KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, June 30, 2010

Kiongozi wa FNL Agathon Rwasa mafichoni

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi ambaye zamani alikuwa kiongozi wa kundi la waasi Agathon Rwasa ,amethibitisha kuwa yuko mafichoni.

Kwenye ujumbe uliorekodiwa na kutumwa kwa radio moja nchini humo, Bw Rwasa amesema amejificha kwa kuhofia usalama wake.








Aliondoka nyumbani kwake wiki moja iliyopita kabla ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatatu huku mgombea pekee akiwa Rais wa sasa Pierre Nkurunziza .

Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza kufanyika nchini humo,tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 12.

Wanadiplomasia wameonya kuwa huenda nchi hiyo ikarejea katika hali ya mzozo wa kivita.

Waandishi wa habari wanasema idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo wa urais, ilikuwa ndogo ikilinganishwa na uchaguzi wa mikoa uliofanyika mwezi uliopita.

Wananitafuta kwasababu nilisema ukweli,nilisema wazi kuwa sitakubali matokeo ya uchaguzi wa mikoa, walitaka kunikamata na nilipopata fununu nikaamua kukimbia

Kiongozi wa chama cha FNL Agathon Rwasa

Vyama vitano vya upinzani vilidai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi wa kura, na vikajiondoa katika uchaguzi wa urais.

Bw Rwasa, ambaye alitia saini mkataba wa amani mwaka jana, hakusema yuko wapi lakini inaripotiwa kuwa yuko katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakati alipotoweka kwa mara ya kwanza ,chama chake kilisema alikuwa ''likizoni''.

Bw Rwasa na Rais Nkurunziza ,waliongoza makundi ya waasi wa Kihutu kupigana na jeshi ambalo lilikuwa likiongozwa na Watutsi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.


Bw Rwasa, alikataa kuhusika katika mpango wa kumaliza mapigano baada ya makundi yaliyokuwa yakizozana kuamua kuunda serikali ya muungano na baadaye uchaguzi ukafuata mwaka 2005.

Aliongoza kundi la National Liberation Forces (FNL) kusalimisha silaha mwezi Aprili mwaka 2009, na anaaminika kuwa mshindani mkubwa wa Rais Nkurunziza.

Watu wapatao 300,000 walikufa wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

'Waliompiga risasi' Nyamwasa, mahakamani

Watu wanne wamefikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini wakishtakiwa kwa njama ya kumuua aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini Rwanda Luteni General Kayumba Nyamwasa.

Inafahamika kuwa washukiwa hao wanne waliofikishwa mahakamani ni kutoka Tanzania, Somalia na Msumbiji.

Wote wanakabiliwa na mashataka ya kupanga njama ya mauaji na watafikishwa tena mahakamani Julai 14.

Watu wengine wawili waliokamatwa wakati wa msako mkuu wa polisi waliachiliwa baada ya mashtaka dhidi yao kufutwa.



Jenerali Nyamwasa anaamini serikali ya Rwanda ndiyo iliyohusika na jaribio la kumuua kwa risasi alipokuwa anaelekea nyumbani kwake mjini Johannesburg.

Serikali ya Rwanda inakanusha madai hayo kwa kusema hakuna sababu yoyote ya kumuua.

Tuesday, June 29, 2010

Aliyekutwa na binti wa mwenye nyumba ahamishwa kinguvu


KIJANA aliyekutwa baa akiwa katika jaribio la kumrubuni mtoto wa mwenye nyumba kimapenzi atakiwa kuhama katika nyumba hiyo bila kupenda siku iliyofuata.

Kutokana na hasira walizokuwa nazo wazazi wa binti huyo walimtaka kijana huyo kuhama ndani humo bila kupenda ili kuepusha ugomvi kati yao.

Bila kuamini anachosikia masikioni kwake kwa wazazi hao usiku huo aliporudi siku ya pili yake baada ya kukutwa na binti huyo maeneo ya Sinza.

Asubuhi yake mama wa binti huyo alimtahadharisha kijana huyo kuwa kutokana na hasira alizokuwa nazo baba wa mtoto huyo alimwambia kwa tahadhari anatakiwa ahame ndani humo ili kusiwe na migongano ya hapa na pale.

Hivyo kijana huyo aliwataka wenye hao amrudishie hela ya kodi iliyobaki ili aeze kutafitia chumba mahali kwingine.

Chanzo cha habari hii kilisema kuwa kwa kua alibakiza miezi miwili kti yam aka mmoj aliopanga humo waliweza kumrudishwia pesa hizo ili aweze kuondoka ndani humo kwa kuamini kuwa angeendelea kubaki ndani humo binti huyo angeweza kudanganyika tena mbali na kipigo alichopewa.

Hivyo kijana huyo alilazimika kutafuta gari na kuhamisha vyombo na kuondoka kwenye nyumba hiyo.

Waliojitokeza kumuomba mtoto wakataliwa na uongozi wa hospitali


MWANAUME mmoja amejitokeza hospitali ya Amana iliyopo Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam kutaka apewe mtoto anayetunzwa hapo kwa kujitambulisha ni mzazi wa mtoto huyo na hakufanikiwa kupewa hadi kupatikane kwa uthibitisho wa kina
Mwanaume huyo amejitokeza hospitalini hapo jana asubuhi, akiongozana na watu wengine huku akijitambulisha kuwa ni baba wa mtoto huyo.

Mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Alphonce, mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatunzwa hospitalini hapo baada ya mama yake kufariki ghafla punde tu alipofikishwa hospitalini hapo akitokea katika kituo cha Afya cha Jeshi la Ulinzi Gongolamboto.

Mama wa mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Mikaela Mikael, alikufa siku kumi zilizopita na mtoto huyo kubaki hapo bila ndugu wa aina yoyote kujitokeza na hadi jana siku ya 11 baba huyo kujitokeza na kudai kuwa ni mtoto wake.

Hivyo walipofika na kuona uongozi husika hawakuruhusiwa kuchukua mtoto huyo na kutakiwa kurudi leo ili kuthibitisha uhalali wa undugu huo.

Wauguzi walisema kuwa mama huyo alipofikishwa hapo walipompima waligundua kuwa alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na baadae walianza kumuona mama huyo akizungumza maneno yasiyofahamika na kuanza kumtundukia madripu kumuongezea nguvu na alfajiri aliaga dunia.

Mwanaume huyo alijitokeza hospitalini hapo siku ya kumi na moja baada ya kuona taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari na kutaka apewe mwili wa marehemu na mtoto huyo.

Alipohojiwa na vyombo vya habari kuhusiana na tukio hilo alisema alikuwa anafahamu ugonjwa uliokuwa unamsumbua mwanamke huyo ni nguvu za giza na hakuwa na taarifa kama alifikishwa hospitalini kwa kuwa jirani yake alimchukua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji.

Hivyo alishtuka kuona taarifa hizo kwenye vyombo vya habari baada ya mwanamke huyo kutoonekana kwa ndugu zake kuuchukua mwili wa marehemu na mtoto huyo akiwa anatunzwa wodini.

Maonyesho ya Sabasaba kuanza leo


MAONYESHO ya 34 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam yanaanza leo rasmi na wananchi kutakiwa kutembelea maonyesho hayo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, amewataka wananchi kuhudhuria maonyesho ya 34 ya Biashara ya Kimataifa yanayoanza rasmi leo.

Lukuvi alitoa wito huo jana katika viwanja vya maonyesho hayo, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya maonyesho hayo.

Maonysho ya mwaka huu yatakuwa na mabadiliko kwa kuwa yameandaliwa kwa ustadi mkubwa na kwa umakini zaidi.

Maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi na Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva.

Katika maonyesho hayo ya kibiashara ya kimataifa yanawapa fursa wanacnhi mbalimbali kujifunza mambo mbalimbali ya kitaifa ikiwemo na kununua bidhaabmalimbali zinazofika katika maonyesho hayo

Nifahamishe juzi,ilishuhudia mabanda mbalimbali yakiwa tayari kwa maonyesho hayo na mengine yakiwa katika hatua za mwisho ya maandalizi

Matatani kwa jaribio la kumrubuni mwanafunzi


KIJANA mmoja [jina tunalo] amejikuta akipewa notisi kwenye nyumba aliyokuwa amepanga baada ya kukutwa akiwa katika jaribio la kumrubuni mtoto wa mwenye nyumba aliyokuwa amepanga huko Manzese jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo alikutwa na binti huyo wa miaka 15 anayesoma kidato cha kwanza akiwa amekaa nae baa katika jaribio la kumrubuni mwanafunzi huyo.

Bila kutambua lolote mjomba wa binti huyo alimuona kijana huyo akiwa anaingia nae baa huko maeneo ya Sinza Mori na kuanza kufanya nae mazungumzo ya hapa na pale huku mjomba huyo akiwa katika kona moja nzuri akiwaangalia wawili hao.

Kwa kuwa mjomba huyo nae alikuwa na machungu ya kutaka mpwa wake huyo apate elimu alipatwa na hasira za ghafla za kutaka amvamie binti huyo lakini wawili aliokuwa amekaa nao mahali hapo walimpoza na kumuamuru amuangalie kwanza.

Kijana huyo bila kutambua lolote alimuagizia chakula binti huyo na huku yeye akiendelea na kinywaji na kisha kuendelea na mazungumzo ya hapa na pale na binti huyo.

Mjomba huyo uzalendo ukamshinda aliinuka na kwenda kwenye meza waliyokuwa wamekaa wawili hao na kumshika binti yake na kumuuliza alikuwa akifanya nini mahali hapo?

Binti huyo alianza kuangua kilio mahali hapo kabla hajaanza kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na kumuomba radhi mjomba wake huyo.

Mjomba huyo alikodi usafiri aina ya tax na kwenda nae hadi nyumbani kwa dada yake na kuanza kumuuliza alikuwa akifanya mazungumzo yepi na kijana huyo.

Ndipo binti huyo alipowaeleza ukweli kuwa alikuwa akimwambia kuwa anamuhitaji katika maisha na alimueleza kuwa amalize masomo ili amuoe.

Kabla hajamaliza maelezo yake mama yake alianza kumpa kichapo cha nguvu huku akisaidiwa na kaka yake huyo kwa kukubali kwenda nae baa huku akijua yeye ni mwanafunzi.

Hivyo wazazi hao walikerwa na kitendo cha kijana huyo kutaka kumuaribia masomo binti yao walimsubiri kijana huyo arudi nyumbani kwao hapo na bila mafanikio siku hiyo kijana huyo hakurudi kwa kuwa aliona hali ya hewa ilishaaribika.

Siku ya pili majira ya usiku wa saa tano kijana huyo alirudi nyumbani kwake hapo na alipoonekana walimdaka na kumpeleka kituoni ili akatoe maelezo na kupewa notisi hiyo huko.

Mtoto afia ndani wakati mama yake amekwenda kununua chips


MTOTO wa kike wa miaka minne amefariki dunia kwa kuzidiwa na moshi na moto uliosababishwa na mshumaa wakati mama yake alipotoka kwenda kunumnua chips na kumfungia mtoto huyo ndani.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea siku mbili zilizopita huko maeneo ya Vingunguti kwa Simba jijini Dar es Salaam majira ya usiku.

Ilidaiwa na mashuhuda wa tukio hilo kuwa, mama huyo alikuwa akiongea na wapangaji wenzake nje ya nyumba hiyo na hatimaye waliachana ilipofika saa 4 na kila mmoja aliingia ndani kwake kwa ajili ya kulala.

Walidai kuwa mama huyo bila kuwataarifu wenzake mtoto wake alipolala alimlaza na kumfungia ndani na kisha yeye kutoka bila kuwataarifu wenzake.

Kwa kuwa nyumba yao hiyo haina umeme walikuwa wakitumia mishumaa na taa nyingine za ziada, ndipo mama huyo alipoamua kuwasha mshumaa na kuuweka mezani na kisha kufunga mlango kwa kuwa mwanae alilala na yeye kutoka kwenda kununua chips bila kutoa taarifa kwa wenzake.

Hivyo haikufahamika mara moja kama mshumaa huo uliangushwa na panya, ama upepo, hivyo uliweza kuanguka na kuunguza vitu vya ndani humo kidogokidogo na mtoto huyo kuanza kuathirika na moshi uliozagaa ndani humo na hakuweza kujisaidia kwa kuwa mlango ulifungwa na alipopiga kelele watu hawakumsikia kwa kuwa walikuwa walishaanza kulala.

Ilidaiwa kuwa wanaume waliokuwa katika banda la nje waliokuwa wakiangalia mpira waliona moshi ukitoka ndani humo na kwenda kuwaamsha wenye nyumba na kuwaambia nyumba inaungua ndipo walipogundua na kuamka na kuanza kumwita mama huyo bila ya jibu lolote kutoka chumbani humo.

BIla kutambua kama mtoto alikuwa ndani humo watu hao walifanya juhudi za hapa na pale kuzima moto na baadae walipoingia ndani walimkuta mtoto huyo yupo katika hali mbaya na kumkibmiza hospitalini.

Ndani ya chumba hicho hakuna kitu ambacho kilipona viliteketea kwa moto vyote.

Wakati watu wakiwa katika hatua za mwisho za uzimaji moto na mtoto ameshakimbizwa hospitalini mama huyo ndipo alipokuwa akirudi akiwa na chips zake mkononi na kukuta hali hiyo na ghafla alipoteza fahamu papohapo.

Mtoto huyo aliweza kupoteza maisha dakika chache wakati amefishwa hospitali

Wakamatwa na kilo 31 za Cocaine


RAIA wawili wa kigeni wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine wakiwa wameweka kwenye makasha maalum ya kimataifa yenye nembo ya ubalozi.

Watuhumiwa hao ni Diaka Kaba (52) raia wa Guinea na Abubakar Ndijane (50), raia wa Liberia, walikuwa wamehifadhi dawa hizo mabazo wakaguzi hawakugundua mapema na hata mashine zisingeaini uihaliofu huo.

Mkuu wa Kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa alisema watuhumiwa hao walikamatwa Juni 23 majira ya saa 1.30 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema watuhumiwa hao walitumia ujanja wa kupaka kahawa mifuko hiyo na hata mbwa wanaotumika kukagua mizigo uanjani hapo hawakugundua waliponusa na kutokana na karatasi hizo walizotumia kufunga hazikuonyesha kwenye mashine ya ugunduzi.

Alisema katika ukaguzi wa kina katika mabegi yao waliwapekua na kuwakuta na pakiti zenye kilo 31 za dawa za Cocaine ambazo walipaki kwenye mifuko na kuweka nembo ya ubalozi wa Guinea na mihuri mbalimbali.

Alisema walipofanya mawasiliano na ubalozi husika kama wanahusika na watu hao walidai hawawatambui na kuwa chini ya ulinzi wa polisi.

Nzowa alisema katika mahojiano ya kina na kibano watuhumiwa hao walipohojiwa walibainisha kuwa walianza safari yao nchini Trinidad and Tobago kupitia Panama, Brazil na Johanesburg Afrika Kusini na hatimaye kuingia nchini Tanzania.

Wanaowania kiti cha urais Zanzibar wafika 10


MBALI ya saba waliotangaza nia kwa muda mrefu na kuchukua fomu visiwani Zanzibar kuwania kiti cha uraisi wengine watatu wamejitokeza kuwania kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi [CCM]
Walioanza kuchukua fomu hiyo juzi makao makuu ya chama hicho zilizopo Kisiwandui ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Balozi Ali Abeid Karume, Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna.

Wengine ni Hamadi Bakari Mshindo, Waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohammed Gharib Billal na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud.

Wengine watatu waliotangaza nia na kupangiwa kuchukua fomu hizo kesho ni pamoja na Mohammed Raza, aliyewahi kuwa mshauri wa Michezo wa Rais wa Awamu ya Tano wa Zanzibar.

Wengine ni Waziri wa Elimu Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman na Mohammed Yusuph, ambaye wadhifa wake haufafanuliwa.

Wanachama hao kila mmoja anatakiwa kutafuta wadhamini 250 katika mikoa mitatu ya Zanzibar na kati ya mikoa hiyo mmoja lazima uwe wa Pemba na watatakiwa kurudisha fomu hizo Julai mosi mwaka huu.

Ndugu wawili wa familia moja wajinyonga


VIJANA wawili ndugu wa familia moja wamejinyonga kwa nyakati tofauti kwa sababu ambayo bado haijafahamika mara moja
Ndugu hao ni Joachim Luciani (27) na Dominic Lucian [33] walijinyonga kati ya Juni 17 na 19 mwaka huu ambao walikuwa wakazi wa Kata ya Kaloleni, Moshi.

Aliyeanza kujinyonga ni Joachim kwa sababu ambayo bado haijafahamika na ndugu yake huyo alishiriki katika zoezi la uchimbaji kaburi na kuwaaga wengine kuwa alikuwa anakwenda kunywa maji kwa kuwa alikuwa na kiu.

Wakati wa maziko ya mdogo wake Dominic hakuonekana makaburini na watu kudhani labda ni uchungu aliokuwa nao amekaa mahali na watu wengine kuendelea na mazishi.

Ilidaiwa hadi mazishi hayo yanamalizika ndugu huyo hakuonekana kuja kumzika mdogo wake, na kesho yake alionekana akining’inia kwenye mti katika msitu wa Njoro akiwa amejinyonga na kuinua msiba mpya wa waombolezaji waliokuwa katika matanga ya ndugu yake.

Mwili huo ulikuja kuchukuliwa na polisi mkoani humo na umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi na uchunguzi wa kina unaendelea kuhusiana tukio hilo.

Mwaupulo aahidi kuteketeza changamoto zinazoikabili jimbo la Kawe


KIJANA Undule Hezron Mwampulo[34] ametangaza nia ya kugombea kiti cha Ubunge katika jimbo la Kawe kwa tiketi ya [CCM] ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazoikabili jimbo hilo kwa muda mrefu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, jijini Dar es Salaam, Mwampulo amesema amejitokeza kuwania kiti hicho ili kukabiliana na matatizo sugu ya jimbo hilo.

Amesema lengo lililomvutia kuwania kiti hicho ni kuguswa na matatizo ya muda mrefu yasiyotekelezeka yakiwemoya huduma za afya, maji, elimu.

Amesema kubwa ya yote ni kutaka kumaliza matatizo ya ardhi yanayoikabili jimbo hilo na kuahidi matatizo hayo atayatatua.

MBali na hilo amesema wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakilalamikia ana matatizo ya usafiri, pia miundombinu mibovu hjaa katika kata ya Msasani.

Hivyo amesema kutokana na kero hizo zilizodumu kwa muda mrefu atahakikisha atamaliza matatizo hayo kwa kutumia uzoefu wake wa kielimu kumaliza matatizo ya jimbo hilo.

Mwampulo amesema ametangaza nia hiyo kutokana na kuvutiwa na wito wa Rais Kikwete ya kuwataka vijana warudi nyumbani kuendeleza nchi yao.

Mwampulo ameitikia wito huo wa rais na amerudi nyumbani akitokea nchini Uingereza alipokuwa akiendesha shughuli zake na kupata degree mbalimbali akiwa nchini humo.

Aliyemuua Mtanzania Baada ya Kutukanwa Kwenye Facebook Jela Miaka 14


Kijana wa Kiingereza ambaye alimuua kijana wa Kitanzania aliyekuwa akiishi nchini Uingereza baada ya kukasirishwa na maoni yake mabaya kwenye Facebook, amehukumiwa kwenda jela miaka 14.
Kijana huyo wa Kiingereza ambaye wakati wa tukio mwezi disemba mwaka jana alikuwa na umri wa miaka 15, alimuua kwa kumchoma na kisu kifuani kijana wa Kitanzania Salum Kombo aliyekuwa na umri wa miaka 18 ambaye alikuwa akiishi na kusoma nchini Uingereza.

Kijana huyo wa Kiingereza ambaye jina lake halikutajwa kutokana na umri wake mdogo amehukumiwa jana jijini London kutumikia kifungo jela zaidi ya miaka 14.

Kijana huyo alikuwa ni rafiki wa karibu wa Salum na chanzo cha mauaji hayo ni maoni mabaya aliyoandika Salum kwenye Facebook kuhusiana na rafiki yake huyo.

Inasemekana kwamba rafiki huyo wa Salum aliandika maoni kwenye ukurasa wake wa Facebook akionyesha hasira zake kwa kutoalikwa katika party iliyoandaliwa na rafiki zake.

Salum alijibu maoni hayo kwa kuandika maoni ya kumkashifu rafiki yake huyo ambaye kutokana na kukasirishwa kwake alitishia kumuua lakini hakuna mtu aliyetilia maanani vitisho hivyo.

Salum aliuliwa kwenye uwanja wa mpira wa kikapu karibu na nyumbani kwao. Alijaribu kujikongoja kuelekea kwao huku damu kibao zikimtiririka lakini hakufika mbali na alifariki dakika chache baadae wakati akipewa huduma ya kwanza kwenye eneo la tukio hilo.

Akijitetea mahakamani kijana huyo alisema kuwa alimshambulia Salum katika kujilinda asidhuriwe na Salum lakini hakimu aliutupilia mbali utetezi wake.

Akitoa hukumu jaji Nicholas Loraine-Smith aliamuru kijana huyo atumikie miaka 14 jela kabla ya kufikiriwa kupewa msamaha au kutolewa jela.

Salum alikuwa akisomea Sanaa kwenye chuo cha Tower Hamlets College jijini London na aliwasili Uingereza miaka saba iliyopita na alikuwa akiishi na shangazi yake jijini London

JK aja na Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi


RAIS Jakaya Kikwete jana wakati alipokwenda kuchukua fomu ya kuwania urais alikuja na kauli mbiu mpya ya kutetea nafasi hiyo iliyosema Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi hii ni katika kuboresha kauli mbiu ilioyopita ktka kutimiza ahadi zake kwa w
Rais Kikwete alisema pindi atakapochukua kiti hicho ataboresha zaidi na ameshaweka vipaumbele kumi muhimu ikiwemo kuongeza kasi ya mapambano ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Alisema vipaumbele vingine ni kuongeza jitihada na mipango zaidi ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa wa hali ya chini zaidi ili waweze kushiriki na kunufaika na uchumi unaokua.

Vipaumbele vingine atahakikisha serikali ijayo itaongeza jitihada za kupanua wigo na kuboresha huduma muhimu za kijamii hasa afya na maji mbazo zimeonekana ni kero kubwa kwa wananchi walio wengi.

Pia alisema atahakikisha huduma za umeme, miundombinu na mawasiliano zitaboreshwa zaidi.

Rais Kikwete aliyasema hayo mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisini ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Bw. Yusuf Makamba aliongozana na familia yake na wadhamini wake mjini Dodoma.

Pia Kikwete alitimiza na kulipia shilingi millioni moja kama ada ya kuchukulia fomu na kuonyesha wananchi risiti waliohudhuria hafla hiyo

Waziri Mkuu wa Kenya afanyiwa upasuaji


Daktari wa Waziri Mkuu Raila Odinga, Oluoch Olunya, amethibitisha kuwa Odinga amefanyiwa upasuaji katika ubongo wake baada ya kubainika kuwa kulikuwepo na shinikizo kubwa katika kichwa chake.

Daktari Olunya aliyekuwa akihutubia waandishi wa habari kuhusiana na kulazwa kwa Waziri Mkuu katika hospitali ya Nairobi, amesema kwamba Waziri Mkuu aliwaambia kuwa aligonga kichwa chake kwenye gari lake majuma matatu yaliyopita.

Mtaalamu huyo wa upasuaji wa ubongo amesema kuwa Odinga anaendelea kupata nafuu na kwamba ameweza kukaa kwa urahisi katika chumba chake hospitalini.

Muuguzi huyo pia amesema Raila ana uchovu mwingi mwilini na anahitaji kulazwa kwa siku tano zijazo.

Awali taarifa kutoka kwa ofisi yake ilidai kwamba alikuwa na uchovu tu.

Bwana Odinga alipelekwa hospitalini Jumatatu mchana baada ya kushiriki mkutano wa kisiasa na madaktari wake waliamuru apumzike hospitalini.

Hadi sasa Raila Odinga mwenye umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mkakamavu.

Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya kiafya.

Taarifa ya kupasualiwa kwake imewashangaza wengi.

Hadi sasa , maswali mengi kuhusu afya ya kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa rais Mwai kibaki.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi. Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya

Waziri Mkuu wa Kenya alazwa hospitalini


Hadi sasa Raila Odinga mwenye umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mwenye nguvu.

Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya kimwili.

Kwa hiyo taarifa iliyotolewa hii leo na msemaji wake imewashangaza wengi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo madaktari wameamuru Odinga alazwe hospitalini kwa muda wakisema tu kwamba ana uchovu. Cha kukanganya ni kwamba taarifa hiyo iliwanukuu madaktari hao pia wakisema Odinga ana uwezo wa kufanya kazi kama kawaida ikiwa atajisikia kufanya hivyo. Japo hawatamruhusu kufanya hivyo.

Hadi sasa, maswali mengi kuhusu afya ya kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa Rais Mwai kibaki ambaye baada ya uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi.

Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya.

Luanda, Angola mji ghali zaidi duniani


Utafiti wa kimataifa umebaini kuwa Luanda,mji mkuu wa Aangola ndiyo mji wenye gharama ya juu kwa wataalamu wanaotoka nje na kwenda kufanya kazi huko.

Ripoti iliyonadiwa na kampuni ya masuala ya kifedha ya - Mecer imesema gharama za kupanga nyumba mjini Luanda ni mara dufu ikilinganishwa na jiji la London.

Mji wa Luanda umetajwa kuwa ghali zaidi, ukifuatwa na Tokyo, Ndjamena na Moscow. Bara Afrika lina miji mitatu miongoni mwa miji kumi ambayo ni ghali duniani.

Jiji la Libreville, Gabon likishikilia nafasi ya saba. Uchunguzi ulifanyiwa katika miji 214 katika mabaraza yote matano. Mambo yaliyoangaziwa ni pamoja na gharama za maisha ikiwemo usafiri, chakula, mavazi na starehe.

Tiketi moja ya kutazama filamu mjini Luanda inauzwa dola 13.

Licha ya raia wengi wa Angola na Gabon kuishi katika lindi la umasikini, hali ni tofauti kwa wageni ambapo gharama za maisha miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni za mafuta zinaambatana na usalama wao pamoja na ada ya kuagiza bidhaa kutoka nchi zao.

Gharama za juu zimawalazimu wenyeji wengi kuondoka mijini kwani hawawezi kukimu maisha.

Milipuko Burundi wakati wa kuhesabiwa kura za urais


Hali ya wasiwasi imetanda mjini Bujumbura,Burundi baada ya mabomu ya guruneti kulipuka katika eneo moja lenye watu wengi jana usiku.

Hakuna aliyekufa kwenye tukio hilo lililotokea wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais inaendelea katika sehemu zengine nchini humo.

Kumekuwa na matukio ya mashambulio ya maguruneti katika siku za hivi karibuni.

Wakati huo huo vyama vya upinzani nchini Burundi vimesema kwamba havitatambua matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu wa jana ambapo rais Pierre Nkurunziza alikuwa mgombea wa pekee.

Wapinzani wa rais Nkurunziza walijiondoa mchuano wa urais wakidai udanganyifu kwenye uchaguzi wa mabaraza.

Muungano wa vyama 12 vya upinzani umesema ni asili mia 30 pekee ya wapiga kura waliojitokeza kwenye zoezi la jana na kuapongeza raia waliosusia uchaguzi huo.

Uchaguzi wa jana ndiyo wa kwanza tangu kundi la mwisho la waasi kujiunga na mpango wa amani na kuitikia kushiriki katika mchakato wa kisiasa

Watu 10 Wakamatwa Marekani kwa kuipelelezea Urusi


Watu kumi wamekamatwa nchini Marekani kwa kushukiwa kuwa majasusi wa Urusi.Watu hao walikamatwa kwenye msako uliofanyika katika miji ya NewYork, Boston, New Jersey na Virginia. Mshukiwa mwingine angali anasakwa.

Idara ya Sheria ya Marekani imetoa stakabadhi kudhibitisha kuwa watu iliowazuilia wamekuwa wakikusanya habari za kijasusi a kuzipokeza kwa serikali ya Urusi.

Idara hiyo inasema baada ya uchunguzi wa muda mrefu imewanasa watu hao wakiwemo wanaume wanne na wake zao ambao wamekuwa wakifanya kazi kichichini ili kupata habari muhimu kutoka kwa ofisi za serikali na idara zingine muhimu.

Maafisa hao wa marekani pia wanasema washukiwa hao wamekuwa wakiwasajili watu wengine kwa kazi hiyo ya kijasusi. Mmoja wao anadai kuwa alikuwa ametumwa kuchunguza hasa jinsi serikali ya Rais Obama inavyoiona Urusi kabla ya rais huyo wa Marekani kuzuru urusi.

Habari hizi zimeitia serikali ya Marekani wasiwasi hasa kwa sababu rais Obama amekuwa akijaribu kuoberesha uhusiano wa serikali hiyo na Urusi.

Matukio haya yanarudisha kumbukumbu ya vita baridi kati ya mataifa hayo ambavyo vilidumu kwa zaidi ya miongo mitatu.

Katika miaka ya 60 hadi ile ya 80 karibu ulimwengu mzima ulijipata umenaswa katika vita hivyo baridi na matai. Mataifa hayo mawili yalikuwa yanang'aninia kuwa na ushawishi na hata udhibiti wa karibu mataifa yote duniani.

Na ili kufanikisha kampeni zao serikali ya Marekani na ile ya muungano wa Usovieti ziliwaweka majasusi karibu kote duniani. Na sasa takriban miaka 20 tangu vita hivyo kukoma mbinu hizo hizo bado zinaendelea kutumiwa.

Uingereza kupunguza idadi ya wahamiaji


Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza, kwa mara ya kwanza imeweka kikwazo kuhusu idadi ya wahamiaji kutoka nje ya Umoja wa Ulaya watakaoruhusiwa kuingia nchini humo.

Waziri wa mambo ya ndani,Theresa May amesema hatua hiyo ni katika juhudi za kupunguza idadi ya wahamiaji hadi itakapofikia jinsi ilivyokuwa miaka ya tisini.

Ni wafanyikazi elfu ishirini na nne pekee kutoka nje ya Umoja wa Ulaya watakaoruhusiwa kuingia nchini Uingereza kati ya sasa na mwezi Aprili, mwaka ujao ambapo serikali inapanga kuanzisha sheria mpya ya kudhibiti wahamiaji.

Serikali bado haijasema sheria hiyo mpya inalenga kupunguza idadi ya wahamiji kwa kiwango gani.

Idadi ya wahamiaji nchini Uingereza imeripotiwa kuongezeka kwa kasi zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Hatahivyo,hatua ya serikali ya Uingereza kupunguza idadi ya wahamiaji haijashabikiwa na viongozi wa kibiashara na kisiasa, ambao wameikosoa vikali, wakisema itaathiri uchumi wa nchi na haitachangia kwa njia yoyote katika kupunguza wahamiaji haramu.

Wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni,kura ya maoni ilionyesha kuwa uhamiaji na uchumi ndiyo yalikuwa maswala muhimu zaidi kwa wapigaji kura, huku wengi wao wakilalamika kuwa idadi ya wahamiaji imeongezeka sana.

Mauaji ya Rugambage washukiwa wakamatwa


Watu wawili wamekamatwa na polisi nchini Rwanda kwa shutma za mauaji ya mwandishi wa habari wiki iliyopita. Polisi wanasema lilikuwa shambulizi la kulipiza kisasi.

Watu walioshuhudia wanasema Jean Leonard Rugambage, ambaye alikuwa mhariri wa gazeti za Umuvugizi ,alipigwa risasi na watu wawili na kisha wakaingia ndani ya gari na kukimbia.

Serikali ya Rwanda imesema madai kuwa ilihusika katika mauaji hayo hayana msingi.

Taarifa ya polisi inasema mmoja wa washukiwa ni kutoka familia ya mtu ambaye aliuawa na Bw Rugambage wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Rugambage, aliondolewa mashtaka ya kuhusika katika mauji hayo na mahakama ya Gacaca mwaka 2006.

Mashirika ya kutetea haki za bianadam yamemshtumu Rais Paul Kagame kwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na upinzani ,kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Agosti.

Hivi karibuni serikali ilisimamisha gazeti la Umuvugizi na likalazimika kuchapisha habari kwenye tovuti pekee. Aliyekuwa mhariri Jean Bosco Gasasira, ambaye alikimbilia Uganda mwezi Aprili amesema serikali ilihusika katika mauaji ya Rugambage ambaye alikufa akiwa hospitalini baada ya kupigwa risasi.

"Nina uhakika idara ya usalama wa kitaifa ndiyo ilimpiga risasi,'' amelimbia shirika la habari la Marekani VOA.

Bw Gasasira, amesema mauaji hayo yalifanywa baada ya taarifa iliyochapishwa katika gazeti la Umuvugizi kuhusu jaribio la mauaji dhidi ya aliyekuwa mkuu wa jeshi Generali Faustin Kayumba Nyamwasa nchini Afrika Kusini.

Lakini waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amekanusha madai hayo.

''Kwa hakika sio ya kweli na hayana msingi,''ameliambia shirika la habari la AFP.

Serikali pia imekanusha shutma za kuhusika katika shambulizi shidi ya Generali Nyamwasa.

Alihamia Afrika Kusini mapema mwaka huu baada ya kutofautiana na Rais Kagame

Blatter aomba radhi kwa makosa ya waamuzi


Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter ameomba msamaha kwa ajili ya makosa yaliyofanywa na waamuzi kwenye Kombe la Dunia, ambapo bao llilofungwa na Frank Lampard wa England dhidi ya Ujerumani lilikataliwa, na pia kukubaliwa kwa bao la kuotea lililofungwa na Carloz Tevez wa Argentina dhidi ya Mexico.

Bwana Blatter amesema mdahalo kuhusu haja ya kutumia teknolojia kubaini iwapo mpira umevuka mstari wa goli au la utaanzishwa upya kwenye mkutano wa bodi ya kimataifa ya vyama vya soka utakaofanyika mwezi Julai.

Mkutano wa bodi hiyo uliofanyika mwezi Machi uliamua kukataa kutumika kwa teknolojia hiyo kwenye Kombe la Dunia, kwa tetesi kwamba kusimamisha mechi kwa ajili kuthibitisha kwenye video ikiwa mpira umevuka mstari au la kutaathiri mtiririko wa mchezo na pia kuzinyima timu fursa ya kufunga.

Mjadala kuhusu haja ya kutumika kwa teknolojia hiyo uliibuka tena siku ya Jumapili wakati Ujerumani ilipoifunga England mabao 4-1 mjini Bloemfontein na kuiondoa kwenye mashindano.

Kwenye mechi hiyo, mwamuzi kutoka Uruguay Jorge Larriando na msaidizi wake walikataa kutambua kwamba mpira uliopigwa na Frank Lampard katika dakika ya 38 ulivuka mstari wa lango la Ujerumani na kuingia kabla ya mlinda mlango kuuondosha.

Bao hilo lingeiwezesha England kusawazisha kabla ya mapumziko.

Baadaye siku hiyo katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg kulitokea utata mwingine kwenye mechi kati ya Argentina na Mexico.

Mwamuzi aliruhusu bao la kwanza la Argentina lililofungwa na Carlos Tevez akionekana kuwa ameotea.

Kulitokea mabishano makali uwanjani wakati wa mapumziko baada ya tukio hilo kuonyeshwa tena kwenye skrini kubwa ndani ya uwanja.

Blatter amesema amezungumza na vyama vya soka vya England na Mexico na kuomba msamaha.

Robo fainali ya kukata na shoka

Robo fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini itakutanisha mabingwa mara tano Brazil na Uholanzi siku ya Ijumaa mjini Port Elizabeth, baada ya timu hizo kufuzu kufuatia ushindi wa Jumatatu.

Brazil iliendelea kudhihirisha azma yake ya kulitwaa kombe hilo kwa mara ya sita ilipowafunga Chile mabao 3-0 katika uwanja wa Ellis Park mjini Johannesburg.

Awali katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, Arjen Robben na Wesley Sneider walifunga mabao yaliyoiwezesha Uholanzi kuishinda Slovakia 2-1 na hivyo kujiandikishia nafasi miongoni mwa nane bora.

Mabao ya Brazil dhidi ya Chile yalipatikana kupitia mlinzi Juan aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 38, kabla ya Luis Fabiano kuongeza la pili dakika 4 baadaye.

Robinho alifunga bao la tatu na la ushindi kwa Brazil katika dakika ya 59 kufuatia pasi kutoka Ramires.
Wesley Sneijder

Wesley Sneijder

Robo fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini itakutanisha mabingwa mara tano Brazil na Uholanzi siku ya Ijumaa mjini Port Elizabeth, baada ya timu hizo kufuzu kufuatia ushindi wa Jumatatu.

Brazil iliendelea kudhihirisha azma yake ya kulitwaa kombe hilo kwa mara ya sita ilipowafunga Chile mabao 3-0 katika uwanja wa Ellis Park mjini Johannesburg.

Awali katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, Arjen Robben na Wesley Sneider walifunga mabao yaliyoiwezesha Uholanzi kuishinda Slovakia 2-1 na hivyo kujiandikishia nafasi miongoni mwa nane bora.

Mabao ya Brazil dhidi ya Chile yalipatikana kupitia mlinzi Juan aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 38, kabla ya Luis Fabiano kuongeza la pili dakika 4 baadaye.

Robinho alifunga bao la tatu na la ushindi kwa Brazil katika dakika ya 59 kufuatia pasi kutoka Ramires.
Wesley Sneijder

Wesley Sneijder

Uholanzi walionekana kuelekea kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Slovakia hadi muda wa ziada, wakati mlinda mlango Maarten Stekelenburg alipomwangusha Martin Jakubo kwenye eneo la hatari, na hivyo Slovakia wakapata penalti iliyofungwa na Robert Vittek.

Uholanzi haijapata kushinda Kombe la Dunia na imeshafikia hatua ya fainali mwaka 74 na 78, na wakati huu wanajitahidi kutimiza hamu ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Robo fainali nyingine siku ya Ijumaa itakuwa kati ya Ghana na Uruguay katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg, hii ikiwa ni mara ya tatu katika historia ya Kombe la Dunia kwa timu kutoka Afrika kufikia hatua ya nane bora.

Siku ya Jumamosi itafanyika robo fainali ya tatu kati ya Ujerumani na Argentina katika uwanja wa Green Point mjini Cape Town.

Timu zitakazochuana kwenye robo fainali ya mwisho zitafahamika Jumanne, baada ya mechi za mwisho za raundi ya pili, Paraguay ikicheza dhidi ya Japan mjini Pretoria huku Uhispania na Ureno zikipambana mjini Cape Town

Oprah Winfrey, atisha kwa utajiri


Mtangazaji wa televisheni Marekani Oprah Winfrey ametajwa kuwa mtu mwenye mvuto na utajiri mkubwa duniani kupitia jarida la Forbes.

Winfrey amempiku muigizaji wa filamu Angelina Jolie kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya watu 100 mashuhuri kwa mwaka katika jarida la Forbes.

Nafasi hizo hupangwa kutokana na mapato ya mtu na kiwango anachoonekana kwenye vyombo vya habari.

Muimbaji Beyonce, amechukua nafasi ya pili, huku mkurugenzi wa filamu James Cameron akiingia tena kwenye chati na kuchukua nafasi ya tatu kufuatia mafanikio yake ya filamu ya Avatar.

Lady Gaga amepanda katika nafasi mpya ya orodha hizo akiwa nafasi ya nne.

Kama ilivyo kwa Beyonce, mapato yake na taarifa za maisha yake kwa ufupi zimeongezeka katika miaka 12 iliyopita kutokana na ziara zake duniani na mikataba mbalimbali.

Jolie, wakati huo huo, ameteleza kutoka nafasi ya juu hadi kufikia nafasi ya 18.

Nyota wa gofu aliyezingirwa na matatizo mengi Tiger Woods ni nyota pekee wa michezo kuwa katika 10 bora.


Simon Cowell

Simon Cowell

Britney Spears amekuwa wa sita, ikufuatiwa na U2 kwenye nafasi ya saba, wakiwa wamerudi katika 100 bora.

Sandra Bullock, aliyeshinda tuzo ya Oscar mwaka huu ya muigizaji bora wa kike, amepanda chati kwa kasi kutoka nafasi ya 92 hadi kufikia ya nane.

Johnny Depp naye amerudi kwenye chati katika nafasi ya tisa.

Kigogo wa muziki Simon Cowell ameongoza kwa upande wa Uingereza, kwa kupanda nafasi 14 hadi kufikia nambari 11.

Lakini Clodplay imeshuka kwa nafasi 20 na kuwa ya 35 katika mwaka ambao bendi hiyo imepumzika kufanya ziara na kuamua kurejea studio.

Nyota wa Harry Potter Daniel Radcliffe ameshika nafasi ya 82.

Umaarufu wa mfululizo wa Twilight ulionekana kwa kuwepo muigizaji wa kike Kirsten Stewart akiwa nafasi ya 66 na Robert Pattinson nafasi ya 50, wote wakiwa kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza.

Mwaka huu, Forbes iliongeza kigezo cha mtu maarufu kuwepo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook au Twitter, pamoja na mapato na kiwango cha kuonekana kupitia vyombo vya habari.

Saturday, June 26, 2010

WATU saba wa familia moja wamekufa baada ya kuteketea kwa moto


WATU saba wa familia moja wamekufa baada ya kuteketea kwa moto uliozuka ghafla usiku katika nyumba waliyokuwa wakiishi huko maeneo ya Soweto mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya. Bw. Nyombi alisema chanzo cha awali kutoka jeshi la polisi kilibaini, moto huo uliwashwa na mtoto wa mwenye nyumba hiyo kwa makusudi kutokana na chuki aliyolimbikiza kwa baba yake kwa kuwa alimuacha mama yake na kuoa mke mwengine.

Moto huo ulizuka usiku wa kuamkia jana ulioanza majira ya saa 5:00 usiku baada ya nyumba hiyo kumwagiwa mafuta ya petrol na kuwashwa moto baada ya watu wote wakiwa wameshaingia ndani kwa ajili ya kulala.

Hata hivyo zimamoto ilipofika mahali hapo walikuta miili hiyo ipo katika hali mbaya na walikuaw wakijitahidi moto usifike katika nyumba nyingine ili usiweze kumaliza watu werngi zaidi.

Hivyo miili hiyo ilichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Kamanda Nyombi alisema chanzo cha moto huo kinaendelea kuchunguzwa zaidi mbali na hiyo iliyotolewa awali na mtoto huyo anashikiliwa na polisi.

Waliokufa katika tukio hilo ni baba mwenye nyumba hiyo Daniel Mwang’ombe (75) Anita Richard (46) mke ,Salome Mwang'ombe (18).

Wengine ni Diana Samson (18), Jane Samson, Claud na msichana wa kazi aliyefahamika kwa jina la Mariam

Mtikila kizimbani tena kwa uchochezi


MCHUNGAJI Christopher Mtikila amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la uchochezi kwa mara nyingine kwa kusambaza walaka wa maneno ya uchochezi mitaani
Mtikila alifikishwa katika mahakama hiyo jana mbele ya Hakimu Michael Mteite wa mahakama hiyo.

Akisoma hati ya mashitaka, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Francis Mboya alidai mahakamani hapo kuwa, mshitakiwa huyo alifanya kosa hilo kati ya Novemba Mosi, 2009 na Aprili 17, mwaka huu katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Mboya alidai kuwa, Mtikila alisambaza walaka wenye maneno ya uchochezi kwa wananchi a jiji hilo.

Mboya alidai kuwa walaka aliosambaza Mtikila ulikuwa maneno yanayosema: “Rais Kikwete kaangamiza kabisa ukristo kutokana na imani yake, na kuongezea kuwa Kikwete yuko Ikulu kwa kuusambaratisha ukristo, hivyo aliwataka wakristo waungana upesi kupeleka ukristo Ikulu”.

Ilidaiwa kuwa katika shtaka la pili Mchungaji huyo alikutwa akimiliki pasipo halali waraka huo wa uchochezi Aprili 16, mwaka huu huko Mikocheni Dar es Salaam.

Hivyo kutokana na mashitaka hayo mtikila kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti, Sura ya 229, kifungu cha 32(i) (c) mshitakiwa huyo alitoa uchochezi ndani ya nchi kinyume na sheria.


Alipotakiwa kujibu mashitaka hayo Mtikila alikana kuhusika na matukio hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo mshitakwia huyo aliachiwa huru bada ya kukamilisha masharti ya dhamana alipotakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika wenye uwezo wa kusaini laki tano kila mmoja pamoja na hati yenye thamani hiyo.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 6, mwaka huu itakapokuja tena ka kutajwa

KATIKA hali iliyowashangaza wengi na kufanya wakinamama waogope kijana Beatus Alex (29) aliingia kwenye wodi ya wanawake


KATIKA hali iliyowashangaza wengi na kufanya wakinamama waogope kijana Beatus Alex (29) aliingia kwenye wodi ya wanawake ya kujifungulia kwa madai kuwa alikuwa akimfata mchumba wake aliyekuja kujifungua hospitalini hapo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi huko katika hospitali ya KKKT Machame wakati kijana huyo alipobuni vazi na kujifunika mithili ya mwanamke na kufanikiwa kupenya wodini humo hali iliyofanya baadhi ya akina mama kumshtukia na kuanza kupiga mayowe ya kuomba msaada.

Uongozi wa hospitali hiyo ulifanikiwa kumkamata kijana huyo na baada ya kukamata na kufunuliwa mavazi hayo aligundulika kuwa aliwahi kuwa mtumishi hospitalini hapo kwa cheo cha Afisa tabibu wa hospitali hiyo na alishafukuzwa kazi Februari mwaka huu kwa kosa la kujidunga sindano za usingizi ambazo alikuwa akitumia kama dawa ya kulevya.

Hata hivyo katika mahojiano ya kina alipoulizwa ni kwanini aliingia wodini humo ambapo haruhusiwi mtu kuingia zaidi ya mama mjamzito na wakunga alijieleza kuwa kuna mchumba wake aliyemtaja kwa jina la Josiphine alikuja kujifungua na yalipoangaliwa mafaili hakukuwa na mwanamke mwenye jina kama hilo.

Hata hivyo iligundulika kuwa mtuhumiwa huyo alifanya mbinu hiyo ya kujifunga ushungi kuingia wodini humo ili aweze kuiba dawa za usingizi zinazotambulika kitaalam kama DDA zinazotumika kuwachoma wagonjwa na alikuwa akijichoma mwenyewe akizitumia kama dawa za kulevya

JK kuchukua fomu leo Dodoma, wanane nao kuchukua Zanzibar


















MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Jakaya Mrisho Kikwete leo anatarajia kuchukua fomu ya kugombania Urais ambapo hadi sasa hana mpinzani ndani ya CCM huku Tanzania Zanzibar 8 wamejitokeza kuchukua fomu kugombea urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Kikwete anatarajiwa kuchukua fomu asubuhi hii huko Dodoma kwa ajili ya kuomba kuwania kiti hicho kwa awamu ya pili kugombania ufais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi [CCM].

Hadi sasa kwa upande a Tanzania Bara hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu mbali ya JAkaya Kikwete kwa tiketi ya CCM japo inasadikiwa wengine watajitokeza.

Kwa upande wa urais wa Tanzania Zanzibar, tayari vigogo nane wameshajitokeza kuchukua fomu hiyo kwa tiketi ya CCM.

Akiwemo Makamu wa Rais Tanzania Bara, DK, Mohamed Shein, Waziri Kiongozi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna, Waziri Kiongozi mstaafu, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Ali Abeid Karume na akiwemo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Hamad Bakari Mshindo.

KAtika kuwania kiti hicho Dk. Shein anaonekana kuwekewa vikwazo mbalimbali huku ikidaiwa kuwa hana vigezo vya kugombania kiti hicho kwa kuwa jina lake haliko katika daftari la kudumu la wapiga kura Zanzibar kwakuwa yeye alijiandikisha katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Na vilevile kwa mijibu wa katiba ya Zanzibar, kifungu 26(2) C na kifungu 27(4) vinasema kuwa mtu anayestahili kuwa Rais anatakiwa kuwa na sifa za kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi

Hivyo kutokana na vifungu hivyo Shein ameonekana kutokuwa na sifa ya kugombania kiti hicho visiwani Zanziba