KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, September 23, 2010

Nitapunguza Maambukizi ya Ukimwi -JKMGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa ahadi ya kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi pindi atakapopewa ridhaa ya kuongoza miaka mitano ijayo.


Ahadi hiyo aliitoa jana mkoani Iringa wilaya ya Iringa vijijini wakati akihutubia uma katika kampeni zake zinazoendela mkoani humo.Kikwete alishangazwa na takwimu ya maambukizi mkoani humo na kukerwa na tatizo hilo na kuwataka wananchi hao wamchague ili aweze kudhibiti mambukizi hayo ambayo yamefikia zaidi ya asilimia 16 mkoani humo.

Alisema ataandaa mikakati maalum itakayofanya maambukizi hayo yapungue, pia serikali yake itazidi kusambaza dawa za kupunguza makali ya virusi wakati huohuo serikali yake itajitahidi kupunguza tatizo hilo kila pembe ya nchi

No comments:

Post a Comment