KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, October 28, 2010

Mtoto ajeruhiwa kwa risasi na askariMTOTO Juma Hamza (12) amejeruhiwa kwa kupigwa risasi maeneo ya tumboni, wakati askari walipokuwa wakijihami na wananchi.


Mtoto huyo alijeruhiwa na mmoja wa askari hao wa kituo cha polisi Chang’ombe wakati walipokuwa wakitoka kukamata waharifu.

Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Temeke, Kamishna wa Polisi, David Misime, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi Keko, karibu na ukumbi unaojulikana kwa jina la Jumba la Dhahabu.

Misime alisema, askari hao walipata taarifa kuwa kuna watu walipora kamera kutoka kwa mtu aliyekuwa akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa MWalimu Nyerere kwa kumtishia kwa panga muibia na kufanikiwa kupora kamera hiyo na kut oweka nayo..

Hivyo askari hao walifanikiwa kukamata waharifu hao na katika harakati za kupambana nao ndipo mtoto huyo alijeruhiwa maeneo yake ya tumboni kwa kuwa kulikuwa na mpambano mkali akti ya skari na waharifu hao kwa kufytua risasi kati yao

Hivyo katika harakati hiyo mtoto huyo aliweza kujeruhiwa na amechukuliwa na kukimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na hali yake kudaiwa inaendela vizuri.

Misime alisema, hakuna askari yeyote anayeshikiliwa katika tukio hilo kwa kuwa ajali hiyo imetokea kwa bahati mbaya

No comments:

Post a Comment