KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, November 25, 2009

A.Kusini kuanzisha korti za kombe la dunia


A.Kusini kuanzisha korti za kombe la dunia

Afrika Kusini inajiandaa kuanzisha mahakama maalum zitakazoshughulikia uhalifu utakaofanyika wakati wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010.
Serikali inatumai kwamba mpango huo wa kuharakisha kesi utawawezesha wageni kutoa ushahidi watakapokuwa nchini humo kwa muda mfupi, jambo litakalofanya wahalifu wengi kuogopa.

Jumla ya mahakama 54 zitafanya kazi katika miji tisa itakayokuwa wenyeji wa michuano ya kombe la dunia.

Wizara ya sheria imesema endapo wageni watahusika katika uhalifu kama watuhumiwa au waathirika, kesi zao zitapewa kipaumbele.

Afrika Kusini ni mojawapo ya mataifa yenye vitendo vingi vya uhalifu duniani, lakini tangu rais Jacob Zuma alipochukua madaraka mwezi Mei, serikali imeweka kipaumbele kupambana na uhalifu.

No comments:

Post a Comment