KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, September 29, 2010

Kahaba Ajitamba Kula Uroda na Beckham



Kahaba Irma Nici ameendelea kujitamba kuwa alikula uroda na mcheza soka maarufu wa Uingereza, David Beckham ingawa Beckham anajiandaa kufungua kesi ya madai ya fidia kiasi cha dola milioni 16.
Pamoja na kwamba wanasheria wa mcheza soka maarufu wa Uingereza, David Beckham anayesakata kabumbu nchini Marekani wako kwenye jitihada za kufungua kesi mahakamani kumdai fidia ya dola milioni 16, kahaba anayedai kutembea na Beckham ameibuka na kutamba ana ushahidi wa kuthibitisha madai yake.

Kahaba Irma Nici mwenye asili ya Bosnia amedai kuwa anaweza kuithibitishia mahakama kuwa alilala na nyota huyo wa soka mjini London na mjini New York mnamo mwaka 2007.

Nici amedai kuwa Beckham ana alama za kipekee kwenye sehemu zake nyeti hivyo ajiandae kuvua suruali yake mahakamani ili kuzithibitisha alama hizo.

Nici mwenye umri wa miaka 26 amekuwa akiwakwepa wanasheria wa Beckham na amekuwa akijificha kwenye hoteli mjini New York.

Beckham mwenye umri wa miaka 35 anamshtaki Nici kutokana na habari iliyotoka kwenye jarida moja la Marekani kuwa Beckham alinunua penzi la kahaba Nici.

Nici aliliambia jarida hilo kuwa alishea kitanda kimoja na Beckham wakati Beckham alipofanya mapenzi yaliyowahusisha wanawake wawili kwa mpigo. Mwanamke wa pili aliyezungumziwa katika habari hiyo bado hajajulikana.

Beckham anamshtaki Nici na jarida hilo kwa kuandika habari za kumpakazia kuwa aliisaliti ndoa yake na Victoria Beckham, 36,

Beckham pia anamshtaki Nici na jarida hilo kwa habari ambayo imemfanya Beckham aonekane aliyatia maisha ya mkewe hatarini kwa kutembea na kahaba

Watano Wafariki Katika Mashindano ya Kunywa Pombe




Watu Watano wamefariki wakati wakishindana kunywa pombe katika mji mmoja kaskazini mwa Msumbiji.
Watu watano wafanyakazi wa kiwanda kimoja cha bia nchini Msumbiji wamefariki wakati wakishandana na atamaliza mapema kunywa chupa tano za pombe kali.

Wanaume hao walifariki katika mashindano ya kunywa pombe yaliyofanyika kaskazini mwa Msumbiji, shirika la habari la Msumbiji la Noticias lilisema.

Vifo vya wanaume hao vilitokea katika hatua tofauti za mashindano hayo ya kunywa kwa haraka chupa tano za bia mpya ya kiwanda cha bia cha mji wa Nampula.

Polisi wametoa taarifa ya tukio hilo ikiwa ni mwezi mmoja baada ya tukio hilo kutokea katika mji wa Alto Molocue.

Taarifa zilisema kuwa vifo vya wanaume hao ambao walikuwa ni wafanyakazi wa kiwanda kilichotengeneza bia hizo, vilitokea wakati wa promosheni ya kuzitangaza bia hizo.

Baadhi ya washiriki walifariki punde tu baada ya kupiga fundo chache za bia hiyo, liliripoti gazeti la Noticias.

Mkuu wa mkoa wa Alto Molocue ameanzisha uchunguzi kuhusiana na vifo hivyo

Msafara wa Lipumba wapata ajali tena



MSAFARA wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, umepata ajali kwa mara nyingine na kusababisha askari mmoja kujeruhiwa kichwani.
Askari huyo PC Johnson mwenye namba E.9551 aliyekuwa katika msafara wa Profesa Lipumba, amelazwa kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Basilio Matei, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi, majira ya jioni katika eneo la Oysterbay katika Manispaa ya Arusha.

Na kusema kuwa, askari polisi PC Jophnson aliyekuwa na namba E.9551 alijeruhiwa kichwani katika ajali hiyo.

Alisema gari aina ya Toyota Land Cruiser, lilipita kwa kasi kwenye tuta, hali ilifanya kumtupa askari huyo nje ya gari.Pia gari jingine liligongana na gari hilo la polisi kwa mbele na gari alilokuwemo mgombea huyo kuyumba na dereva kutetea lisipinduke.

Hii ni ajali ya pili kutokea katika msafara wa Profesa Lipumba baada ya nyingine iliyotokea wilayani Kilindi, mkoani Tanga wiki iliyopita.

Katika ajali hiyo, gari moja lilichomoka tairi na jingine lililokuwa limebeba waandishi wa habari kupinduka lakini katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha ila kulikuwa na majeruhi.

Akiri kupata mtaji kwa njia ya udanganyifu



KIJANA aliyejitambulisha kwa jina moja la Seid, anayefanya shughuli zake za biashara katika maeneo ya Kariakoo amekiri kuwa kukosa elimu siyo kigezo cha kukosa msingi wa masiha.
Hayo aliyasema katika mazungumzo maalum na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.

Seid aliweza kuiambia NIFAHAMISHE kuwa miaka mitatu nyumba alifika jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Shinyanga ambapo alidai aliweza kuwatoroka wazazi wake kwa lengo la kuja kujitafutia maisha jijini humo.

Alidai kuwa, aliingia jijini humo huku akijua ataweza kutimiza ndoto zake kwa kuwa alikuwa na lengo la kuja kufanya biashara na alipowaeleza wazazi wake walimzuia abaki na kufanya shughuli hizo nyumbani kwao.

Alidai alipoingia jijini humu aliwatafuta jamaa zake na aliweza kupita katika maofisi mbalimbali akidai anaomba misaada wa nauli ili aweze kurudi nyumbani kwao.

Alidai Mungu aliweza kumsaidia na aliweza kupata wasamaria mbalimbali wakimpa pesa taslimu ili aweze kutumia nauli hiyo na alidai alikuwa akizihifadhi pesa hizo ili uwe mtaji wake wa kuanzia biashara.

Alidai katika zoezi hilo aliweza kujikusanyia kiasi cha shilingi laki mbili na kuacha kuomba msaada huo na aliunganisha na kiasi cha shilingi laki moja ambazo alikuwa nazo na kuanza kufanya biashara ya mitumba maeneo ya Manzese kwa jamaa yake huyo.

Alidai kuwa mtaji wake uliweza kukua kidogokidogo na hadi sasa anaendeleza biashara zake hizo

Kiongozi wa NK anuia kumpokeza mwanaye.



Mwanaye kiongozi wa N.K Kim Jong un

Mtoto wa kiume wa mwisho wa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-il, ameteuliwa katika nyadhifa mbili za juu nchini humo. Kijana huyo Kim Jong-un aliye na chini ya miaka 30 hajawahi kuhudumu katika afisi yoyote ya umma nchini humo na hatua ya kumteua inaonekana kuwa maandalizi yake kuchukuwa wadhifa wa baba yake kama kiongozi wa nchi.

Uongozi wa Korea Kaskazini

Kuchambua uongozi wa Korea Kaskakazini wenye usiri mwingi sio kazi rahisi, lakini inaonekana wazi kuwa Kim Jong-Un sasa ameteuliwa kuchukua uongozi wa nchi hiyo.

Hii inashiria mwanzo wa kipindi cha mpito ambacho muda wake bado haujajulikana.

Babake, Kim Jong-Un anaugua na inaaminika kuwa alipooza mara mbili , mwaka wa 2008. Uamuzi wake wa kuanzisha kipindi hiki cha mpito ni ishara kwamba hali yake ni mbaya.

Kim Jong - Un ni nani?

Machache yanajulikana kuhusu Kim Jong-Un tangu wakati alipokuwa akisomea nchini Uswizi. Hata umri wake haujulikani na inadhaniwa kuwa ana umri wa miaka 27.

Hali ya wasiwasi inazingira mipango ya kumrithi Kim Jong-Il. Huenda Kiongozi huyo wa kikomunisti akaondoka madarakani polepole au huenda kiongozi mwenye ushawishi ,mwenye cheo cha tatu cha juu katika utawala huo, Jang Song-Thaek, ambaye pia ni mwenyekiti wa tume kuu ya kitaifa ya ulinzi, akafanywa kuwa mshauri wa kijana Kim Jong-Un?

Swali lingine ni kuhusu shughuli ya kumuandaa kijana Un. Je! itachukua muda gani kabla ya yeye hatimaye kushikilia wadhifa huo?

Hii ndio sababu waangalizi wa nje wa masuala ya Korea Kaskazini wana wasiwasi sana.

Korea Kaskazini bado inatawaliwa kijeshi. Kama kutafanyika mabadiliko machache katika tume kuu ya jeshi la nchi hiyo, basi huenda uhusiano na nchi za nje usibadilike

Uokoaji wa Marekani waisha vibaya



Mashua nyepesi

Takriban watu 13 walizama na wengine wanane hawajulikani walipo baada ya manowari ya kijeshi ya Marekani yalipojaribu kusaidia mashua nyepesi ndogo tena nyembamba iliyoharibika kwenye ghuba ya Aden.

Maafisa wa manowari hayo ya kijeshi mjini Washington walisema USS Winston Churchill ilijaribu lakini ilishindwa kurekebisha injini ya mashua hayo mepesi.

Ikaanza tena kuyavuta manowari hayo pwani ya Somalia.

Lakini jitihada za uokoaji zilibadilika na kuwa balaa wakati abiria walipokimbilia upande mmoja wa chombo hicho kupata chakula na misaada, na kusababishia ipinduke.

Abiria wote 85 walirushwa kwenye maji, japo wengi wao waliokolewa.

Jeshi hilo la majini la Marekani lilikuwa na Waethiopia 75 na Wasomali 10, na boti hiyo ilikuwa ikitokea Somalia.

Uchunguzi
Boti hiyo mwanzo iligunduliwa katika ghuba ya Aden siku ya Jumapili.

Baada ya mabaharia kutoka kwenye manowari kushindwa kurekebisha injini ya mashua hayo madogo, walianza kukivuta chombo hicho pwani ya Somalia.

Abiria 61 waliokolewa na kwa sasa wako kwenye meli ya USS Churchill, lakini 13 walizama na wanane hawajulikani walipo.

Jeshi hilo lilisema bado linafanya uchunguzi kujua kitu gani kilitokea.

Haijajulikana wazi kwanini mashua hayo yalikuwepo eneo hilo, njia inayopita meli nyingi iliyokumbwa na mashambulio na maharamia wa Kisomali.

Lakini Umoja wa Mataifa umesema takriban Waafrika 74,000- zaidi kutoka Ethiopia na Somalia- walivuka ghuba ya Aden kuelekea Yemen mwaka 2009 wakikimbia umaskini na migogoro

Bepari wa Misri afungwa kwa mauaji



Suzanne Tamim


Bepari wa Misri amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kuamrisha mauaji ya mwimbaji maarufu wa Lebanon Suzanne Tamim, baada ya kesi hiyo kusikilizwa tena.

Hisham Talaat Moustafa, mwanachama mwandamizi wa chama tawala cha Misri, alihukumiwa kifo baada ya kesi yake kusikilizwa mwanzo- lakini majaji walipinga kifungo hicho na kuamuru kesi kusikilizwa upya.

Mwenzake Mohsen al-Sukkari alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kumwuua Tamim.

Alikutwa kwenye hoteli huko Dubai mwaka 2008 huku shingo yake ikiwa imekatwa.

Keshi hiyo imepata ushabiki mkubwa, kutokana na Moustafa kuonekana ni mwenye hadhi kubwa nchini humo.

Mahakama ilisikia namna Moustafa, ambaye alikuwa na uhusiano na mwimbaji huyo, alivyoamuru mauaji hayo.

Inaaminiwa kuwa alimlipa Sukkari dola za kimarekani milioni mbili kumwuua Tamim ikiwa hatua ya kulipiza kisasi baada ya kukataa ombi la kufunga naye ndoa.

Tamim alikuwa mwimbaji huku akijulikana kwa misukosuko katika maisha yake binafsi na kipaji chake.

Alianza kupata umaarufu baada ya kushinda katika onyesho la vipaji kwenye televisheni ya Arabuni miaka ya 90.

Mwanawe Kim Jong-il ateuliwa Generali



Shirika la habari la Korea Kaskazini limesema mtoto wa kiume wa mwisho wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Il, ameteuliwa kuwa Jenerali wa ngazi ya juu katika jeshi la nchi hiyo.

Ni mara ya kwanza kwa jina la Kim Jong Un ambaye anadhaniwa anakaribia umri wa miaka thelathini, kuchapishwa na vyombo vya habari nchini humo, licha ya kuongezeka kwa fununu kuwa kiongozi wa nchi hiyo anamwandaa mwanawe kumrithi.

Mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini amesema ikiwa Kim Jong Un atateuilwa kuwa mmoja wa maafisa wakuu wa chama wakati wa mkutano wa baraza kuu la chama hicho ambao unaanza hivi karibuni, itakuwa ni ishara kuwa Korea Kaskazini inanuia kuendeleza utawala wa kurithishana kuelekea kizazi cha tatu cha familia hiyo

Haramia wa Kisomali akamatwa Tanzania


Jeshi la Tanzania



Maharamia wa Kisomali


Jeshi la Tanzania limesema limemkamata mshukiwa mmoja wa Uharamia raia Somalia, kufuatia makabiliano makali ya ufyatulianaji wa risasi katika bahari ya Hindi.

Ripoti zinasema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili iliyopita katika eneo la Kusini mwa pwani ya Tanzania, eneo ambalo meli ya kampuni ya kuchimba mafuta ya Ophir inafanya utafiti ili kubainisha ikiwa eneo hilo lina utajiri wa mafuta ya Petroli.

Msemaji wa jeshi la wanamaji nchini Tanzania, Steve Buyuya, amesema manuawari ya kijeshi ilishambuliwa kwa risasi na maharamia waliokuwa kwenye mashua ndogo.

Lakini baada ya ufyatulianaji wa risasi uliodumu kwa muda, maharamia kadhaa walifanikiwa kutoroka huku mmoja wao akikamatwa na wanamaji wake.

..Mjumbe wa UN, Wallstrom kuzur DRC leo


Mjumbe wa Umoja wa Mataifa

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya dhuluma za kimapenzi katika maeneo yenye mizozo, Margot Wallstrom, anatarajiwa kuwasili Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hivi leo.

Ziara hiyo inajiri baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyobainisha kuwa mamia ya raia walibakwa katika kipindi cha siku nne kati ya mwezi Julai na Agosti katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Makundi matatu ya waasi yanadaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya ubakaji dhidi ya kina mama, wasichana na hata wavulana.

Akizungumza na BBC, Bi Wallstrom, amesema huenda kuna waathiriwa zaidi ya mia tano wa mkasa huo.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa umoja huo kutoa mafunzo zaidi kwa maafisa wake wa kutunza amani ambao wameshutumiwa kwa kutochukua hatua za kuzuia dhuluma dhidi ya raia

Monday, September 27, 2010

Couple makes 4,000-mile trek to see Team USA play



OSTRAVA, Czech Republic – Betty and Jonathan Hutchinson traveled 4,000 miles by plane and train to Eastern Europe for the women's world basketball championships, eager to watch Diana Taurasi, Sue Bird and anyone else with ties to the University of Connecticut.

The Hutchinsons certainly are dedicated to Huskies hoops. And to each other, too — she's 90, he's 88, and they're a long, long way from their New Hampshire home.

"Our son Jack really encouraged us to do this," Jonathan said over breakfast Sunday. "We thought it would be a really great last hoorah."

Connecticut coach Geno Auriemma, who's guiding the U.S. team, was astounded when he learned about the couple. He knows the UConn fan base is passionate, but still found it incredible they made the trip.

"It's unbelievable. I was shocked when I heard they were here," he said. "I think it makes what we're doing at Connecticut seem that much more rewarding and important because you have people take it that seriously that they'd come halfway around the world."

The 56-year-old Auriemma plans to meet with the Hutchinsons — married 60 years — before Monday's game against Canada.

The pair left their home in Concord and flew to Prague before taking a 3 1/2-hour ride to Ostrava to watch the first two rounds. The two have already become instant celebrities. They've been given a tour of the town by the president of the local rotary club and were given VIP seats at the arena.

"I don't know what they are making such a fuss about," said Jonathan, who graduated UConn in 1943 and played soccer at the school. "My wife and I would have been happy just sitting anywhere. But I learned a long time ago if someone offers you assistance to take it."

Auriemma has inspired the Hutchinsons, who plan to donate a dollar for every point the U.S. scores during the tournament to the All Baskets Count charity. It's the same charity that the Huskies coach pledged $50 to for every 3-pointer his team makes during the worlds.

The money will go to the construction of a "House for All Generations," where young men and women between 18 and 20 years of age will live together and take care of seniors requiring assistance.

"That's awesome," said Taurasi, who is Betty's favorite player. "When you have people that are in a position to help others and actually do it there's something special to be said about that."

The Hutchinsons have been helping people for years. Betty was a nurse and teacher before retiring, while Jonathan also taught and coached track and field. The couple met after Betty's sister lost her husband in World War II. Jonathan had been fraternity brothers with him and the two were married a short time later.

Even though he's been retired from coaching for a while, Jonathan still has one special athlete he trains: his wife. When he turned 80, the pair ran in the annual Thanksgiving road race in Manchester, Conn. — where Auriemma lives. She set the course record for her age group that year and has been running ever since.

She trains every day, running a few miles up and down hills near her home. She'll compete again in the race this year with a new challenge.

"My goal is to put up a record for 90-plus that will stand for a long while," she said.

Jonathan quickly pointed out: "Until you break it the next year."

Amchinja Mkewe na Kwenda na Kichwa Chake Baa!



Mwanaume mmoja wa nchini Hispania alimchinja mkewe na kukiweka kichwa chake kwenye begi na kwenda nacho baa kunywa pombe huku akiwatambia marafiki zake kuwa amemchinja mkewe.
Mwanaume huyo wa nchini Hispania alikunywa pombe na marafiki zake baa huku akiwa na kichwa cha mpenzi wake kwenye begi.

Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la kila siku la nchini humo la ABC Daily, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 34, aliwatambia marafiki zake aliokuwa akinywa nao pombe kwenye baa moja mjini Cordoba, kusini mwa Hispania kuwa amemchinja mkewe mwenye umri wa miaka 30 na kichwa chake kipo kwenye begi alilokuwa amelibeba.

Kwa jinsi alivyoonyesha utulivu hakuna mtu aliyemuamini mwanaume huyo kuwa amemchinja kweli mkewe pamoja na kwamba nguo zake zilikuwa na madoa ya damu.

Taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo lililotokea jumanne wiki hii zilisema kuwa mwanaume huyo baada ya kupata ulabu na marafiki zake, alitoka nje ya baa na kuparamia mlingoti wa umeme wenye urefu wa mita 30. Alipigwa shoti ya umeme akiwa kileleni baada ya kugusa waya wa umeme alidondoka chini na kupelekea kifo chake alipofikishwa hospitali.

"Muda mfupi baada ya watu kuanza kuondoka baa waliona dimbwi la damu barabarani na ndipo walipogundua kuwa mwanaume huyo hakuwa akitania, waligundua begi pembeni ya baa likiwa na kichwa cha mke wa mwanaume huyo", ilisema taarifa ya gazeti la ABC Daily.

Polisi wamethibitisha kuugundua mwili wa mwanamke aliyechinjwa na pia walithibitisha kuwa muuaji wake aliyetambulishwa kwa herufi za majina yake MRTR alifariki dunia hospitalini baada ya kudondoka toka kwenye mlingoti wa umeme.

Pembeni ya mlingoti wa umeme walikuta kisu ambacho kinaaminika kilitumiwa na mwanaume huyo kumchinjia mkewe, ilisema taarifa ya polisi.

Polisi wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha mauaji hayo

Mdahalo vijana wang'ara



MDAHALO uliowashirikisha wagombea ubunge wa vyama pinzani umevutia kwa wagombea hao kila mmoja kumwaga sera zake na kutetea ilani za vyama vyao katika uchaguzi mkuu ujao.
Wagombea hao vijana kutoika chama cha Wananchi [CUF], Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF), wameonyesha uwezo mkubwa wa kuzinadi sera zao na ushujaa wa kujibu maswali ya papo kwa papo.

Mdahalo huo ulifanyika juzi katika Hoteli ya MovenPick ya jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ITV na kuhudhuriwa na wadau wapatao 200.

Wagombea hao wote kwa pamoja waliwasilisha hoja na kuahidi kubadili na kufanya marekebisho ya katiba na mfumo wa utawala nchini pindi watakapoingia Ikulu.

Katika kuwasilisha hoja hizo mgombea ubunge jimbo la Kawe kupitia Chadema, Bi. Halima Mdee alsiema pia watashughulikia swala la ufisadi na kuahidi kuunda mahakama maalum itayowashughulikia mafisadi hao.

Nae John Mnyika [Chadema] Ubungo alisema watakapopewa ridhaa hiyo na wananchi wataweza kuekebisha kero za ajira zinazoisumbuba nchi na kurekebisha vikwazo vyote vinavyosababisha vijana kukosa ajira wanapotoka vyuoni.

Nae Zitto Kabwe, mgobmea ubunge Kigoma Kaskazini kupitia Chadema, alisema chama hicho kikipata ridhaa ya wananchi itaboresha katika sekta ya madini ambayo chama hichdo hawakubaliani na serimali ya chama cha Mapinduzi.

Kwa Upande wa wagombe kutoka CUF akiwemo Miraji Mitubuliko, alisema kitapitia upya mikataba ya madini, na kueleza kuwa wataunda serikali tatu ambayo itaruhusu masuala ya Zanzibar kuamuliwa na Wanzibar wenyewe

Wanafunzi mbaroni kwa mauaji



WANAFUNZI wanne wakiume wa Shule ya Msingi Ufukoni iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, wenye umri kati ya miaka 15 hadi 17 wametiwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa darasa la tano Jesica Ngosi (10).
Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema kuwa, tukio hilo la mauaji lilitokea juzi majira ya saa 2 usiku.

Kamanda Misime alisema kuwa wanafunzi hao wanashikiliwakwa kuhusika katika tuiko hilo na mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa ukiwa na majeraha mbalimbali mwilini yaliyotokana na kuchomwa na vitu vyenye ncha kali.

Aliendela kusem kuwa kabla ya mauaji hayo marehemu aliondoka nyumbani hapo na binamu [17] jina limehifadhiwa, mkazi wa Tungi Kigamboni na binamu yake huyo alirudi majira ya saa mbili usiku akiwa mwenyewe na alipoulizwa mwenzake huyo alikwua wapi alijibu amekwenda kucheza na wenzake wengine wka kwua walimuita.

Alisema kutokana na jibu hilo, dada wa marehemu alipatwa na wasiwasi baada ya kumuona binamu yao huyo akihha kutafuta maji na kunawa mikono na kuvua shati lake na kuanza kulisafisha hali ambayo ilimshangaza na alipotoka kwenda kumtafuta mtoto huyo alimzuia na dada huyo aliendelea kumsaka mdogo wake huyo na binamu yake kumfata nyuma na alimkataza asipite njia ya makaburini walipofanya tukio hilo.

Ndipo dada huyo alipoamua kurudi nyuma kwanza kwenda kutoa taarifa kwa baba yao kufuatia tukio hilo na kwa pamoja akiwa na baba yake walipofuatilia njia hiyo walikuta mwili huo ukiwa mfu na ukiwa na majeraha maeneo ya shingoni, sehemu zake za matiti kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali.

Baada ya hapo walitoa taarifa kituo cha polisi na polisi walianza msako kumsaka kijana ambae ni binamu wa marehemu na kumkuta akiwa chumbani kwake akiwa amejitundika kamba tayari kwa kujinyonga na alipohojiwa na skari alikiri kuhusika na aatukio hilo na kueleza likuwa na wenzake wengine watatu na waliweza kukamatwa mara moja.

Kamanda Misime amesema kuwa majina ya wanafunzi hao kwa sasa yanahifadhiwa kwa sababu za kipolisi na yatawekwa bayana pindi upelelezi utakapokamilika

Mombasa Raha yaua watano



WATU watano wamefariki dunia papo hapo na wengine 11 kujeruhiwa, kufuatia ajali mbaya ya magari kugongana uso kwa uso iliyohusisha basi la kampuni ya Mombasa Raha.
Ajali hiyo, ilitokea juzi, majira ya saa 11:45 jioni huko eneo la Usanda Wilayani Shinyanga.

Basi hilo la abiria lilikuwa lenye namba za usajili T 854 DDF, lilikuwa likitokea wilayani Kahama kwenda mkoani Mwanza na, liligongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya Scania yenye namba za usajili T 295 AHH, lililokuwa likitoka jijini Mwanza kwenda mkoani Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Bw., Daudi Siasi, alitoa taarifa hiyo na kusema kuwa watu wanne waliokuwemo ndani ya lori hilo, walipoteza maisha pamoja na abiria mmoja aliyekuwa ndani ya basi hilo la abiria.

Kamanda Siasi alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe uliosababishwa na dereva wa lori kuhama njia yake na kulifata bsi hilo la abiria.

Aliwataja marehemu hao kuwa ni dereva wa lori hilo, Bw.Josia Mandago (37), konda wake Hoti Safari (27) na wanaume wengine wawili waliokuwa wakisafiri na lori hilo ambao majina yao hayakupatikana mara moja na abiria mmoja aliyekuwa kwenye basi aliyetambulika kwa jina la Ramadhan Magoma (45) mkazi wa Ndembezi mjini Shinyanga

Marekani mbioni kunusuru mazungumzo ya amani



Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani PJ Crowley amesema msimamo wa Marekani haujabadilika. Taarifa hiyo imetolewa baada ya kumazilika kwa marufuku ya miezi kumi yaliyowekwa na Israel dhidi ya ujenzi wa makaazi hayo.

Marekani imejikuta katikati ya mgogoro ambao kila mtu alijua huenda ukatokea. Rais Abbas daima amekuwa akisema kuwa ujenzi wa Israel wa makazi mapya lazima usitishwe, ili kumuezesha kuendelea na mazungumzo ya amani kati yake na uongozi wa Israel.

Lakini usitishwaji wa muda wa ujenzi wa makazi hayo kwa sasa umemalizika.Hata hivyo Marekani inaishinikiza Israel iongoze muda wa usitishaji wa ujenzi huo.

Waziri mkuu wa Israel , Benjamin Netanyahu , amemtaka bw Abbas kutojitoa katika mazumgumzo ya amani kama njia ya kupinga mpango wa Israel wa ujenzi wa makazi mapya, na badala yake amemtaka kuendelea na moyo wa uaminifu ili kufikia mkataba wa amani wa kihistoria kati ya pande hizo mbili.

Mstakabali wa mazungumzo hayo unatengemea maoni ya viongozi wengine wa nchi za kiarabu ambao wanatarajiwa kukutana mjini Cairo Misri, siku kumi zijazo.

Bw Abbas anasema hatajiondoa kwenye mchakato wa mazungumzo hayo hadi hapo viongozi hao watakapo shauriana naye.


"Kuna chaguo moja tu, kuendelea kwa ujenzi wa makazi au amani. Israel lazima ichague amani. Iwapo Israel itachagua amaniu tutaendelea na mazungumzo, lakini ikishindwa kuchagua hilo, basi hii itakuwa ni kupoteza muda au kupoteza fursa ya kufikia amani."Amesisitiza rais wa Palestina.

Walowezi wa kiyahudi katika maeneo yanayokaliwa ya ukingo wa magharibi wa mto Jordon wamekuwa wakisheherekea kumalizika kwa muda uliowekwa wa kusitisha ujenzi katika maeneo hayo.

Walianza kusherekea hata kabla ya muda wenyewe kumalizika. Katika moja ya makazi hayo walirusha maputo na kuchimba kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya watoto wadogo, licha ya ombi la Waziri mkuu wa Palestina Benjamin ya kutaka kujizuia na aina yoyote ya ghasia baada ya kumalizika kwa muda huo

Rwanda yaahidi kushirikiana na Umoja wa Mataifa



Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amempongeza rais wa Rwanda Paul Kagame kwa kubadilisha msimamo wa awali kuwaondoa wanajeshi wake kushiriki katika shughuli ya amani ya Umoja wa Mataifa huko Darfur, Sudan.

Rwanda ilitishia kusimamisha ushirikiano wake na Umoja wa Mataifa mwezi jana kufuatia ripoti iliyofichuka ambapo jeshi la nchi hiyo lilituhumiwa kutekeleza uhalifu wa kivita katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema kwenye kikao kilichofanyika pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, rais Kagame alijadili kuhusu ripoti hiyo inayotarajiwa kutolewa mwezi ujao na na katibu Mkuu Ban Ki Moon.

Ripoti hiyo imenadi visa 600 vya dhuluma dhidi ya binadamu vilivyotekelezwa katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya mwaka 1993 na 2003.

Rais wa Somalia aomba msaada zaidi - UN


Rais wa Somalia, Sharif Sheikh Ahmed ameliomba baraza kuu la Umoja wa Mataifa kusaidia serikali yake ya mpito na pia juhudi zake za kuleta uthabiti nchini humo.

Rais Ahmed pia ametoa wito kwa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio litakalosaidia kuzuia kusambaa wa mitandao ya Al Qaeda, na makundi mengine ya wapiganaji wa kiislamu kama vile Al Shabaab.

Akihutubia baraza kuu la Umoja huo mjini New York, rais Ahmed alikariri haja ya kutatua kwa dharura matatizo ya kisiasa na kiuchumi yanayokumba Somalia

Meli ya Ugiriki yatekwa nyara- Somalia


Maharamia wa Kisomali


Jeshi la muungano wa ulaya linaloshika doria katika pwani ya somalia, limesema meli moja ya mizigo ya Ugiriki imeshambuliwa na kutekwa nyara na maharamia.

Jeshi hilo la EU limesema meli hiyo kwa jina Lugela lilikuwa umbali wa maili 900 kutoka pwani ya somalia wakati ilipotuma mawasiliano ya dharura.

Tangu wakati huo, hakuna habari zozote kuhusu meli hiyo iliyokuwa imesheheni bidhaa za chuma. Wanajeshi hao wa EU wanasema meili hiyo ilibadilisha mkondo wake na kuelekea Somalia.

Meli hiyo ilikuwa na mabaharia 12 raia wa Ukraine.

Umoja wa Mataifa na AU kuunda tume ya pamoja


Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika imebuni kamati ya pamoja itakayoshughulikia masuala ya amani na Usalama.

Kamati hiyo natarajiwa kukutana mara mbili kila mwaka ili kujadili masuala yanayopaswa kufanyika kwa wakati huo na pia kupanga mikakati ya siku zijazo.

Kamati hiyo inanuiwa kuimarisha ushirikiano katika harakati za kuzuia mizozo na masuala ya kutunza amani barani Afrika.

Jeshi la Pamoja la muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa limekuwa likihudumu katika jimbo la Darfur tangu mwaka wa 2008.

Umoja wa Mataifa vile vile hutoa msaada kwa jeshi la muungano wa Afrika linalohudumu nchini Somalia

Watu milioni 2 wahama makwao-Nigeria



Maafisa wa serikali nchini Nigeria, wanasema zaidi ya watu milioni 2 wameyahama makwao baada ya utawala wa nchi hiyo, kufungua milango ya kuzuia maji katika mabwawa mawili.

Hatua hiyo ilisababisha mafuriko katika maeneo ya Jigawa karibu na jimbo linalopakana na jangwa la Sahara.

Maafisa wa serikali wanasema, milango hiyo ilifunguliwa baada ya uchunguzi kubainisha kuwa mabwawa hayo huenda yakafurika na kusababisha maafa zaidi.

Watu zaidi wanaendela kuhamishwa kutoka maeneo ya mabonde hadi maeneo ya milima.

Majimbo kadhaa nchini humo yameathiriwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha miezi miwili iliyopita nchini humo

Kura ya maamuzi Sudan kufanyika Januari


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Rais wa Marekani, Barrack Obama wameliambia kongamano la Umoja wa Mataifa linaloendelea jijini New York Marekani kuwa kura ya maamuzi kuhusu uhuru wa eneo la Sudan Kusini ni sharti iandaliwe kama ilivyopangwa na kwa njia ya amani.

Viongozi hao wawili wametoa wito kwa serikali za Sudan Kaskazini na Kusini kuandaa kura hiyo, kama ilivyopangwa mwezi Januari hapo mwakani na kuheshimu matokeo yake.

Maandalizi ya kura hiyo ya maamuzi yamecheleweshwa na kiongozi wa Sudan Kusini, Salva Kirr amesema kuchelewa huko kunaweza kusababisha ghasia na machafuko.

Inaaminika kuwa raia wa Sudan Kusini watapiga kura kuunga mkono uhuru wa eneo hilo.

Wakati huo huo Muungano wa Afrika, AU, umetoa wito kwa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuchelewesha mashtaka dhidi ya rais wa Sudan Omar Al Bashir kwa mwaka mmoja zaidi, ili kutohujumu maandalizi ya kura hiyo.


Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa rais Bashir, kwa shutuma za kuhusika na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki katika Jimbo la Darfur magharibi mwa taifa hilo.

Hotuba ya rais wa Iran yazua hisia kali



Rais wa Marekani, Barrack Obama ameyakashifu matamshi ya rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa na kuyataja kama matusi na ya kuudhi.

Rais Ahmedinejad aliliambia mkutano wa baraza hilo kuwa Marekani ilihusika yenyewe katika mashambulio ya kigaidi ya Septemba Kumi na Moja




Katika Mahojiano na BBC, Rais Obama amesema matamshi hayo ni tofauti kabisa na maoni ya raia wa Iran kuhusu mashambulio hayo.

Lakini katika kikao na waandishi wa Habari jijini New York, Ahmedinajad alitetea matamshi yake na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi kamili kuhusu mashambulio hayo ya Septemba 11 ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu alfu tatu.

Ahmadinejad azua tafrani katika mkutano wa UN


Rais wa Iran Ahmedinejad: Amedai huenda Marekani ilipanga mashambulizi ya Septemba 11, 2001



Zaidi ya wajumbe thelathini wakiongozwa na Marekani walitoka nje kwa hasira katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa hotuba ya rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad.

Waliondoka baada ya rais Ahmadinejad kuelezea kwamba Marekani yenyewe huenda ilihusika kupanga mashambulio ya Septemba 11, 2001, ili kuimarisha mashambulizi yake mashariki ya kati na kuilinda Israeli.


Marekani imeelezea kauli hiyo kama isiyovumika.

Akizungumza kuhusu mpango wa Nuklia wa serikali yake rais huyo wa Iran alikosoa vikwazo vya kimataifa dhidi ya nchi yake na kuelezea nishati ya nuklia kama zawadi kubwa

Thursday, September 23, 2010

“Tanzania bila ya Ukimwi inawezekana” yazaa mtunda





IMEDAIWA kuwa kasi ya wimbi ya mambukizi nchini Tanzania inapungua kwa kasi kutokana na juhudi zinazofanyika kumaliza maambukizi hayo.



Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk. Fatuma Mrisho katika mjadala uliowakutanisha watalamu wa afya jijini Dar es Salaam kujadili mbinu mbalimbali kukabiliana na tatizo hilo.



Alisema kuwa kwa sasa kasi ya maambukizi inapungua na kutoa takwimu kuwa kuwa watu million 1.8 ndido wanaoishi na virusi kwa sasa nchini.

Alisema serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali inatumia kila aina ya mbinu kuhakikisha maambukizi yanapungua nchini.

Alisema Tacaids imepata mafanikio makubwa toka kuanzishwa kwake na lengo la kumaliza tatizo hilo na kubaki na Tanzania isiyo na ukimwi inavuka lengo.

Alisema Tacaids imekwua ikizunguka nchini kote kutoa elimu ya ukimwi ambayo kwa sasa imeonekana kuzaa matunda na wananchi kuelewa vizuri elimu hiyo.

Hata hivyo alibainisha kuwa katika maambukizi hayo wanawake ndio wameonekana kuambukizwa zaidi kuliko wanaume

Michezo ya Jumuiya ya Madola Delhi yaanza




Michezo ya Jumuiya ya Madola 2010 imeanza vyema huku sherehe za ufunguzi zikifanyika katika uwanja wa Jawaharlal Nehru.

Wanamichezo kutoka nchi 71 walipita mbele ya uwanja huo waliongozwa na wenyeji wa 2006 na mwisho walikuwa wenyeji wa mwaka huu India.

Mwanamfalme wa Uingereza Charles na rais wa India Pratibha Patil alitangaza kuanza rasmi kwa michezo hio,lakini mwenyekiti wa kamati iliyoandaa michezo chair Suresh Kalmadi alizomewa na umati uliokuwepo uwanjani.

Licha ya matatizo yaliyotatiza maandalizi,sherehe ya ufunguzi iliyokua na washiriki 9,000 walioonyesha utamaduni wa India zilienda vizuri.

Katika taarifa yake,Kalmadi alisema kuwa India iko tayari kuwa mwenyeji wa michezo hio.


''Tumekuwa na changamoto nyingi lakini tumejitahidi na kukabiliana nazo," alisema.

Inakisiwa kuwa $6bn (£3.8bn) zilitumika - mara 60 zaidi ya kiwango kilichotengwa wakati walipopewa uwenyeji mwaka 2003

Ujumbe wa UN kuzuru Sudan



Hali ya wasi wasi imeikumba jamii ya kimataifa kuhusu mstakabali wa Sudan.Moja wapo ya maafikiano ya mpango wa amani ilikuwa kufanyika kura ya maoni kuamua uhuru wa Sudan Kusini ambayo imepangwa mwakani.

Hata hivyo mipango kufanikisha kura hiyo ingali kufanyika hali inayotishia kuzuka upya kwa mapigano.Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulifanya kikao maalum kujadili Sudan ambapo rais Barack Obama alikuwa miongoni mwa waliohudhuria.Kuanzia leo ujumbe kutoka Baraza la Usalama utazuru Sudan ambapo utapitia Uganda.

Katika siku chache watakazokuwa Sudan,wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa watakapa nafasi ya kujionea baadhi tu ya matatizo mengi yanayoikumba nchi hiyo.

Ziara yao inaanzia Juba ambapo raia wa Sudan Kusini wamekuwa na wasiwasi kuhusu matayarisho yasiyoridhisha ya kura ya maoni.Uandikishaji wa wapiga kura haujaanza bado na wengi Sudan Kusini wanashuku kuwa viongozi wa kaskazini wanahusika katika ucheleweshwaji wa usajili wa wapiga kura.

Kwa saa chache watakuwepo El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur,magharibi mwa Sudan ambapo mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanaendelea.Lakini miongoni mwa orodha ya wanasiasa watakao kutana nao mmoja hawatakutana naye.

Rais Al Bashir anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya ICC kwa madai ya uhalifu wa kivita,uhalifu dhidi ya binaadamu na mauaji ya halaiki yote akidaiwa kuyatakeleza Darfur.Baraza la usalama la umoja wa mataifa limesema halitakutana naye,jambo lililokasirisha sana serikali ya Sudan,Khartoum.

Kila mtu aliye ndani ya Sudan na wale walio nje wanakubaliana kuwa huu ni wakati muhimu katika historia ya nchi hiyo,lakini haifahamiki kuwa ziara hii itakuwa na athari gani kubwa kwa nchi ya Sudan

Nigeria: Mshukiwa wa bomu akamatwa SA



Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi nchini Nigeria ametiwa nguvuni kuhusiana na mashambulio ya bomu nchini Nigeria ya Ijumaa iliyopita.



Henry Okah alikamatwa na maafisa wa polisi wa Afrika Kuisni katika nyumba yake mjini Johannesburg. Okah aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la MEND kundi la waasi lililofanya mashambulio mengi dhidi ya maeneo ya mafuta.



Kundi hilo limedaiwa kuhusika katika mashambulio hayo japo lilikuwa linastahili kutekeleza usitishwaji wa vita chini ya makubaliano kati yake na serikali

TZ:Jeshi laahidi usalama katika uchaguzi



Jeshi la Tanzania limetoa onyo kwa wanasiasa dhidi ya kuchochea mapigano huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu.

Mkuu wa jeshi Genereli leteni Abdulrahman Shimbo amesema kuwa wamepata vidokezo kuwa kuna baadhi ya wanasiasa na makundi wanaonuia kuvuruga shughuli za kampeini kabla ya kufanyika uchaguzi huo.

Hata hivyo amesema kuwa jeshi liko tayari kukabili vurugu zozote. Siku ya Alhamisi, mmoja wa wanasiasa wa upinzani nchiniTanzania aliwaambia wanahabari kuwa kutatokea umwagaji wa damu iwapo uchaguzi huo wa 31st October hautafanyika kwa haki na uwazi.

Wanasiasa sita wa upinzani wamejitokeza kugombea kiti hicho cha urais kumpinga kiongozi wa sasa Jakaya Kikwete

Vipaji Vingine Mhh!



Mrembo wa Ujerumani mwenye matiti makubwa yenye ukubwa wa 46H aliwaacha hoi watazamaji na majaji wa shoo ya luninga ya kutafuta watu wenye vipaji vya kipekee nchini humo baada ya kuonyesha kipaji chake cha kipekee.

Mwanamke huyo aliwashangaza watu kwa jinsi alivyoyatumia matiti yake kuvunja mbao na matikiti maji.

Mwanamke huyo aliwafanya baadhi ya majaji wa shoo hiyo washindwe kuangalia mbele kwa kutoamini vitu alivyokuwa akivifanya

Nyota wa R&B Matatani Kwa Kumpiga Mama Yake



Nyota wa muziki wa R&B, Mario Barret, au maarufu kama Mario amefunguliwa mashtaka kwa kumshambulia mama yake aliyekuwa akiishi naye katika nyumba yao iliyopo Baltimore, Maryland nchini Marekani.

Maafisa wa polisi waliitwa nyumbani kwao ambapo mama wa nyota huyo wa muziki, Shawntia Hardaway, aliwaambia kuwa mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 24 amemjeruhi.

Shawntia aliwaambia polisi kuwa Mario alimsukuma na kukibamiza kichwa chake ukutani na kumsababishia maumivu makali ya kichwa.

Shawntia aliongeza kuwa anahofia maisha yake kutokana na kwamba hilo ni tukio la pili mtoto wake amemshambulia ndani ya wiki moja.

Mwanasheria wa Mario, William "Hassan" Murphy III, alisema kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya kati ya mtoto mwenye mapenzi na mama yake ambaye anatumia madawa ya kulevya.

Mario alifunguliwa mashtaka na yuko nje kwa dhamana ya dola 50,000.

Waziri Mkuu Avaa Soksi Zenye Matobo



Anaiongoza mojawapo ya nchi tajiri duniani, pamoja na kwamba analipwa mshahara mkubwa sana, waziri mkuu wa Uingereza alienda kwenye kipindi cha luninga akiwa amevaa soksi zenye matobo.
David Cameron, waziri mkuu wa Uingereza ambaye analipwa mshahara wa paundi 142,500 (Takribani Milioni 336) kwa mwaka alinaswa na kamera akiwa amevaa soksi yenye tundu.

Cameron alifika kwenye studio ya televisheni ya ITV kwenye kipindi cha "This Morning" ili kuzungumzia maisha ya familia yake na kuzaliwa kwa mtoto wao mchanga wa kike.

Watazamaji wa kipindi hicho walishangazwa kuona soksi alizovaa waziri mkuu wao zikiwa na tundu.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeliongelea tukio hilo kwa kumbeza waziri mkuu kwa kusema "Anaiongoza nchi lakini ameshindwa hata kujinunulia soksi".

Ajiua Baada ya Video Akilawitiwa Kuwekwa Online



Mwanafunzi wa kiume wa nchini Marekani ambaye marafiki zake walirekodi kwa siri video wakati akiingiliwa kinyume cha maumbile na mwanaume mwenzie na kisha kuiweka video hiyo kwenye internet amejiua kwa kujirusha toka kwenye daraja.
Tyler Clementi, Mwanafunzi wa kiume wa mwaka wa kwanza wa chuo kikuu cha Rutgers University cha nchini Marekani mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa akifanya ushoga kwa siri, amejiua mwenyewe kwa kujirusha toka kwenye daraja baada ya video yake akiingiliwa kinyume cha maumbile na mwanaume mwingine kurushwa LIVE kwenye internet.

Clementi alijirusha wiki iliyopita toka kwenye daraja la George Washington na kuangukia kwenye mto mkubwa wa Hudson River, last week, maiti yake ilipatikana juzi kwenye mto huo.

Clementi alichukua uamuzi wa kujiua baada ya kugundua marafiki zake aliokuwa akikaa nao chumba kimoja walimrekodi kwa siri wakati akifanya mapenzi na mwanaume mwingine na VIDEO za tukio hilo zilirushwa LIVE kwenye internet kupitia Webcam.

"Kama angekuwa kitandani na mwanamke, haya yote yasingetokea", alisema mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho.

"Kama asingeanikwa LIVE kwenye internet, mambo yake ya ndani yasingeanikwa na leo tungekuwa naye hapa", aliongeza mwanafunzi huyo.

Wanafunzi wawili mmoja wa kiume Dhraun Ravi na mwingine wa kike Molly Wei, ambao wote wana umri wa miaka 18, wamefunguliwa mashtaka ya kuvunja haki za msingi za Clementi.

Mahakama iliambiwa kuwa webcam ilitumika kurusha LIVE tukio la Clementi akiingiliwa na mwanaume mwingine mnamo septemba 19 na Ravi alijaribu kulirusha LIVE tena tukio la pili lililofanyika septemba 21 ambayo ni siku moja kabla ya Clementi kujiua.

Taasisi za kutetea haki za mashoga zimeichachamalia kesi hii zikitaka Ravi na mwenzake wahukumiwe adhabu kali.

Taasisi hizo zimesema kuwa Ravi na mwenzake wameonyesha chuki waliyo nayo kwa mashoga na wasagaji na wameitaka mahakama itoe adhabu kali.

Ravi na mwenzake huenda wakahukumiwa kwenda jela miaka mitano iwapo watapatikana na hatia ya kuingilia undani wa mtu bila ya ridhaa yake

'Mama Yako ni Adui wa Taifa'



Kijana mmoja wa nchini Marekani ambaye alijifanya ni jasusi wa shirika la ujasusi la Marekani la CIA, amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumshawishi rafiki yake kumuua mama yake mzazi kwakuwa mama yake huyo alikuwa ni hatari kwa taifa.
Corderral Smith kijana mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikuwa mwanafunzi aliyefukuzwa shule alipokuwa sekondari, aliwaongopea watu wengi akiwemo mpenzi wake mjamzito kuwa yeye ni jajusi wa CIA na watu wote waliamini kuwa yeye ni jasusi kutokana na hati feki alizokuwa akizionyesha.

Smith kwa kutumia staili zake za ulaghai alifanikiwa kumshawishi rafiki yake Jason Rizzi, 20 aliyefahamiana naye kupitia mtandao wa MySpace amuue mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 50, Gloria Ryan baada ya kumuambia kuwa mama yake huyo ni "Mtu hatari sana kwa usalama wa taifa na hafai kuwa karibu na mtu yoyote".

Smith alimuahidi Rizzi kuwa iwapo atalilinda taifa kwa kumuua mama yake mzazi atachukuliwa na CIA kama askari kanzu.

Rizzi aliamini maneno aliyoambiwa kwasababu mama yake alikuwa akijua mambo mengi ya serikali. Rizzi alimuua mama yake akiamini anaifanyia kazi serikali.

Hata baada ya kukamatwa kwa kumuua mama yake kwa kumpiga risasi, Rizzi aliendelea kuamini kuwa Smith alikuwa ni jasusi wa CIA.

"Hivi mna uhakika kuwa Smith sio jasusi?", aliuliza Rizzi alipotiwa mbaroni mjini Cleveland, Texas.

Mbali ya kujifanya kuwa yeye ni jasusi, Smith pia alijifanya kuwa yeye ni promota mkubwa wa wasanii wa Hip Hop akionyesha picha mbalimbali akiwa amekaa mbele ya silaha mbalimbali zilizotundikwa ukutani.

Mahakama iliambiwa kuwa mpenzi wa Smith ambaye ni mjamzito pamoja na watu wengine waliamini kuwa Smith ni jasusi kwani mara kadhaa alikuwa akitoa nyaraka feki zilizofanana na nyaraka za kweli za CIA.

Lakini mahakama iliambiwa kuwa Smith hakuwa jasusi bali kibarua katika kampuni za ujenzi.

Smith ambaye alikuwa akitambulisha kama CJ Shaw alikanusha kuhusika na mauaji ya mama yake Rizizi lakini alihukumiwa kwenda jela maisha.

Rizzi atasomewa hukumu yake mwezi ujao

Ajiua baada ya kuambiwa shoga



DEOGRATIUS Paul (39), mkazi wa Kinondoni amekutwa akiwa amekufa chumbani kwake kwa kujinyonga na kuacha ujumbe mfupi juu ya maamuzi hayo.
Akitoa taraifa hiyo kwa wanahabari, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Bw. Elias Kalinga alisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi, saa 12 alfajiri huko Kinondoni.

Alisema kuwa marehemu huyo alichukua maamuzi ya kujinyonga baada ya kukerwa na mambo aliyokuwa akizushiwa mtaani.

Alisema kuwa, mwili huo ulikutwa chumbani kwake ukiwa unaning'inia darini ambako alijitundika kwa kutumia shuka.

Marehemu aliacha ujumbe uliosema “ mimi sio shoga kama mnavyodai mimi ni mwanaume mkamilifu na hata mtoto ninae na Mungu ndio shahidi yangu” ulimaliza ujumbe huo

Mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na upelelezi zaidi juu ya atukio hilo unaendelea

Mahakama yaamuru Chenge akamatwe


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Kinondoni, jana imetoa maamuzi na kutoa ruhusa ya kukamatwa kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Serikali baada kushindwa kufika mahakamani .

Chenge anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuendesha gari kizembe na kusababisha vifo vya watu wawili-Victoria George na Betrice Costantine- na shtaka jingine la kuendesha gari bila ya bima, lakini jana hakuwepo mahakamani.

Hakimu Sundi Fimbo alitoa kibali cha kukamatwa kwa mshitakiwa huyo kwa kosa la kutohudhuria Mahakamdani bila taarifa.

Kabla ya kutoa kibali hicho mahakamani, Hakimu alipotaka kujua mshitakiwa huyo alikuwa wapi, wakili mtetezi wa mshitakiwa huyo Simon Mponda alimjibu Hakimu kuwa mteja wake yupo kwenye msafara wa Kikwete kwa kuwa jana mgombea huyo wa urais alikuwa kwenye kampeni katika jimbo lake la Bariadi Magharibi.

Hata hivyo Hakimu hakukubaliana na jibu hilo na kumwambia wakili kuwa ombi hilo lilitakwia litolewe na mshitakiwa mwenyewe hivyo na kutoa kibali hicho kwa kukiuka mahakama.

Kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kuanzwa kusikilizwa baada ya mshitakiwa huyo kuonekana kuwa ana shauri la kujibu bada ya upelelezi kukamilika.

Andrew Chenge anakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuendesha gari kizembe na kusababisha vifo vya watu wawili Bi.Victoria George na Beatrice Costantine.

Na shtaka jingine la kuendesha gari bila ya bima

Sudan yachelewesha uandikishwaji wa kura


Sudan


Sudan imechelewesha uandikishwaji wa wapiga kura kwa ajili ya kura ya maoni ya Januari ya kuamua iwapo upande wa kusini ujitenge mpaka mwezi Novemba, wakionyesha wasiwasi juu ya ratiba.

Mwenyekiti wa tume ya kura hiyo alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kuruhusu mafunzo ya wafanyakazi na uwasilishaji wa makaratasi ya kupigia kura.

Aliyekuwa Rais wa Tanzania Benjamin Mkapa, aliyeteuliwa na Umoja wa Mataifa kusimamia mchakato wa kura hizo, aliiambia BBC bado kuna changamoto nyingi.

Lakini alisema kama vyama vyote viko radhi, ratiba itafanyika kama ilivyopangwa.

Kura ya maoni ni sehemu ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005 ya kumaliza miongo miwili ya mgogoro baina ya upande wa kaskazini na upande wa kusini wenye utajiri wa mafuta ambapo takriban watu milioni 1.5 walifariki dunia.

Wachambuzi wanahofia kuna hatari ya mgogoro huo kuanza upya iwapo raia wa upande wa Kusini wakihisi Khartoum inajaribu kuchelewesha au kuvuruga kura upande wa kusini- miongoni mwa maeneo maskini duniani.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Muhammed Ibrahim Khalil, alisema uandikishwaji ulicheleweshwa kwa wiki tatu hadi Novemba 15.

Kulingana na shirika la habari la Reuters, fomu za uandikishwaji bado hazijawasili kutoka Afrika Kusini- na hazitarajiwi kufika hadi Oktoba mwishoni.

Bw Mkapa aliteuliwa wiki iliyopita na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuongoza jopo maalum la waangalizi kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa salama.

Akihojiwa BBC iwapo atathubutu kuchelewesha kura hiyo ya maoni kama maandalizi hayakukamilika, Bw Mkapa alisema: "Tutakabiliana na hilo, muda utakapofika."

"Lakini kwa sasa naona wajibu wetu ni kuhakikisha inafanyika tarehe 9 Januari."

Zana za mawe zilianza kale zaidi Afrika




Zana za mawe

Timu ya watafiti imeripoti kuwa imegundua upya nyenzo za zama za zana za mawe zinazopendekeza kuwa mwanadamu ametokea kwenye ardhi "ndani ya Afrika" mapema na ilivyotarajiwa.

Wataalamu wa masuala ya kale wanakadiria kuwa uhamiaji kutoka Afrika kuelekea kusini-mashariki mwa Asia na Australia ulifanyika takriban miaka 60,000 iliyopita.

Lakini Dr Michael Petraglia, wa chuo kikuu cha Oxford, na wenzake walisema zana za kale za mawe zilizogunduliwa kwenye rasi ya Uarabuni na India zinaonyesha kuanza takriban miaka 70,000 mpaka 80,000 iliyopita, na hata kabla ya hapo.

Dr Petraglia, ambao wenzake ni pamoja na watafiti kutoka Australia na India, aliwakilisha fikra zake katika tamasha la wanasayansi wa Uingereza, linalofanywa katika chuo kikuu cha Aston mwaka huu.

"Ninaamini jamii ya watu mbalimbali ilitoka Afrika katika kipindi cha miaka 120,000 na 70,000 iliyopita," alisema. " Ushahidi wetu ni zana za mawe tunazoweza kujua zilitengenezwa wakati gani."

Zana nyingi zimetoka ndani ya nchi- kilomita nyingi kutoka pwani. Alisema, hii inamaanisha kuna uwezekano mkubwa binadamu walihama kupitia ardhini kuliko hata kwenye boti.

Zana hizo zimepatikana kwenye maeneo ambayo aghlabu huonekana hazikaliki, lakini kwa wakati huo zilionyesha kuwa nzuri zaidi kwa uhamiaji.

Aliiambia BBC, " Kwa muda huo tunaouzungumzia, mazingira kwa hakika yalikuwa mazuri." "Kwahiyo maeneo ambayo yana jangwa leo hii, wakati huo kulikuwa na mito na maziwa, na kulikuwa na mimea na wanyama tele."




Machimbo ya mawe

Watafiti hao waligundua zana hizo- zilizo na urefu wa sentimita kadhaa hadi kufikia sm 10- katika safu wanazoweza kujua muda wake kwa kutumia mchanga na vitu vinavyotokana na volcano zinazopatikana juu na chini ya zana hizo



Zana hizo zilikuwa zaidi mikuki na miparuzo.

Baadhi ya zana hizo zilibananishwa na majivu kutokana na mripuko wa volacno maarufu ya Toba ambao wataalmu wa jiolojia wanaweza kwa umakini kujua muda wake ni miaka 74,000 iliyopita.

Baadhi ya viumbe hasa binadamu wa awali kwa hakika waliondoka Afrika kabla ya sisi (Homo sapiens), lakini timu ya Dr Petraglia anafikiri zana walizogundua ni zile zilizotengenezwa na binadamu wa sasa.

Utafiti wa awali ulikuwa ukitathmini zaidi asidi nasaba ya watu wa jamii mbalimbali kujua ni muda gani uliopita waliokuwa wametoka kwenye ukoo unaofanana- kizazi cha Afrika kinachofanana.

Profesa Chris Stringer, kutoka makumbusho ya Historia ya London, alisema taarifa hizo za asidi nasaba zinaonyesha binadamu waliondoka Afrika takriban miaka 60,000 iliyopita au hata kabla ya hapo.

Alikubali, " zana hizi zinaonyesha watu waliishi katika maeneo haya, lakini asidi nasaba zinaonyesha waliondoka Afrika baada ya miaka 60,000 iliyopita. Watu wa India wangepotea kabisa."

Hata hivyo, Dr Petraglia, alisema kufanya utafiti wa uhamiaji kwa kutumia asidi nasaba za watu huenda kusitoe matokeo sahihi, kwasababu utafiti wote wa sasa unachunguza watu wa sasa pekee.

Alidai kwamba, kutokuwepo asidi nasaba ya watu wa kale ili kufanya uchunguzi wa ziada umesababisha utafiti huu kutokuwa na uhakika

JITAMBUE NA KUTAMBUA DUNIA KUPITIA MAISHANI

Nitapunguza Maambukizi ya Ukimwi -JK



MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa ahadi ya kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi pindi atakapopewa ridhaa ya kuongoza miaka mitano ijayo.


Ahadi hiyo aliitoa jana mkoani Iringa wilaya ya Iringa vijijini wakati akihutubia uma katika kampeni zake zinazoendela mkoani humo.



Kikwete alishangazwa na takwimu ya maambukizi mkoani humo na kukerwa na tatizo hilo na kuwataka wananchi hao wamchague ili aweze kudhibiti mambukizi hayo ambayo yamefikia zaidi ya asilimia 16 mkoani humo.

Alisema ataandaa mikakati maalum itakayofanya maambukizi hayo yapungue, pia serikali yake itazidi kusambaza dawa za kupunguza makali ya virusi wakati huohuo serikali yake itajitahidi kupunguza tatizo hilo kila pembe ya nchi