KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, November 25, 2009

Arsenal wapiga hatua Liverpool wakwama


Arsenal wapiga hatua Liverpool wakwama
Vijana wa Arsenal walifunga mabao mawili dhidi ya Standard Liege ya Ubelgiji kuimarisha nafasi yao katika mashindano ya kilabu bingwa barani Ulaya huku Liverpool wakifungishwa virago licha ya kupata ushindi.
Arsenal hawakuonyesha kutatizwa na mnamo dakika ya 35, Samir Nasri alifunga bao la kwanza naye Denilson akiongeza la pili kabla ya kipindi cha mapumziko.

Huku Arsenal wakisherehekea kujinyakulia nafasi katika timu 16 zilizosalia kwenye dimba hilo la kilabu bingwa Ulaya, wenzao wa Uingereza, Liverpool walibaki kujuta.

Ingawa walicheza kufa na kupona hadi kuishindi timu ya Debrecen ushindi huo haukuwa na maana kwa kuwa nafasi waliyokuwa wakitegemea ilinyakuliwa na Lyon.

Liverpool iliichapa Debrecen bao 1-0 na kutegemea kwamba Lyon ingetoka sare au hata kuishinda Fiorentina.

Liverpool sasa watasalia kung’ang’ana katika ligi ya Europa.

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Liverpool kukosa kuingia katika raundi za mchujo tangu msimu wa 2002 – 2003.

Timu ya Rangers kutoka Uskochi nayo pia imefungishwa virago na VfB Stuggart.

Basi leo Jumatano usikose kijasho katika uwanja wa Old Trafford wakati Manchester United ikipambana na Besiktas huku Chelsea ikiwa ugenini kucheza na FC Porto ya Ureno.

No comments:

Post a Comment