KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, November 27, 2010
Wasio wavutaji hufa kwa kuvuta sigara
Mvutaji sigara
Utafiti mpya uliofanywa na shirika la afya duniani WHO unaonyesha kuwa watu 600,00 wasio wavutaji sigara hufariki kila mwaka kutokana na kuvuta moshi unotokana na kukaa karibu na watu wanaovuta sigara.
Utafiti huo uliochapishwa siku ya Ijumaa ndio wa kwanza duniani kuangazia hasa madhara ya moshi wa sigara.
Shirika la WHO lilichukua takwimu kutoka karibu kila taifa duniani. Takriban asilimia 40 ya watoto na zaidi ya asilimia 30 ya watu wazima ambao hawavuti sigara huwa wanakabiliana na moshi kutoka kwa wavuta sigara.
Kulingana na utafiti huo watu 600,000 hufariki kila mwaka thuluthi yake wakiwa watoto.
Moshi unaowafikia watu ambao hawavuti sigara unaweza kusababisha maradhi ya moyo, pumu na hata saratani ya mapafu kama tu inavyofanya kwa wavuta sigara.
Tofauti hata hivyo ni kwamba wale wanaofikiwa na huo moshi hawafanyi hivyo kwa uamuzi wao wa kuhatarisha afya yao kwa kutumia tumbaku.
Hofu kubwa kulingana na waliochapisha ripoti hiyo ni athari kwa watoto hata katika mataifa ambayo yana sheria kali dhidi ya uvutaji sigara kwa sababu bado wanaathirika kutokana na watu wanaovuta nyumbani.
Ingawaje ni vigumu kuunda sheria kubana watu kuvuta sigara nyumbani, WHO inakiri kuwa kuna haja ya hatua kuchukuliwa ili kulinda watoto kutokana na madhara ya moshi wa sigara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment