KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 27, 2010

Watu milioni 2 wahama makwao-NigeriaMaafisa wa serikali nchini Nigeria, wanasema zaidi ya watu milioni 2 wameyahama makwao baada ya utawala wa nchi hiyo, kufungua milango ya kuzuia maji katika mabwawa mawili.

Hatua hiyo ilisababisha mafuriko katika maeneo ya Jigawa karibu na jimbo linalopakana na jangwa la Sahara.

Maafisa wa serikali wanasema, milango hiyo ilifunguliwa baada ya uchunguzi kubainisha kuwa mabwawa hayo huenda yakafurika na kusababisha maafa zaidi.

Watu zaidi wanaendela kuhamishwa kutoka maeneo ya mabonde hadi maeneo ya milima.

Majimbo kadhaa nchini humo yameathiriwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha miezi miwili iliyopita nchini humo

No comments:

Post a Comment