KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 27, 2010

Marekani mbioni kunusuru mazungumzo ya amani



Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani PJ Crowley amesema msimamo wa Marekani haujabadilika. Taarifa hiyo imetolewa baada ya kumazilika kwa marufuku ya miezi kumi yaliyowekwa na Israel dhidi ya ujenzi wa makaazi hayo.

Marekani imejikuta katikati ya mgogoro ambao kila mtu alijua huenda ukatokea. Rais Abbas daima amekuwa akisema kuwa ujenzi wa Israel wa makazi mapya lazima usitishwe, ili kumuezesha kuendelea na mazungumzo ya amani kati yake na uongozi wa Israel.

Lakini usitishwaji wa muda wa ujenzi wa makazi hayo kwa sasa umemalizika.Hata hivyo Marekani inaishinikiza Israel iongoze muda wa usitishaji wa ujenzi huo.

Waziri mkuu wa Israel , Benjamin Netanyahu , amemtaka bw Abbas kutojitoa katika mazumgumzo ya amani kama njia ya kupinga mpango wa Israel wa ujenzi wa makazi mapya, na badala yake amemtaka kuendelea na moyo wa uaminifu ili kufikia mkataba wa amani wa kihistoria kati ya pande hizo mbili.

Mstakabali wa mazungumzo hayo unatengemea maoni ya viongozi wengine wa nchi za kiarabu ambao wanatarajiwa kukutana mjini Cairo Misri, siku kumi zijazo.

Bw Abbas anasema hatajiondoa kwenye mchakato wa mazungumzo hayo hadi hapo viongozi hao watakapo shauriana naye.


"Kuna chaguo moja tu, kuendelea kwa ujenzi wa makazi au amani. Israel lazima ichague amani. Iwapo Israel itachagua amaniu tutaendelea na mazungumzo, lakini ikishindwa kuchagua hilo, basi hii itakuwa ni kupoteza muda au kupoteza fursa ya kufikia amani."Amesisitiza rais wa Palestina.

Walowezi wa kiyahudi katika maeneo yanayokaliwa ya ukingo wa magharibi wa mto Jordon wamekuwa wakisheherekea kumalizika kwa muda uliowekwa wa kusitisha ujenzi katika maeneo hayo.

Walianza kusherekea hata kabla ya muda wenyewe kumalizika. Katika moja ya makazi hayo walirusha maputo na kuchimba kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya watoto wadogo, licha ya ombi la Waziri mkuu wa Palestina Benjamin ya kutaka kujizuia na aina yoyote ya ghasia baada ya kumalizika kwa muda huo

No comments:

Post a Comment