KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 25, 2009

Sunderland yasubiri vipimo vya Bent


Sunderland yasubiri vipimo vya Bent

Sunderland ina wasiwasi huenda Darren Bent akawa nje kwa wiki tatu baada ya mfungaji wao huyo kufanyiwa vipimo kutokana na kuumia goti.
Mshambuliaji huyo ambaye pia huchezea timu ya taifa ya soka ya England aliumia goti baada ya kufunga bao la ushindi siku ya Jumamosi, dhidi ya Arsenal.Meneja wa Black Cats Steve Bruce ameeleza katika mtandao wa klabu hiyo, "iwapo itakuwa goti ndio linamsumbua, hapana shaka atakaa nje kwa wiki tatu".

Mshambuliaji huyo kuna wasiwasi asicheze mchezo na Wigan na kukosekana kwake kuna leta hofu ya nani atakayeongoza safu ya ushambuliaji, wakati huu Kenwyne Jones akiwa amefungiwa baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu walipocheza na West Ham mwezi wa Oktoba.

No comments:

Post a Comment