KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, November 27, 2010
Daladala kutishia kugoma Ijumaa
CHAMA cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), umetishia kufanya mgomo wa kutoa huduma hiyo ifikapo Ijumaa ya wiki hii endapo utaratibu wa kukamata na kuzishikilia daladala hizo isivyo halali hautasitishwa mara moja.
Hayo yalithibitishwa jana na Mwenyekiti wa Darcoboa, Bw. Sabri Mabruk jijini Dar es Salaam.
Alisema mgomo huo utakuwepo endapo askari wa barabarani wataendelea na utaratibu wa kukamata gari hizo isivyo halali na kusumbua wamiliki wa gari hizo na kuchukulia utaratibu huo ni ukandamizaji.
Alisema, trafiki wamekuwa wakikamata daladala mbalimbali na kuzipeleka kwenye ofisi za Wakala wa Umeme na Ufundi (Temesa), badala ya kituo cha polisi.
Hata hivyo aliendelea kulalamika kuwa, askari hao wamekuwa wakisumbua wamiliki hao na kuwapeleka Tamesa na kukuta madeni ya makosa tofauti yaliyofanyika nyuma na kutotambua makosa hayo uliyafanya lini na kwa kipoindi gani kwa kuwa huko unakuta namba ya gari iliyofanyakosan hilo bila kutambua.
Hivyo alisema vitendo hivyo vimeanza muda mrefu na kuvimezea mate na sasa kuonekana kuota mizizi kwa kuwa gari likikamatwa huchukua hata siku nne halijatoka na wao kukosa vipato vyao vya kila siku
Wamilika hao waliongeza kuwa utaratibu huo hawakubaliani nao kwa kuwa hauonyeshi vithibitisho ya makosa hayo na kuwakosesha uhuru
Daladala kutishia kugoma Ijumaa
CHAMA cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), umetishia kufanya mgomo wa kutoa huduma hiyo ifikapo Ijumaa ya wiki hii endapo utaratibu wa kukamata na kuzishikilia daladala hizo isivyo halali hautasitishwa mara moja.
Hayo yalithibitishwa jana na Mwenyekiti wa Darcoboa, Bw. Sabri Mabruk jijini Dar es Salaam.
Alisema mgomo huo utakuwepo endapo askari wa barabarani wataendelea na utaratibu wa kukamata gari hizo isivyo halali na kusumbua wamiliki wa gari hizo na kuchukulia utaratibu huo ni ukandamizaji.
Alisema, trafiki wamekuwa wakikamata daladala mbalimbali na kuzipeleka kwenye ofisi za Wakala wa Umeme na Ufundi (Temesa), badala ya kituo cha polisi.
Hata hivyo aliendelea kulalamika kuwa, askari hao wamekuwa wakisumbua wamiliki hao na kuwapeleka Tamesa na kukuta madeni ya makosa tofauti yaliyofanyika nyuma na kutotambua makosa hayo uliyafanya lini na kwa kipoindi gani kwa kuwa huko unakuta namba ya gari iliyofanyakosan hilo bila kutambua.
Hivyo alisema vitendo hivyo vimeanza muda mrefu na kuvimezea mate na sasa kuonekana kuota mizizi kwa kuwa gari likikamatwa huchukua hata siku nne halijatoka na wao kukosa vipato vyao vya kila siku
Wamilika hao waliongeza kuwa utaratibu huo hawakubaliani nao kwa kuwa hauonyeshi vithibitisho ya makosa hayo na kuwakosesha uhuru
Mgomo baridi ustawi wa jamii
NI SIKU kadhaa saa toka kuanze kwa migogoro ndani ya chuo hicho na jana kupelekea wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii cha jijini Dar es Salaam kufanya mgomo baridi wakidai marekebisho ya mambo mbalmbali chuoni hapo.
Uanzishwaji wa mgomo huo ulitokana na Madai ya huduma mbovu za vyoo na mfumo wa utumiaji wa hosteli za chuoni hapo urekebishwe.
Madai mengine yakiwemo na kutoridhika na uongozi wa sasa chuoni hapo, ikiwemo na wanafunzi wenzao wapatao 400 hawajapatiwa udahili.
Kufuatia mgomo huo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alifika chuoni hapo majira ya mchana na kukutana na uongozi wa chuo hicho huku wanafunzi wakiwa wamebeba mabango mbalimbali yenye ujumbe tofauti tofauti.
Serikali hiyo ya wanafunzi chuo hapo ilisema kuwa wamejipanga kwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kukutana na Waziri wa Afya, kutafuta muafaka kuhusiana na chuo hicho.
Pia walisema, matatizo chuoni hapo yanatokana na ucheleweshaji wa kuundwa kwa bodi na waliipa serikali muda wa wiki moja kutatatua matatizo hayo
Za mwizi arubaini
MWANAUME mmoja [45] [jina kapuni] mkazi wa Sinza, amejikuta akihaha huku na huku kurudisha amani katika ndoa yake baada ya kufumaniwa akiwa na msichana wa kazi bafuni wakika uroda.
Hayo yametokea juzi, majira ya alfajiri, ndani ya nyumba yake hiyo kumshinikiza msichana huyo amfate bafuni.
Ilidaiwa kuwa, mwanaume huyo alikuwa akimvizia msichana huyo aliyetambulika kwa jina moja la Lucy pindi mke wake anapokuwa akiingia zamu ya usiku kutokana na kazi yake anayoifanya.
Ilidaiwa siku ya tukio mwanamke huyo aliaga anakwenda kazini lakini njiani alipata simu iliyomtaka na kumuomba asiende muda huo k wa kuwa alimuomba amshikie zamu hiyo na yeye aingie zamu yake.
Ilidaiwa mwanamke huyo, alipopata simu hiyo ilibidi arudi nyumbani kwa muda na ajitayarishe kwa kuingia kazini jioni.
Mume huyo ilidaiwa, wakati mke wake anatoka alikuwa yu kitandani lakini alishangazwa alipoingia chumbani kwake hakumkuta mumewe huyo na alishangaa na kwenda kumuuliza msichana na huko pia hakukuta mtu na ndipo alipoanza kumuuita msichana huyo.
Kabla binti huyo hajaitikia, mwanamake alikwenda kumuangalia binti huyo bafuni labla atkuwa amekwenda kuoga lakini alichokiona huko ni nusu ya kuzimia na kumkuta mumewe akiwa na binti huyo na mwanamke huyo kuwaacha waendelee na shughuli yao hiyo.
HAta hivyo chanzo cha habari hii kilidai kuwa, mwanamke huyo huwa ana shida sana ya kukaa na wasichana wake wa kazi kwa kuwa wasichana hao wanapokuwa wamepata kukaa zaidi ya mwezi huwa wanamtaka mwanbamke huyo awarudishe nyumbani kwao na alikuwa haelewi tatizo lilikuwa wapi.
Ilidawa mwanamke huyo ana mtoto wa mwaka mmoja sasa na toka ajifungue mtoto huyo, inadaiwa alishabadilsha wasichana wa kazi zaidi ya mara tatu kw kuwa wasichana hao walikuwa hawawezi kukaa humo kwa sababu ambayo alikuwa hajaielewa.
Hivyo mwanamke huyo alichofanya ni kwenda chumbani kumchukua mwanae na kumbeba na kuchukua nguo mbili tatu na kuondoka kwenda nyumbani kwao maeneo ya Boko akapumzike huko.
Imedaiwa mwanaume huyo alikuwa hajui aanzie wapi na kuona aibu kumuoimba mradhi mke wake huyo kutokana na kiitendo hicho alichomfanyia mke wake.
Kwa muendelezo zaidi juu ya kisa hiki endelea kusoma mtandano huu kwakuhabalishwa zaidi kinachoendelea
Waziri atoa ushuhuda alivyorubuniwa na fatak
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Luoga Hovisa jana alitoas ushuhuda wa kusikitisha wa maisha yake katika kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), alipoeleza kuwa alipewa uja uzito na 'Fataki' wakati akisoma Chuo Kikuu.
Waziri Luoga alilazimika kushirikisha vijana hao kuhusu maisha yake kutaka kuwaonyesha alivyomudu kuvumilia na kupambana na maisha hadi kufikia mafanikio aliyoyapata sasa, akisema badala yake sasa anaweza "kuchakachua" hadi wanaume watano lakini "haoni sababu" na kuwataka wanafunzi kuepuka watu wenye tabia za kifataki kwa kuwa wanaweza kuwaharibia mwelekeo wa maisha.
Fataki ni jina maarufu waliopachikwa wanaume ambao wana tabia ya kufuata mabinti wadogo na kuwatelekeza baada ya kuwaharibia maisha kwa kuwapa mimba. Waziri Luoga alieleza jinsi alivyokutana na mwanamume huyo ambaye alimpa uja uzito, lakini akaongeza kuwa baadaye mtu huyo alimsomesha na hivyo kumaliza vizuri masomo. "Sio kwamba muige mfano nilioutoa," alisema Waziri Luoga akiwaambia wanafunzi hao. "Si kwamba na nyie kama wanafunzi mkayafanye haya, la asha! Badala yake ninawapa changamoto kwamba katika maisha silaha mnayopaswa kuing’angania ni elimu peke yake na si vibaka wa mitaani," alisema Dk Luoga. “Acheni kudanganywa na mafataki ambao ni matapeli na ambao huweza kuwapotezea dira ya maisha, badala yake msome kwa bidii, kwa ajili ya mafanikio ya maisha yenu.” Dk Luoga alisema kuwa vijana wengi, hasa wanafunzi wamekuwa wakirubuniwa kutokana na kushindwa kustahimili tamaa za maisha na kuamua kujiingiza kwa vijana wa mitaani ambao aliwaelezea kuwa hawana sera.
Waziri huyo, ambaye ni sura mpya katika baraza lililoundwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, alikumbushia taaluma yake ya ualimu kwa kutumia kalamu na kuwafundisha washiriki wa kongamano hilo masuala ya maisha na athari za ukimwi kwa vijana, huku akijitangza kuwa naye ni mtoto wa mkulima. “Ni bora kuacha kabisa na kuamua kusubiri kwani kwa kuwa mahusiano katika masomo ni hatari... badala yake mzidi kumuomba Mungu na kuwa waadilifu,” alisisitiza “Leo hii, ninamshukulu Mungu kwa Elimu aliyonipa kwa sababu alinijua mimi ni mtoto wa mkulima, hivyo niliamua kutochezea maisha yangu kiholela. "Hapa unavyoniona, kama waziri nina fedha za kutosha; gari la kifahari ninalo ehe! Unadhani nikitaka kuwa na mafataki hata watano, nitashindwa?" “Nikiamua kuchakachua wanaume hata watano, naweza kwa sababu uwezo ninao na fedha ninayo.
Lakini sioni faida yeyote badala yake ni kujitumbikiza mahali ambapo ni hatari zaidi,” alisema. “Cha msingi hapa ni kuhakikisha mnajenga maadili mema mnapokuwa shuleni na nyumbani ili kuepuka kurubuniwa na kupoteza mwelekeo wa elimu mliopata.” Naye mtaalamu wa ushauri wa afya katika kamati ya vijana, Dk Telesphoy Kyaruzi alisema tatizo kubwa linalowapelekea vijana wengi kujiingiza katika ngono zembe na kupata maambukizi ni uchumi mbovu. Dk Kyaruzi alisema kwa kuliona hilo, wanaiomba serikali kuhakikisha inatoa mikopo kwa vijana ili kuwasaidia waweze kujiendesha na kuepuka vishawishi
Prof Tibaijuka atangaza vita na wenye pesa Ardhi
Nora Damian
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ametangaza vita dhidi ya wanaotumia jeuri ya pesa kupora viwanja wakati akiweka hadharani mikakati yake kwenye wizara hiyo iliyojaa migogoro ya ardhi.
Profesa Tibaijuka, mmoja wa mawaziri 24 wapya walioingia kwenye Baraza la Mawaziri, alikuwa akiweka aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumzia mikakati yake kwenye wizara hiyo.
Wizara hiyo ni moja ya wizara zilizo na tuhuma nyingi za ufisadi kutokana na maofisa wake kusaidia kufanikisha uporaji viwanja, uuzwaji wa maeneo ya wazi, ubadilishaji wa matumizi ya viwanja kwa lengo la kunufaisha mafisadi na kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika kuhudumia wananchi.
Lakini Tibaijuka, ambaye anakuwa waziri wa pili kutangaza mikakati yake baada ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, alisema atapambana na watu wenye fedha ambao wanasababisha migogoro ya viwanja kwenye wizara yake.
Prof Tibaijuka, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawata) lililopigwa marufuku nchini kabla ya kurejeshwa kwa hukumu ya mahakama, alisema watu wenye jeuri ya pesa wamekuwa wakisababisha migogoro katika sekta hiyo kutokana na kupora viwanja vikiwemo vya wazi na vile vilivyotengwa kwa ajili ya huduma za jamii.
“Kama kuna mtu amepora kiwanja, bora akisalimishe angalau tutaongee yaishe kabla hatujamchukulia hatua,” alisema Prof Tibaijuka.
Tibaijuka, ambaye alikuwa mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UNHabitat), aliongeza kusema: “Kama mtu akileta jeuri ya pesa, sisi wengine hizi za chakula zinatutosha hivyo hatubabaiki sana.”
Alisema atapambana na migogoro hiyo kwa kutumia sheria kwa sababu bila utawala wa sheria, maendeleo yatakuwa magumu.
Alisema mbali ya kufanya kazi na wizara na wataalamu mbalimbali, pia atafanya kazi na wananchi ili wamsaidie.
Alisema wako watu wachache ambao hawatambui kama ardhi ni muhimu kuliko fedha na kwamba atahakikisha haki inatendeka na kwamba hakutakuwa na tabia ya kuzungusha wananchi katika mazingira ambayo mtu ana haki ya kupewa kiwanja.
Waziri huyo ametoa tamko hilo wakati wizara yake ikikabiliwa na tuhuma nyingi za uuzaji viwanja kiholela unaofanywa na watendaji kwenye ngazi za wilaya, ikiwa ni pamoja na uuzwaji wa viwanja vya wazi na maeneo ya fukwe za bahari na kubadilisha matumizi ya viwanja kwa lengo la kunufaisha wachache.
Tibaijuka, ambaye ni mbunge wa Muleba Mashariki, alisema pia atarudisha ajira ya walinzi wa ardhi ili kumaliza migogoro katika sekta hiyo kwa masuala ya ardhi yasipofanyiwa kazi, sekta nyingine zinaweza kudorora kwa kuwa Sekta ya Ardhi inabeba nyingine zote.
“Migogoro ya ardhi tunaiunda wenyewe kwa hiyo wakati mwingine hatuhitaji pesa yoyote kuimaliza. Tutarudisha walinzi wa ardhi kwa sababu ni kada ya watumishi ambayo ilipotea na imetugharimu sana,” alisema.
Alisema pia katika uongozi wake atahakikisha anailinda miji kwa sababu mingi haiko katika hali inayotakiwa kutokana na kuwepo kwa tatizo la ukuaji na ujenzi holela.
“Kazi hii nimeifanya takribani miaka 10, lakini sasa mtazamo wangu unabadilika kutoka ngazi ya kimataifa na ninajikita katika utekelezaji kwenye ngazi ya taifa langu, hivyo hatutalala,” alisema.
Waziri huyo aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano wanapoona mambo mbalimbali yanaenda kinyume na kwamba katika tovuti ya wizara hiyo itawekwa nafasi maalumu ya watu kutoa kero yake.
Naye Katibu Mkuu Patrick Rutabanzibwa alisema kuwa tayari ameanza kupangua watu kwenye wizara hiyo ili kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma.
Alisema kati ya watumishi waliohamishwa, baadhi wanahusika na uuzwaji holela wa maeneo ya wazi jijini Dar es Salaam na kwamba amewalazimisha watumishi wengine waliopora viwanja wavirudishe
Hali tete Ivory Coast baada uchaguzi
Wafuasi wa upizani wanasema Rais Gbagbo hataki kuondoka mamlakani
Vurugu zimetokea katika makao makuu ya tume ya uchaguzi nchini Ivory Coast, baada ya wafuasi wa Rais Laurent Gbabgo kupinga kutangazwa kwa matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi.
Mfuasi sugu wa Rais Gbabgo ambaye pia anahudumu kwenye tume ya uchaguzi, alizua utata pale alipochana karatasi iliokuwa na matokeo ya awali, akidai kuwa hayakuwa sahihi.
Vurugu hizo zimetokea huku wasiwasi ukitanda mjini Abidjan, siku ya tatu baada ya duru ya pili ya uchaguzi kufanyika.
Rais Gbabgo anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa aliyekuwa Waziri mkuu Alassane Ouattara.
Wafuasi wa Bw Ouattara wanadai kuwa Rais Gbabgo anataka kulazimisha utawala wake kwa kuzuia kutangazwa kwa matokeo hayo na wanaamini kuwa wameshinda uchaguzi huo.
Uchaguzi huo umelenga kuunganisha nchi hiyo iliogawanyika kwa pande mbili, kusini na kaskazini baada ya vita kutokea mwaka wa 2002.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton, amewataka viongozi hao waheshimu matokeo ya uchaguzi na walinde amani kwenye nchi ambayo inazalisha zao kubwa zaidi la kakao duniani
Wakazi Mogadishu hawawataki Al Shabaab
Maandamano ya kupinga kundi la Al Shabaab
Matokeo ya utafiti wa kura ya maoni iliofanywa mjini Mogadishu, kwa niaba ya BBC, yamebainisha robo tatu ya wakaazi wa mji huo, hawataki wapiganaji wa kundi la Kiislamu wa Al Shabaab, kutwaa uongozi wa Somalia.
Uchunguzi huo umeonesha wengi wa wakaazi wa Mogadishu wanaamini kuwa kundi la Al Shabaab ni la kigaidi.
Wengi wao wahisi kundi hilo ni la upinzani. Asilimia hamsini ya wakaazi wa mji wa Mogadishu wanasema jamii ya kimataifa imelipuuza taifa lao ambalo halijawa na serikali kwa karibu miaka ishirini.
Utafiti huo umeendelea kuonesha asilimia tisini na mbili ya wakaazi wa mji huo hawana uwezo wa kukidhi mahitaji muhimu na ya kimsingi kama chakula na ulifanywa katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo la Al Shabaab
Korea Kusini yafuta mazoezi ya kijeshi
Serikali ya Korea Kusini imetangaza kufutiliwa mbali mazoezi ya kijeshi ambayo yangehusisha matumizi wa silaha, katika kisiwa kilichoshambuliwa na wanajeshi wa Korea Kaskazini wiki iliyopita.
Korea Kusini yafuta mazoezi ya kijeshi
Jeshi la nchi hiyo limesema mazoezi hayo ni sehemu ya mazoezi ya pamoja yanayoendelea kati ya nchi hiyo na Marekani.
Hata hivyo hakuna sababu yoyote iliyotolewa kuhusu sababu zilizosababisha harakati hizo za mazoezi ya kijeshi zifutiliwe mbali.
Utawala wa Korea Kaskazini umesema mazoezi hayo yanayohusisha ufyatuaji risasi yalichochea uamuzi wake wa kushambulia kisiwa cha Yeonpyeong island siku ya jumanne wiki iliyopita.
Rais wa Korea Kusini, Lee Myungt Bak amesema atakabiliana vikali na serikali ya Korea Kaskazini endapo itajaribu kufanya mashambulio kama hayo
Wikileaks yafichua siri za Marekani
Mjumbe mmoja wa baraza la Congress amependekeza Wikileaks iorodheshwe kama kundi la kigaidi
Tovuti ya Wikileaks, maarufu kwa kutetea sera za uwazi, imeanza kuchapisha mawasiliano ya siri kati ya balozi za Marekani kuhusu viongozi wakuu duniani.
Baadhi ya mawasiliano yaliochapishwa ni yale kati ya Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia na Marekani, pale alipopendekeza vikali kuwa Iran ishambuliwe kijeshi.
Serikali ya Marekani imekashifu hatua hiyo ya kuchapisha mawasiliano hayo. Imesema kuwa kitendo hicho kinahatarisha maisha na mabalozi wake.
Lakini mwanzilishi wa tovuti ya Wikileaks Jullian Assange, anasema serikali ya Marekani haitaki kuwajibishwa.
Wikileaks imechapisha nakala mia mbili kati ya zaidi ya laki mbili ilizonazo ya mawasiliano hayo. Hata hivyo nyaraka zote hizo zimesambazwa kwa magazeti kama vile New York Times la Marekani na The Guardian la Uingereza.
Masuala yalioangaziwa zaidi kwenye mawasiliano hayo ni mpango wa nuklia wa Iran, ufisadi katika serikali ya Afghanistan na uhusiano kati ya serikali ya Urusi na genge la mafia.
Amri ya waziri wa mambo ya nje wa marekani Hilary Clinton kuwa vigogo wa Umoja wa Mataifa akiwemo katibu mkuu achunguzwe pia imechapishwa
Tovuti ya Wikileaks, maarufu kwa kutetea sera za uwazi, imeanza kuchapisha mawasiliano ya siri kati ya balozi za Marekani kuhusu viongozi wakuu duniani.
Baadhi ya mawasiliano yaliochapishwa ni yale kati ya Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia na Marekani, pale alipopendekeza vikali kuwa Iran ishambuliwe kijeshi.
Serikali ya Marekani imekashifu hatua hiyo ya kuchapisha mawasiliano hayo. Imesema kuwa kitendo hicho kinahatarisha maisha na mabalozi wake.
Lakini mwanzilishi wa tovuti ya Wikileaks Jullian Assange, anasema serikali ya Marekani haitaki kuwajibishwa.
Wikileaks imechapisha nakala mia mbili kati ya zaidi ya laki mbili ilizonazo ya mawasiliano hayo. Hata hivyo nyaraka zote hizo zimesambazwa kwa magazeti kama vile New York Times la Marekani na The Guardian la Uingereza.
Masuala yalioangaziwa zaidi kwenye mawasiliano hayo ni mpango wa nuklia wa Iran, ufisadi katika serikali ya Afghanistan na uhusiano kati ya serikali ya Urusi na genge la mafia.
Amri ya waziri wa mambo ya nje wa marekani Hilary Clinton kuwa vigogo wa Umoja wa Mataifa akiwemo katibu mkuu achunguzwe pia imechapishwa
Pakistan wakanusha madai ya Wikileaks
Ripoti ya Wikileaks
Wizara ya Mambo ya Nje nchini Pakistan imekanusha madai kuwa Marekani inahusika na shughuli ya kusafirisha madini yaliyorotubishwa ya uranium kutoka katika viwanda vyake vya Nukilia.
Msemaji wa wizara hiyo ameiambia BBC, habari hizo zilijitokeza kwenye nyaraka zilizochapishwa na mtandao wa Wikileaks.
Nyaraka hizo zimeonyesha matamshi yaliyotolewa na mfalme Abdullah wa Saudi Arabi kuhusu Rais wa nchi hiyo Asif Zardari
Kinara wa mihadarati Mexico akiri kuua
Mapambano ya polisi na genge la wauza dawa za kulevya
Polisi nchini Mexico wamesema kiongozi wa genge moja la wauzaji mihadarati mjini Ciudad Juarez, anayezuiliwa na polisi amekiri kuidhinisha mauaji ya watu wengi katika eneo hilo mwaka mmoja uliopita.
Arturo Gallegos Castrellon alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita pamoja na viongozi wengine wawili wanaoshukiwa kuwa wa genge lake.
Makao makuu ya polisi yamesema miongoni mwa mauaji aliyokiri ni pamoja na kupigwa risasi kwa mama mmoja mja mzito aliyekuwa akifanya kazi katika ubalozi wa Marekani mjini Ciudad Juarez na pia shambulio la sherehe moja lililosababisha vifo vya watu kumi na watano wengi wao wakiwa vijana.
Hata hivyo madai hayo ya Castrellon hayajathibitishwa rasmi
Polisi nchini Mexico wamesema kiongozi wa genge moja la wauzaji mihadarati mjini Ciudad Juarez, anayezuiliwa na polisi amekiri kuidhinisha mauaji ya watu wengi katika eneo hilo mwaka mmoja uliopita.
Arturo Gallegos Castrellon alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita pamoja na viongozi wengine wawili wanaoshukiwa kuwa wa genge lake.
Makao makuu ya polisi yamesema miongoni mwa mauaji aliyokiri ni pamoja na kupigwa risasi kwa mama mmoja mja mzito aliyekuwa akifanya kazi katika ubalozi wa Marekani mjini Ciudad Juarez na pia shambulio la sherehe moja lililosababisha vifo vya watu kumi na watano wengi wao wakiwa vijana.
Hata hivyo madai hayo ya Castrellon hayajathibitishwa rasmi
Waziri Mkuu wa Kenya alaani mashoga
Wanaharakati wa kutetea wapenzi wa jinsia moja wanasema kauli hiyo huenda ikachochea mashambulizi dhidi yao
Waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga amesema nchi hiyo haipo tayari kuwatambua wapenzi wa jinsia moja.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la bunge mjini Nairobi, Bw Odinga alisema suala la wapenzi wa jinsia moja lilitumiwa kama propaganda kupinga katiba mpya.
Waziri Mkuu huyo amesisitiza katiba mpya ya Kenya haikubali kuwepo wapenzi wa jinsia moja. Na amependekeza wapenzi hao wa jinsia moja wakamatwe na polisi endapo watajitokeza hadharani.
Lakini kauli hiyo imepingwa na David Kuria, mwanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja.
Bw Kuria ameiambia BBC kuwa kauli hiyo itaathiri kampeni zao za kutetea haki sawa za huduma ya afya kwa watu hao, hasa kuhusu suala la kudhibiti maambukizi ya Ukimwi
Nyota wa Sinema Amuua Mama Yake Akidai ni Shetani
Nyota wa filamu wa Marekani amemuua mama yake kwa kumkata vipande vipande kwa kutumia jambia akidai kuwa alitumwa na mungu amuue shetani aliyekuwa ndani ya mwili wa mama yake.
Michael Brea mwenye umri wa miaka 31, nyota wa filamu ya "Step Up 3D" na tamthilia maarufu ya "Ugly Betty" ametupwa rumande akisubiria hukumu yake kwa kumuua mama yake kwa jambia.
"Sikumuua yeye, nimemuua shetani aliyekuwa ndani ya mwili wake", alisema Brea alipokuwa akiongea na gazeti la New York Daily News akiwa kwenye wadi ya hospitali ya jela ambako aliwekwa tangu alipotiwa mbaroni kwa kosa la mauaji.
"Niliendelea kumkatakata vipande vipande na hakuna mtu aliyeweza kunizuia. Nilikuwa nikifanya kazi ya mungu", aliendelea kusema Brea.
Kwenye majira ya saa saba na nusu usiku siku ya jumanne majirani walisikia kelele Brea akimwambia mama yake "Tubia tubia" huku akimsomea mistari ya biblia.
Majirani walisema kuwa Brea alikuwa akimkimbiza mama yake nyumba nzima huku akimlazimisha atubie.
Majirani waliita polisi ambao walipofika walikuta tayari Brea ameishamchinja mama yake.
Maiti ya mama yake, Yanick Brea, 55, ilikutwa bafuni ndani ya nyumba yake iliyopo Brooklyn, taarifa ya polisi ilisema.
Brea, alikutwa na polisi akiwa amekaa chumbani huku ameshikilia jambia lenye urefu wa futi tatu.
Ndugu wa marehemu wametoa taarifa ya kuonyesha kumtetea Brea ambaye wamesema alikuwa ni mwanaume mpole, mwenye huruma na mwenye mapenzi kwa mama yake lakini alikuwa akihitaji msaada kwa matatizo yaliyokuwa yakimkabili.
"Familia yake na marafiki zake wanajua fika kuwa Michael hakuwa akijitambua wakati alipokuwa akimuua mama yake", ilisema taarifa ya familia ya Brea
China yatoa pendekezo mzozo wa Korea
Huku mvutano ukiendelea baina ya Korea Kaskazini na Kusini, China imetoa wito kufanyike mazungumzo ya dharura, baina ya mataifa sita yaliyohusika na upatanishi katika mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini.
China yavalia njuga kumaliza mzozo wa Korea
Afisa mmoja wa China, aliwaambia waandishi wa habari mjini Beijing, kwamba China ina wasiwasi mkubwa kuhusu yaliyotokea hivi karibuni katika Rasi ya Korea na inataka mataifa sita, Marekani, Urusi, Japani, China yenyewe na Korea mbili, yakutane mwanzo wa mwezi ujao.
Lakini Korea Kusini imesema huu si wakati wa kurejea tena kwenye mazungumzo ya pande hizo sita
Obama Achanika Mdomo Baada ya Kupigwa 'Kipepsi'
Rais wa Marekani, Barack Obama ameshonwa nyuzi 12 kwenye mdomo wake baada ya kupigwa kiwiko kwenye mdomo wake wakati akicheza mpira wa kikapu pamoja na ndugu na jamaa zake wa karibu.
Obama alikuwa akicheza mpira wa kikapu pamoja na ndugu na jamaa kwenye kambi ya jeshi la Marekani ya Fort McNair mjini Washington, wakati kwa bahati mbaya mcheza wa timu pinzani aliporusha kiwiko chake na kumtandika Obama mdomoni.
Msemaji wa ikulu ya Marekani alisema kuwa Obama alipasuka mdomo na alipatiwa matibabu na madaktari wa ikulu.
Hata hivyo taarifa ya ikulu ya Marekani haikusema ni nani ndiye aliyempasua Obama mdomo wake kwa kiwiko
Maalim Seif 'aiteka' Pemba
Salma Said, Zanzibar
WANANCHI mbali mbali wa Kisiwani Pemba, wamejitokeza kwa wingi kumlaki Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye kwa mara ya kwanza amefanya ziara yake kisiwani humo tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo mapema mwezi huu.
Uteuzi huo ulifanywa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.
Kuwasili kwa Maalim Seif katika kisiwa hicho alichozaliwa na ambayo ni sehemu ya Zanzibar, kuliwavutia mamia ya wananchi ambao walijitokeza kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Karume.
Wananchi hao walikuwa wamejipanga barabarani kama ishara ya kumuunga mkono kiongozi huyo ambaye sasa yuko katika serikali ya umoja wa kitaifa.
Pamoja na wananchi, pia kulikuwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa kisiasa waliomlaki Maalim Seif ambaye baadaye, alipanda gari lake katika viwanja vya Tibirinzi ambako alifanya mkutano wa hadhara.
Katika viwanja hivyo, ngoma mbali mbali na burudani za kiasili , zilitawala kuashiria furaha ya wananchi wa Pemba kwa Maalim Seif.
Katibu wa Vijana wa Chama cha CUF, Khalifa Mohammed alisoma risala iliyowahimiza wananchi wote wa Unguja na Pemba, kuungana na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kuleta maendeleo nchini.
Katika uwanja wa ndege, baadhi ya wananchi walisema hawaamini kwamba Maalim Seif angepokelewa na viongozi wa serikali huku akiongozwa na magari ya polisi, ili kuimarisha usalama wake.
"Nimekuja si kumuona Maalim Seif , lakini kujionea mwenyewe kama kweli anaongozwa na vimulimuli, ni kweli anafuatwa na walinzi, nilitaka nijionee mwenyewe," alisema Salim Said Kombo.
Idadi kubwa ya watu waliojitokeza kumpokea Makamu wa Kwanza wa Rais, walikuwa wamevalia mavazi yenye rangi zinazoitambulisha CUF na wengine walikuwa wamevaa fulana na kanga za CCM, kama ilivyokuwa juzi katika Uwanja wa Kibanda Maiti, mjini Unguja.
Akizungumza na wananchi, Maalim Seif aliwashukuru kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa salama na kwamba kwamba uhusiano wake na viongozi wenzake wa serikali ni nzuri.
Alisema chini ya serikali ya umoja kitaifa, watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Rais wake na pamoja na Makamu wa Pili wa Rais.
Alisema kwa msingi huo, wananchi wa Zanzibar, lazima watarajie maendeleo makubwa yatakayotokana na ushirikiano huo katika kutekeleza majukumu ya serikali.
Maalim Seif alisema yeye, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd watafanya kazi pamoja na kamwe hawatatoa nafasi kwa waovu, kuwavuruga.
Aliwahakikishia wananchi kuwa umoja na ushirikiano wao katika serikali, ndio utakaoleta mabadiliko ya haraka katika kuiendeleza Zanzibar .
Makamu wa Kwanza wa Rais, alisema katu hawatakubali kuwarejesha Wazanzibari katika siasa za chuki na uhasama na kwamba sasa ni wakati wa wananchi bila ya kujali tofauti zao za kisiasa, kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuiunga mkono serikali yao.
"Nakuhakikishieni mimi na rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd , ni kitu kimoja tumeshikamana sana na katu hatugawanyiki, Inshallah hatutoi nafasi kwa kidudu mtu kutugawa," alisisitiza.
Katika mkutano huo, Maalim Seif pia aliwatambulisha baadhi ya mawaziri walioteuliwa na Rais Dk Shein wakiwemo wale wa chama cha CUF na kuwataka wananchi wawaunge mkono na kuwapa ushirikiano mkubwa.
Katika hotuba yake, alisisitiza kuwa kampeni za kistaarabu bila ya kuingiza matusi, chuki na jazba, zimesaidia kwa kiasi kikubwa,kupunguza matatizo yaliyokuwa yamezoeleka katika siasa za Zanzibar.
“Faida ya kampeni za kistaarabu tumeziona na leo hii tunakaa pamoja na kushauriana laiti tungefanya kampeni za kutukanana na kufanyiana chuki basi tungechukua zaidi ya miezi mitatu mimi na Dk Shein tungegombana," alisema.
Alisema urithi nzuri wa kuwepo kwa amani na utulivu ulioachwa na rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, unahitaji kuendelezwa na kila Mzanzibari, ili kuiletea nchi maendeleo na matumaini makubwa.
Pia alisema chini ya mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa, Zanzibar ni nchi isiyokuwa na Serikali ya Mapinduzi kama ilivyokuwa awali.
"Serikali ya sasa ina Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu wa Pili wa Rais na tunafanya kazi kwa maslahi ya wananchi wote wa Zanzibar,” alisema Maalim Seif.
Kiongozi huyo pia aliahidi kusimamia nidhamu na uadilifu wa viongozi wa serikali ili matarajio ya wananchi yafikiwe .
Wakizungumza katika mkutano huo wakati wa kujitambulisha mawaziri wanane na manaibu wawili walioteuliwa kutoka chama cha CUF waliahidi kuwatumikia wananchi wote wa Zanzibar bila ya ubaguzi
Magufuli aanza kazi kwa moto, aagiza wakandarasi wasiofaa wafukuzwe nc
NI SIKU moja toka Rais Kikwete kuwaapisha Mawaziri, Waziri wa Ujenzi,Dk. John Magufuli ameanza kazi rasmi jana na kuzungumza na watendaji wakuu wa wizara hiyo na kuwakabidhi ilani ya Chama cha Mapinduzi huku akitoa maagizo yake yatekelezwe mara moja
Waziri Magufuli aliwataka watendaji wakuu na wakuu wa idara katika wizara hiyo, kufanya kazi kwa bidii na atakayeonekana mzembe atafukuzwa kazi mara moja bila hata ya kuoneana aibu wala huruma.
Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na watendaji hao kuwataka wawe makini na wajiandae kufanya kazi kwani katika miaka mitatu ya mwanzo ni utekelezaji na miwili ya mwisho ni kukamilisha kazi zzote za wizara hiyo.
KAtika kiako hicho Magufuli alitaka wakandrasi wote wabobu kufukuzwa nchini hasa wale wanaochelewesha ujenzi wa barabara kama ya Mandela, uwanja wa ndegew a Songwe na kuwa kero kwa wananchi.
“Lazima wakandarasi hao waondoke na wafutiwe mkataba na hata wakikibmilia nchi jirani tutawasiliana na mawaziri wakuu wan chi hizo” alisiema Magufuli.
Pia Magufuli alishangaa ni kwanini ujenzi wa daraja la Kigamboni unacheleweshwa, hivyo aliagiza lijengwe haraka na kama Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wameshindwa kazi hiyo watoe ripoti haraka ili liweze kufanyiwa kazi.
Waziri MAgufuli ameahdidi kumaliza tatizo la msongamano wa magari barabarani kwani wizara hiyo itahakikisha watajenga barabara za angani (Flyovers).
Pia aliagiza kitengo cha ujenzi kuweka kivuko cha kuanzia Kivukoni hadi Tegeta ili kupunguza msongamano wa wananchi wanaokesha barabarani.
Pia alitoa mwezi mmoja kwa wale waliokopeshwa nyumba za serikali na hawajamaliza kulipa madeni hnayo, aliwataka waandikiwe barua za kutakiwa kumaliza madeni hayo na katika muda utakaowekwa wasiomaliza madeni wafukuzwe katika nyumba hizo kwani wataona wanabembelezwa na hawaoni wanafanya makosa kukalia nyumba hizo za serikali bila kuzilipia.
Pia Waziri Magufuli alishukuru kwa kupewa msaidizi wake, msoni Mwakyembe kwa kuwa ni mchapa kazi hodari wataweza kuiongoza vyeema wizara hiyo.
“Halafu nyinyi watendaji mmekalia majungu tu hapa wizarani, sasa miaka hii mitano ni yakufanya kazi, hakuna kuoneana aibu wala kuogopwa kurogwa” alimalizia Magufuli
Polisi wadhibiti mtaa wenye fujo Brazil
Polisi Brazil wadhibiti eneo lenye fujo
Wanajeshi wa Brazil wenye silaha nzito, wameuteka mtaa wa maskini wa Rio de Janeiro wenye fujo nyingi, ambako mamia ya wauza mihadarati walikuwa wamezingirwa kwa siku kadha.
Wanajeshi na polisi zaidi ya elfu mbili walianza shambulio lao alfajiri, katika mtaa wa Alemao mjini Rio, wakisaidiwa na helikopta na magari ya deraya.
Mapambano makali ya risasi yalisikika. Mwandishi wa BBC mjini Rio, alisema kazi inaendelea hivi sasa, ambapo askari wa usalama, wanafanya msako katika kila nyumba kuwatafuta wauza dawa za kulevya.
Tangu msako kuanza siku chache zilizopita, watu wapatao 45 wameuwawa na magari yanayofikia mia yameangamizwa
Mashangingi ya mawaziri yazua utata
Sadick Mtulya
WAKATI mawaziri na manaibu wawaziri wakikabidhiwa magari mapya, baada ya kuapishwa Jumamosi iliyopita, serikali imeibuka na kusema sio mapya ni ya zamani.
Kauli hiyo inaibua utata kutokana na kuwa baada ya kuapishwa viwanja vya Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, kila waziri alikabidhiwa dereva mpya na gari jipya aina ya Toyota GX V8,
badala ya gari aina ya Toyota VX V8 iliyokuwa ikitumiwa na mawaziri waliopita.
Ununuzi wa Toyota GX V8 mpya, unashiria serikali bado haijawa tayari kuunga mkono msimamo wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye amekuwa akisikika akitaka kusitishwa ununuzi wa magari ya kifahari ili kupunguza matumizi ndani ya serikali.
Toyota GX V8 moja huuzwa kati ya Sh210 milioni hadi Sh240 milioni, hukuToyota VX V8 moja inauzwa sio chini ya Sh180 milioni.
Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo, alisema magari hayo sio mapya na kwamba, yaliyotumiwa na mawaziri waliopita.
Rais Jakaya Kikwete ameigawanya iliyokuwa Wizara ya Miundombinu na kuwa wizara mbili; Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.
“Yale magari sio mapya, yalikuwepo. Kwanza uliyaona au unasema tu, hamjayachunguza vizuri jamani, fanyeni uchunguzi,’’ alisema Chambo na kukata simu.
Mawaziri wote na baadhi ya manaibu walikabidhiwa magari hayo (GX V8), huku manaibu wengine wakikabidhiwa VX V8.
Sababu ya baadhi ya manaibu mawaziri kukabidhiwa VX V8 badala ya GX V8, ni kutokana na kutokamilishwa kwa taratibu za kutokamilika.
Mmoja wa manaibu mawaziri (jina tunalo), alikabidhiwa VX V8 iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi, John Magufuli, ambaye sasa ni Waziri wa Ujenzi.
Gazeti moja la kila siku (si Mwananchi) limeeleza kuwa ununuzi wa magari hayo, umegharimu serikali Sh9.3 bilioni na kwamba, takwimu za iliyokuwa Wizara ya Miundombinu zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha wa 2005/06 magari makubwa ya kifahari yapatayo 6,000 yalikuwa yamenunuliwa na serikali kwa gharama inayokadiriwa kufikia Sh160 bilioni.
Miongoni mwa magari hayo ni Toyota Land Cruiser (VX/ GX V8, Prado) yapatayo 1,655, Nissan Patrol na Land Cruiser 885, Mitsubishi Pajero 400 na mengineyo.
Tangu kipindi cha serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kumekuwepo na mjadala kuhusu matumizi makubwa ya serikali hasa katika ununuzi wa magari ya kifahari kutokana na kuendeshwa kwa gharama kubwa.
Wadau wengi wanataka viongozi watumie magari ya kawaida kama ilivyo kwa nchi ya Kenya na Rwanda
Bashir kuhudhuria mkutano Afrika, Ulaya
Jenerali Omar al-Bashir
Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki ametangaza kuwa Rais wa Sudan, Jenerali Omar al-Bashir, anayetakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu, atahudhuria mkutano wa viongozi wa Africa na Ulaya utakaofanyika wiki hii.
Mkutano huo unafanyika nchini Libya ambayo si mwanachama wa ICC na kwa hivyo haiwajibiki kumkamata Rais Bashir.
Lakini waandishi wa habari wanasema kuhudhuria kwake kutasabisha tatizo la kidiplomasia kwa wawakilishi wa Muungano wa Ulaya ambao wana wajibu wa kutekeleza hati za kukamatwa kwa washukiwa zinazotolewa na mahakama hiyo
Mtoto azaliwa ubongo nje
MSHANGAO mkubwa umeibuka kwa madaktari na wauguzi wa hospitali ya wilaya ya Ulanga Morogoro baada ya mwanamke kujifungua mtoto ukiwa ubongo nje kwa kukosekana na ngozi ya kichwa mahala hapo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Amani Kombe, alitoa taarifa hiyo kwa wanahabari kuwa, mtoto huyo alizaliwa Novemba 22 mwaka huu, kwenye majira ya saa 3 usiku.
Dk. Kombe, alisema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika hospitali hiyo, na ksuema motto huyo alizaliwa na uzito wa kilo 2.9.
Kombe alisema kitaalamu mtoto anaweza kuzaliwa na matatizo hayo kutokana na kusababishwa na ukosefu wa madini tofauti kwa mama wakati wa ujauzito wake.
Hata hivyo katika kuthibitisha hilo, mama wa mtoto huyo, Bi. Silvia Lyombo (20) mkazi wa Ulanga alipohojiwa kujua wakati wa ujauzito wake alikuwa na hali gani, alijieleza kuwa hakuwahi kupata tatizo lolote la kiafya katika kipindi cha ujauzito wake na huo ulikuwa ujauzito wake wa kwanza.
Dk. Kombe alisema kuwa mtoto huyo wanamuhamishia katika hospitali ya Mkoa Morogoro kwa uchunguzi zaidi wa madaktari bingwa
Baba Amzalisha Binti Yake Watoto 10
Mwanaume mmoja wa nchini Argentina huenda akahukumiwa kwenda jela miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake mara nyingi sana katika kipindi cha miaka 30 na kumzalisha jumla ya watoto 10.
Tukio hili la Argentina linakumbushia kesi ya Josef Fritzl wa Austria ambaye alihukumiwa kwenda jela maisha baada ya kumfungia kwenye kichumba binti yake na kumbaka na kumzalisha jumla ya watoto 7.
Katika kesi ya Argentina, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 62 ambaye jina lake liliwekwa kapuni, alikanusha kumbaka binti yake lakini vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa watoto wote 10 aliowazaa binti yake ni wa kwake.
"Mtuhumiwa alikanusha kumbaka binti yake lakini vipimo vya DNA vimethibitisha kuwa ni watoto wake", alisema jaji Virgilio Palud alipokuwa akiongea na mojawapo ya radio za Argentina.
Mtuhumiwa huyo alimbaka binti yake mara nyingi sana kwa muda wa miaka 30 kosa ambalo adhabu yake ni kwenda jela miaka 20, alisema jaji Palud.
Binti wa mtuhumiwa ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 43, alisema kuwa baba yake alianza kumbaka tangu alipokuwa na umri wa miaka 13.
Binti huyo wa mtuhumiwa alisema kuwa alisubiri muda mrefu kumtia hatiani baba yake kwakuwa baba yake alikuwa akitishia kumuua iwapo atatoa siri nje. Aliamua kuripoti siri hiyo polisi baada ya baba yake kukamatwa na polisi kwa kuiba mifugo.
"Hii ni kesi mbaya kuliko hata ya Josef Fritzl wa Austria", alisema jaji Palud.
Hii ni kesi ya pili kutokea nchini Argentina ambapo baba wakware waliwabaka watoto wao.
Mwaka jana, kesi ya baba wa nchini Argentina aliyembaka na kumzalisha binti yake watoto saba, ilichukua nafasi kubwa sana kwenye vyombo vya habari nchini Argentina
Mwanaume Abakwa na Wanawake 10
Kijana mwenye umri wa miaka 17 wa nchini Papua New Guinea amelazwa hospitali akipatiwa matibabu baada ya kubakwa genge la wahuni wanawake wapatao 10.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa Southern Highland, nchini Papua New Guinea, Teddy Tei, kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 alikumbana na zahama hilo siku ya ijumaa wakati alipovamiwa na kundi la wahuni wanawake wapatao 10.
Wanawake hao wakiwa na visu walimshambulia kijana huyo kabla ya kupokezana kumbaka kwa zamu.
"Hii ni kesi tunayoifualia kwa ukaribu zaidi, tunawatafuta wanawake waliofanya unyama huu", alisema kamanda huyo wa polisi.
Taarifa ya polisi ilisema kwamba wanawake 10 wakiwa na visu walimshambulia kijana huyo na wanawake wanne kati yao walimuingilia kinguvu kijana huyo.
Kamanda Tei aliongeza kuwa kijana huyo aliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Kijana huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni, anafanyiwa uchunguzi ili kujua kama ameambukizwa magonjwa ya zinaa au la.
"Ugonjwa wa ukimwi ni tatizo kubwa hapa Papua New Guinea, ninahofia huenda baadhi ya wanawake waliombaka huenda wakawa ni waathirika", alisema Kamanda Tei na kuongeza.
"Nimekuwa nikiwaonya wanawake wawe waangalifu sasa inanibidi nianze kuwaonya na wanaume nao wawe waangalifu mitaani".
Fred Mpendazoe akamatwa
Sadick Mtulya
ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chadema, Fred Mpendazoe janaalipatwa na msukosuko wakati alipokamatwa na askari wa Jeshi la Polisi ambao walidai kuwa alikuwa anamiliki na kutumia gari la wizi, tukio ambalo amelielezea kuwa lilipangwa kwa lengo la kumchafua.
Mpendazoe, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi huo wa ubunge kwa njia ambayo ameielezea kuwa ilijaa ukiukwaji wa sheria, alihojiwa na polisi kwenye kituo cha Buguruni kwa takriban saa mbili kabla ya kuachiwa bila ya masharti.
Mpendazoe, mmoja wa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya ufisadi, alikamatwa jana majira ya saa 3:30 asubuhi eneo la Uwanja Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na diwani wa Chadema wa Kata ya Segerea, Azuri Mwamboji pamoja na Buhari Mgonyezi ambaye aligombea udiwani wa Kata ya Kinyerezi.
Hata hivyo, Mpendazoe, ambaye alihama CCM mapema mwaka huu wakati akiwa mbunge wa Jimbo la Kishapu na kujiunga katika Chama cha Jamii (CCJ) na baadaye Chadema, aliachiwa majira ya saa 5:44 asubuhi na maafisa upelelezi wakamueleza kuwa wataendelea na uchunguzi.
"Kwa kuwa namba zako za simu umetuachia, wewe nenda. Sisi tutatimiza wajibu wetu wa kuendelea na uchunguzi. Hatua tutakayofikia tutakufahamisha,'' alisema afisa upelelezi mmoja.
Mpendazoe amefungua kesi Mahakama Kuu kupinga matokeo ya ushindi wa Dk Makongoro Mahanga kwenye Jimbo la Segerea, baada ya zoezi la kuhesabu kura kuingiwa na dosari kubwa zilizocheleweshwa kutangazwa kwa matokeo.
Hata hivyo, Dk Makongoro ameshateuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira.
Mpendazoe anatuhumiwa kumiliki na kutumia gari la wizi aina ya Toyota Corona, lenye rangi nyeupe ambalo inadaiwa liliripotiwa kuibwa tangu Juni mosi, 2010.
Lakini mbunge huyo wa zamani wa Kishapu aliiambia Mwananchi jana kuwa tuhuma hizo zimelenga kumchafua na kwamba ni hujuma.
"Askari walinikamata kwa nguvu kubwa, hadi kufikia hatua ya kutishia kutumia silaha endapo ningeendelea na msimamo wangu wa kutaka kujieleza... sisi ni raia na katika mazingira haya inabidi tusaidiwe,'' alisema Mpendazoe ambaye aliruhusiwa kuondoka na gari hilo.
Alifafanua kuwa tukio hilo lilipangwa kwa makusudi na kusisitiza kuwa gari hilo ni lake na amekuwa akilimiliki tangu mwaka 2007.
"Hadi sasa polisi hawajaniambia ni mtu gani aliyefungua mashtaka haya (ya kudai kuibiwa gari hilo). Hii ni hujuma kutoka kwa watu ambao hawanitakii mema pamoja na dola kuendelea kunikandamiza. Gari nimelitumia katika kipindi chote cha kampeni zilizopita za uchaguzi mkuu,'' alisema.
"Jana (juzi) tu, nilikuwa nalo kituo cha polisi cha Sitakishari, Ukonga nilipokuwa nimekwenda kuomba kibali cha kufanya mkutano wa harambee ili kuwaomba wananchi kunichangia fedha kwa ajili ya kuendeshea kesi niliyofungua kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Makongoro.''
Hata hivyo, Mpendazoe alisema kuwa polisi walimnyima kibali hicho na kulalama kuwa eneo alilokuwa amekusudia kufanya mkutano ndilo aliloruhisiwa Dk Mahanga wiki iliyopita kufanya mkutano wa kuwashukuru wakazi wa Segerea kwa kumchagua.
Mpendazoe pia alidai kuwa wiki iliyopita alitumia gari hilo kwenda kituo kikuu cha kati cha polisi kuomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara.
"Ajabu nyingine gari hili hili, wiki iliyopita nilikuwa nalo... mbona hawakunikamata,'' alihoji Mpendazoe.
Alikwenda mbali na kusema: " Kulingana na mazingira haya, hisia zangu ni kwamba hizi ni hujuma na demokrasia inaaza kukandamizwa.''
Kamanda wa Polisi Ilala, Faustine Shilogile hakutaka kuzunghumzia suala hilo kwa maelezo kuwa hakuwa ofisini.
"Nitafute baadaye; kwa sasa sina taarifa kamili na muda huu ( saa 6:30 mchana) nipo njiani natoka uwanja wa ndege.... naenda hapo kituoni,'' alisema.
Alipopigiwa simu baadaye, hakupokea
UDSM yaunga mkono kusudio la JK
Fredy Azzah
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kueleza kusudio la serikali yake la kuunda tume huru ya kupitia upya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), baadhi ya wahadhiri na viongizi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wameunga mkono uamuzi huo huku wakitaja maeneo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa.
Wakizungumza na Mwananchi jijini Dar es Saal jana, walilitaja mambo makubwa yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kuondoa matatizo ya mikopo kwa wanafunzi kuwa ni pamoja na utendaji wa HESLB.
Mambo mengine ni pamoja kutafuta njia sahihi ya kufanya utambuzi wa uwezo wa mwanafunzi, ili aweze kupewa mkopo unaolingana na hali yake ya maisha.
Pia baadhi ha waadhiri na wanafunzi hao, walisema bodi ya mikopo inapaswa iwe na ofisi huru katika kila kanda au katika mikoa yote.
Hali kadhalika, walishauri idadi ya watumishi wa bodi hiyo, iongezwe kulingana na mahitaji ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu kila mwaka.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mikopo wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Silvanus Joseph, alisema kigezo cha kuangalia mtu kasoma shule gani bila kujua aliyemsomesha kipaswa kutumika katika kutambua uwezo wa mwanafunzi.
Aliongeza kuwa, tume hiyo itapaswa kuongeza fedha ambazo zimekuwa zikitoa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na pia kutatua tatizo la ucheleweshwaji wa fedha hizo.
"Lakini tunapata shida kuamini kama haya aliyosema Rais yatatekelezwa kweli, mwaka 2007 alisema hakuna mtoto atakayekosa elimu ya juu kwa sababu ya umasikini wake, lakini tumeshuhudia masikini hao wakikosa nafasi hiyo," alisema.
Alisema mapema mwaka huu, Rais Kikwete alisema fedha za bodi zitaanza kutoka moja kwa moja hazina, ili kuepuka ucheleweshwaji, lakini nalo halikutekelezwa.
Wakati akifungua Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi kushirikiana na viongozi wengine kuhakikisha kuwa tume hiyo inaundwa na mapendekezo yake kutumika katika kuboresha utendaji wa HESLB.
Muhadhiri wa Chuo hicho Profesa Yunus Mgaya, alisema, alisema bodi inapaswa ilipe karo yote kwa wanafunzi
MAUAJI YA ALBINO: Polisi lawamani
Elias Msuya
TAASISI inayotetea watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ya Under The Same Sun, imelilalamikia Jeshi la Polisi kuwa limekalia majina ya watu wanaofadhili mauaji ya walemavu hao bila kuwashtaki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Peter Ash, amevitaka vyombo vya dola kutaja majina ya watuhumiwa hao na kuwafikisha mahakamani, ili haki itendeke.
Huku akionyesha hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu kesi ya mauaji ya mlemavu wa ngozi iliyotolewa Juni 11 mwaka huu, mkoani Tabora, Ash alisema mahakama imethibitisha kuwa kuna majina ya vigogo wanaofadhili mauaji hayo na kwamba majina hayo yako mikononi mwa Jeshi la Polisi.
Alisema hata hivyo, mahakama haikuyataja kwa kuwa bado watuhumiwa, hawajafikishwa mahakamani.
Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Augustine Ramadhan, katika mahakama ya Rufani mkoani Tabora, yenye namba 318, 319, 320 ya mwaka 2009, imehusisha warufani watatu waliotuhumiwa kumuua mtoto mwenye ulemavu wa ngozi mwenye umri wa miaka 13.
Mmoja wa watuhumiwa hao waliokata rufani, ametaja majina ya vigogo wanofadhili mauaji hayo, lakini mahakama imeyahifadhi kwa kuwa hawajafikishwa mahakamani.
“Kuna majina ambayo yametajwa katika ushahidi wa Exh P4, katika maelezo ya awali ya mshtakiwa namba moja, lakini hatuwezi kuyatangaza kwa kuwa huenda pia watu hawa wakawa hawana hatia," ilisema sehemu ya hukumu hiyo.
"Tunatarajia kuwa vyombo vya dola vitaweza kutumia ushahidi huu uliopo mikononi mwa polisi, kuiokoa nchi yetu hii ya amani kutoka kwenye vitendo vya ukatili," ilisisitiza hukumu hiyo.
Ash alisema huo ni ushahidi kuwa wanaotekeleza mauaji hayo ni vigogo na watu matajiri na si watuhumiwa wachache wanaokamatwa na kuishauri serikali, kuwakamata watu hao na kuwahukumu haraka.
“Siyo sisi tuliyosema hayo, ni Jaji mkuu. Tunaitaka serikali iwachukulie hatua watu hao, kwa kuwa mtu wa akawaida hawezi kununua mkono kama kwa dola 2000, au mwili wangu wote huu, ni matajiri ndiyo wenye uwezo huo,” alisema Ash.
Hata hivyo, viongozi wa Jeshi la Polisi, walipotafutwa jana kuzungumzia suala hilo, walisita kulizungumzia. Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, alisema anayepaswa kulitolea maelezo suala hilo ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora.
“Hilo mulize RPC wa Tabora ndiye anaweza kukupa maelezo zaidi,” alisema Manumba. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Liberatus Barlow, alisema yuko kwenye kikao na kwa hiyo, hana nafasi ya kulizungumzia.
“Niko kwenye kikao,” alijibu na kukata simu. Hata hivyo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Said Mwema alipotafutwa kulizungumzia suala hilo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa kwa muda mrefu.
Mauaji hayo yaliyotokea Oktoba 4 mwaka huu, ambapo mlemavu wa ngozi kutoka Tanzania aliuawa na watu waliomteka wakitokea nchini Burundi,
Mauaji mengine kama hayo yaliyotokea mpakani wa Zambia na Tanzania.
Ash alisema ingawa mauaji hayo yamepungua nchini, lakini sasa yamehamia mipakani mwa nchi.
Aliwataka wabunge na mawaziri wapya, kulivalia njuga janga hilo na kwamba huo ni wajibu wao kama viongozi waliochaguliwa na wananchi.
Hivi karibuni, Waziri mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa ameshapata ekari 50 mkoani Arusha kwa ajili ya kujenga kituo cha kulelea watu wenye ulemavu wa ngozi.
Tangu mauaji hayo yalipoanza mwaka 2007, walemavu 59 wameshauawa na tisa wengine kujeruhiwa.
mwisho
MCT kuchunguza tishio la Serikali kwa Mwananchi
Salim Said na Jackline Lema
BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limeunda Kamati Maalumu ya watu watatu, kuchunguza tuhuma za tishio la Serikali kulifungia na kulifuta Gazeti la Mwananchi, linalochapwa na Kampuni ya Mwananchi Communicatios Ltd (MCL) kwa madai kuwa linachapisha habari za uchochezi.
Hatua ya MCT kuunda kamati hiyo kuchunguza malalamiko ya chombo cha habari, ni ya kwanza katika tasnia ya habari Tanzania, ingawa fursa hiyo ilikuwepo kwa miaka mingi tangu kuanzishwa kwa chombo hicho.
Oktoba 20 mwaka huu, Mwananchi iliiripoti kwa mara ya kwanza taarifa kuhusu serikali kutishia kulifungia au kulifutia usajili gazeti la Mwananchi kwa madai kwamba linaandika habari za uchochezi dhidi ya Serikali ya Awamu ya Nne.
Katika taarifa hiyo Mwananchi iliweka hadharani barua ya serikali yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/76 iliyoandikwa kwa mhariri mtendaji wa gazeti hili, ikionya kwamba kama gazeti litaendelea kuandika habari ambazo iliziita kuwa ni za uchochezi dhidi yake, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi.
Lakini akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za MCT jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Baraza hilo, Jaji mstaafu Robert Kisanga, alisema ameamua kuunda kamati hiyo kwa kuwa ombi lililofikishwa kwake na mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi lina maslahi kwa umma.
"Leo tumewaita hapa, ili kuwatangazia kuhusu kuundwa kwa kamati maalumu ambayo ni ya kwanza na ya aina yake katika historia ya tasnia ya habari katika nchi yetu," alisema Jaji Kisanga.
"Hii ni kamati maalumu ya kuchunguza tuhuma za tishio la serikali dhidi ya gazeti la Mwananchi na jinsi lilivyoripoti habari za uchaguzi mkuu 2010," alisema Rais wa MCT.
Alisema moja ya malengo ya MCT kama ilivyoainishwa katika Katiba kifungu cha 3(e), ni kuweka jalada la matukio yanayoweza kukwaza usambazaji wa habari za maslahi kwa jamii, kulihuisha na kuchunguza matendo ya watu moja moja, mashirika au vyombo vya serikali katika ngazi zote yanayolenga vyombo vya habari na kuweka hadharani ripoti zake.
"Kifungu 23(1) cha katiba ya MCT kinaongeza kuwa kwa mapendekezo ya Bodi ya Baraza, Rais wa MCT anaweza kuunda kamati ya watu wasiopungua watatu,"alinukuu Jaji Kisanga.
Alisema jukumu la kamati hiyo ni kuendesha uchunguzi katika jambo lenye umuhimu kwa umma, kuhusu mwenendo wa chombo cha habari au madai kuhusu chombo cha habari au jambo lolote ambalo kwa maoni ya bodi, linatajika kutolewa tafsiri katika muktadha wa kanuni za maadili.
Alisema kutokana na maelekezo hayo ya kikatiba, Bodi ya MCT illikutana Novemba 18 mwaka huu na kujadili shauri lililofikishwa na Mhariri Mtendaji wa MCL na kwamba ilijiridhisha kuwa lilihusu suala muhimu kwa umma na uhuru wa vyombo vya habari.
"Kwa hiyo basi, bodi ilinishauri kuunda kamati ya watu watatu ili kufanya uchunguzi wa suala hilo na kutoa ripoti yake, na mimi nikakubali," alisema Jaji Kisanga.
Jaji Kisanga alifafanua kuwa, kamati imeandaliwa hadidu za rejea za kina na inatafanya kazi ndani ya siku 30 na kuwasilisha ripoti kwake.
"Lengo kuu la uchunguzi litakuwa kwanza, kuangalia ikiwa madai ya serikali dhidi ya gazeti la Mwananchi yana uhalali, pili kama tishio la serikali linaingilia isivyostahili uhuru wa vyombo vya habari na uhariri," alisema Jaji Kisanga.
Jaji Kisanga aliongeza kuwa, lengo la tatu la kamati hiyo ni kuchunguza kama uandishi na mwenendo wa gazeti la Mwananchi katika kipindi cha uchaguzi, vilikiuka mwongozo wa maadili katika kuripoti habari za uchaguzi mkuu kama ilivyoafikiwa na Jukwaa la Wahariri Agosti 13, 2010 huko Morogoro.
Alisema mwongozo huo pia uliridhiwa na mkutano wa wadau uliofanyika katika jijini Dar es Salaam Agosti 18, 2010.
Alisema kamati hiyo pia itaangalia ikiwa uandishi na mwenendo wa gazeti la Mwananchi ulikiuka kanuni za maadili ya waandishi wa habari, kama zilivyofanyiwa marekebisho na kupitishwa na mkutano mkuu wa MCT uliofanyika mkoani Tanga, Juni 23 2010.
"Ninayo furaha kutajia majina ya wajumbe wa kamati maalumu ya kuchunguza tuhuma na tishio la serikali dhidi ya gazeti la Mwananchi na jinsi lilivyoripoti habari za uchaguzi wa mwaka 2010,"alisema Jaji Kisanga.
Alisema Kamati hiyo itaongozwa na Profesa Luitfried Mbunda ambaye ni profesa wa sheria aliyebobea katika sheria za uhuru wa habari.
Jaji Kisanga aliwataja wajumbe wengine kuwa ni Gema Akilimali ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kijinsia na haki za binadamu na Attilio Tagalile ambaye ni mwandishi na mhariri wa siku nyingi katika vyombo vya serikali na binafsi ndani na nje ya nchi.
Alisema kamati itafanya kazi kwa uhuru bila ya kuingiliwa au kushinikizwa na mtu au taasisi yoyote na kwamba itawasilisha ripoti kwa Rais wa MCT ambaye baadaye, ataifikisha kwa bodi kabla ya kuwekwa hadharani kwa manufaa ya jamii na tasnia ya habari.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema kazi hiyo ni ya MCT na kwamba baraza limetenga kiasi cha Sh10 hadi 12 milioni kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo.
.
Alisema uteuzi wa kamati hiyo, umezingatia vigezo kama vilivyoelezwa katika kifungu cha 23 kifungu kidogo cha pili na tatu kwamba, miongoni mwa wajumbe wa kamati lazima awemo mwanasheria wa viwango vya juu na aliyebobea katika fani hiyo ambapo alisema ni Profesa Mbunda
CAG awapa 'mtihani' wabunge
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amewataka wabunge wa Bunge la Kumi kuhakisha wanatumia vizuri ripoti za ofisi hiyo ili waweze kuidhibiti serikali katika matumizi.
CAG alitoa kauli hiyo juzi jioni jijini Dar es salaam wakati akifunga semina ya siku nne ya kuwajengea uwezo makatibu wa kamati za kudumu za Bunge, ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kuchanganua ipasavyo maeneo muhimu katika ripoti zake za matumizi ya fedha za serikali.
Kaimu mdhibiti mkuu wa ofisi hiyo, Jumaa Mshihiri alisema pamoja na mambo mengine wabunge wawatumie makatibu wa kamati za bunge kuwafafanulia baadhi ya vipengele wasivyovielewa vizuri wakati wa kujadili ripoti zake.
“Tunataka ufanisi zaidi katika Bunge la Kumi; tumewajengeeni uwezo makatibu ili... muweze kuwashauri wabunge ipasavyo ili waweze kuhoji vizuri matumizi yaliyofanywa na yakatofanywa na serikali kwa lengo la kudhibiti matumizi holela pamoja na kuboresha utendaji wao,’’ alisema Mshihiri
Alisema kutokana na sababu mbalimbali wabunge pamoja na makatibu hao wameshindwa kuzichanganua vizuri ripoti za CAG na kwamba hali hiyo imesababisha kwa kiasi fulani wabunge kushindwa kuibana au kuhoji vizuri matumizi ya serikali.
“Mkazo wetu mkubwa upo kwa makatibu wa Kamati ya Mashirika ya Umma (Poac), Hesabu za Serikali Kuu(Pac) pamoja na Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC)," alisema.
“Kamati hizi ndizo tunashughulika nazo moja kwa moja katika utendaji wetu wa kila siku,’’ Mshihiri aliongeza.
Mkurugenzi wa Bunge, Charles Mloka alisema mafunzo hayo yatakiwezesha chombo hicho cha wawakilishi wa wananchi kuwa na ufanisi zaidi katika kuisimamia serikali na kwamba changamoto kubwa itakuwa katika kuwafafanulia ipasavyo wabunge, vipengele muhimu vya ripoti za CAG.
“Changamoto kubwa ni jinsi makatibu wa bunge watakavyoweza kuzichambua ipasavyo ripoti za CAG na kuwashauri wabunge katika masuala ya kitaalamu wakati watakapotakiwa,’’ alisema Mloka
Mloka alifafanua kwamba wabunge pamoja na makatibu wa kamati za Bunge walikuwa wakipata changamoto nyingi katika kuzipitia ripoti za CAG na kwamba hali hiyo ilisababisha washindwe kufanya kazi yao vizuri.
Awali akizunguza kwa niaba ya makatibu hao, mkurugenzi msaidizi wa Bunge, Anselm Mrema alisema changamoto kubwa waliyoiona ni sheria ya uteuzi wa anayekagua matumizi ya ofisi ya CAG.
Kwa mujibu wa sheria, PAC ndiyo inayoteua mkaguzi wa matumizi ya CAG.
“Pamoja na mambo mengine, tunataka ofisi ya Bunge ihusike moja kwa moja katika kumteua mkaguzi wa matumizi ya CAG,’’ alisema Mrema
Katika mafunzo hayo yaliyogharimiwa na serikali ya Sweden kwa kutumia Shirika la Misaada la Sweden (Sida), makatibu hao walifundishwa wajibu na mamlaka ya Bunge pamoja na kamati zake katika kuisimamia serikali na taasisi zake pamoja na masuala ya ukaguzi wa fedha unavyofanywa, sheria ya ukaguzi wa fedha na kanuni zake
Wasio wavutaji hufa kwa kuvuta sigara
Mvutaji sigara
Utafiti mpya uliofanywa na shirika la afya duniani WHO unaonyesha kuwa watu 600,00 wasio wavutaji sigara hufariki kila mwaka kutokana na kuvuta moshi unotokana na kukaa karibu na watu wanaovuta sigara.
Utafiti huo uliochapishwa siku ya Ijumaa ndio wa kwanza duniani kuangazia hasa madhara ya moshi wa sigara.
Shirika la WHO lilichukua takwimu kutoka karibu kila taifa duniani. Takriban asilimia 40 ya watoto na zaidi ya asilimia 30 ya watu wazima ambao hawavuti sigara huwa wanakabiliana na moshi kutoka kwa wavuta sigara.
Kulingana na utafiti huo watu 600,000 hufariki kila mwaka thuluthi yake wakiwa watoto.
Moshi unaowafikia watu ambao hawavuti sigara unaweza kusababisha maradhi ya moyo, pumu na hata saratani ya mapafu kama tu inavyofanya kwa wavuta sigara.
Tofauti hata hivyo ni kwamba wale wanaofikiwa na huo moshi hawafanyi hivyo kwa uamuzi wao wa kuhatarisha afya yao kwa kutumia tumbaku.
Hofu kubwa kulingana na waliochapisha ripoti hiyo ni athari kwa watoto hata katika mataifa ambayo yana sheria kali dhidi ya uvutaji sigara kwa sababu bado wanaathirika kutokana na watu wanaovuta nyumbani.
Ingawaje ni vigumu kuunda sheria kubana watu kuvuta sigara nyumbani, WHO inakiri kuwa kuna haja ya hatua kuchukuliwa ili kulinda watoto kutokana na madhara ya moshi wa sigara.
Utekelezaji wa katiba Kenya mashakani
Wabunge wa Kenya
Mchakato wa utekelezwaji wa katiba mpya nchini Kenya, umepata pigo kubwa baada ya wabunge kukataa kuidhinisha makamishna wa tume mbili muhimu waliokuwa wamependekezwa.
Wabunge walisema orodha hiyo haijazingatia uwakilishi wa mikoa yote na inapaswa kurejeshwa kwa Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga.
Wabunge pia walikataa kuidhinisha kamati iliyopendekezwa kusimamia ugawaji wa rasilimali.
Kufuatia uamuzi huo wa wabunge, huenda ikatoa fursa kwa kwa raia yeyote wa Kenya kwenda mahakamani kuwasilisha kesi ya kutaka bunge livunjwe.
Hata hivyo wataalamu wa masuala ya sheria nchini Kenya,wanasema uamuzi huo wa wabunge huenda ukasababisha mzozo wa kisiasa na kikatiba.
Akizungumza na BBC mkuu wa kitivo cha sheria cha chuo kikuu cha African Nazarene Dkt. Morris Mbondenyi amesema kuwa hatua hii itachelewesha utekelezaji wa katiba mpya.
Hasara ya mabilioni yakadiriwa Sudan
Uchumi wa Sudan huenda ukaathirika vibaya ikiwa vita vitazuka upya kati ya kusini na kaskazini
Utafiti kuhusu athari za kiuchumi zitakazotokea ikiwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vitaibuka nchini Sudan unaonyesha kuwa taifa hilo na jirani zake litapata hasara ya $100 bilioni.
Ripoti iliochapishwa na baraza la ushauri wa maswala ya kiuchumi la Frontier Economics, inafichua kuwa iwapo kura ya maamuzi kuhusu uhuru wa Sudan Kusini itasababisha vita, huenda hasara ya asilimia thelathini na nne ya pato la kitaifa la Sudan katika kipindi cha miaka kumi ikashuhudiwa.
Wadidisi kutoka baraza hilo la kiuchumu, wameongeza kuwa uchumi wa nchi jirani kama vile Kenya na Ethiopia huenda ukapoteza dola bilioni moja kila mwaka baada ya vita kuanza.
Wakaazi wa kusini mwa Sudan, eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta wanatarajiwa kupiga kura ya kuunga mkono mpango wa kujitenga na kaskazini mwezi Januari mwakani.
Wachambuzi wanasema mzozo mpya utazuia wawekezaji kuingia nchini Sudan, utaongeza garama ya kijeshi na kuleta uhaba wa fedha za misaada wa kibinadamu
Polisi wadaiwa kushiriki wizi wa makontena
Mwandishi Wetu
BAADHI ya askari polisi wanadaiwa kushirikiana na mtandao wa ujambazi unaoendeshwa kwa kushirikiana na genge la wahalifu kupora mali na kunyanyasa wafanyabiashara wanaosafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.
Wahalifu hao wamekuwa wakiteka magari ya mizigo inayosafirishwa kwenda mikoa au nje ya nchi na malori hayo kupelekwa njia tofauti ambako mizigo hupakuliwa bila ya idhini ya mwenye mali.
Habari zinasema kuwa mzigo ambao ulikusudiwa kupelekwa Burundi huingiliwa njiani na kuelekezwa barabara iendayo Arusha na njiani polisi walio kwenye mtandao huo hufanya mawasiliano na wenzao ili kulinda wasiikamate endapo watabaini kuwa nyaraka za mizigo hiyo zinaonyesha njia tofauti.
Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kwamba mtandao huo umejikita katika barabara itokayo Dar es Salaam kwenda Arusha na ile ielekeayo nchi jirani za Burundi na Rwanda.
Polisi hao wamekuwa wakishirikishwa kwenye mtandao huo kwa kufanya mawasiliano ili kuhakikisha usalama wa majambazi hao baada ya tukio la kupora.
Habari hizo, ambazo zimethibitishwa na baadhi ya makamamnda wa polisi wa mikoa, zinadai kuwa katika kuhakikisha wahalifu hao wanakuwa salama baada ya kupora, askari wa Jeshi la Polisi wanadaiwa kuwaweka ndani watu wanaotoa taarifa za matukio ya uporaji.
Mtandao huo umeelezwa kudiriki hata kuwatesa watu wanaotoa taarifa za kuporwa kwa mali zao na hata kuwatishia maisha ili kuwafunga mdomo.
"Ni kweli kuna wizi wa namna hiyo," alisema kamanda wa polisi wa mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile lakini akaongeza kuwa mtu aliyelalamika ambaye suala lake liko kituo cha Msimbazi ndiye anayetuhumiwa kwa ujambazi.
"Mimi mwenyewe ndiye niliamrisha akamatwe na tutamfikisha mahakamani kujibu mashtaka.''
Katika tukio la hivi karibuni, polisi wa kituo cha Msimbazi wanadaiwa kumweka ndani mtendaji na ofisa wa kampuni moja ya kusafirisha mizigo ya jijini Dar es Salaam ambao walikwenda kituoni hapo kutoa taarifa za wizi wa mizigo yenye thamani ya Sh90 milioni iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea mkoani Mbeya.
Mizigo hiyo iliibwa na kusafirishwa kuelekea mkoani Arusha.
Kama hiyo haitoshi, polisi hao waliwakamata na kuwasweka lupango maofisa wengine wa kampuni hiyo waliokuwa na maelezo ya namna mali zao zilivyoporwa.
Waporaji hao walikamatwa na polisi pamoja na gari walilotumia kutorosha mali hizo, lakini baadaye waliachiwa katika mazingira yaliyoelezwa kuwa ni tata. Habari zinasema kuwa hata mtu aliyekutwa akiwa ameficha nyumbani kwake sehemu ya mali zilizoporwa, aliachiwa bila kufikishwa polisi kutoa maelezo.
Hata hivyo, gari lililosafirisha mzigo huo (namba tunazo) ambalo baadaye lilikamatwa mjini Moshi likiwa limebeba sehemu ya mzigo huo na kupelekwa kituo cha Msimbazi ambako jalada la wizi huo lilifunguliwa. Gari hilo liliruhusiwa kuondoka kituoni Jumanne wiki hii, huku sehemu ya mzigo uliokamatwa ambao ungetumika kama kidhibiti, ukiteremshwa kutoka gari hilo.
Inadaiwa kuwa kabla ya gari hilo kuachiwa, wamiliki wake ambao wana asili ya Kisomali walionekana wakifanya vikao vya siri pamoja na mawasiliano ya simu na polisi ambao wanaonekana kuwa kwenye mtandao huo na ambao vituo vyao vya kazi ni Dar es Salaam, Moshi na Arusha.
Wakati wahalifu hao wakiachiwa huru, inaelezwa kwamba walalamikaji waliendelea kusumbuliwa kwa kuwekwa rumande na katika vituo vya polisi tofauti mkoni Arusha, Moshi na Dar es Salaam na kuambiwa kuwa wao ndio wahalifu.
Akizungumza na gazeti hili mmoja wa wafanyabiashara hao Geogre Mateso anayemiliki kampuni ya Mateso Group & Company Limited alieleza kushangazwa kuona polisi wakiwasumbua watu wema wanaotoa taarifa za uhalifu.
"Badala ya watu wema kuona polisi ni mahali salama pa kukimbilia, kwetu hali ti tofauti," alisema.
"Sisi tuliotoa taarifa za uhalifu wa mali tulizokuwa tukisafirisha, ndio tuliofanyiwa unyanyasaji na kuwekwa rumande. Cha ajabu ni polisi hao kuwachia wamiliki wa magari yaliyotumika katika uhalifu pamoja na madereva waliohusika."
Aliongeza kusema: “Tunakimbilia polisi kutafuta msaada wa kupata haki zetu, lakini inakuwa kinyume. Tunaotafuta haki tunadidimizwa; tunaodai ndiyo tunakamatwa na kuwekwa ndani; pesa tunatolewa na polisi Msimbazi.
"Sipo peke yangu najua yapo makampuni mengine yenye shida kama yangu hapo Polisi Msimbazi.”
Alisema mkasa huo ulimkumba Oktoba 27, mwaka huu wakati kampuni yake ikisafirisha mzigo kwenda Mbeya.
Alisema kuwa walipofuatilia walibaini kuwa mzigo huo haukupelekwa Mbeya na badala yake ulipelekwa mkoani Arusha.
Alisema kuwa alitoa taarifa polisi Novemba tatu mwaka huu na kupewa RB namba MS/RB/12331/2010 pamoja na barua kuwawezesha kufuatilia suala hilo mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Baada ya kufuatilia walibaini kuwa gari hilo lilipita na kupima uzito katika mizani ya Chalinze Oktoba 28.
Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, walifuatilia mizigo hiyo hadi Moshi mkoani Kilimanjaro na kupewa askari waliokwenda nao hadi Arusha.
Alisema walifanikiwa kukamata sehemu ya mzigo huo tani 10 kwa mkazi mmoja wa Himo baada ya kulikamata gari lililobeba mzigo huo Namanga ambako ni mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Hata hivyo, alisema baada ya kupata taarifa ya gari hilo kuonekana eneo la Namanga, waliwekwa rumande mkoani humo kwa siku nne kuanzia Novemba 7 hadi Novemba 10 na kubadilishiwa 'kibao' wakituhumiwa kwa wizi.
"Tulitaka kufuatilia tukiwa pamoja na askari na wakala wa mmiliki wa gari, lakini sisi tukazuiwa kwenda; wakaenda polisi na huyo wakala, badala yake sisi tukawekwa ndani siku nne," alilalamika mmiliki huyo wa kampuni ya usafirishaji.
Wakati walalamikaji wakiwa rumande, inadaiwa wahalifu hawakukamatwa licha ya kukutwa na mali hizo za wizi jambo ambalo linaashiria kwamba kulikuwa na mchezo mchafu kati ya polisi na watuhumiwa hao wa uhalifu.
Watu hao pia waliwekwa rumande walipokwenda kituo cha Msimbazi, Dar es Salaam ambako pia inadaiwa kuna kesi nyingine tano za watu wanaolalamikia mizigo yao kuibwa katika mazingira hayo yanayoelezwa kuwa ya utata.
Mwananchi imedokezwa kuwa katika tukio moja la hivi karibuni, mmoja wa polisi anayeshiriki kwenye mtandao huoalimtisha mtu aliyekuwa anafuatilia mizigo yake iliyoporwa na wahalifu hao na kumkejeli kuwa "haki mbinguni pekee".
“Kama hamjui duniani hakuna haki, mtajua leo! Haki ipo mbinguni tu,” mmoja wa wapashaji wetu alimnukuu polisi huyo ambaye ni mmoja wa vigogo wa jeshi hilo wanaojihusisha na mtandao huo katika njia ya Dar es Salaam na Arusha.
Kituo cha polisi cha Msimbazi jijini Dar es salaam kimetajwa kuwa kina maofisa wengi wanaojihusisha na mtandao huo.
Kwa mujibu wa habari hizo, inapotokea askari polisi aliye nje ya mtandao huo amekamata mali au miongoni mwa wanaojihusisha na genge la uhalifu, juhudi kubwa hufanyika ili kesi isiende mahakamani na baadaye watuhumiwa huachiwa pamoja na gari walizotumia huku walalamikaji wakinyanyaswa na kuwekwa rumande hadi uhalifu unapokamilika.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba matukio ya namna hiyo yanawakumba wafanyabiashara wengine, wakiwepo wale wanaosafirisha mafuta kwenda nchi jirani.
“Malalamikio haya hayakufanyika kwa mfanyabiashara huyo pekee. Wapo mengi na unyanyasaji huo upo hasa kitengo cha upelelezi. Kila ukienda kuripoti tukio la uhalifu, wewe ndio utawekwa ndani bila maelezo. Kesho tena atawekwa mfanyakazi wako lakini kutoka lazima uwape fedha," alieleza mpashaji wetu.
“Kibaya zaidi ni kwamba mtu akiibiwa anawekwa ndani, lakini sehemu ya watuhumiwa wa wizi ambao wanamiliki gari lililobeba mzigo wanaachiwa huru.”
Mtandao huo wa uhalifu unadaiwa pia una mbinu nyingine ya wizi ya kujipatia fedha kwa njia haramu ya kuhakikisha kila msafirishaji anatoa fedha taslimu kila mali zao zinapopita kwenye vituo vyao.
Inadaiwa kuwa msafirishaji mmoja anayetoa mali yake kwenda Arusha au Mbeya hulazimika kutenga kati ya Sh 300,000 hadi 600,000 kuwapa wanamtandao hao ili kuepuka kunyanyaswa.
Habari zinadai kuwa mtandao huo wa kihalifu ndani ya Jeshi la Polisi una ushirikiano na makundi mengine ya kihalifu kwenye nchi jirani za Burundi na Rwanda.
Wahalifu hao wa nchi jirani inadaiwa kuwa wana silaha kali za kivita na hutekeleza uhalifu huo katika maeneo mbalimbali, ikiwemo ya kanda ya Ziwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alikiri kuwepo kwa tukio hilo, lakini akasema anachojua katika kituo cha polisi Msimbazi lipo tukio moja la aina hiyo akitaja mhusika kuwa ni Mateso na kwamba ndiye anayehusika na matukio ya wizi.
"Sina taarifa ya matukio mengine ya wizi wa mizigo, kama yapo watu hao waje kuniona moja kwa moja. Lakini ninachojua ni kukamatwa kwa Mateso ambaye anatuhumiwa kwa wizi na ndiye anayehusika na uibaji wa mizingo,'' alisema Shilogile.
Kamanda Shilogile aliongeza kusema: ''Mimi mwenyewe ndiye niliamrisha akamatwe na tutamfikisha mahakamani kujibu mashtaka.''
Ingawa kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha hakupatikana kuzungumzia suala hilo jana, kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Lucas Ngh'oboko alisema hana taarifa za kuwepo kwa mtandao huo.
Hata hivyo alisema iwapo kuna wafanyabiashara waliopatwa na mkasa huo waende wakamuone ili ashughulikie suala lao.
"Sina taarifa ya hali hiyo, lakini kama wapo wasafirishaji waliofanyiwa hivyo na askari wangu, waje wanione nitalishughulikia," alisema.
Kama polisi wangu wanahusika na mtandao huo ikithibitika nitachukua hatua," alisema Kamanda Ngh'oboko.
Hata hivyo, alisema kuwa iwapo askari wake waliwaachia watuhumiwa bila kuwakamata huo ni uzembe ambao hautavumilika na akasisitiza kwamba apelekewe taarifa sahihi ili hatua zichukuliwe.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Senso alisema: "Nitalichunguza suala hilo, lakini ni vyema anayetoa taarifa hizo kwako akatusaidia kujua zaidi namna polisi wanavyohusika na wizi huo."
Waziri wa Korea ya Kusini ajiuzulu
Waziri wa ulinzi wa Korea ya Kusini, Kim Tae-young, amejiuzulu, siku mbili baada ya wanajeshi wa Korea ya Kaskazini kukishambulia kwa makombora kisiwa kimoja cha nchi yake.
Waziri wa ulinzi wa Korea ya Kusini aliyejiuzulu
Barua yake ya kujiuzulu imekubaliwa na Rais Lee Myung-bak.
Bw Kim alilaumiwa na baadhi ya watu kwa kutochukua hatua za kutosha kujibu mashambulio yaliyofanywa na Korea ya Kaskazini.
Korea ya Kusini sasa imetangaza kwamba inabadilisha baadhi ya utaratibu wake wa kijeshi, na vile vile kuongeza idadi ya vikosi katika kisiwa ambacho kilishambuliwa.
Hayo yakiendelea, Uchina imeelezea wasiwasi wake kutokana na ushirikiano wa shughuli ya kijeshi kati ya Korea ya Kusini na Marekani, kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Dk. Slaa ashindwa kutokea kwenye usuluhishi wa kesi
James Magai
ALIYEKUWA mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi mkuu, Dk Willibrod Slaa hakutokea kwenye kikao cha usuluhishi wa kesi inayomkabili ya kumdhalilisha mkazi mmoja wa jijini Dar es salaam kwa kupora mke na kuzini naye.
Aminile Mahimbo, ambaye anadai ni mume halali wa ndoa wa Josephine Mushumbushi anayedaiwa kuchukuliwa na Dk Slaa, amefungua kesi ya madai akitaka alipwe fidia ya Sh1 bilioni kwa tuhuma kwamba katibu huyo wa Chadema aliingilia ndoa yake na kuzini na mkewe huyo.
Kesi hiyo ilikuwa isikilizwe jana mbele ya msuluhishi Zainabu Mruke ambaye ni jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaa.
Hata hivyo Dk. Slaa hakutokea mahakamani hapo wala wakili wake na hakukuwa na taarifa zozote za kutokuwepo kwao.
Katika hatua, pande zote mbili zilitarajiwa kujadiliana juu ya kumaliza suala hilo kukubaliana kulimaliza nje ya mahakama na hivyo kesi kufikia tamati.
Wakili wa mlalamikaji, Abduel Kitururu aliwaleza waandishi wa habari kuwa kitendo cha upande wa mdaiwa kutokufika katika kikao hicho cha usuluhishi bila kutoa taarifa zozote kinatafsiriwa na msuluhishi pamoja na upande wa madai kuwa mdaiwa hayuko tayari au hataki usuluhishi.
Alisema hatua inayofuata ni Jaji Mruke kuandika taarifa yake na kupeleka jalada la kesi hiyo kwa jaji mfawidhi kwa lengo la kuipangia jaji wa kuisikiliza rasmi kesi hiyo.
Wakili Marando alipoulizwa kuhusu kutoonekana kwao kwenye kikao hicho, alisema kuwa alimtuma mwenzake kuhudhuria lakini alishangaa kupata habari kuwa hawakutokea mahakamani na kusema hajui huyo mwenzake alikwama wapi.
Hata hivyo, Marando alisema kuwa pamoja na hayo mteja wake anasema hayuko tayari kulipa pesa hiyo na kwamba kumdai fidia hiyo ni kumnyanyasa kwa kuwa mwanamke hamtaki mlalamiaji.
Wakati pande hizo zilipokutana katika hatua ya kupanga kesi hiyo Oktoba 15 mwaka huu, zilikubaliana kuwa iwapo usuluhishi utashindikana, kesi itaendelea kwa kila upande ukuwaita mahakamani mashahidi wanne.
Katika maelezo yake ya utetezi, Dk Slaa alikiri kuwa na uhusiano na mwanamke huyo, lakini akajitetea kuwa alikuwa hajui kuwa ni mke wa mtu kwa kuwa mwanamke huyo hakuwahi kumwambia kuwa ameolewa.
Dk Slaa alidai kuwa alijua kwa mara ya kwanza kuwa mwanamke huyo ameolewa baada ya kusoma na kusikia taarifa hizo katika vyombo vya habari.
Licha ya kukiri kuwa na uhusiano na mwanamke huyo ambao hata hivyo hakuufafanua kuwa ni wa aina gani, Dk Slaa alikanusha tuhuma za kuzini naye wala kumtambulisha kuwa mke wake.
Lakini katika majibu, Mahimbo alisisitiza kuwa Dk Slaa alifanya uzinzi na mke wake na kwamba alifanya hivyo akiwa anajua kuwa ni mke wa mtu.
Alidai baada ya Dk Slaa kumtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, habari hizo ziliandikwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini jambo ambalo lilitosha kumjulisha kuwa alikuwa akifanya uzinzi na mke wa mtu, lakini aliendelea kuzini naye.
Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010 ilifunguliwa mahakamani hapo Septemba 7 mwaka huu, siku chache baada ya Dk Slaa kumtambulisha Josephine mara kadhaa kupitia kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa ni mchumba wake
Friday, November 19, 2010
Maadhimisho miaka 50 UDSM leo
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema sherehe hizo zitafanyika katika Ukumbi wa Nkurumah kuanzia saa 3 asubuhi leo na mgeni raanatarajiwa kwua Waziri Mkuu .
Mukandala alisema sherehe za maadhdimisho hayo ni moja ya fursa za kutafakari na kuangalia changamoto za chuo hicho na kuagnalia walikotoka na wanakokwenda juu ya maendeleo ya chuo hicho.
Aidha alisema kuna baadhi ya changamoto zinazowakabili chuoni hapo na wanatarajia kwuasilisha mbele ya mgeni rasmi ikiwa na pamoja ukosefu wa sehemu za kulala wanafunzi, na kuhitaji nyongeza ya motisha kwa walimu na wafanyakazi wka ujumla chuoni hapo
Subscribe to:
Posts (Atom)