KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, October 28, 2010

Msalaba Mwekundu kutoa huduma ya kwanza siku ya uchaguzi.KATIKA hali ya kuonekana serikali imejipanga vizuri katika harakati za uchaguzi mkuu, Chama cha Msalaba Mwekundu[RedCross] kimeandaliwa kuhakikisha kinatoa huduma ya kwanza ya dharura kwa wapiga kura katika vituo vyote siku ya uchaguzi Oktoba 31,
Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Mayasa Mikidadi.

Mikidadi alisema kuwa, chama hicho kimejiandaa vya kutosha kutoa huduma ya kwanza ya dharura siku ya uchaguzi kwa wapiga kura katika vituo vyote kwa kuwa siku hiyo huwa na mlundikanao wa watu wengi mahala pamoja..

“Tutasaidia watu watakaokuwa wamezidiwa katika foleni, ambao wengine wana BP, na magonjwa mengine ambayo yatawafanya wakose amani, wagonjwa kuwasaidia”

No comments:

Post a Comment