KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, September 23, 2010
'Mama Yako ni Adui wa Taifa'
Kijana mmoja wa nchini Marekani ambaye alijifanya ni jasusi wa shirika la ujasusi la Marekani la CIA, amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumshawishi rafiki yake kumuua mama yake mzazi kwakuwa mama yake huyo alikuwa ni hatari kwa taifa.
Corderral Smith kijana mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikuwa mwanafunzi aliyefukuzwa shule alipokuwa sekondari, aliwaongopea watu wengi akiwemo mpenzi wake mjamzito kuwa yeye ni jajusi wa CIA na watu wote waliamini kuwa yeye ni jasusi kutokana na hati feki alizokuwa akizionyesha.
Smith kwa kutumia staili zake za ulaghai alifanikiwa kumshawishi rafiki yake Jason Rizzi, 20 aliyefahamiana naye kupitia mtandao wa MySpace amuue mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 50, Gloria Ryan baada ya kumuambia kuwa mama yake huyo ni "Mtu hatari sana kwa usalama wa taifa na hafai kuwa karibu na mtu yoyote".
Smith alimuahidi Rizzi kuwa iwapo atalilinda taifa kwa kumuua mama yake mzazi atachukuliwa na CIA kama askari kanzu.
Rizzi aliamini maneno aliyoambiwa kwasababu mama yake alikuwa akijua mambo mengi ya serikali. Rizzi alimuua mama yake akiamini anaifanyia kazi serikali.
Hata baada ya kukamatwa kwa kumuua mama yake kwa kumpiga risasi, Rizzi aliendelea kuamini kuwa Smith alikuwa ni jasusi wa CIA.
"Hivi mna uhakika kuwa Smith sio jasusi?", aliuliza Rizzi alipotiwa mbaroni mjini Cleveland, Texas.
Mbali ya kujifanya kuwa yeye ni jasusi, Smith pia alijifanya kuwa yeye ni promota mkubwa wa wasanii wa Hip Hop akionyesha picha mbalimbali akiwa amekaa mbele ya silaha mbalimbali zilizotundikwa ukutani.
Mahakama iliambiwa kuwa mpenzi wa Smith ambaye ni mjamzito pamoja na watu wengine waliamini kuwa Smith ni jasusi kwani mara kadhaa alikuwa akitoa nyaraka feki zilizofanana na nyaraka za kweli za CIA.
Lakini mahakama iliambiwa kuwa Smith hakuwa jasusi bali kibarua katika kampuni za ujenzi.
Smith ambaye alikuwa akitambulisha kama CJ Shaw alikanusha kuhusika na mauaji ya mama yake Rizizi lakini alihukumiwa kwenda jela maisha.
Rizzi atasomewa hukumu yake mwezi ujao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment