KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 27, 2009

Waandishi mateka waachiliwa Somalia


Waandishi wawili wa habari wa kigeni waliotekwa nyara na wanamgambo wa kisomali Agosti 2008 wameachiliwa huru na watekaji hao.
Amanda Lindhout kutoka Canada na Nigel Brennan wa Australia wanasemekana kuwa katika hoteli moja kwenye mji mkuu Mogadishu.Bi Lindhout alivieleza vyombo vya habari vya Canada kwamba watekaji nyara walimtesa na kuwa kikombozi kililipwa kabla ya kuachiliwa kwake.

Mwandishi huyo aliileza televisheni ya Canada, CTV kuwa walikuwa wakihamishwa nyumba moja hadi nyingine na wanamgambo hao kwa kipindi cha miezi 15 ya kuwa mateka

No comments:

Post a Comment