KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, November 27, 2010

Mtoto azaliwa ubongo nje


MSHANGAO mkubwa umeibuka kwa madaktari na wauguzi wa hospitali ya wilaya ya Ulanga Morogoro baada ya mwanamke kujifungua mtoto ukiwa ubongo nje kwa kukosekana na ngozi ya kichwa mahala hapo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Amani Kombe, alitoa taarifa hiyo kwa wanahabari kuwa, mtoto huyo alizaliwa Novemba 22 mwaka huu, kwenye majira ya saa 3 usiku.

Dk. Kombe, alisema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika hospitali hiyo, na ksuema motto huyo alizaliwa na uzito wa kilo 2.9.

Kombe alisema kitaalamu mtoto anaweza kuzaliwa na matatizo hayo kutokana na kusababishwa na ukosefu wa madini tofauti kwa mama wakati wa ujauzito wake.

Hata hivyo katika kuthibitisha hilo, mama wa mtoto huyo, Bi. Silvia Lyombo (20) mkazi wa Ulanga alipohojiwa kujua wakati wa ujauzito wake alikuwa na hali gani, alijieleza kuwa hakuwahi kupata tatizo lolote la kiafya katika kipindi cha ujauzito wake na huo ulikuwa ujauzito wake wa kwanza.

Dk. Kombe alisema kuwa mtoto huyo wanamuhamishia katika hospitali ya Mkoa Morogoro kwa uchunguzi zaidi wa madaktari bingwa

No comments:

Post a Comment