KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, September 23, 2010

Ajiua baada ya kuambiwa shogaDEOGRATIUS Paul (39), mkazi wa Kinondoni amekutwa akiwa amekufa chumbani kwake kwa kujinyonga na kuacha ujumbe mfupi juu ya maamuzi hayo.
Akitoa taraifa hiyo kwa wanahabari, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Bw. Elias Kalinga alisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi, saa 12 alfajiri huko Kinondoni.

Alisema kuwa marehemu huyo alichukua maamuzi ya kujinyonga baada ya kukerwa na mambo aliyokuwa akizushiwa mtaani.

Alisema kuwa, mwili huo ulikutwa chumbani kwake ukiwa unaning'inia darini ambako alijitundika kwa kutumia shuka.

Marehemu aliacha ujumbe uliosema “ mimi sio shoga kama mnavyodai mimi ni mwanaume mkamilifu na hata mtoto ninae na Mungu ndio shahidi yangu” ulimaliza ujumbe huo

Mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na upelelezi zaidi juu ya atukio hilo unaendelea

No comments:

Post a Comment