KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 27, 2009

Ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Westerwelle katika mashariki ya kati , mgomo wa wanafunzi na siku ya waajiri ndio masuala yaliyoshughu


Ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Westerwelle katika mashariki ya kati , mgomo wa wanafunzi na siku ya waajiri ndio masuala yaliyoshughulikiwa na wahariri hii leo.

Leo hii katika udondozi wa maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani , wahariri wamezungumzia zaidi ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle katika mashariki ya kati, mgomo wa wanafunzi hapa nchini, na siku ya waajiri.

Tukianza na mada ya ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani katika mashariki ya kati , gazeti la Ostsee-Zeitung linalochapishwa mjini Rostock, linadokeza kuwa ziara ya hivi karibuni kabisa ya waziri Westerwelle katika mashariki ya kati inabaki kuwa katika milio ya kugonganisha glas tu.

Gazeti linaandika:

Akiikosoa kwa kiasi fulani sera ya Israel ya ujenzi wa makaazi ya Wayahudi katika eneo la ukingo wa magharibi, waziri Westerwelle hakufika mbali sana katika suala hilo. Hii ni sawa kwa ziara hii ya kwanza. Hata hivyo ni lazima Westerwelle atoe matamshi ya wazi kuhusu Israel kutokana na urafiki uliopo. Na kudai mengi zaidi kwa Wapalestina kama inavyohitajika katika suluhisho la mataifa mawili. Israel inamtaka kufanya hivyo binafsi. Lakini njia ya kuelekea huko inatia shaka. Kwa hili jibu litakuwa la dharura ambalo halitakuwa rahisi kwa waziri Westerwelle. Kutokana na hali ilivyo katika mashariki ya kati hali ya kujizuwia haipo tena.

Gazeti la Berliner Morgenpost likiandika kuhusu ziara hiyo ya Westerwelle linaandika:

Westerwelle ameonekana kutumia busara lakini sio kwamba alifanya vizuri na hakufanya hivyo , kama kwamba alikuwa na jibu katika suala gumu la mashariki ya kati. Westerwelle alijizuwia na kutoa maneno makali na ya wazi, lakini ameweka msimamo wake wazi, kutokana na kile kinachoitwa ramani ya njia, Road Map kuhusiana na mpango wa amani wa mashariki ya kati. Katika ramani hiyo kuna lengo ambalo ni wazi, nalo ni ujenzi mpya wa makaazi ya Wayahudi ni lazima uzitishwe.

Mada yetu ya pili ni mgomo wa wanafunzi hapa nchini. Gazeti la Sächsische Zeitung la mjini Dresden kuhusu hilo linaandika.Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Wanafunzi wakitundika mabango wakati wa mgomo wao nchini Ujerumani.
Kunahitajika vitu vingi vya masomo katika miaka mitatu ya kusomea shahada ya kwanza. Baadhi ya nyakati ilikuwa inahitaji hata miaka mitano kuweza kukamilisha. Na kwa ajili ya shahada ya uzamili hakuna hata nafasi, mara nyingi ni mwanafunzi mmoja tu hupata nafasi kwa kila wanafunzi 15.

Kwa mfumo mpya wa masomo ya juu katika bara la Ulaya kwa wanafunzi hilo halieleweki. Serikali ya shirikisho, majimbo na vyuo vikuu vinalazimika hivi sasa haraka iwezekanavyo kuuokoa mfumo huo wa mageuzi, kama kuna cha kuokoa.Masomo yabadilishwe ama shahada ya mwanzo irefushwe hadi miaka minne.

Kuhusiana na siku ya waajiri , gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung linaandika.

Sigmar Gabriel anajitumbukiza zaidi katika pango la simba. Katika siku ya waajiri kumekuwa na hali ya kumkaribisha kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha SPD bila ya kuwa na wasi wasi. Waziri wa uchumi Rainer Brüderle analazimika kuikaribisha hali hiyo kwa njia ya kirafiki. Hali ya kufikirika haipotena. Serikali ya nyeusi na njano ambayo viongozi wa makampuni walikuwa wakiihitaji imezongwa na mivutano kuhusu kodi na matumaini ya ukuaju wa uchumi. Habari nzuri ni kwamba: fedha za malipo ya ajira fupi , kansela anataka kuziongeza ; Habari mbaya ni kwamba mchango wa serikali kwa mafao ya kijamii huenda yasitolewe na serikali kwa waajiri.

Kwa hilo mzozo wa kiuchumi hautaondoka na bado kuna hatari ya kuporomoka tena kwa uchumi. Uongozi wa masuala ya kiuchumi nchini Ujerumani umekalia kuti kavu.

Na mpendwa msikizaji hayo ndio maoni ya baadhi ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani kwa leo. Nilikuwa nae Sekione Kitojo.

Korti moja ya Niedersachsen yahoji uhalalifu wa watu kuendelea kuchangia katika fuko la kuijenga upya sehemu ya mashariki ya Ujerumani,miaka 18 baadae


Korti moja ya Niedersachsen yahoji uhalalifu wa watu kuendelea kuchangia katika fuko la kuijenga upya sehemu ya mashariki ya Ujerumani,miaka 18 baadae

Mchango wa mshikamano kwaajili ya ujenzi mpya wa sehemu ya mashariki ya Ujerumani na hatima ya kampuni la magari la Opel ndizo mada zilizohanikiza magazetini hii leo.

Tuanze lakini na mchango wa mshikamano,au "Soli" kama unavyojulikana humu nchini.Gazeti la "REUTLINGER GENERAL-ANZEIGER" linaandika:

Suala hapa sio kujipigania.Na wala hili si suala la kuoneana kijicho kati ya sehemu ya Magharibi na Mashariki-kwasababu wanaochangia katika fuko la mshikamano ni walipa kodi.Suala hapa ni kuhusu kuaminiwa wanasiasa.Na haiwezekani kuwaona wanasiasa wakiendelea kunga'ang'ania mchango huo kwasababu miaka nenda miaka rudi umekua ukimimina mabilioni katika makasha ya hazina ya serikali-ili kugharimia miradi jumla.Mchango wa mshikamano-Soli,lazma ufutwe.Naiwe kupitia hukmu ya korti ya katiba au la.Busara ya kisiasa itumike kutathmini kiwango cha mahitaji .Na ukweli ni kwamba,sisi walipa kodi,mabilioni yatakayopungua,tutalazimika kuchangia,naiwe kupitia mchango wa mshikamano-Soli au bila ya mchango huo."

Gazeti la Sächsischer Zeitung la mjini Dresden linahisi hata kama korti ya katiba ikiunga mkono uamuzi wa korti inayoshughulikia masuala ya fedha ya Niedersachsen,haitomaanisha mwisho wa dunia.Gazeti linaendelea kuandika:

Ni kiroja kuona kwamba ndio kwanza sasa,miaka 18 baada ya kuanzishwa,Soli inawekewa suala la kuuliza na jaji wa korti ya masuala ya fedha,kama mchango huzo uendelee kutolewa.Na hata kama korti ya katiba itaunga mkono hoja hizo,haimaanishi kua dunia ndio inamalizika.Kwasababu zile pesa ambazo miongoni mwa mengineyo,zinatumika kuijenga upya sehemu ya mashariki,zitabidi zikusanywe kupitia njia nyengine.Au waziri wa fedha atalazimika kufutilia mbali mpango ambao tokea hapo unazusha mabishano wa kupunguza kodi za mapato.

Gazeti la Darmstädter Echo" lina maoni sawa na hayo na linaandika.

Ikiwa kweli korti ya katiba mjini Karlsruhe itafutilia mbali mchango wa mshikamano,basi patahitajika njia nyengine ya kujipatia fedha hizo.Pengine walipa kodi watavunjika moyo.Lakini kufutwa moja kwa moja mchango wa mshikamano bila ya kuwepo njia mbadala,si jambo linaloingia akilini kwasababu ,itapelekea mfumo mzima wa sera za fedha kuvurugika.

Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Makao makuu ya General Motors huko Rüsselsheim
Mada yetu ya mwisho inahusu kasheshe ya kampuni mama ya General Motor kuhusu matawi yake ya Opel nchini Ujerumani.Gazeti la FRÄNKISCHER TAG linaandika:



Baada ya kasheshe ya miezi kadhaa iliyopita,hatimae General Motors linaonyesha limeamua kweli kufanya marekebisho.:hatari lakini kwamba Opel linaweza kupotelewa na imani kuelekea kampuni mama la General Motors ,hivi sasa ni ndogo ikilinganishwa na hali namna ilivyokua mwaka uliopita.

Gazeti la NORDBAYERISCHER KURIER la mjini Bayreuth linaandika:

Msimamo usiokadirika wa General Motors unaweza kuendelea hivyo hivyo siku za mbele.Ingawa GM imeamua matawi yake ya Ujerumani na Ulaya yataendelea kuwepo.Lakini nini mameneja walioko Detroit watalazimisha kupatiwa badala yake kutoka kwa wanasiasa?Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya imejaribu kuzuwia mashindano ya kuania nafasi za kazi yasitokee miongoni mwa nchi za Ulaya.Lakini kama dhamiri za nchi kutoshindana wenyewe kwa wenyewe ni madhu,hakauna anaeweza kuashiria.

Rais wa Nigeria aumwa maradhi ya moyo


Rais Umaru Yar'Adua wa Nigeria ana matatizo ya moyo, msemaji wake ameeleza, baada ya kusafirishwa kwenda Saudi Arabia siku ya Jumatatu kupata matibabu.
Bw Yar'Adua ana maradhi yajulikanayo kama pericarditis, au kiungulia kuzunguka moyo wake, msemaji wake ameieleza BBC.

Alisema kuwa rais huyo, mwenye umri wa miaka 58, anaendelea vyema baada ya kuanza kutibiwa. Maafisa walikanusha taarifa za awali kwamba rais Yar'Adua alikuwa katika hali mahututi.

Bw Yar'Adua amekuwa na maradhi yasiyopona ya figo kwa miaka takriban 10.

Amekuwa akishindwa shughuli kadhaa za kiserikali kutokana na afya yake kumsumbua mara kwa mara.

Mafuriko yaua watu 77 Saudi Arabia


Mafuriko huko Saudi Arabia yameua watu 77 na wengine wengi hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa ambayo haijatokea kwa miaka mingi kunyesha.
Hakuna mtu hata mmoja aliyekufa ambaye ni miongoni wa mamilioni ya watu kutoka sehemu mbali mbali dunia ambao wanafanya Hajj, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Saudi alieleza.

Mvua nzito zinazoambatana na kimbunga zilinyesha siku ya Jumatano na kuchelewesha kuanza kwa shughuli za Hajj za kila mwaka katika mji mtukufu wa Makka.

Watu waliokufa kwa mafuriko walikuwa katika mji wenye bandari wa Jeddah, Rabigh na Makka, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali - Saudi Press Agency.

Ocampo aomba kupeleleza ghasia Kenya


Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa, Luis Moreno-Ocampo, anasema kuwa amewaomba majaji wa mahakama hiyo ruhusa ya kuanzisha upelelezi kuhusu ghasia za mwaka jana nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu.
Takriban watu elfu moja waliuawa katika ghasia hizo ziliozuka baada ya Rais Mwai Kibaki kutangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi mnamo Desemba mwaka 2007.

Upinzani ulidai kura ziliibiwa katika Uchaguzi huo.

Akizungumza na BBC Bw Ocampo amesema kuna sababu za kimsingi kuamini kwamba raia walitendewa maovu na vitendo vilivyokiuka haki za binadamu.

Kwa hiyo ikiwa majaji hao watalikubali ombi lake atakwenda Kenya kukusanya ushahidi kwa kuwasaili watuhumiwa na pia mashahidi na hapo ndipo wataamua kama kunastahili kufungua kesi ama la.

Ocampo alifafanua kuwa hawajibiki kutekeleza maelezo kuhusu orodha ya majina ya watuhumiwa ambayo ilikuwemo ndani ya bahasha aliyokabidhiwa mapema mwaka huu akisema hayo ni maoni ya wajumbe wa tume iliyochunguza mauaji hayo.

Yeye inampasa atoe uamuzi wake mwenyewe.

Fifa yalaumiwa kwa ubabe Afrika Kusini


Waandishi wa habari wa Afrika Kusini wamelishutumu shirikisho la soka la dunia kwa kuweka masharti magumu kuandika habari za kombe la dunia mwaka 2010.
Waandishi hao wanasema kulingana na masharti hayo, vibali vya waandishi vinaweza kufutwa endapo wataandika taarifa zinazolikosoa shirikisho hilo.

Wanaasema Fifa imekataa kufafanua swala hilo licha ya jitihada za mara kwa mara kutoka kwa waandishi.

Lakini Fifa imesema masharti hayo yameeleweka vibaya na hayatakwamisha uhuru wa waandishi wa habari.

Hata hivyo, Raymond Louw, msemaji wa jukwaa la wahariri wa Afrika Kusini lijulikanalo kama Sanef, ameieleza BBC kuwa Fifa ina maswali mengi ya kujibu.

Waandishi mateka waachiliwa Somalia


Waandishi wawili wa habari wa kigeni waliotekwa nyara na wanamgambo wa kisomali Agosti 2008 wameachiliwa huru na watekaji hao.
Amanda Lindhout kutoka Canada na Nigel Brennan wa Australia wanasemekana kuwa katika hoteli moja kwenye mji mkuu Mogadishu.



Bi Lindhout alivieleza vyombo vya habari vya Canada kwamba watekaji nyara walimtesa na kuwa kikombozi kililipwa kabla ya kuachiliwa kwake.

Mwandishi huyo aliileza televisheni ya Canada, CTV kuwa walikuwa wakihamishwa nyumba moja hadi nyingine na wanamgambo hao kwa kipindi cha miezi 15 ya kuwa mateka

Mke wa Berlusconi adai mamilioni


Aliyekuwa Mke wa Waziri Mkuu wa Italy Silvio Berlusconi amewasilisha madai ya kutaka alipwe fidia ya kuachika ya euro milioni 43, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.
Veronica Lario aliwasilisha ombi la kuachika mnamo mwezi May, baada ya kuchukizwa na tetesi za mumewe kutoka na binti mwenye umri mdogo wa miaka 18.

Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia linasema kuwa Bw. Berlusconi amekubali kumpa Bi Lario, aliyezaa naye watoto watatu euro laki mbili kwa kila mwezi.

Duru zilizo karibu na kiongozi huyo zinasema kuwa takriban euro milioni 60 hadi sabini zimeisha kabidhiwa kwa Bi Veronica Lario. Bi Lario mwenye umri wa miaka 52 aliolewa na Bw.Berlusconi mnamo mwaka 1990 miaka kumi baada ya kukutana naye.

Mshukiwa wa mauaji nchini Ufilipino ajisalimisha


Mtu mmoja maarufu huko Ufilipino ambaye anatoka ukoo wa Ampatuan amejisalimisha kwa maafisa wanaochunguza mauaji yaliofanyika mapema wiki hii.
Andal Ampatuan Junior, ambaye ni Meya katika eneo la kusini mwa kisiwa cha Mindanao, alisafirishwa kwa helkopta ya kijeshi hadi katika mji mkuu wa Manila na kwa sasa anafanyiwa uchunguzi.

Bw. Ampatuan amekanusha kushambulia familia ya mpinzani wake wa kisiasa, ambapo watu wasiopungua 57 waliuawa.

Ukoo wa Ampatuan kwa miaka mingi umekuwa ukimuunga mkono rais Gloria Arroyo.

Mkuu wa majeshi Ujerumani aachia ngazi


Jenerali wa Ujerumani amejiuzulu kufwatia mashambulio ya angani ya vikosi vya kujihami vya Nato ambapo raia waliuawa, waziri wa ulinzi amesema.
Wolfgang Schneiderhan amejiuzulu kutokana na shambulio la Septemba 4 eneo la Kunduz.

Uamuzi wake umetokana na ripoti kuwa taarifa kuhusu shambulio hilo-liloamrishwa na kamanda wa Ujerumani - hazikuwekwa wazi, waziri wa ulinzi alisema.

Inasemakana kuwa shambulio hilo liliwauwa raia wengi waliokuwa wakichota mafuta.

Wapiganaji wa Taliban waliteka magari mawili ya mafuta yakitoka Tajikistan kuelekea Kabul yakiwa na bidhaa za vikosi vya Nato.

Idadi ya raia waliouawa haijulikani.

Uchaguzi Namibia mashakani


Kampeni za uchaguzi nchini Namibia zimekumbwa na mizozo ya kisheria kabla ya kura za hapo kesho ijumaa.
Chama cha National Society for Human Rights kimewasilisha kesi kortini baada ya tume ya uchaguzi kuondoa hadhi yake ya msimamizi kwa madai kuwa na upendeleo.

Wakati huo huo chama kilichojitenga kutoka chama kikuu cha Swapo kimeiambia BBC kuwa kiongozi wake anadaiwa dollar za Marekani milioni kumi na tatu kwa kudai kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa na dosari.



Mgombea wa chama cha Swapo akiwa ni Rais Hifipekunye Pohamba anawania muhula wa pili baada ya ushindi wqa kishindo katika uchaguzi wa mwaka 2004.

Kiongozi wa upinzani, Hidipo Hamutenya, aliyejitenga kutoka Swapo mnamo mwaka 2004 anatarajiwa kumsumbuwa Bw.Pohamba katika uchaguzi utakaofanyika kwa siku mbili

Mahujaji leo waingia katika bonde la Arafa


Zaidi ya mahujaji millioni mbili wamewasili katika nyanda za Arafat katika siku ya pili ya ibada ya Hijjah.
Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na dhoruba kali ilinyesha mwanzoni mwa ibada hii takatifu siku ya Jumanne na kusababisha uharibifu katika maeneo matakatifu na vifo vya takriban watu 44.

Lakini hali ya hewa inaonekana kutulia na mamilioni ya mahujaji wamekusanyika katika nyanda za Arafat. Kwa mahujaji wengi huu ni wakati wa msisimko mkubwa unaozingatiwa kuwa ni kilele cha hijjah takatifu.

Hapa ndipo mtume Muhammad(SAW) alisimama karne 14 zilizopita na kutoa hotuba yake ya mwisho.Tangu wakati huo kila mwaka waislamu wamekuwa wakikusanyika hapo kusali na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu

Man United yapoteza nyumbani


Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson hakusikitishwa na kichapo cha 1-0 katika mchuano wa Ligi ya mabingwa na Besiktas.
Kipigo hicho kinatokea baada ya mechi 23 za Ulaya bila kupoteza kwenye uwanja wa Old Trafford na bado Man.united inahitaji pointi moja kuongoza kundi la B.

Lakini Ferguson, aliyefanya mabadiliko nane tafauti ya timu iliyochuana na Everton siku nne kabla alisema baada ya mechi kwamba nadhani tulipuuza kwa kiasi na ni makosa. Hata hivyo hawa ni vijana wadogo.

Besktas ilipata bao lake kupitia Rodrigo Tello ingawa lilimgusa beki wa United Rafael da Silva.

Avram Grant ateuliwa kuifunza Portsmouth


Aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea hapo zamani, Avram Grant, ametangazwa kuwa meneja wa Portsmouth baada ya Paul Hart kutimuliwa kufuatia kiwango cha timu hiyo kuzidi kuzorota.
Hii ni mara ya pili kwa Grant kufanya kazi kwenye klabu hiyo, mara ya kwanza alitumika chini ya Harry Redknap ambaye sasa yuko na Tottenham.

Raia huyo wa Israili aliwahi kushika wadhifa kama huo wa mkurugenzi mtendaji wa soka wa klabu ya Chelsea kabla ya Mourinho kutimuliwa na yeye kuteuliwa kama kocha.

Grant ataanza kwa mchuano utakaotangazwa na ''Ulimwengu wa Sokar'' Jumamosi hii kati ya Portsmouth na Manchester United.

Panga kumkosakosa Benitez


Mkurugenzi mkuu wa Liverpool Christian Purslow amesisitiza nafasi ya Rafael Benitez ni madhubuti, licha ya kutolewa ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Liverpool imeshindwa kusonga mbele hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita, licha ya ushindi kuifunga Debrecen bao 1-0.


Lakini Purslow amesema Benitez ataendelea kufundisha na akaongeza: "Hayupo hatarini.

Amesisitiza kwamba Benitez amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na ndio kwanza amemaliza miezi minne chini ya mkataba huo, kwa hiyo kuujadili mkataba wake sio sahihi.

Wednesday, November 25, 2009

Al Shabab lashutumu shirika la WFP




Moja ya makundi ya wapiganaji nchini Somalia limesema kwamba msaada wa chakula unaotolewa na Umoja wa Mataifa umezorotesha kilimo nchini humo.
Katika taarifa wapiganaji wa Al Shabab ambao sasa wanadhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia wanalishutumu shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP kwa kuhujumu juhudi za wasomali za kuzalisha chakula chao wenyewe.



Kundi hilo la Al Shabab linataka Umoja wa Mataifa kuacha kuagiza chakula kutoka nje na badala yake kununua chakula kutoka wakulima wa Somalia. Shirika hilo la mpango wa chakula halijasema lolote kuhusu taarifa hiyo ya Al Shabab

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani atilia mkazo haki ya Israel kuishi kwa amani na haki ya Palastina kuwa na taifa lao


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani atilia mkazo haki ya Israel kuishi kwa amani na haki ya Palastina kuwa na taifa lao



Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle leo amekataa kufuta uwezekano kwa Iran kuwekewa vikwazo vikali zaidi kutokana na tamaa yake ya kuwa na silaha za nuklea.

_________________________

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Jerusalem waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema kwao wao kuwepo kwa Iran yenye kumiliki silaha za nuklea kwa njia yoyote ile ni jambo lisilokubalika.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman, Westerwelle amesema usalama wa Israel ni jambo lisilokuwa na mjadala kwa kila mtu na hususan kwa Wajerumani.

Amesema hilo ni suala linalohusu jumuiya nzima ya kimataifa na sio tu Israel.

Lieberamn kwa uwpande wake amesema wakati umefika kwa kuliweka wazi suala hilo na kufanya maamuzi yasiotetereka.

Rais Shimon Peres wa Israel pia ameitaka Ujerumani kuendelea kuishinikiza Iran.

Peres amesema vitisho vya maangamizi, kukanusha kutokea kwa maangamizi ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia yaliofanywa na Manazi wa Ujerumani,kugharamia kwa kiasi kikubwa cha fedha na kuunga mkono makundi ya kigaidi ikiwa ni pamoja na Hezbollah nchii Lebanon na Hamas huko Gaza ni mambo mazito ambayo hayapaswi kupuuzwa.

Ujerumani ni mojawapo ya mataifa sita makubwa yenye nguvu duniani yanayozungumza na Iran juu ya mpango wake wa nuklea ambao mataifa ya magharibi yanautilia mashaka kuwa ni kwa ajili ya kutengeneza silaha za nuklea.

Waziri mpya wa mambo ya nje wa Ujerumani amesisitiza msimamo wa nchi yake kuiunga mkono Israel laki pia kuwepo kwa ufumbuzi wa mataifa mawili kwa mzozo kati ya nchi hiyo na Wapalestina.



Westerwelle pia amesema kwamba lengo lao ni kuwepo kwa ufumbuzi wa kweli wa mataifa mawili ambapo taifa la Israel liheshimiwe na mataifa yote jirani na kuwepo kwa taifa la Palestina lenye kufanya kazi.

Ameepuka kuikosoa Israel kwa ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina.

Mapema akiwa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi Westerwelle amewataka Waisrael na Wapalestina kurudi katika meza ya mazungumzo ya amani kwa haraka iwezekanavyo.

Kaimu Waziri Mkuu wa Wapalestina Salama Fayyad amesema baada ya kukutana na Westerwelle mjini Ramallah kwamba waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani anaunga mkono madai ya Wapalestina ya kusitishwa kabisa kwa ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu na Israel ikiwa ni pamoja na Jerusalem ya Mashariki.

Fayyad ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba wamezungumzia matakwa ya mpango wa ramani ya amani ambapo Israel inapaswa kusitisha harakati zote za ujenzi wa makaazi katika maeneo yote na kwamba kulikuwa na makubaliano na waziri huyo wa Ujerumani juu ya jambo hilo.

Serikali ya Ujerumani ilielezea kusikitishwa kwake sana na uamuzi wa Israel kujenga makaazi katika ardhi ilioinyakua na kuikalia kwa mabavu katika vita vya mwaka 1967 na kuijumuisha kwenye mipaka ya manispaa ya Jerusalem.

Ujerumani inaona ujenzi wa makaazi hayo kuwa kikwazo kikubwa katika njia ya kusonga mbele na mchakato wa amani.

Waziri huyo mpya wa mambo ya nje wa Ujerumani alifanya safari hiyo fupi huko Ramallah akitokea Jerusalem ambapo baada ya kuwasili kwake hapo jana alitembelea kumbukumbu ya Maangamizi ya Wayahudi ya Yad Vashem kabla ya kuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman hapo jioni.

Akitembelea eneo la kumbukumbu ya Maangamizi ya Wayahudi ya Yad Vashem ya Wayahudi milioni sita waliouwawa na Manazi wa Ujerumani wakati wa Vita Vikuu vya Pili Westerwelle amesema Ujerumani ina wajibu maalum kwa Israel.

Ziara ya Westerwelle Mashariki ya Kati inakuja wiki moja kabla ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kukutana mjini Berlin na Kansela Angela Merkel na mawaziri wa Israel na Ujerumani kuwa na kikao cha pamoja.

Ziara yake inafanyika wakati kukiwa na repoti za juhudi mpya na hata uwezekano wa kufikiwa makubaliano katika mazungumzo yanayosuluhishwa na Ujerumani ya kumuachilia huru askari wa Israel anayeshikiliwa na kundi la Hamas la Wapalestina kwa zaidi ya miaka mitatu katika Ukanda wa Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Lieberman akikutana na Westerwelle hapo jana alimshukuru waziri mwenzake kwa juhudi za serikali ya Ujerumani kufanikisha makubaliano hayo akisema kwamba bado haiko wazi iwapo kutafikiwa kwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa kati ya Israel na kundi hilo la Hamas.

Gaddafi 'kusuluhisha' mzozo wa Misri-Algeria


Gaddafi 'kusuluhisha' mzozo wa Misri-Algeria

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amekubali kuwa mpatanishi katika mzozo kati ya Algeria na Misri,shirika la habari la serikali limesema.
Shirika la habari la Libya lijulikanalo kama Jana limeripoti kuwa Jumuiya ya Waarabu imemuomba Gaddafi kupatanisha mataifa hayo mawili.

Kila upande umeshtumu mashabiki wengine kwa kufanya ghasia baada ya mechi muhimu ya kuania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia wiki iliyopita,ambapo Algeria ilishinda.

Wakati huo huo,takriban wasomi 150 wa Misri na Algeria wametoa wito wa kukomeshwa kwa mzozo huo.

Ibada ya kila mwaka ya Hajj, imeanza rasmi leo mjini Mecca


Ibada ya kila mwaka ya Hajj, imeanza rasmi leo mjini Mecca. Kiasi cha milioni mbili na laki tano ya Waislamu, wamekusanyika mjini Mecca, kutekeleza ibada hiyo.

Hajj ya mwaka huu pia inafanyika wakati kuna wasiwasi wa kusambaa kwa homa ya nguruwe, ambayo tayari imewaua mahujaji wanne.

Jana ndio ilikuwa siku ya mwisho ya mahujaji kuwasili katika mji wa Mecca, tayari kwa kuanza rasmi kwa ibada ya hajj leo hii. Waislamu kutoka kila pembe ya dunia, wa tabaka mbali mbali, wakubwa kwa wadogo, wanawake kwa wanaume wamemiminika mjini Mecca, kutekeleza ibada hii ya Hajj ambayo ni nguzo moja kati ya nguzo tano za dini ya kiislamu. Na kila muislamu mwenye uwezo na afya njema anawajibika kufika kutekeleza ibada ya Hajj angalau mara moja maishani.

Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Bonde la Jamarat, huko Mina, Mahujaji wanaporusha vijiwe kumpiga shetani. Ibada ya mwaka huu hata hivyo, imezongwa na wasiwasi wa maambukizi ya homa ya nguruwe. Tayari mahujaji wanne wamefariki kutokana na kuambukizwa virusi vya homa hiyo ya nguruwe. Serikali ya Saudia Arabia hata hivyo imesema imechukua tahadhari zote na hakuna hofu ya kusambaa kwa virusi vya homa hiyo.

Hajj inaanza rasmi leo, kwa ile ibada ya tawaf, ambayo ukipenda ni zoezi la kuzunguka Kaaba mara saba- Kaaba ni jengo la mraba lililokati kati mwa msikiti mkuu mjini Mecca, na ni eneo ambalo waislamu kote duniani huelekeza wanapotekeleza ibada zao tano za sala kila siku.

Mahujaji baadaye wataelekea huko Mina, watakakokaa usiku kabla ya kuamkia kupanda mlima Arafa, hapo kesho. Arafa ndio eneo mtume Muhammad alipotoa risala zake za mwisho. Amina Abdalla anatoka nchini Kenya, amefika Hajj mwaka huu, anasema,

'' Najisikia nimepata bahati kubwa kwamba mimi ni mmoja kati ya milioni mbili ya Waislamu waliofika Mecca mwaka huu kutekeleza Ibada ya Hajj. Nimetoka nchini Kenya, na kiasi cha wakenya 2000 wako hapa Mecca kwa Ibada hii ya Hajj. Najisikia kwamba huu sio ufanisi wangu bali Mwenyezi Mungu ndio ameniwezesha.''

Bildunterschrift: Maafisa wa Usalama Saudia Arabia, wanaimarisha usalama wakati wa Hajj. Huku ibada ya Hajj ikiendelea, mafundi walikuwa bado wanaendeleza ukarabati wa kupanua sehemu za msikiti mkuu kutoa nafasi zaidi kwa mahujaji. Msikiti huo mkuu wa sasa una uwezo wa kuingia watu milioni moja.

Sehemu zingine ambazo zimepanuliwa ni ile njia inayoelekea katika milima ya Safa na Marwa. Ni wakati wa kupanda safa na Marwa ndio mara kwa mara imegeuka kuwa eneo la mkasa, mahujaji wanapokanyagana, wanapokuwa wanapanda na kushuka milima hiyo miwili.Mwaka wa 2006, mahujaji 364 walikufa kwa kukanyagwa katika bonde la Jamarat huko Minna, katika siku ya mwisho ya kutekeleza ile ibada ya kurusha vijiwe, mithili ya kumpiga shetani. Kuzuia visa hivi, serikali ya Saudia imejenga daraja la ngazi tano, kutoa nafasi ya watu kufanya safwa na Marwa bila ya msongamano mkubwa.

Usalama pia umeimarishwa vilivyo, zaidi ya laki moja ya maafisa wa usalama wamesambazwa kote katika maeneo Hajj inafanyika.

Mwandishi: Munira Muhammad/ AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman.

Vinyonga wapya wagunduliwa Tanzania


Vinyonga wapya wagunduliwa Tanzania

Mwanasayansi mmoja wa Uingereza aliyekuwa akifanya utafiti wa viumbe hai katika msitu wa Magombera huko Tanzania ametangazwa rasmi kugundua aina mpya ya vinyonga ambao hawapatikani sehemu nyingine duniani isipokuwa Tanzania.
Dr Andrew Marshall kutoka chuo kikuu cha York nchini Uingereza alimgundua mnyama huyo ambaye hatimaye alipewa jina la ni Kinyongia magomberae, miaka minne iliyopita, lakini sasa ndiyo amethibitishwa rasmi na wataalam wenzie.


Kinyongia magomberae aliyegunduliwa na Dr Andrew Marshall. Picha kwa hisani ya Andrew Marshall.



Dr Andrew Marshall, mwanaikolojia kutoka chuo kikuu cha York, ameieleza BBC kuwa alikuwa akifanya utafiti wa mbega wekundu, ndipo siku moja alipokumbana na nyoka ambaye alishtuka na kumtema kinyonga huyo miguuni mwake na kukimbia.

Ingawa mwenzake alimshauri asimguse kutokana na wasi wasi wa kuathirika na sumu ya nyoka, Dr Marshall alihisi kiumbe huyo alikuwa mpya machoni mwa wanasayansi akampiga picha na kuwatumia wenzake ambao walithibitisha aliyokuwa akifikiria.

Kinyongia magomberae

Kinyongia magomberae, ikiwa na maana ya "kinyonga wa Magombera", ni matokeo ya mkasa huo na akaieleza BBC kwamba haikuwa rahisi kwake kumtambua ndiyo maana akavutiwa kumchunguza.

"Unajua, rangi si kigezo kizuri kuwatofautisha vinyonga, kwasababu wanabadilika rangi kutokana na mazingira. Kwa kawaida hutambuliwa kutokana na maumbile ya vichwa vyao, na mpangilio wa magamba. Kwa tukio hili ilikuwa ni magamba yaliyotuna juu ya pua yake."

Kwa bahati njema, Dr Marshall alifanikiwa kumwona kinyonga wa pili akiwa hai na alifanikiwa kumpiga picha.

Viumbe hao walipatikana umbali wa kilometa 10 kutoka kila mmoja, jambo linalomfanya aamini inaweza kuwa umbali halisi wa eneo linalokaliwa na Kinyongia magomberae.

Utafiti

Ingawa aliwagundua viumbe hao mwaka 2005, nyaraka zake za utafiti zilizochapishwa Novemba 2009, zinatambulisha rasmi uvumbuzi huo.

"Inachukua muda mrefu kuzishawishi mamlaka kuwa umevumbua aina mpya ya viumbe," alieleza.

"Tulipowasilisha matokeo ya ufafiti wetu kwa wanakijiji wa eneo hilo walifurahishwa kwamba dunia sasa inatambua mnyama huyo kwa jina la kienyeji Magombera," alisema.

Magombera ni msitu wa asili ulioko eneo la hifadhi ya Udzungwa mpakani mwa mikoa ya Morogoro na Iringa.

Mataifa makubwa duniani yamerasimu azimio litakalopigiwa kura na Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki baadae wiki hii ambalo linailani Ir


Mataifa makubwa duniani yamerasimu azimio litakalopigiwa kura na Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki baadae wiki hii ambalo linailani Iran kwa kuuficha mtambo wake wa pili wa kurutubisha uranium.

Mataifa matano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Uingereza,China,Ufaransa,Urusi na Marekani pamoja na Ujerumani wameandaa rasimu ya azimio hilo ambalo litawasilishwa kwa bodi ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA katika mkutano wao wa siku mbili unaoanza hapo kesho.

Lakini kwa mujibu wa wanadiplomasia bado hakuna uhakika iwapo rasimu hiyo itaweza kuungwa mkono na wajumbe wengi wa bodi hiyo katika mazungumzo kabla ya mkutano wao kwa hiyo mataifa hayo sita hatimae yumkini yakaamua kutoa azimio hilo kama taarifa tu badala ya kutaka lipigiwe kura.

Shirika la IAEA halikupitisha azimio juu ya Iran tokea mwezi wa Februari mwaka 2006.Lakini tangazo la kushtua la Iran hapo mwezi wa Septemba kwamba imekuwa ikijenga mtambo wa pili wa kurutubisha uranium kwa kukaidi vikwazo vya Umoja wa Mataifa kusitisha kabisa urutubishaji huo limeikasirisha hata Urusi na China ambazo huko nyuma zilikuwa zikisita sita kujiunga na wito wa mataifa ya magharibi kuiwekea Iran vikwazo vikali zaidi.

Mataifa hayo sita yalikutana mjini Brussels wiki iliopita ambapo walifikia makubaliano makubwa juu ya uzito wa tangazo hilo la karibuni la Iran.

Iran iliijulisha IAEA hapo mwezi wa Septemba kwamba imejenga mtambo wa pili wa kurutubisha madini ya uranium ndani ya mlima karibu na mji wa Qom na kuzusha shutuma mpya kutoka kwa mataifa ya magharibi juu ya mpango wake huo wa nuklea juu ya kwamba Iran inakanusha kwamba inajaribu kutengeneza bomu la nyuklia.


Iran imekuwa ikirutubisha uranium kwa miaka kadhaa kwenye mtambo katika mji wa kati wa Natanz kwa kukaidi vikwazo vilivyowekwa mara tatu na Umoja wa Mataifa dhidi yake.Madini ya uranium yanatumiwa kwa ajili ya nishati ya mitambo ya shughuli za kiraia lakini kwa uranium inayorutubishwa kwa hali ya juu inaweza kutumiwa kwa ajili ya kutengeneza mabomu ya atomiki.

Katika ziara yake ya Mashariki ya Kati waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ambaye nchi yake ni mojawapo ya nchi sita zinazoishinikiza Iran kusitisha mpango wake huo hapo jana akiwa nchini Israel amesema kwamba ni jambo lisilokubalika kwa Iran kumiliki silaha za nyuklia.



Katika repoti yake ya kwanza tokea wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA kukagua mtambo wa Qom mwezi uliopita shirika hilo limelalamika kwamba kuchelewa kwa Iran kutangaza kuwepo kwa mtambo huo hakusaidii kujenga imani.

Iran imesema mtambo huo ulikuwa umepangwa uwe mbadala iwapo mtambo wa Natanz utashambuliwa kwa mabomu.

Wakati haya yanajiri Rais Mahmoud Ahmeadinejad wa Iran amewasili Caracas Venezuela kwa mkutano na Rais Hugo Chavez masaa machache baada ya kiongozi huyo wa Iran kutua kwa muda mjini La Paz kwa mkutano na Rais wa Bolivia.

Ahmadinejad na Chavez viongozi wawili wanaopingana na Marekani ambao nchi zao ni wazalishaji wakubwa wa mafuta wanakutana leo hii kwa lengo la kuongeza ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Vyama vya upinzani na jumuiya Wayahudi wameishutumu ziara hiyo ya Ahmadinejad nchini Venezuela kutokana na kiongozi huyo kukanusha kutokea kwa maangamizi ya Wayahudi,ukiukaji wa haki za binadamu na mpango wake huo wa nyuklia.

Ripoti: Wajanja wageuza yatima biashara


Ripoti mpya inaeleza kuwa watoto wanne kati ya watano wanaoishi katika makazi ya yatima kote duniani wana mzazi angalau mmoja.
Shirika la hisani la kusaidia watoto la Save the Children, limesena baadhi ya taasisi zinawarubuni wazazi masikini kuwatoa watoto wao.

Matokeo yake, ripoti inasema, maisha ya mamilioni ya watoto yako hatarini kwa kuishi katika nyumba za yatima, na wanakabiliwa na ubakaji, kutoroshwa nje ya nchi na vipigo.

Save the Children inasema misaada inatakiwa kuelekezwa katika miradi inayosaidia familia kuwatunza watoto wao.

Ripoti inadai viituo vya kutunzia yatima imegeuka kuwa biashara kubwa katika baadhi ya nchi, ambao wanaoviendesha hupokea msaada wa kifedha kutoka serikali na wahisani wenye nia njema.

Rais Obama akusudia kumaliza kazi Afghanistan


Rais Obama akusudia kumaliza kazi Afghanistan

WASHINGTON




Rais Barack Obama wa Marekani amesema anakusudia kumaliza kazi nchini Afghanistan wakati akijiandaa kutangaza uamuzi wake mpya kuhusu mkakati wa nchi yake nchini humo, wiki ijayo. Kamanda wa Marekani, Stanley McChrystal alitoa ombi kwa Rais Obama la kuidhinisha wanajeshi elfu 40 zaidi kupelekwa Afghanistan kwa ajili ya kupambana na wanamgambo wa Taliban.

Uamuzi wa Rais Obama unaosubiriwa kwa muda mrefu huenda ukabadili sera za washirika wake katika Jumuiya ya Kujihami ya NATO. Kuna taarifa kuwa Rais Obama atapeleka kati ya wanajeshi 30,000 na 40,000 zaidi nchini Afghanistan. Kwa sasa Marekani ina wanajeshi 68,000 nchini humo kati ya wanajeshi 110,000 wanaoongozwa na NATO.

Marekani imefungua ukurasa mpya wa uhusiano na India kwa kuahidi kuishirikisha kwa karibu zaidi katika masuala ya kupambana na ugaidi,nishati


Marekani imefungua ukurasa mpya wa uhusiano na India kwa kuahidi kuishirikisha kwa karibu zaidi katika masuala ya kupambana na ugaidi,nishati mbadala na kuzuwia utapakazaji wa silaha za nuklia.

Kauli hizo zimetolewa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh huko Marekani alipofanya mazungumzo na Rais Barack Obama.Hii ni mara ya kwanza Rais Obama anamkaribisha rasmi kiongozi wa taifa tangu aushike wadhifa huo.Ajenda ya kikao chao hicho ilijikita zaidi katika harakati za kuuimarsha uhusiano wao kiuchumi hasa baada ya biashara ya India kukua kwasababu ya mageuzi makubwa katika sekta hiyo yaliyofanyika mwanzoni mwa miaka ya tisaini.

Rais Barack Obama alizielekeza zaidi juhudi zake kumhakikishia mgeni wake wa kwanza rasmi Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh kuwa ataendelea kuuimarisha uhusiano kati ya mataifa yao mawili,''Leo hii tunajitahidi kuutimiza wajibu wetu wa kuuimarisha uhusiano kati ya mataifa yetu mawili.Leo hii tunaufurahia mwelekeo utakaouimarisha ushirikiano wetu na urafiki kati ya watu wetu,''alieleza.

Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Rais Barack Obama na Waziri Mkuu Manmohan Singh wakiwa na wake zaoItakumbukwa kuwa Rais Obama amekuwa akikosolewa nchini mwake kwa kuyapa kipa umbele mataifa hasimu wa India yaani China na Pakistan hasa baada ya kuikamilisha ziara yake ya bara la Asia hivi karibuni.Kwa upande wake serikali ya India ililitaraji hilo kwani uhusiano kati ya mataifa yao ulikuwa mzuri tangu wakati wa utawala wa George W Bush.Pindi baada ya karamu ya chakula cha jioni kufunguliwa rasmi, alipopanda jukwaani, Waziri Mkuu wa lndia Manmohan Singh alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na mbinu mpya za ushirikiano wa kimataifa kwasababu ya changamoto,''Tunahitaji kuwa na mbinu mpya za kuuimarisha ushirikiano wa kimataifa zitakazoweza kupambana na changamoto kubwa zinazojitokeza kwasababu ya nchi kutegemeana.''

Katika hotuba yake ya ufunguzi Rais Obama alisema kuwa India ni mshirika muhimu katika masuala ya usalama kote ulimwenguni na ustawi,''Mafanikio tunayoyasherehekea leo ni hatua muhimu…nafasi ya kujiendeleza ukizizingatia changamoto na mafanikio ya baadaye.Ya kale yamepita…tugange yajayo,'' alisisitiza.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh alimshukuru mwenyeji wake na akamuelezea kuwa mfano kwa watu wa India kwani anawawakilisha wote wanaoiheshimu demokrasia,mchanganyiko wa watu mbalimbali na usawa.

Ajenda ya mazungumzo ya viongozi hao wawili ilijikita katika masuala ya kuuimarisha ushirikiano wa kiuchumi hasa baada ya sekta ya biashara ya India kukua kwasababu ya mageuzi iliyofanyikwa.Kwa mujibu wa takwimu za mwaka uliopita biashara kati ya mataifa hayo mawili inakadiriwa kuongezeka hadi kiasi cha dola bilioni 50 ikilinganishwa na kile cha mwaka 1990 cha bilioni 5.

Viongozi hao waliwaeleza waandishi wa habari kuwa wanajitahidi kuyakamilisha makubaliano ya mwaka 2005 ya kutengeneza nishati ya nuklia ya matumizi ya kawaida.Kwasababu ya hilo India itaweza kuwekeza katika soko la nishati lililo na thamani ya dola bilioni 150.Maelezo kamili ya hatua hiyo bado hayajabainika.


Hata hivyo India bado inatiwa wasiwasi na msimamo wa Marekani na Pakistan inayoilaumu kuwa chanzo cha ghasia zinazosababishwa na wapiganaji wa kiislamu kama lile shambulio lililotokea Mumbai mwaka 2008.Suala jengine linaloisumbua India ni uhusiano unaopewa uzito mkubwa kati ya Marekani na China iliyo hasimu wake wa jadi.Kulingana na afisa wa serikali wa Marekani fikra hizo ni potofu.

Bildunterschrift: Wanajeshi wa kigeni walioko AfghanistanWakati huohuo Rais Obama anasubiriwa kuutangaza msimamo wake kuhusu suala la kuviongeza vikosi zaidi Afghanistan jambo ambalo huenda likaubadili mtazamo wa washirika wake wakuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.Kiongozi huyo wa Marekani aliweka bayana kuwa ana azma ya kupunguza mivutano kati ya India na Pakistan,mataifa yaliyo jirani.Marekani inataraji kuwa Jeshi la Pakistan litauimarisha uwezo wake ili kupambana na wapiganaji wa kiislamu wanaoutishia ustawi wake pamoja na wa nchi jirani ya Afghanistan.

Baada ya mazungumzo yao Rais Obama na Waziri Mkuu Manmohan Singh walisisitiza kuwa wana imani makubaliano ya msingi yatafikiwa katika kikao cha kilele cha mazingira kijacho cha Copenhagen,Denmark. Hata hivyo viongozi hao hawakuonyesha ishara yoyote kuwa wameibadili misimamo yao inayotofautiana kuhusu suala la kupunguza viwango vya gesi za viwanda zinazochangia katika athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

A.Kusini kuanzisha korti za kombe la dunia


A.Kusini kuanzisha korti za kombe la dunia

Afrika Kusini inajiandaa kuanzisha mahakama maalum zitakazoshughulikia uhalifu utakaofanyika wakati wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010.
Serikali inatumai kwamba mpango huo wa kuharakisha kesi utawawezesha wageni kutoa ushahidi watakapokuwa nchini humo kwa muda mfupi, jambo litakalofanya wahalifu wengi kuogopa.

Jumla ya mahakama 54 zitafanya kazi katika miji tisa itakayokuwa wenyeji wa michuano ya kombe la dunia.

Wizara ya sheria imesema endapo wageni watahusika katika uhalifu kama watuhumiwa au waathirika, kesi zao zitapewa kipaumbele.

Afrika Kusini ni mojawapo ya mataifa yenye vitendo vingi vya uhalifu duniani, lakini tangu rais Jacob Zuma alipochukua madaraka mwezi Mei, serikali imeweka kipaumbele kupambana na uhalifu.

Arsenal wapiga hatua Liverpool wakwama


Arsenal wapiga hatua Liverpool wakwama
Vijana wa Arsenal walifunga mabao mawili dhidi ya Standard Liege ya Ubelgiji kuimarisha nafasi yao katika mashindano ya kilabu bingwa barani Ulaya huku Liverpool wakifungishwa virago licha ya kupata ushindi.
Arsenal hawakuonyesha kutatizwa na mnamo dakika ya 35, Samir Nasri alifunga bao la kwanza naye Denilson akiongeza la pili kabla ya kipindi cha mapumziko.

Huku Arsenal wakisherehekea kujinyakulia nafasi katika timu 16 zilizosalia kwenye dimba hilo la kilabu bingwa Ulaya, wenzao wa Uingereza, Liverpool walibaki kujuta.

Ingawa walicheza kufa na kupona hadi kuishindi timu ya Debrecen ushindi huo haukuwa na maana kwa kuwa nafasi waliyokuwa wakitegemea ilinyakuliwa na Lyon.

Liverpool iliichapa Debrecen bao 1-0 na kutegemea kwamba Lyon ingetoka sare au hata kuishinda Fiorentina.

Liverpool sasa watasalia kung’ang’ana katika ligi ya Europa.

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Liverpool kukosa kuingia katika raundi za mchujo tangu msimu wa 2002 – 2003.

Timu ya Rangers kutoka Uskochi nayo pia imefungishwa virago na VfB Stuggart.

Basi leo Jumatano usikose kijasho katika uwanja wa Old Trafford wakati Manchester United ikipambana na Besiktas huku Chelsea ikiwa ugenini kucheza na FC Porto ya Ureno.

Sunderland yasubiri vipimo vya Bent


Sunderland yasubiri vipimo vya Bent

Sunderland ina wasiwasi huenda Darren Bent akawa nje kwa wiki tatu baada ya mfungaji wao huyo kufanyiwa vipimo kutokana na kuumia goti.
Mshambuliaji huyo ambaye pia huchezea timu ya taifa ya soka ya England aliumia goti baada ya kufunga bao la ushindi siku ya Jumamosi, dhidi ya Arsenal.



Meneja wa Black Cats Steve Bruce ameeleza katika mtandao wa klabu hiyo, "iwapo itakuwa goti ndio linamsumbua, hapana shaka atakaa nje kwa wiki tatu".

Mshambuliaji huyo kuna wasiwasi asicheze mchezo na Wigan na kukosekana kwake kuna leta hofu ya nani atakayeongoza safu ya ushambuliaji, wakati huu Kenwyne Jones akiwa amefungiwa baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu walipocheza na West Ham mwezi wa Oktoba.

Mlinzi wa klabu ya Liverpool ya Uingereza, Jamie Carragher, ameelezea kwamba ikiwa timu yake itaondolewa katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulay


Mlinzi wa klabu ya Liverpool ya Uingereza, Jamie Carragher, ameelezea kwamba ikiwa timu yake itaondolewa katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, hili halitakuwa ni tatizo kubwa, kwani bado kitakuwemo katika ligi ya Europa.
Liverpool inahitaji Jumanne jioni kuishinda Debrecen ya Hungary, na ikitazamia pia wapinzani wao wakuu katika kundi la E, Lyon ya Ufaransa, watafanikiwa kuishinda Fiorentina ya Uhispania.

La sivyo, Liverpool haitafanikiwa kujiunga na timu 16 ambazo zitaendelea kuwepo katika mashindano.

Carragher alisema: "Bado tunaamini kwamba tunaweza kuendelea katika ligi ya klabu bingwa. La sivyo, tutaangazia yanayokuja".

"Klabu hakitakufa kwa kuondolewa kutoka ligi ya klabu bingwa".

FIFA yajikuna kichwa kuhusu kashfa


Shirikisho la kandanda duniani, Fifa, linaandaa mkutano maalum mwezi ujao kujadili matukio mbalimbali ambayo yameghubika ulimwengu wa soka mnamo siku au wiki chache zilizopita.
Hoja kubwa ni kashfa ambazo zimekumba baadhi ya mechi za kufuzu kwa fainali za kombe la dunia.

Kwa wiki nzima sasa mshambuliaji Thierry Henry ametupiwa tope na lawama kuushika mpira na kutoa pasi kwa mwenzake, William Gallas ambaye alifunga bao la ushindi kati ya Ufaransa na Ireland.

Fifa imekataa ombi la Ireland kwamba mechi hiyo ichezwe upya.

Huenda Fifa wakajadili pia kiini cha ghasia na mkwaruzano kati ya Algeria na Misri.

Algeria iliitandika Misri bao 1-0 katika mechi iliyochezewa nchini Sudan kuamua nani atakwenda Afrika Kusini mwaka ujao.

Kwenye ajenda ya shirikisho hilo pia ni vitendo vya kutumia kamari kwa nia ya kushawishi matokeo ya mechi barani ulaya.

Isitoshe, shirika la kandanda la Iraq lilisimamishwa kwa muda kutokana na serikali kuingilia shughuli zake, kinyume na kanuni za Fifa.

Monday, November 23, 2009

Henry anafikiria kuacha timu ya taifa


Thierry Henry anafikiria kuacha soka ya kimataifa kufuatia kuushika mpira wakati Ufaransa walipocheza na Jamhuri ya Ireland kuwania nafasi ya Kombe la Dunia.
Mshambuliaji huyo amejikuta katika mzozo mkubwa kutokana na kitendo chake hicho ambacho kiliisaidia Ufaransa kuitoa Ireland na kujipatia nafasi kwenda Afrika Kusini.

Alipoulizwa iwapo anafikiria kustaafu kufuatia utata uliojitokeza wa bao la kusawazisha dhidi ya Ireland, Henry alilieleza gazeti la Ufaransa la L'Equipe: "Ndiyo".

Chama cha soka cha Ireland kiliandika barua kwa Fifa wakitaka warudiane na Ufaransa.

Maombi hayo yalikataliwa licha ya Henry kutoa taarifa akisema kurudiana na Ireland ndio suluhisho.

Messi kukosa mechi na Inter Milan


Kuna wasiwasi Lionel Messi akakosa mechi baina ya timu ya Barcelona na Inter Milan kuwania Ubingwa wa Ulaya siku ya Jumanne.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anafanyiwa uchunguzi kuhusiana na maumivu ya paja aliyopata siku ya Jumamosi walipotoka sare ya bao 1-1 na Athletic Bilbao.

Kuumia kwa Messi kumekuja wakati tumu yake inamuhitaji zaidi ambapo siku ya Jumapili wanakabiliwa na pambano gumu na watani wao wa jadi Real Madrid.

Zlatan Ibrahimovic, Yaya Toure na Eric Abidal kwa sasa nao ni wagonjwa, lakini meneja wa Barcelona Pep Guardiola amesisitiza watacheza na kile walichonacho.

Guardiola pia anasubiri taarifa za mlinzi Rafael Marquez, ambaye anafanyiwa uchunguzi wa homa ya mafua ya nguruwe iliyowapata pia Toure na Abidal.