KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 23, 2010

Zana za mawe zilianza kale zaidi Afrika




Zana za mawe

Timu ya watafiti imeripoti kuwa imegundua upya nyenzo za zama za zana za mawe zinazopendekeza kuwa mwanadamu ametokea kwenye ardhi "ndani ya Afrika" mapema na ilivyotarajiwa.

Wataalamu wa masuala ya kale wanakadiria kuwa uhamiaji kutoka Afrika kuelekea kusini-mashariki mwa Asia na Australia ulifanyika takriban miaka 60,000 iliyopita.

Lakini Dr Michael Petraglia, wa chuo kikuu cha Oxford, na wenzake walisema zana za kale za mawe zilizogunduliwa kwenye rasi ya Uarabuni na India zinaonyesha kuanza takriban miaka 70,000 mpaka 80,000 iliyopita, na hata kabla ya hapo.

Dr Petraglia, ambao wenzake ni pamoja na watafiti kutoka Australia na India, aliwakilisha fikra zake katika tamasha la wanasayansi wa Uingereza, linalofanywa katika chuo kikuu cha Aston mwaka huu.

"Ninaamini jamii ya watu mbalimbali ilitoka Afrika katika kipindi cha miaka 120,000 na 70,000 iliyopita," alisema. " Ushahidi wetu ni zana za mawe tunazoweza kujua zilitengenezwa wakati gani."

Zana nyingi zimetoka ndani ya nchi- kilomita nyingi kutoka pwani. Alisema, hii inamaanisha kuna uwezekano mkubwa binadamu walihama kupitia ardhini kuliko hata kwenye boti.

Zana hizo zimepatikana kwenye maeneo ambayo aghlabu huonekana hazikaliki, lakini kwa wakati huo zilionyesha kuwa nzuri zaidi kwa uhamiaji.

Aliiambia BBC, " Kwa muda huo tunaouzungumzia, mazingira kwa hakika yalikuwa mazuri." "Kwahiyo maeneo ambayo yana jangwa leo hii, wakati huo kulikuwa na mito na maziwa, na kulikuwa na mimea na wanyama tele."




Machimbo ya mawe

Watafiti hao waligundua zana hizo- zilizo na urefu wa sentimita kadhaa hadi kufikia sm 10- katika safu wanazoweza kujua muda wake kwa kutumia mchanga na vitu vinavyotokana na volcano zinazopatikana juu na chini ya zana hizo



Zana hizo zilikuwa zaidi mikuki na miparuzo.

Baadhi ya zana hizo zilibananishwa na majivu kutokana na mripuko wa volacno maarufu ya Toba ambao wataalmu wa jiolojia wanaweza kwa umakini kujua muda wake ni miaka 74,000 iliyopita.

Baadhi ya viumbe hasa binadamu wa awali kwa hakika waliondoka Afrika kabla ya sisi (Homo sapiens), lakini timu ya Dr Petraglia anafikiri zana walizogundua ni zile zilizotengenezwa na binadamu wa sasa.

Utafiti wa awali ulikuwa ukitathmini zaidi asidi nasaba ya watu wa jamii mbalimbali kujua ni muda gani uliopita waliokuwa wametoka kwenye ukoo unaofanana- kizazi cha Afrika kinachofanana.

Profesa Chris Stringer, kutoka makumbusho ya Historia ya London, alisema taarifa hizo za asidi nasaba zinaonyesha binadamu waliondoka Afrika takriban miaka 60,000 iliyopita au hata kabla ya hapo.

Alikubali, " zana hizi zinaonyesha watu waliishi katika maeneo haya, lakini asidi nasaba zinaonyesha waliondoka Afrika baada ya miaka 60,000 iliyopita. Watu wa India wangepotea kabisa."

Hata hivyo, Dr Petraglia, alisema kufanya utafiti wa uhamiaji kwa kutumia asidi nasaba za watu huenda kusitoe matokeo sahihi, kwasababu utafiti wote wa sasa unachunguza watu wa sasa pekee.

Alidai kwamba, kutokuwepo asidi nasaba ya watu wa kale ili kufanya uchunguzi wa ziada umesababisha utafiti huu kutokuwa na uhakika

No comments:

Post a Comment