KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, October 28, 2010

Lipumba leo ITVLEO kituo cha luninga cha ITV kinatarajia kurusha mdahalo wa moja kwa moja utakaofanya wananchi kuuliza maswali ya moja kwa moja kwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.
Mdahalo unatarajia kuwa wa masaa mawili ambapo utaanza majira ya saa 1 hadi saa 3 usiku na utarushwa moja kwa moja kutokea katika Hotel ya MovenPick ya jijini Dar es Salaam.

Mgombea huyo atapata fursa ya kumwaga sera zake aktika ungwe ya lala salama na wageni waalikwa walioko ukumbini hapo watapata fursa ya kuuliza maswali ya papo kwa hapo kuhusiana na uchaguzi mkuu.

Hivyo Lipumba atatumia nafasi hiyo kueleza sera zake na malengo yake kwa ujumla na endapo akipata ridhaa kupata urais atawafanyia nini watanzania na serikali yake.

Imedaiwa kuwa, Profesa Lipumba, atafunga kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani kesho, na atapata fursa ya kukutana na wananchi katika mkutano maalumu utakaofanyika leo kwenye Hoteli ya Landmark, Ubungo jijini hapa kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:30 mchana na baadae usiku atakwua MovenPick

No comments:

Post a Comment