KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 23, 2010

Ujumbe wa UN kuzuru Sudan



Hali ya wasi wasi imeikumba jamii ya kimataifa kuhusu mstakabali wa Sudan.Moja wapo ya maafikiano ya mpango wa amani ilikuwa kufanyika kura ya maoni kuamua uhuru wa Sudan Kusini ambayo imepangwa mwakani.

Hata hivyo mipango kufanikisha kura hiyo ingali kufanyika hali inayotishia kuzuka upya kwa mapigano.Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulifanya kikao maalum kujadili Sudan ambapo rais Barack Obama alikuwa miongoni mwa waliohudhuria.Kuanzia leo ujumbe kutoka Baraza la Usalama utazuru Sudan ambapo utapitia Uganda.

Katika siku chache watakazokuwa Sudan,wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa watakapa nafasi ya kujionea baadhi tu ya matatizo mengi yanayoikumba nchi hiyo.

Ziara yao inaanzia Juba ambapo raia wa Sudan Kusini wamekuwa na wasiwasi kuhusu matayarisho yasiyoridhisha ya kura ya maoni.Uandikishaji wa wapiga kura haujaanza bado na wengi Sudan Kusini wanashuku kuwa viongozi wa kaskazini wanahusika katika ucheleweshwaji wa usajili wa wapiga kura.

Kwa saa chache watakuwepo El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur,magharibi mwa Sudan ambapo mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanaendelea.Lakini miongoni mwa orodha ya wanasiasa watakao kutana nao mmoja hawatakutana naye.

Rais Al Bashir anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya ICC kwa madai ya uhalifu wa kivita,uhalifu dhidi ya binaadamu na mauaji ya halaiki yote akidaiwa kuyatakeleza Darfur.Baraza la usalama la umoja wa mataifa limesema halitakutana naye,jambo lililokasirisha sana serikali ya Sudan,Khartoum.

Kila mtu aliye ndani ya Sudan na wale walio nje wanakubaliana kuwa huu ni wakati muhimu katika historia ya nchi hiyo,lakini haifahamiki kuwa ziara hii itakuwa na athari gani kubwa kwa nchi ya Sudan

No comments:

Post a Comment