KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, November 27, 2010

Dk. Slaa ashindwa kutokea kwenye usuluhishi wa kesi


James Magai
ALIYEKUWA mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi mkuu, Dk Willibrod Slaa hakutokea kwenye kikao cha usuluhishi wa kesi inayomkabili ya kumdhalilisha mkazi mmoja wa jijini Dar es salaam kwa kupora mke na kuzini naye.

Aminile Mahimbo, ambaye anadai ni mume halali wa ndoa wa Josephine Mushumbushi anayedaiwa kuchukuliwa na Dk Slaa, amefungua kesi ya madai akitaka alipwe fidia ya Sh1 bilioni kwa tuhuma kwamba katibu huyo wa Chadema aliingilia ndoa yake na kuzini na mkewe huyo.
Kesi hiyo ilikuwa isikilizwe jana mbele ya msuluhishi Zainabu Mruke ambaye ni jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaa.
Hata hivyo Dk. Slaa hakutokea mahakamani hapo wala wakili wake na hakukuwa na taarifa zozote za kutokuwepo kwao.
Katika hatua, pande zote mbili zilitarajiwa kujadiliana juu ya kumaliza suala hilo kukubaliana kulimaliza nje ya mahakama na hivyo kesi kufikia tamati.

Wakili wa mlalamikaji, Abduel Kitururu aliwaleza waandishi wa habari kuwa kitendo cha upande wa mdaiwa kutokufika katika kikao hicho cha usuluhishi bila kutoa taarifa zozote kinatafsiriwa na msuluhishi pamoja na upande wa madai kuwa mdaiwa hayuko tayari au hataki usuluhishi.

Alisema hatua inayofuata ni Jaji Mruke kuandika taarifa yake na kupeleka jalada la kesi hiyo kwa jaji mfawidhi kwa lengo la kuipangia jaji wa kuisikiliza rasmi kesi hiyo.
Wakili Marando alipoulizwa kuhusu kutoonekana kwao kwenye kikao hicho, alisema kuwa alimtuma mwenzake kuhudhuria lakini alishangaa kupata habari kuwa hawakutokea mahakamani na kusema hajui huyo mwenzake alikwama wapi.
Hata hivyo, Marando alisema kuwa pamoja na hayo mteja wake anasema hayuko tayari kulipa pesa hiyo na kwamba kumdai fidia hiyo ni kumnyanyasa kwa kuwa mwanamke hamtaki mlalamiaji.

Wakati pande hizo zilipokutana katika hatua ya kupanga kesi hiyo Oktoba 15 mwaka huu, zilikubaliana kuwa iwapo usuluhishi utashindikana, kesi itaendelea kwa kila upande ukuwaita mahakamani mashahidi wanne.
Katika maelezo yake ya utetezi, Dk Slaa alikiri kuwa na uhusiano na mwanamke huyo, lakini akajitetea kuwa alikuwa hajui kuwa ni mke wa mtu kwa kuwa mwanamke huyo hakuwahi kumwambia kuwa ameolewa.
Dk Slaa alidai kuwa alijua kwa mara ya kwanza kuwa mwanamke huyo ameolewa baada ya kusoma na kusikia taarifa hizo katika vyombo vya habari.

Licha ya kukiri kuwa na uhusiano na mwanamke huyo ambao hata hivyo hakuufafanua kuwa ni wa aina gani, Dk Slaa alikanusha tuhuma za kuzini naye wala kumtambulisha kuwa mke wake.
Lakini katika majibu, Mahimbo alisisitiza kuwa Dk Slaa alifanya uzinzi na mke wake na kwamba alifanya hivyo akiwa anajua kuwa ni mke wa mtu.
Alidai baada ya Dk Slaa kumtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, habari hizo ziliandikwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini jambo ambalo lilitosha kumjulisha kuwa alikuwa akifanya uzinzi na mke wa mtu, lakini aliendelea kuzini naye.
Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010 ilifunguliwa mahakamani hapo Septemba 7 mwaka huu, siku chache baada ya Dk Slaa kumtambulisha Josephine mara kadhaa kupitia kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa ni mchumba wake

No comments:

Post a Comment