KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, September 29, 2010

Bepari wa Misri afungwa kwa mauaji



Suzanne Tamim


Bepari wa Misri amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kuamrisha mauaji ya mwimbaji maarufu wa Lebanon Suzanne Tamim, baada ya kesi hiyo kusikilizwa tena.

Hisham Talaat Moustafa, mwanachama mwandamizi wa chama tawala cha Misri, alihukumiwa kifo baada ya kesi yake kusikilizwa mwanzo- lakini majaji walipinga kifungo hicho na kuamuru kesi kusikilizwa upya.

Mwenzake Mohsen al-Sukkari alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kumwuua Tamim.

Alikutwa kwenye hoteli huko Dubai mwaka 2008 huku shingo yake ikiwa imekatwa.

Keshi hiyo imepata ushabiki mkubwa, kutokana na Moustafa kuonekana ni mwenye hadhi kubwa nchini humo.

Mahakama ilisikia namna Moustafa, ambaye alikuwa na uhusiano na mwimbaji huyo, alivyoamuru mauaji hayo.

Inaaminiwa kuwa alimlipa Sukkari dola za kimarekani milioni mbili kumwuua Tamim ikiwa hatua ya kulipiza kisasi baada ya kukataa ombi la kufunga naye ndoa.

Tamim alikuwa mwimbaji huku akijulikana kwa misukosuko katika maisha yake binafsi na kipaji chake.

Alianza kupata umaarufu baada ya kushinda katika onyesho la vipaji kwenye televisheni ya Arabuni miaka ya 90.

No comments:

Post a Comment