KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, September 29, 2010

Msafara wa Lipumba wapata ajali tenaMSAFARA wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, umepata ajali kwa mara nyingine na kusababisha askari mmoja kujeruhiwa kichwani.
Askari huyo PC Johnson mwenye namba E.9551 aliyekuwa katika msafara wa Profesa Lipumba, amelazwa kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Basilio Matei, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi, majira ya jioni katika eneo la Oysterbay katika Manispaa ya Arusha.

Na kusema kuwa, askari polisi PC Jophnson aliyekuwa na namba E.9551 alijeruhiwa kichwani katika ajali hiyo.

Alisema gari aina ya Toyota Land Cruiser, lilipita kwa kasi kwenye tuta, hali ilifanya kumtupa askari huyo nje ya gari.Pia gari jingine liligongana na gari hilo la polisi kwa mbele na gari alilokuwemo mgombea huyo kuyumba na dereva kutetea lisipinduke.

Hii ni ajali ya pili kutokea katika msafara wa Profesa Lipumba baada ya nyingine iliyotokea wilayani Kilindi, mkoani Tanga wiki iliyopita.

Katika ajali hiyo, gari moja lilichomoka tairi na jingine lililokuwa limebeba waandishi wa habari kupinduka lakini katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha ila kulikuwa na majeruhi.

No comments:

Post a Comment