KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, September 23, 2010

TZ:Jeshi laahidi usalama katika uchaguziJeshi la Tanzania limetoa onyo kwa wanasiasa dhidi ya kuchochea mapigano huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu.

Mkuu wa jeshi Genereli leteni Abdulrahman Shimbo amesema kuwa wamepata vidokezo kuwa kuna baadhi ya wanasiasa na makundi wanaonuia kuvuruga shughuli za kampeini kabla ya kufanyika uchaguzi huo.

Hata hivyo amesema kuwa jeshi liko tayari kukabili vurugu zozote. Siku ya Alhamisi, mmoja wa wanasiasa wa upinzani nchiniTanzania aliwaambia wanahabari kuwa kutatokea umwagaji wa damu iwapo uchaguzi huo wa 31st October hautafanyika kwa haki na uwazi.

Wanasiasa sita wa upinzani wamejitokeza kugombea kiti hicho cha urais kumpinga kiongozi wa sasa Jakaya Kikwete

No comments:

Post a Comment