KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 23, 2009

Messi kukosa mechi na Inter Milan


Kuna wasiwasi Lionel Messi akakosa mechi baina ya timu ya Barcelona na Inter Milan kuwania Ubingwa wa Ulaya siku ya Jumanne.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anafanyiwa uchunguzi kuhusiana na maumivu ya paja aliyopata siku ya Jumamosi walipotoka sare ya bao 1-1 na Athletic Bilbao.

Kuumia kwa Messi kumekuja wakati tumu yake inamuhitaji zaidi ambapo siku ya Jumapili wanakabiliwa na pambano gumu na watani wao wa jadi Real Madrid.

Zlatan Ibrahimovic, Yaya Toure na Eric Abidal kwa sasa nao ni wagonjwa, lakini meneja wa Barcelona Pep Guardiola amesisitiza watacheza na kile walichonacho.

Guardiola pia anasubiri taarifa za mlinzi Rafael Marquez, ambaye anafanyiwa uchunguzi wa homa ya mafua ya nguruwe iliyowapata pia Toure na Abidal.

No comments:

Post a Comment