KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 27, 2009

Ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Westerwelle katika mashariki ya kati , mgomo wa wanafunzi na siku ya waajiri ndio masuala yaliyoshughu


Ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Westerwelle katika mashariki ya kati , mgomo wa wanafunzi na siku ya waajiri ndio masuala yaliyoshughulikiwa na wahariri hii leo.

Leo hii katika udondozi wa maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani , wahariri wamezungumzia zaidi ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle katika mashariki ya kati, mgomo wa wanafunzi hapa nchini, na siku ya waajiri.

Tukianza na mada ya ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani katika mashariki ya kati , gazeti la Ostsee-Zeitung linalochapishwa mjini Rostock, linadokeza kuwa ziara ya hivi karibuni kabisa ya waziri Westerwelle katika mashariki ya kati inabaki kuwa katika milio ya kugonganisha glas tu.

Gazeti linaandika:

Akiikosoa kwa kiasi fulani sera ya Israel ya ujenzi wa makaazi ya Wayahudi katika eneo la ukingo wa magharibi, waziri Westerwelle hakufika mbali sana katika suala hilo. Hii ni sawa kwa ziara hii ya kwanza. Hata hivyo ni lazima Westerwelle atoe matamshi ya wazi kuhusu Israel kutokana na urafiki uliopo. Na kudai mengi zaidi kwa Wapalestina kama inavyohitajika katika suluhisho la mataifa mawili. Israel inamtaka kufanya hivyo binafsi. Lakini njia ya kuelekea huko inatia shaka. Kwa hili jibu litakuwa la dharura ambalo halitakuwa rahisi kwa waziri Westerwelle. Kutokana na hali ilivyo katika mashariki ya kati hali ya kujizuwia haipo tena.

Gazeti la Berliner Morgenpost likiandika kuhusu ziara hiyo ya Westerwelle linaandika:

Westerwelle ameonekana kutumia busara lakini sio kwamba alifanya vizuri na hakufanya hivyo , kama kwamba alikuwa na jibu katika suala gumu la mashariki ya kati. Westerwelle alijizuwia na kutoa maneno makali na ya wazi, lakini ameweka msimamo wake wazi, kutokana na kile kinachoitwa ramani ya njia, Road Map kuhusiana na mpango wa amani wa mashariki ya kati. Katika ramani hiyo kuna lengo ambalo ni wazi, nalo ni ujenzi mpya wa makaazi ya Wayahudi ni lazima uzitishwe.

Mada yetu ya pili ni mgomo wa wanafunzi hapa nchini. Gazeti la Sächsische Zeitung la mjini Dresden kuhusu hilo linaandika.Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Wanafunzi wakitundika mabango wakati wa mgomo wao nchini Ujerumani.
Kunahitajika vitu vingi vya masomo katika miaka mitatu ya kusomea shahada ya kwanza. Baadhi ya nyakati ilikuwa inahitaji hata miaka mitano kuweza kukamilisha. Na kwa ajili ya shahada ya uzamili hakuna hata nafasi, mara nyingi ni mwanafunzi mmoja tu hupata nafasi kwa kila wanafunzi 15.

Kwa mfumo mpya wa masomo ya juu katika bara la Ulaya kwa wanafunzi hilo halieleweki. Serikali ya shirikisho, majimbo na vyuo vikuu vinalazimika hivi sasa haraka iwezekanavyo kuuokoa mfumo huo wa mageuzi, kama kuna cha kuokoa.Masomo yabadilishwe ama shahada ya mwanzo irefushwe hadi miaka minne.

Kuhusiana na siku ya waajiri , gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung linaandika.

Sigmar Gabriel anajitumbukiza zaidi katika pango la simba. Katika siku ya waajiri kumekuwa na hali ya kumkaribisha kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha SPD bila ya kuwa na wasi wasi. Waziri wa uchumi Rainer Brüderle analazimika kuikaribisha hali hiyo kwa njia ya kirafiki. Hali ya kufikirika haipotena. Serikali ya nyeusi na njano ambayo viongozi wa makampuni walikuwa wakiihitaji imezongwa na mivutano kuhusu kodi na matumaini ya ukuaju wa uchumi. Habari nzuri ni kwamba: fedha za malipo ya ajira fupi , kansela anataka kuziongeza ; Habari mbaya ni kwamba mchango wa serikali kwa mafao ya kijamii huenda yasitolewe na serikali kwa waajiri.

Kwa hilo mzozo wa kiuchumi hautaondoka na bado kuna hatari ya kuporomoka tena kwa uchumi. Uongozi wa masuala ya kiuchumi nchini Ujerumani umekalia kuti kavu.

Na mpendwa msikizaji hayo ndio maoni ya baadhi ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani kwa leo. Nilikuwa nae Sekione Kitojo.

No comments:

Post a Comment