KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 27, 2010

Mombasa Raha yaua watanoWATU watano wamefariki dunia papo hapo na wengine 11 kujeruhiwa, kufuatia ajali mbaya ya magari kugongana uso kwa uso iliyohusisha basi la kampuni ya Mombasa Raha.
Ajali hiyo, ilitokea juzi, majira ya saa 11:45 jioni huko eneo la Usanda Wilayani Shinyanga.

Basi hilo la abiria lilikuwa lenye namba za usajili T 854 DDF, lilikuwa likitokea wilayani Kahama kwenda mkoani Mwanza na, liligongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya Scania yenye namba za usajili T 295 AHH, lililokuwa likitoka jijini Mwanza kwenda mkoani Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Bw., Daudi Siasi, alitoa taarifa hiyo na kusema kuwa watu wanne waliokuwemo ndani ya lori hilo, walipoteza maisha pamoja na abiria mmoja aliyekuwa ndani ya basi hilo la abiria.

Kamanda Siasi alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe uliosababishwa na dereva wa lori kuhama njia yake na kulifata bsi hilo la abiria.

Aliwataja marehemu hao kuwa ni dereva wa lori hilo, Bw.Josia Mandago (37), konda wake Hoti Safari (27) na wanaume wengine wawili waliokuwa wakisafiri na lori hilo ambao majina yao hayakupatikana mara moja na abiria mmoja aliyekuwa kwenye basi aliyetambulika kwa jina la Ramadhan Magoma (45) mkazi wa Ndembezi mjini Shinyanga

No comments:

Post a Comment