapo inaweza kutuchukua mika mingine 10 au 15 tukihusisha watafiti wapya na wenye upeo mpya katika masuala ya kisayansi”.

Hata hivyo upatikanaji wa fedha unaweza kuwa kikwazo cha kukamilishwa kwa tafiti hizo kutokana na fedha zilizotolewa mwaka jana dunia nzima kuwa dola za Marekani milioni 800 tu ikiwa ni pungufu ya asilimia 10 ya kiasi cha fedha zilizotolewa mwaka 2007.

Wastani wa mahitaji ya kuwatibu watu wanaohishi na virusi vya Ukimwi duniani pamoja na gharama nyingine zinazotokana na ugnjwa huo ni dola za Marekani bilioni 30 kwa mwaka na watafiti wanaona umuhimu wa serikali za dunia kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha tafiti za tiba ya ugonjwa huo ili kupunguza gharama zinazotumika hivi sasa.

Tangu ugonjwa wa Ukimwi ulipogunduliwa mwaka 1983, umesababisha vifo vya watu zaidi ya milioni 25 duniani na inakadiriwa kuwa hivi sasa watu milioni 33 wanaishi na virusi vya Ukimwi na Ukimwi huku kukiwa na nyongeza ya watu 7,400 wanaoambukizwa kila siku

Rwasa aondolewa FNL


BUJUMBURA, Burundi

MGOGORO wa kisiasa unaonekana kuzidi kufukuta nchini Burundi baada ya taarifa zilizopatikana jana kueleza kwamba kiongozi wa chama cha upinzani cha FNL nchini humo, Agathon Rwasa ameondolewa katika mamlaka yake kama mkuu wa chama hicho.

Kikao hicho kilixchotangaza kumuondoa kilihudhuriwa na watu 350, wengi wao vijana na taarifa ya ufunguzi ilieleza kuwa chama cha FNL kimeamua kuisawazisha hali baada ya kupata pigo kubwa kutokana na hatua yake ya kuususia uchaguzi wabunge mwezi uliopita.

Hii ni mara ya tano wapinzani hao wa Agathon Rwasa wanajaribu kumwondoa madarakani kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kundi moja la chama hicho lilifanya kikao maalum ambapo Emmanuel Mibiro aliyekihama chama hicho cha FNL na kujiunga na serikali aliteuliwa kiongozi .

Mibiro ambaye awali alikuwa mshirika wa karibu wa Rwasa na ambaye chama chake kilisusia uchaguzi mkuu mwanzoni mwa mwezi uliopita kwa sasa anahudumu kama mshauri wa Rais Nkurunziza. Jacques Bigirimana ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa FNL.

Hata hivyo washirika wa Rwasa wamepuzilia mbali mkutano huo na kuutaja kama njama za serikali kukisambaratisha chama cha FNL.

Makamu mwenyekiti wa FNL, Alfred Bagaya alisema Agathon Rwasa ndiye kinara wa chama cha FNL na kwamba hakuna kinara mwingine anayetambuliwa na wanachama atiifu wa chama hicho.

Kundi lililomtimua Rwasa lilisema liliamua kuchukua hatua hiyo baada ya Rwasa kuamua kukimbilia mafichoni na hivyo kuhujumu shughuli za chama hasa pale alipotangaza chama hicho kususia uchaguzi mkuu Burundi, wakati yeye akiwa mgombea wa nafasi ya rais dhidi ya Nkuruzinza.

Rwasa ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Rais Nkurunziza katika uchaguzi mkuu wa mwezi Juni, ambapo hatua ya wapinzani kutangaza kususia uchaguzi huo ilimpa ushindi wa nafasi hiyo bila upinzani.

Hatua hiyo ya Rwasa kuongoza vyama vikuu vya upinzani kususia uchaguzi huo ilitokana na malalamiko yao kuhusu kuwepo kwa dosari kwenye mfumo wa uchaguzi. Kwa sasa Rwasa yupo mafichoni akihofia usalama wake

Wabunge sita, raia 32 wauawa Somalia



MUUAJI wa kujitoa mhanga na wapiganaji wenye silaha wamevamia na kushambulia hoteli moja mjini Mogadishu, Somalia, taarifa za awali zikieleza kwamba wamewaua zaidi ya watu 32 wakiwemo baadhi ya wabunge, wanaokadiriwa kufikia sita.

Mmoja wa wabunge aliyekuwepo katika hoteli hiyo ya Muna ambayo ni maarufu kwa viongozi wa serikali ya nchi hiyo alisema ilikuwepo miili ya watu waliofariki dunia kila mahali, na kuita tukio hilo mauaji ya halaiki.

Mbunge huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema mara tu baada ya mashambulizi hayo kutokea yakiambatana ma mlipuko wa bomu aliona miili zaidi ya 27 ikiwa imelala kwenye baraza ya hoteli hiyo, ukiwemo wa mbunge mmoja.

Alisema mlipuaji huyo wa kujitoa muhanga alijipenyeza na kujilipua karibu na sehemu ya mapokezi ya hoteli hiyo na kusababisha mapambani ya silaha yaliyochukua zaidi ya saa moja na nusu.

Msemaji wa Umoja wa Afrika (AU), Meja Barigye Bahoku alisema haikuweza kufahamika idadi kamili ya waliouawa mara moja katika mashambulio hayo kwenye hoteli ya Muna, iliyopo umbali wa kilometa moja kutoka makazi ya rais, ambayo pia hutumi ana wabunge wanapokuwa mjini Mogadishu.

Ofisa huyo wa usalama aliliambia shirika la habari la AFP kuwa hawana hakika ni kundi gani limefanya shambulio hilo lakini wanaamini ni wapiganaji wa kundi la al-Shabab walioingia katika hoteli hiyo wakiwa wamevalia sare za jeshi la usalama.

“Ninachoweza kueleza kwa sasa ni kwamba wamewaua watu kadhaa wakiwemo wabunge. Nafikiri wabunge waliokufa wanafikia wanne,” alisema mmoja wa maofisa wa usalama wa serikali.

Kundi la wapiganaji wa kiislamu la al-Shabab lilianza mashambulizi makali Jumatatu wiki hii, muda mfupi baada ya msemaji wake kutangaza vita kali dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya AU, akisema kwamba askari hao zaidi ya 6,000 wanaoisaidia serikali dhaifu ya nchi hiyo ni “wavamizi”.

Mkuu wa utoaji wa huduma za kusafirisha wagonjwa, Ali Muse alisema tangu Jumatatu wiki hii, mapigano yaliyoibuka katika mji huo wa Mogadishu yameripotiwa kusababisha vifo vya watu 40 na kujeruhi zaidi ya watu 130.

Mwezi uliopita, al-Shabab ilidai kuhusika na milipuko miwili iliyosababisha vifo vya watu 76 nchini Uganda, ikidai mashambulizi hayo yalikuwa ni kulipiza kisasi kwa nchi hiyo kupeleka askari wake kwenye kikosi cha kulinda amani cha AU nchini Somalia.

Mwaka jana, kundi hilo la al-Shabab lilishambulia kwa bomu la kutupwa kwa mkono dhidi ya hoteli hiyo mwaka uliopita na kuwajeruhi wabunge wawili.
AFP

Mtuhumiwa wa vurugu kampeni afia mikononi mwa polisi



Ndeninsia Lisley (RCT)

WAKATI zikiwa zimesalia siku nne kabla ya uchaguzi mkuu, imedaiwa kuwa mtu anayetuhumiwa kufanya vurugu kwenye kampeni za CCM, jimbo la Kawe amefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi.

Kifo hicho cha Alfred Mushi, 35, kilichothibitishwa na Jeshi la Polisi kilitokea juzi wakati mtuhumiwa huyo akiwa mikononi mwa polisi na awali ilidaiwa kuwa baada ya kufanya fujo katika kampeni hizo za udiwani na ubunge za CCM, alikamatwa na kufikishwa katika kituo kidogo cha polisi cha Tegeta kabla ya mauti kumkuta.

Kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Suleimani Kova alithibitisha kutokea kwa kifo hicho akikielezea kuwa ni cha kutatanisha na kudai kuwa baada ya taarifa hiyo kutolewa kwa uongozi wa polisi wilaya ya Kawe, jalada la kifo hicho lilifunguliwa na uchunguzi kuanza mara moja ili kubaini chanzo halisi.

Alisema taarifa walizonazo ni kwamba Mushi alikuwa akijibamiza kichwa ukutani na kupiga mahabusu wengine wakati akiwa kituo kidogo cha polisi cha Kawe ambako alipelekwa na mgambo aliyemkamata na kwamba alikataa kula chakula alicholetewa na ndugu zake.

Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mtuhumiwa huyo alikumbwa na mauti hayo akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu baada ya hali yake kuwa mbaya na kwamba amri ya kumpeleka hospitali ilitolewa na kamanda wa polisi na mkuu wa upelelezi wa wilaya hiyo baada ya ya hali yake kuonekana kuwa mbaya.

Kamanda Kova alisema kuwa Mushi alikamatwa Agosti 21 majira ya saa 10:00 jioni akiwa stendi ya mabasi Tegeta ambako kulikuwa na mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa CCM.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, uchunguzi wa awali ulibaini kuwa Mushi alikamatwa na mgambo aliyemtaja kwa jina la Mohamed Manjolo ambaye alipewa taarifa kuwa mtu huyo alikuwa anafanya vurugu kwenye mkutano wa kampeni.

Alidai kuwa Manjolo aliwaeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na wenzake ambao walitoroka. Alisema watu hao walikuwa wakitoa lugha za matusi na kurusha mawe kwa watu waliohudhuria mkutano huo na kwamba alionekana mlevi, hivyo walimkamata na kumfikisha kituo cha polisi.

Kova alidai kuwa Mushi alikuwa akiwapiga mahabusu wengine wakati akiwa kituoni licha ya kuonekana mlevi.

“Alikuwa akijibamiza kichwa na mwili wake kwenye ukuta ndani ya chumba cha mahabusu,” alisisitiza Kamanda Kova.

Alisema kutokana na vurugu hizo askari waliamua kumfunga pingu ili asiwadhuru wengine.

“Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alijifungua pingu hiyo mkono mmoja, lakini mahabusu wenzake kwa kushirikiana na askari walimfunga mtuhumiwa huyo mikono,” alisema Kova.

Alisema kutokana na hali hiyo mtuhumiwa huyo hakuweza kuchukuliwa maelezo kwa mategemeo kuwa angetulia baadaye na maelezo yake kuandikwa.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, mahabusu wenzake walidai kuwa Mushi alikataa chakula alichopelekewa na ndugu zake.

mwelezea mtuhumiwa huyo kuwa licha ya vurugu alizokuwa akifanya ndani ya mahabusu za kujibamiza kichwa ukutani, kujifungua pingu na kumng’ata mmoja wa mahabusu kidole cha mguu wa kulia cha mwisho lakini pia alikataa hata kula chakula alicholetewa na ndugu yake

Waziri wa Mambo ya Nje Kenya ajiuzulu



Waandishi wa Mwananchi, Nairobi

VIONGOZI wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje nchini Kenya wamejiuzulu kukwepa shinikizo la Bunge la kutaka waachie ngazi kuruhusu uchunguzi dhidi ya kashfa za ubadhirifu na matumizi mabaya ya mali ya umma zinazowakabili. Wakuu hao, Moses Wetangula, ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, na katibu mkuu wake, Thuita Mwangi walijiuzulu jana baada ya kuibuka kashfa za ubadhirifu katika mikataba mitano ya ununuzi wa majengo matano ya balozi za nchi hiyo kwenye nchi tofauti.

Viongozi hao wamejiuzulu muda mfupi baada ya Rais Mwai Kibaki kutangaza kwamba serikali yake haitakuwa na mzaha kwa kiongozi yeyote atakayetuhumiwa kwa rushwa na ufisadi. Wawili hao wamejiuzulu ikiwa ni wiki moja baada ya Rais Kibaki kutangaza kumsimamisha kazi Waziri wa Elimu ya Juu, William Ruto kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili za ubadhirifu baada ya mahakama kutoa uamuzi kwamba anatakiwa kujibu tuhuma hizo mahakamani. Uamuzi wa kujiuzulu kwa Wetangula, ambaye hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia, pamoja na katibu huyo ulifikiwa baada ya majadiliano baina yao na Rais Kibaki kwenye ofisi zilizo kwenye Jengo la Harambee.

Mwangi alianza kwuasilisha barua yake akifuatiwa na Wetangula. Kwa mujibu wa ripoti ya kamati malum ya Bunge, serikali ya Kenya imepoteza dola 14 milioni za Kimarekani katika mpango wa ununuzi wa nyumba kwa ajili ya ofizi za ubalozi wake nchini Japan, huku Wizara hiyo ikituhumiwa kwa ubadhirifu katika mikataba kadhaa ya aina hiyo iliyofanyika nchini Misri, Nigeria, Pakistan na Ubelgiji. Katika tuhuma hizo, Wizara ya Mambo ya Nje inadaiwa kukataa ardhi ya bure kutoka kwa serikali ya Japan katikati mwa jiji la Tokyo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi mpya za ubalozi na kuamua kwenda kununua jengo mbali na eneo hilo, tofauti na ushauri uliotolewa awali na wakala mshauri wa serikali. Wakuu hao walitangaza uamuzi wao wa kujiuzulu kabla ya Bunge kukamilisha mjadala wa taarifa ya kamati hiyo ya Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa.

Katika mjadala wa Bunge uliokuwa ukiendelea wakati wakuu hao wakitangaza kujiuzulu, lawama zilikuwa zikielekezwa kwa Wetangula ambaye juzi alielekeza lawama kwa maofisa wa wizara hiyo kwa kutokuwa makini katika suala hilo. Akitangaza uamuzi wake mbele ya waandishi wa habari waliokusanyika kwenye ofisi yake saa 3:00 baada ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Rais Kibaki, Wetangula alisema anamini kuwa yeye ni mtu safi asiye na hatia. "Nataka kuwaambia Wakenya kuwa dhamiri yangu iko wazi kwa uamuzi wangu mchana huu. Kwa hatua hii ya uwajibikaji wangu kama Waziri wa Mambo ya Nje ni kutoa nafasi kwa wale wanaonituhumu kufanya uchunguzi,” alisema. Wetangula amekuwa akijadiliwa sana katika katika kipindi cha wiki nne cha uchunguzi wa kamati hiyo ambayo inamalizia kukamilisha ripoti yake

CCM imeua TRC, asema Lipumba



Anthony Kayanda, Kigoma

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amewaeleza wakazi wa Kigoma kwamba serikali ya CCM imeliua Shirika la Reli (TRC) na sasa wamekaribisha umasikini mkubwa kwa wananchi wa mikoa ya Kigoma na Tabora, na nchi jirani za Burundi na Congo.

Akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mwananchi iliyo Kitongoji cha Mwanga, Prof Lipumba alisema kwa sasa reli ya kati iliyokuwa tegemeo kubwa la usafirishaji wa abiria na bidhaa, imebaki kuwa historia kutokana na uongozi mbovu na ufisadi.

Kigoma inategemea sana usafiri wa reni kwa ajili ya safari za abiria na mizigo kutoka mkoa huo hadi mikoa ya Kanda ya Kati na Mashariki, lakini pia inategemea usafiri wa maji kutokana na kupakana na Ziwa Tanganyika huku mipango ya usafiri wa barabara ikiwa bado haijakamilika.

Prof Lipumba alieleza kuwa katika eneo la mashariki ya Congo kuna watu zaidi ya milioni 40 ambao wana utajiri mkubwa wa madini ya aina mbalimbali, kiasi kwamba wangeweza kutumia reli ya kati na Bandari ya Kigoma kusafirisha bidhaa zao kuingia na kutoka nje ya mkoa.

‘Serikali baada ya kuona TRC imekuwa hoi na inaeleka kuzama waliamua kuwauzia wawekezaji Wahindi waliokuja eti na Kampuni ya TRL kuendesha reli ya kati, lakini kila mmoja ameshihudia inavyozidi kudidimia siku hadi siku na hivyo kusababisha adha kubwa ya usafiri kwa wakazi wa mikoa ya Kigoma na Tabora wanaoitegemea reli hiyo kwa zaidi ya asilimia 95 kusafiria," alieleza Profesa Lipumba.

"Kwa nini Rais (Jakaya) Kikwete ameitelekeza reli yetu? Nipeni mimi urais niiokoe kutoka katika hali hii mbaya kwa sababu kudorora kwake kumesababisha wengi wenu muendelee kuwa masikini kwa sababu sasa hamuwezi kusafirisha bidhaa kuzipeleka katika masoko kama ilivyokuwa siku za nyuma," alisema mgombea huyo wa CUF.

Lipumba, ambaye kitaalamu ni mchumi aliyebobea, alieleza kuwa mwaka 2002 jumla ya tani milioni 1.446 za bidhaa zilisafirishwa na mwaka 2005 tani milioni 1.169 za bidhaa zilisafirishwa kwa kutumia reli hiyo.

Lakini alisema mwaka 2009 kiwango kiliporomoka zaidi na kufikia tani 237,000 za bidhaa zilizosafirishwa, ikiwa ni upungufu mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya shirika hilo kongwe la usafirishaji nchini.

Profesa Lipumba alibainisha kuwa hali imekuwa tete hata katika usafirishaji wa abiria na kwamba mwaka 2001, watu 728,000 walitumia usafiri wa treni na ilipofika mwaka 2005 idadi ilipungua hadi kufikia watu 514,000 na takwimu zinaonyesha mwaka 2009 idadi imeporomoka na kufikia watu 285,000 tu.

"Kuporomoka huku kwa usafiri wa watu na bidhaa kumeathiri sana sekta ya ajira na mapato kwa kuwa hata kiwango cha fedha kinachokusanywa ni kidogo na kinachoshindwa kukidhi uendeshaji wa Kampuni ya TRL ndiyo maana ninaomba muichague CUF ili turekebishe hizi kasoro," alisema Profesa Lipumba

Mgombea Chadema akamatwa akidaiwa kumtukana JK


Tumsifu Sanga

MGOMBEA ubunge wa Temeke kwa tiketi ya Chadema, Dickson Amas Ng’hilly jana alikamatwa na polisi na kuachiwa kwa dhamana.
Ng’hili, mwenye umri wa miaka 33, alikamatwa jana saa 4:00 asubuhi kwa kosa la kutumia lugha matusi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika juzi kwenye viwanja vya Mwembeyanga vilivyo Temeke jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema walimkamata Ng’hili na kumhoji kwa kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete.
Alisema mtuhumiwa alitoa lugha hiyo ilipofika zamu yake ya kujinadi baada ya kuruhusiwa na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa.

“Ilipofika zamu ya kutoa hotuba, Dickson Amos Ng’hili anatuhumiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya mgombea urais Jakaya Kikwete ambayo ni kinyume cha sheria chini ya kifungu namba 89 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 (Penal Code Cap.16 of the Laws)," alisema Kamanda Kova.

Mtuhumiwa ameandika maelezo yake ya utetezi kwa mujibu wa sheria na upelelezi bado unaendelea, alisema Kova.
Kamanda Kova aliongeza kuwa kwa kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, mtuhumiwa ameachiwa huru kwa dhamana ya polisi akisubiri matokeo ya uchunguzi huo.

Hazta hivyo, Kova hakutaka kutaja maneno yaliyotafsiriwa kuwa ni lugha ya matusi dhidi ya Kikwete, akisema kuwa hawezi kuyarudia na kwamba watapeleka mahakamani kutumika kama ushahidi.
Kova alisema mtuhumiwa alihojiwa kwa kufuata taratibu na tukampa uhuru wa kujitetea kwa kuwa naye anaweza kuwa na mashahidi wake na ndio maana tumempa dhamana wakati upelelezi unaendelea

Kanisa halimpigii debe mgombea yeyote-PCT



Exuper Kachenje
BARAZA la Makanisa ya Pentekoste (PCT) limeeleza kuwa hakuna mgombea ambaye anapewa kipaumbele na baraza hilo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili.

Lakini katika tamko lake, PCT imeitaka Tume ya Uchaguzi (Nec) kusimamia kwa haki uchaguzi mkuu na kutoa haki bila kupindisha, likisema kuwa jaribio lolote la kuupindisha ukweli ni hatari kwa amani ya Taifa.

Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari jana, mwenyekiti PCT, Askofu David Batenzi alisema pia kuwa baraza hilo linapinga msimamo wa udini na ukabilia katika kupata kiongozi wa ngazi yoyote.
“PCT inatoa tamko kwa umma wa Watanzania kwamba haina chama au mgombea anayepewa kipaumbele au kupigiwa kampeni ndani ya umoja wake katika uchaguzi mkuu wa 2010,” alisema Batenzi.

Askofu huyo mkuu alifafanua kuwa “PCT inasisitiza Wakristo na Watanzania wote kuchagua kiongozi yoyote mwenye uwezo, mwadilifu na mwenye nia ya kujenga umoja, amani na utulivu wa Watanzania bila kujali itikadi, rangi au imani ya mgombea”.
Katika mkutano huo ambao ulijumuisha viongozi wengine wa kanisa hilo, Askofu Batenzi alisema tamko hilo limetolewa kwa niaba ya makanisa wanachama wote wa PCT na kwamba PCT inaheshimu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanazania.
Alisema: “PCT inaheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , kwamba ni haki ya kila mwananchi kuchagua au kuchaguliwa kwa nafasi yoyote ya uongozi bila kuangalia dini, kabila au rangi yake.”

Kwa mujibu wa askofu huyo, misingi ya uadilifu, ukweli, uzalendo, umoja, amani na utulivu ndiyo kipimo pekee cha kutumiwa na mwananchi katika kujichagulia kiongozi wanayempenda bila kushurutishwa na mtu au kikundi fulani.
Akieleza sababu za tamko hilo, Askofu Batenzi aliwaambia waandishi kuwa PCT inataka kuweka bayana msimamo wake dhidi ya wananchi kuchagua vionghozi kwa misingi ya kidini na kikabila.

Kuhusu Nec, askofu Batenzi alionya kuwa “ni vizuri Tume ya Uchaguzi isimamie kwa haki uchaguzi huo na itoe matokeo kwa haki kwa kadiri yatakavyokuwa kwa kuwa kupindisha matokeo ni hatari kwa amani ya taifa”.
Aliwataka wagombea kuwa tayari kukubali matokeo na kutokuwa chanzo cha uchochezi na vurugu huku akiwataka Watanzania pia kuwa watulivu baada ya upigaji kura na kukubali matokeo kwa faida ya amani iliyopo nchini

Kikwete aahidi neema Mwanza



Frederick Katulanda, Mwanza na Kizitto Noya, Nyang’hwale
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amesema ataipandisha hadhi Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou-Toure kuwa ya rufaa na kuongeza fedha kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando, huku akiahidi kujenga jengo kubwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.

Alisema tayari hospitali hiyo imeshafanyiwa marekebisho ikiwa ni pamoja na kujengewa wodi maalum ya magonjwa ya akili, kuongezwa wodi ya akinamama na maabara kama sehemu ya mkakati huo wa kuboresha huduma ya afya.

Akizungumza jijini Mwanza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Sahara Jimbo la Nyamagana jijini Mwanza, Kikwete alisema hospitali hiyo imeboreshwa kwa lengo la kutoa huduma bora na kuifanya ifikie ngazi ya rufaa.

“Tayari tumeshaweka vifaa vya kisasa na maabara; tunataka ndiyo iwe ya rufaa na ile ya rufaa ya Bugando tutaifanya kuwa ya rufaa maalum,” alisema Kikwete na kubainisha kuwa katika mpango huo tayari serikali imepanga kutoa Sh8 bilioni kwa ajili ya kuiwezesha Bugando kununulia vifaa maalum vya upimaji.

Kikwete alisema iwapo CCM itachaguliwa tena, mpango wao ni kujenga kituo cha Machinga Complex pamoja na soko kubwa la kisasa jijini Mwanza na soko la zamani libaki kama historia na kubeza ahadi za upinzani akidai kuwa zinatolewa na watu ambao hawana hata viwanda.

“Tumefanya mengi... nawaomba msibabaike na ahadi hewa za wapinzani ambazo wanazitoa kuwa watashusha bei ya vitu wakati hata viwanda hawana,” alieleza Kikwete.

Akizungumzia fujo katika kampeni, Kikwete alisema CCM ni waaminifu kwa kuwa waliahidi amani na amani ipo na kusema kuwa ni CCM pekee inayohubiri amani huku akisema wapinzani wamekuwa wakiahidi fujo.

“Wanafanya fujo; wanapiga watu; wanajeruhi watu na sasa wameua... achaneni nao hao kwa kuwa ukiona mtu anafanya fujo, ujue kuwa amekata tamaa. Kama CCM tungekuwa wabaya, tusingeruhusu vyama vingi; tungevinyongea mbali, lakini tumewaruhusu sasa wanafanya fujo. Siasa siyo kupigana mawe ni sera; waje na sera,” alieleza Kikwete.

Kikwete amekuwa akidaiwa kufuja fedha kwa kusafiri nje kila mara, lakini jana alijitetea kuwa safari hizo ndizo ambazo zimeleta mafanikio, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa serikali ya Marekani kusaidia vyandarua.

“Wapo watu wanasema natembea sana; hivi nisingetembea ningempata wapi (rais wa zamani wa Marekani, George) Bush atuletee vyandarua na vitabu kwa ajili ya shule zetu. Tumegawa vyandarua kupitia hati punguzo na sasa tutagawa zaidi kwa lengo la kuhakikisha kila kitanda kinakuwa na chandarua kwa nchi nzima,” alisisitiza Kikwete.

Alisema tatizo la walimu katika sekondari za kata litamalizika kwa kuwa serikali yake imefundisha vijana 14,000 ambao watahitimu mwaka huu na kusambazwa katika shule hizo, akiahidi kuipa kila shule walimu watano.

Alieleza kuwa serikali yake imekuwa tulivu na sikivu na kila inapoahidi imekuwa ikitimiza na akawaomba wananchi kumchagua tena ili aweze kukamilisha aliyoahidi kwao.

Akihutubia mkutano Nyanghwale, Kikwete alieleza kuwa serikali yake inatambua tatizo la umeme katika jimbo hilo na imejipanga kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

Alisema CCM inaomba kura ili ichaguliwe tena kurudi madarakani kwa sababu kadhaa "kubwa ni kwamba CCM ni chama makini, chenye sera nzuri na kinachojali mahitaji ya wananchi wake”.

Pia alisema serikali itajenga barabara ya lami kutoka Geita, Kahama, Nyang’hwale ili kumaliza tatizo la miundombinu ya usafiri katika eneo hilo.

Aliahidi kumaliza tatizo la benki akisema kuwa “tutazungumza na watu wa mabenki kuwaomba waanze kufungua matawi katika jimbo hili”.

“Ninaposema mtuchague, nina maana kuwa mimi kwa nafasi ya urais, Amar kwa nafasi ya ubunge na wagombea wetu wa udiwani,” alisema na kueleza kuwa anaamini Amar ana uwezo mkubwa wa kuliongoza jimbo hilo kwa mafanikio ya kweli.

Awali kabla hajaingia uwanjani, pikipiki takribani 65 zilizopambwa bendera za CCM na baiskeli kadhaa zilikuwa moja ya vivutio katika mkutano uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyang’hwale lililoko Kata ya Karumwa wilayani Geita, Mwanza.

Kikwete aliyefika kwenye uwanja huo majira ya saa 10:30 jioni, alianza kuhutubia baada ya mgombea ubunge, Hussein Nassor Amar kueleza matatizo kadhaa yanayolikabili jimbo hilo.

“Mheshimiwa mwenyekiti wa CCM na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; ujio wako leo ni faraja kubwa kwa wakazi wa jimbo hili ambalo kwa mara ya mwisho rais alifika mwaka 1972,” alisema Amar.

“Jimbo hili lina matatizo mengi, lakini kubwa ni ukosefu wa umeme, maji na miundombinu ya mawasiliano. Pia katika jimbo hili kuna mzunguko mkubwa wa fedha, lakini hakuna benki. Tunaomba utusaidie kupata benki ili kuwapunguzia muda wa kwenda wilayani watumishi wa umma.”

Tuesday, October 26, 2010

Mafuriko makubwa yaikumba Benin


Mafuriko mjini Cotonou


Theluthi mbili ya raia wa Benin wameathirika na janga baya zaidi la mafuriko kuwahi kulikumba taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

Waandishi wa habari katika mji mkuu Cotonou, wanasema takribabn watu hamsini wamekufa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, wengi wao wakiwa ni watoto.

Mwanamuziki maarufu wa Benin Angelique Kidjo ameiambia BBC kuwa hajawahi kushuhudia maafa ya aina hiyo na kutoa wito wa kupatiwa misaada waathiriwa..


Akizungumza mjini New York Kidjo amesema nchi yake inahitaji sana msaada na kuongeza kuwa licha ya wasamaria wema nchini humo wamejitolea kusaidia, msaada unaotolewa hautoshi.

Kipindupindu chaua zaidi ya 250 Haiti


Idadi ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa maradhi ya kipindupindu nchini Haiti imezidi 250.

Zaidi ya watu 3,000 wameambukizwa, alisema Gabriel Thimote, mkurugenzi mkuu wa Idara ya afya wa Haiti.

Watu watano waligundulika kuwa na kipindupindu katika mji mkuu Port-au-Prince, lakini maafisa wa Umoja wa Mataifa alisema wagonjwa waligundulika mapema na kutengwa.

Maafisa wanasema maradhi hayo ni tishio kubwa kwa watu milioni 1.3 waliosalimika tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Januari na ambao wanaishi kwenye mahema katika kambi zilizoko maeneo yanayouzunguka mji huu.

Hali itakuwa mbaya zaidi endapo tutakuwa na maelfu ya watu wakiwa wagonjwa kwa wakati mmoja," alisema rais wa chama cha madaktari wa Haiti, Claude Surena.

Lakini Bw Thimote alielezea matumaini yake kuwa mlipuko huyo utaweza kudhibitiwa.

Mafuriko makubwa yaikumba Benin


Mafuriko mjini Cotonou


Theluthi mbili ya raia wa Benin wameathirika na janga baya zaidi la mafuriko kuwahi kulikumba taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

Waandishi wa habari katika mji mkuu Cotonou, wanasema takribabn watu hamsini wamekufa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, wengi wao wakiwa ni watoto.

Mwanamuziki maarufu wa Benin Angelique Kidjo ameiambia BBC kuwa hajawahi kushuhudia maafa ya aina hiyo na kutoa wito wa kupatiwa misaada waathiriwa..


Akizungumza mjini New York Kidjo amesema nchi yake inahitaji sana msaada na kuongeza kuwa licha ya wasamaria wema nchini humo wamejitolea kusaidia, msaada unaotolewa hautoshi

Meya wa Nairobi mbaroni kwa ufisadi


Jiji la Nairobi




Meya wa mji mkuu wa Kenya-Nairobi ametiwa nguvuni kuhusiana na sakata la ununuzi wa kipande cha ardhi kiliyopangiwa kuwa eneo la makaburi viungani mwa jiji hilo.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumanne kujibu mashtaka ya ufisadi.

Katika sakata hiyo maafisa wa baraza la jiji la Nairobi wanashutumiwa kupanga njama za kufuja takriban dola milioni tatu nukta mbili kwa kisingizio cha kununua kipande cha ardhi chenye ukubwa wa ekari 120 wakati thamani halisi ya hiyo ilikuwa ndogo.

Msemaji wa tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya Nicholas Simani amethibitisha kukamatwa kwa meya huyo Geofrey Majiwa na kukanusha madai kuwa maafisa wake walivamia makaazi yake bila kibali cha mahakama.