KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 23, 2010

Waziri Mkuu Avaa Soksi Zenye MatoboAnaiongoza mojawapo ya nchi tajiri duniani, pamoja na kwamba analipwa mshahara mkubwa sana, waziri mkuu wa Uingereza alienda kwenye kipindi cha luninga akiwa amevaa soksi zenye matobo.
David Cameron, waziri mkuu wa Uingereza ambaye analipwa mshahara wa paundi 142,500 (Takribani Milioni 336) kwa mwaka alinaswa na kamera akiwa amevaa soksi yenye tundu.

Cameron alifika kwenye studio ya televisheni ya ITV kwenye kipindi cha "This Morning" ili kuzungumzia maisha ya familia yake na kuzaliwa kwa mtoto wao mchanga wa kike.

Watazamaji wa kipindi hicho walishangazwa kuona soksi alizovaa waziri mkuu wao zikiwa na tundu.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeliongelea tukio hilo kwa kumbeza waziri mkuu kwa kusema "Anaiongoza nchi lakini ameshindwa hata kujinunulia soksi".

No comments:

Post a Comment