KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, November 27, 2010

Baba Amzalisha Binti Yake Watoto 10


Mwanaume mmoja wa nchini Argentina huenda akahukumiwa kwenda jela miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake mara nyingi sana katika kipindi cha miaka 30 na kumzalisha jumla ya watoto 10.
Tukio hili la Argentina linakumbushia kesi ya Josef Fritzl wa Austria ambaye alihukumiwa kwenda jela maisha baada ya kumfungia kwenye kichumba binti yake na kumbaka na kumzalisha jumla ya watoto 7.

Katika kesi ya Argentina, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 62 ambaye jina lake liliwekwa kapuni, alikanusha kumbaka binti yake lakini vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa watoto wote 10 aliowazaa binti yake ni wa kwake.

"Mtuhumiwa alikanusha kumbaka binti yake lakini vipimo vya DNA vimethibitisha kuwa ni watoto wake", alisema jaji Virgilio Palud alipokuwa akiongea na mojawapo ya radio za Argentina.

Mtuhumiwa huyo alimbaka binti yake mara nyingi sana kwa muda wa miaka 30 kosa ambalo adhabu yake ni kwenda jela miaka 20, alisema jaji Palud.

Binti wa mtuhumiwa ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 43, alisema kuwa baba yake alianza kumbaka tangu alipokuwa na umri wa miaka 13.

Binti huyo wa mtuhumiwa alisema kuwa alisubiri muda mrefu kumtia hatiani baba yake kwakuwa baba yake alikuwa akitishia kumuua iwapo atatoa siri nje. Aliamua kuripoti siri hiyo polisi baada ya baba yake kukamatwa na polisi kwa kuiba mifugo.

"Hii ni kesi mbaya kuliko hata ya Josef Fritzl wa Austria", alisema jaji Palud.

Hii ni kesi ya pili kutokea nchini Argentina ambapo baba wakware waliwabaka watoto wao.

Mwaka jana, kesi ya baba wa nchini Argentina aliyembaka na kumzalisha binti yake watoto saba, ilichukua nafasi kubwa sana kwenye vyombo vya habari nchini Argentina

No comments:

Post a Comment