KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, September 29, 2010

..Mjumbe wa UN, Wallstrom kuzur DRC leo


Mjumbe wa Umoja wa Mataifa

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya dhuluma za kimapenzi katika maeneo yenye mizozo, Margot Wallstrom, anatarajiwa kuwasili Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hivi leo.

Ziara hiyo inajiri baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyobainisha kuwa mamia ya raia walibakwa katika kipindi cha siku nne kati ya mwezi Julai na Agosti katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Makundi matatu ya waasi yanadaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya ubakaji dhidi ya kina mama, wasichana na hata wavulana.

Akizungumza na BBC, Bi Wallstrom, amesema huenda kuna waathiriwa zaidi ya mia tano wa mkasa huo.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa umoja huo kutoa mafunzo zaidi kwa maafisa wake wa kutunza amani ambao wameshutumiwa kwa kutochukua hatua za kuzuia dhuluma dhidi ya raia

No comments:

Post a Comment