KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, September 29, 2010

Akiri kupata mtaji kwa njia ya udanganyifuKIJANA aliyejitambulisha kwa jina moja la Seid, anayefanya shughuli zake za biashara katika maeneo ya Kariakoo amekiri kuwa kukosa elimu siyo kigezo cha kukosa msingi wa masiha.
Hayo aliyasema katika mazungumzo maalum na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.

Seid aliweza kuiambia NIFAHAMISHE kuwa miaka mitatu nyumba alifika jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Shinyanga ambapo alidai aliweza kuwatoroka wazazi wake kwa lengo la kuja kujitafutia maisha jijini humo.

Alidai kuwa, aliingia jijini humo huku akijua ataweza kutimiza ndoto zake kwa kuwa alikuwa na lengo la kuja kufanya biashara na alipowaeleza wazazi wake walimzuia abaki na kufanya shughuli hizo nyumbani kwao.

Alidai alipoingia jijini humu aliwatafuta jamaa zake na aliweza kupita katika maofisi mbalimbali akidai anaomba misaada wa nauli ili aweze kurudi nyumbani kwao.

Alidai Mungu aliweza kumsaidia na aliweza kupata wasamaria mbalimbali wakimpa pesa taslimu ili aweze kutumia nauli hiyo na alidai alikuwa akizihifadhi pesa hizo ili uwe mtaji wake wa kuanzia biashara.

Alidai katika zoezi hilo aliweza kujikusanyia kiasi cha shilingi laki mbili na kuacha kuomba msaada huo na aliunganisha na kiasi cha shilingi laki moja ambazo alikuwa nazo na kuanza kufanya biashara ya mitumba maeneo ya Manzese kwa jamaa yake huyo.

Alidai kuwa mtaji wake uliweza kukua kidogokidogo na hadi sasa anaendeleza biashara zake hizo

No comments:

Post a Comment