KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, October 28, 2010

Nitaboresha kinywaji aina ya gongo- mgombea TLPMGOMBEA wa urais kupitia Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Mutamwega Mgahywa amesema, akipewa ridhaa ya kuongoza nchi atabadilisha uchumi ikiwa ni pamoja na kujenga viwanda vitakavyomilikiwa na watanzania.
Mgombea huyo anayeomba ridhaa k wa wananchi alisema kuwa atafufua viwanda mama vilivyokufa kitambo na kuimarisha uchumi wa watanzania kwa viwanda hivyo.

Hivyo katika mkutano wake alisema hata kinyaji aina ya gongo kitakublika katika uongozi wka kuwa ataboresha kinywaji hiko katik ngazi za kimataifa kwa kuzalishwa kiwandani.

“Gongo itakuwa inazalishwa kiwandani, na si kama inavyofanyika sasa haina ubora ndio mana kinywaji hicho kinapigwa vita, hivyo itaboreshwa kwa kiwango vya hali ya juu” alisema

Hata hivyo baadhi ya wananchi walifurahi na kupiga makofi na kusikia ahadi hiyo ambayo baaadhi huwa wanaendesha uuzaji wa kinywaji hicho kwa shida kwa kuwa kinywaji hicho kinapigwa vita na serikali

Alisema, Tanzania haina viwanda vya uhakika jambo ambalo linachangia umasikini na vichache vilivyopo vinamilikiwa na watu kutoka nje.

No comments:

Post a Comment