KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 23, 2010

Mahakama yaamuru Chenge akamatwe


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Kinondoni, jana imetoa maamuzi na kutoa ruhusa ya kukamatwa kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Serikali baada kushindwa kufika mahakamani .

Chenge anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuendesha gari kizembe na kusababisha vifo vya watu wawili-Victoria George na Betrice Costantine- na shtaka jingine la kuendesha gari bila ya bima, lakini jana hakuwepo mahakamani.

Hakimu Sundi Fimbo alitoa kibali cha kukamatwa kwa mshitakiwa huyo kwa kosa la kutohudhuria Mahakamdani bila taarifa.

Kabla ya kutoa kibali hicho mahakamani, Hakimu alipotaka kujua mshitakiwa huyo alikuwa wapi, wakili mtetezi wa mshitakiwa huyo Simon Mponda alimjibu Hakimu kuwa mteja wake yupo kwenye msafara wa Kikwete kwa kuwa jana mgombea huyo wa urais alikuwa kwenye kampeni katika jimbo lake la Bariadi Magharibi.

Hata hivyo Hakimu hakukubaliana na jibu hilo na kumwambia wakili kuwa ombi hilo lilitakwia litolewe na mshitakiwa mwenyewe hivyo na kutoa kibali hicho kwa kukiuka mahakama.

Kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kuanzwa kusikilizwa baada ya mshitakiwa huyo kuonekana kuwa ana shauri la kujibu bada ya upelelezi kukamilika.

Andrew Chenge anakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuendesha gari kizembe na kusababisha vifo vya watu wawili Bi.Victoria George na Beatrice Costantine.

Na shtaka jingine la kuendesha gari bila ya bima

No comments:

Post a Comment