KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Sunday, December 27, 2009
Kenya yafuta Polisi 88
Taarifa kutoka Kenya zinasema serikali imewafuta kazi maafisa 88 wa Polisi kwa kukiuka taratibu za serikali.
Radio ya shirika la utangazaji la Kenya KBC imemnukuu afisa wa ngazi za juu katika Polisi Bwana Kinuthia Mbugua , akisema uamuzi huo umechukulia ili kurekebisha hadhi ya kikosi cha Polisi na kuwapa watu imani.
Bwana Mbugua ameripotiwa kusema kwamba umma umepoteza imani na Polisi kutokana na tabia ya maafisa wanaokiuka sheria.
Amesema wakuu wa Polisi wanajaribu kwa kila njia kurejesha heshima ya kikosi cha Polisi nchini Kenya.
Waisrael wauwa Wapalestina sita
Hiki ni kizazi cha baba wetu wa imani kinachopambana wenyewe kwa wenyewe kwa msaada wa nchi za magharibi na marekani.
mpaka sasa Tatizo la kizazi cha wana Wa Nabii Ibrahimu limekuwa janga na maslahi kwa baadhi ya watu Duniani.
Kizazi cha Israel au nabii Jakubu ndicho kizazi Kinachotokana na Mtoto wa Pili wa Ibrahimu ambae ni Isihaka (Isack) na kizazi cha Warabu kinatokana na mtoto wakwanza wa Nabii Ibrahimu, ambae ni Ismail.
Tatizo la wapalestina na waisrael lina misingi miwili mikubwa duniani, ambayo ni Dini na Siasa katika umiliki wa ardhi.
Waisrael wauwa Wapalestina sita
Wanajeshi wa Israeli wamewauwa Wapalestina sita, watatu katika ukanda wa Gaza na wengine watatu katika Ukingo wa Magharibi.
Msemaji wa Israel ameliambia shirika la habari la Uingereza la Reuters kuwa Wapalestina watatu waliouwawa Gaza ni kutokana na shambulio la anga.
Katika Ukingo wa Magharibi, wanajeshi wa Israel wanaarifiwa kuwapiga risasi na kuwauwa Wapalestina watatu katika mji wa Nablus.
Mashambulio hayo yametokea siku mbili baada ya raia mmoja wa Israel kuuwawa katika shambulio la kuvizia katika Ukingo wa Magharibi.
Baba wa kijana ambaye alitaka kulipua ndege iliyokuwa imewabeba abiria karibu 300,
Baba wa kijana ambaye alitaka kulipua ndege iliyokuwa imewabeba abiria karibu 300, alionya Marekani kuhusu vitendo vya mwanawe na hasa msimamo wake mkali wa kisiasa.
Babake mzazi, Alhaji Umaru Mutallab, ambaye ni mfanyibiashara maarufu nchini Nigeria alikuwa ametoa ripoti kwa ubalonzi wa Marekani jijini Abuja.
Mnamo michache iliyopita alielezea wasiwasi wake kuhusu msimamo mkali wa kisiasa wa mtoto wake ambaye anasomea uhandisi kwenye chuo kikuu kimoja mjini London, University College London.
Kutokana na jaribio hilo mnamo siku ya Krismasi, usalama umeimarishwa katika viwanja mbalimbali duniani kote.
Maswali mazito
Kijana huyo amefunguliwa mashtaka akiwa hospitalini Michigan ambako amelazwa na majeraha ya mguu aliyopata alipojaribu kuwasha mabomu ambayo alikuwa amejifunga mwilini na kwenye suruali yake ya ndani.
Wakati akijaribu kujilipua, abiria wenzake na wahudumu wa ndege walimwandama kwa nguvu huku ndege hiyo iliyokuwa imesafiri kutoka Uholanzi ikijiandaa kutua mjini Detroit, Marekani.
Familia ya kijana huyo pia iliilezea Idhaa ya Hausa ya BBC kwamba hawakuwa tena na mawasiliano na mtoto wao tangu mwezi Oktoba alipokuwa akiishi Yemen.
Inaripotiwa kwamba aliondoka Yemen akaelekea Ethiopia, halafu Ghana na kisha Nigeria.
Bado kuna maswali mazito kuhusu jinsi Mutallab ambaye ana Visa halisi ya kusafiri hadi Marekani, alivyopanda ndege kutoka Lagos hadi Amsterdam licha ya kuwepo na taarifa kuhusu vitendo na mienendo yake.
Tuesday, December 8, 2009
Mgomo wa Daladala wazua kashehe Tz
Mgomo wa Daladala wazua kashehe Tz
Madereva wa mabasi zaidi ya tisini yanayotoa huduma ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam, nchini Tanzania hii leo wanakabiliwa na hatua za kisheria kutokana na mgomo wa jana wa kusitisha huduma hiyo.
Mgomo huo unafuatia operesheni inayoendeshwa kwa pamoja na Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu, SUMATRA, jeshi la polisi na kampuni ya uwakala ya Majembe Auction Mart katika kukabiliana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani.
Madereva wa mabasi hayo maarufu kama DALADALA wanasema faini za sasa ni kubwa mno ikilinganishwa na walivyokuwa wakitozwa kati ya dola ishirini na thelathini za Kimarekani kabla ya operesheni hiyo.
Shambulio la bomu laua 118 Baghdad
Shambulio la bomu laua 118 Baghdad
Taarifa kutoka Iraq, zinaeleza kuwa watu zaidi ya 118 wameuawa katika mashambulio ya mabomu mjini Baghdad.
Inaarifiwa kuwa mabomu hayo yalikuwa yametegwa ndani ya magari yaliyokuwa yameegeshwa maeneo tofauti.
Mabomu hayo manne yalilipuka kwa wakati mmoja, la kwanza likilipuka karibu na kituo cha polisi eneo la Doura lenye waisilamu wengi wa Sunni.
Wenye kufanya mashambulizi hayo wanasemekana walilenga hasa ofisi za serikali au vyuo vikuu.
Wizara ya mambo ya ndani ni miongoni mwa majengo yaliyoshambuliwa. Hakuna aliyekiri kutega mabomu hayo.
Ntaganda akanusha kushirikiana na FLEC
Ntaganda akanusha kushirikiana na FLEC
Huku maafa yakiendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda amekana madai ya kushirikiana na kundi jingine la waasi.
Ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa inasema kundi linaloongozwa na Bosco Ntaganda linalowasaka waasi wa FDLR huenda likawa tishio kubwa mashariki mwa Congo.
Bosco Ntaganda amekanusha madai ya umoja wa mataifa kuwa, anashirikiana na kundi la waasi lijulikanalo kama Front for the Liberation and Emancipation of the Congo (FLEC).
Bw Ntaganda amekanusha madai hayo katika mahojiano aliyofanya na Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wafungwa Burundi wafanya ghasia
Wafungwa Burundi wafanya ghasia
Wafungwa katika gereza kubwa zaidi la Burundi wamefanya ghasia wakilalamikia walichotaja kama hali mbaya ya maisha na msongamano, huku wakitaka kundi fulani la wafungwa waachiliwe.
Baadhi ya wafungwa walivunja na kuondoka katika gereza la Mpimba nje ya mji mkuu wa Bujumbura kabla ya maafisa wa polisi kuwathibiti.
Mapema moto uliowashwa na wafungwa hao uliteketeza mafaili ya wafungwa.
Mkereketwa wa haki za kibinadamu, Pierre Mbonimpa, alisema wafungwa walikuwa wakilalamikia hali mbaya zinazokiuka haki za kibinadamu na walitaka kuachiliwa mapema wa wafungwa wakisiasa, wazee na watoto.
Gereza la Mpimba lilijengewa wafungwa 800 lakini kwa sasa lina wafungwa 3,500
Maandamano Sudan kupinga Serikali
Waandamanaji nchini Sudan wameteketeza afisi za chama cha rais Omar Al Bashir zilizoko mji wa kusini kulalamikia kukamatwa kwa viongozi watatu wa chama cha SPLM.
Hakuna taarifa kuhusu waathirika katika majengo ya chama cha National Congress mjini Wau. Baadaye polisi waliwaachia huru wanasiasa hao.
Chama cha SPLM kilijiunga na serikali mwaka wa 2005 na kumaliza vita kati ya eneo la Kusini na Kaskazini.
Hata hivyo taharuki kati ya SPLM na washirika wao serikalini kutoka chama cha NCP imeendelea huku uchaguzi mkuu ukikaribia hapo mwakani.
Huu ndio uchaguzi mkuu wa kwanza kwa miaka 24 ambapo raia watamchagua rais, wabunge na wakuu wa mabaraza.
Friday, November 27, 2009
Ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Westerwelle katika mashariki ya kati , mgomo wa wanafunzi na siku ya waajiri ndio masuala yaliyoshughu
Ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Westerwelle katika mashariki ya kati , mgomo wa wanafunzi na siku ya waajiri ndio masuala yaliyoshughulikiwa na wahariri hii leo.
Leo hii katika udondozi wa maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani , wahariri wamezungumzia zaidi ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle katika mashariki ya kati, mgomo wa wanafunzi hapa nchini, na siku ya waajiri.
Tukianza na mada ya ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani katika mashariki ya kati , gazeti la Ostsee-Zeitung linalochapishwa mjini Rostock, linadokeza kuwa ziara ya hivi karibuni kabisa ya waziri Westerwelle katika mashariki ya kati inabaki kuwa katika milio ya kugonganisha glas tu.
Gazeti linaandika:
Akiikosoa kwa kiasi fulani sera ya Israel ya ujenzi wa makaazi ya Wayahudi katika eneo la ukingo wa magharibi, waziri Westerwelle hakufika mbali sana katika suala hilo. Hii ni sawa kwa ziara hii ya kwanza. Hata hivyo ni lazima Westerwelle atoe matamshi ya wazi kuhusu Israel kutokana na urafiki uliopo. Na kudai mengi zaidi kwa Wapalestina kama inavyohitajika katika suluhisho la mataifa mawili. Israel inamtaka kufanya hivyo binafsi. Lakini njia ya kuelekea huko inatia shaka. Kwa hili jibu litakuwa la dharura ambalo halitakuwa rahisi kwa waziri Westerwelle. Kutokana na hali ilivyo katika mashariki ya kati hali ya kujizuwia haipo tena.
Gazeti la Berliner Morgenpost likiandika kuhusu ziara hiyo ya Westerwelle linaandika:
Westerwelle ameonekana kutumia busara lakini sio kwamba alifanya vizuri na hakufanya hivyo , kama kwamba alikuwa na jibu katika suala gumu la mashariki ya kati. Westerwelle alijizuwia na kutoa maneno makali na ya wazi, lakini ameweka msimamo wake wazi, kutokana na kile kinachoitwa ramani ya njia, Road Map kuhusiana na mpango wa amani wa mashariki ya kati. Katika ramani hiyo kuna lengo ambalo ni wazi, nalo ni ujenzi mpya wa makaazi ya Wayahudi ni lazima uzitishwe.
Mada yetu ya pili ni mgomo wa wanafunzi hapa nchini. Gazeti la Sächsische Zeitung la mjini Dresden kuhusu hilo linaandika.Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Wanafunzi wakitundika mabango wakati wa mgomo wao nchini Ujerumani.
Kunahitajika vitu vingi vya masomo katika miaka mitatu ya kusomea shahada ya kwanza. Baadhi ya nyakati ilikuwa inahitaji hata miaka mitano kuweza kukamilisha. Na kwa ajili ya shahada ya uzamili hakuna hata nafasi, mara nyingi ni mwanafunzi mmoja tu hupata nafasi kwa kila wanafunzi 15.
Kwa mfumo mpya wa masomo ya juu katika bara la Ulaya kwa wanafunzi hilo halieleweki. Serikali ya shirikisho, majimbo na vyuo vikuu vinalazimika hivi sasa haraka iwezekanavyo kuuokoa mfumo huo wa mageuzi, kama kuna cha kuokoa.Masomo yabadilishwe ama shahada ya mwanzo irefushwe hadi miaka minne.
Kuhusiana na siku ya waajiri , gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung linaandika.
Sigmar Gabriel anajitumbukiza zaidi katika pango la simba. Katika siku ya waajiri kumekuwa na hali ya kumkaribisha kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha SPD bila ya kuwa na wasi wasi. Waziri wa uchumi Rainer Brüderle analazimika kuikaribisha hali hiyo kwa njia ya kirafiki. Hali ya kufikirika haipotena. Serikali ya nyeusi na njano ambayo viongozi wa makampuni walikuwa wakiihitaji imezongwa na mivutano kuhusu kodi na matumaini ya ukuaju wa uchumi. Habari nzuri ni kwamba: fedha za malipo ya ajira fupi , kansela anataka kuziongeza ; Habari mbaya ni kwamba mchango wa serikali kwa mafao ya kijamii huenda yasitolewe na serikali kwa waajiri.
Kwa hilo mzozo wa kiuchumi hautaondoka na bado kuna hatari ya kuporomoka tena kwa uchumi. Uongozi wa masuala ya kiuchumi nchini Ujerumani umekalia kuti kavu.
Na mpendwa msikizaji hayo ndio maoni ya baadhi ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani kwa leo. Nilikuwa nae Sekione Kitojo.
Korti moja ya Niedersachsen yahoji uhalalifu wa watu kuendelea kuchangia katika fuko la kuijenga upya sehemu ya mashariki ya Ujerumani,miaka 18 baadae
Korti moja ya Niedersachsen yahoji uhalalifu wa watu kuendelea kuchangia katika fuko la kuijenga upya sehemu ya mashariki ya Ujerumani,miaka 18 baadae
Mchango wa mshikamano kwaajili ya ujenzi mpya wa sehemu ya mashariki ya Ujerumani na hatima ya kampuni la magari la Opel ndizo mada zilizohanikiza magazetini hii leo.
Tuanze lakini na mchango wa mshikamano,au "Soli" kama unavyojulikana humu nchini.Gazeti la "REUTLINGER GENERAL-ANZEIGER" linaandika:
Suala hapa sio kujipigania.Na wala hili si suala la kuoneana kijicho kati ya sehemu ya Magharibi na Mashariki-kwasababu wanaochangia katika fuko la mshikamano ni walipa kodi.Suala hapa ni kuhusu kuaminiwa wanasiasa.Na haiwezekani kuwaona wanasiasa wakiendelea kunga'ang'ania mchango huo kwasababu miaka nenda miaka rudi umekua ukimimina mabilioni katika makasha ya hazina ya serikali-ili kugharimia miradi jumla.Mchango wa mshikamano-Soli,lazma ufutwe.Naiwe kupitia hukmu ya korti ya katiba au la.Busara ya kisiasa itumike kutathmini kiwango cha mahitaji .Na ukweli ni kwamba,sisi walipa kodi,mabilioni yatakayopungua,tutalazimika kuchangia,naiwe kupitia mchango wa mshikamano-Soli au bila ya mchango huo."
Gazeti la Sächsischer Zeitung la mjini Dresden linahisi hata kama korti ya katiba ikiunga mkono uamuzi wa korti inayoshughulikia masuala ya fedha ya Niedersachsen,haitomaanisha mwisho wa dunia.Gazeti linaendelea kuandika:
Ni kiroja kuona kwamba ndio kwanza sasa,miaka 18 baada ya kuanzishwa,Soli inawekewa suala la kuuliza na jaji wa korti ya masuala ya fedha,kama mchango huzo uendelee kutolewa.Na hata kama korti ya katiba itaunga mkono hoja hizo,haimaanishi kua dunia ndio inamalizika.Kwasababu zile pesa ambazo miongoni mwa mengineyo,zinatumika kuijenga upya sehemu ya mashariki,zitabidi zikusanywe kupitia njia nyengine.Au waziri wa fedha atalazimika kufutilia mbali mpango ambao tokea hapo unazusha mabishano wa kupunguza kodi za mapato.
Gazeti la Darmstädter Echo" lina maoni sawa na hayo na linaandika.
Ikiwa kweli korti ya katiba mjini Karlsruhe itafutilia mbali mchango wa mshikamano,basi patahitajika njia nyengine ya kujipatia fedha hizo.Pengine walipa kodi watavunjika moyo.Lakini kufutwa moja kwa moja mchango wa mshikamano bila ya kuwepo njia mbadala,si jambo linaloingia akilini kwasababu ,itapelekea mfumo mzima wa sera za fedha kuvurugika.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Makao makuu ya General Motors huko Rüsselsheim
Mada yetu ya mwisho inahusu kasheshe ya kampuni mama ya General Motor kuhusu matawi yake ya Opel nchini Ujerumani.Gazeti la FRÄNKISCHER TAG linaandika:
Baada ya kasheshe ya miezi kadhaa iliyopita,hatimae General Motors linaonyesha limeamua kweli kufanya marekebisho.:hatari lakini kwamba Opel linaweza kupotelewa na imani kuelekea kampuni mama la General Motors ,hivi sasa ni ndogo ikilinganishwa na hali namna ilivyokua mwaka uliopita.
Gazeti la NORDBAYERISCHER KURIER la mjini Bayreuth linaandika:
Msimamo usiokadirika wa General Motors unaweza kuendelea hivyo hivyo siku za mbele.Ingawa GM imeamua matawi yake ya Ujerumani na Ulaya yataendelea kuwepo.Lakini nini mameneja walioko Detroit watalazimisha kupatiwa badala yake kutoka kwa wanasiasa?Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya imejaribu kuzuwia mashindano ya kuania nafasi za kazi yasitokee miongoni mwa nchi za Ulaya.Lakini kama dhamiri za nchi kutoshindana wenyewe kwa wenyewe ni madhu,hakauna anaeweza kuashiria.
Rais wa Nigeria aumwa maradhi ya moyo
Rais Umaru Yar'Adua wa Nigeria ana matatizo ya moyo, msemaji wake ameeleza, baada ya kusafirishwa kwenda Saudi Arabia siku ya Jumatatu kupata matibabu.
Bw Yar'Adua ana maradhi yajulikanayo kama pericarditis, au kiungulia kuzunguka moyo wake, msemaji wake ameieleza BBC.
Alisema kuwa rais huyo, mwenye umri wa miaka 58, anaendelea vyema baada ya kuanza kutibiwa. Maafisa walikanusha taarifa za awali kwamba rais Yar'Adua alikuwa katika hali mahututi.
Bw Yar'Adua amekuwa na maradhi yasiyopona ya figo kwa miaka takriban 10.
Amekuwa akishindwa shughuli kadhaa za kiserikali kutokana na afya yake kumsumbua mara kwa mara.
Mafuriko yaua watu 77 Saudi Arabia
Mafuriko huko Saudi Arabia yameua watu 77 na wengine wengi hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa ambayo haijatokea kwa miaka mingi kunyesha.
Hakuna mtu hata mmoja aliyekufa ambaye ni miongoni wa mamilioni ya watu kutoka sehemu mbali mbali dunia ambao wanafanya Hajj, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Saudi alieleza.
Mvua nzito zinazoambatana na kimbunga zilinyesha siku ya Jumatano na kuchelewesha kuanza kwa shughuli za Hajj za kila mwaka katika mji mtukufu wa Makka.
Watu waliokufa kwa mafuriko walikuwa katika mji wenye bandari wa Jeddah, Rabigh na Makka, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali - Saudi Press Agency.
Ocampo aomba kupeleleza ghasia Kenya
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa, Luis Moreno-Ocampo, anasema kuwa amewaomba majaji wa mahakama hiyo ruhusa ya kuanzisha upelelezi kuhusu ghasia za mwaka jana nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu.
Takriban watu elfu moja waliuawa katika ghasia hizo ziliozuka baada ya Rais Mwai Kibaki kutangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi mnamo Desemba mwaka 2007.
Upinzani ulidai kura ziliibiwa katika Uchaguzi huo.
Akizungumza na BBC Bw Ocampo amesema kuna sababu za kimsingi kuamini kwamba raia walitendewa maovu na vitendo vilivyokiuka haki za binadamu.
Kwa hiyo ikiwa majaji hao watalikubali ombi lake atakwenda Kenya kukusanya ushahidi kwa kuwasaili watuhumiwa na pia mashahidi na hapo ndipo wataamua kama kunastahili kufungua kesi ama la.
Ocampo alifafanua kuwa hawajibiki kutekeleza maelezo kuhusu orodha ya majina ya watuhumiwa ambayo ilikuwemo ndani ya bahasha aliyokabidhiwa mapema mwaka huu akisema hayo ni maoni ya wajumbe wa tume iliyochunguza mauaji hayo.
Yeye inampasa atoe uamuzi wake mwenyewe.
Fifa yalaumiwa kwa ubabe Afrika Kusini
Waandishi wa habari wa Afrika Kusini wamelishutumu shirikisho la soka la dunia kwa kuweka masharti magumu kuandika habari za kombe la dunia mwaka 2010.
Waandishi hao wanasema kulingana na masharti hayo, vibali vya waandishi vinaweza kufutwa endapo wataandika taarifa zinazolikosoa shirikisho hilo.
Wanaasema Fifa imekataa kufafanua swala hilo licha ya jitihada za mara kwa mara kutoka kwa waandishi.
Lakini Fifa imesema masharti hayo yameeleweka vibaya na hayatakwamisha uhuru wa waandishi wa habari.
Hata hivyo, Raymond Louw, msemaji wa jukwaa la wahariri wa Afrika Kusini lijulikanalo kama Sanef, ameieleza BBC kuwa Fifa ina maswali mengi ya kujibu.
Waandishi mateka waachiliwa Somalia
Waandishi wawili wa habari wa kigeni waliotekwa nyara na wanamgambo wa kisomali Agosti 2008 wameachiliwa huru na watekaji hao.
Amanda Lindhout kutoka Canada na Nigel Brennan wa Australia wanasemekana kuwa katika hoteli moja kwenye mji mkuu Mogadishu.
Bi Lindhout alivieleza vyombo vya habari vya Canada kwamba watekaji nyara walimtesa na kuwa kikombozi kililipwa kabla ya kuachiliwa kwake.
Mwandishi huyo aliileza televisheni ya Canada, CTV kuwa walikuwa wakihamishwa nyumba moja hadi nyingine na wanamgambo hao kwa kipindi cha miezi 15 ya kuwa mateka
Mke wa Berlusconi adai mamilioni
Aliyekuwa Mke wa Waziri Mkuu wa Italy Silvio Berlusconi amewasilisha madai ya kutaka alipwe fidia ya kuachika ya euro milioni 43, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.
Veronica Lario aliwasilisha ombi la kuachika mnamo mwezi May, baada ya kuchukizwa na tetesi za mumewe kutoka na binti mwenye umri mdogo wa miaka 18.
Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia linasema kuwa Bw. Berlusconi amekubali kumpa Bi Lario, aliyezaa naye watoto watatu euro laki mbili kwa kila mwezi.
Duru zilizo karibu na kiongozi huyo zinasema kuwa takriban euro milioni 60 hadi sabini zimeisha kabidhiwa kwa Bi Veronica Lario. Bi Lario mwenye umri wa miaka 52 aliolewa na Bw.Berlusconi mnamo mwaka 1990 miaka kumi baada ya kukutana naye.
Mshukiwa wa mauaji nchini Ufilipino ajisalimisha
Mtu mmoja maarufu huko Ufilipino ambaye anatoka ukoo wa Ampatuan amejisalimisha kwa maafisa wanaochunguza mauaji yaliofanyika mapema wiki hii.
Andal Ampatuan Junior, ambaye ni Meya katika eneo la kusini mwa kisiwa cha Mindanao, alisafirishwa kwa helkopta ya kijeshi hadi katika mji mkuu wa Manila na kwa sasa anafanyiwa uchunguzi.
Bw. Ampatuan amekanusha kushambulia familia ya mpinzani wake wa kisiasa, ambapo watu wasiopungua 57 waliuawa.
Ukoo wa Ampatuan kwa miaka mingi umekuwa ukimuunga mkono rais Gloria Arroyo.
Mkuu wa majeshi Ujerumani aachia ngazi
Jenerali wa Ujerumani amejiuzulu kufwatia mashambulio ya angani ya vikosi vya kujihami vya Nato ambapo raia waliuawa, waziri wa ulinzi amesema.
Wolfgang Schneiderhan amejiuzulu kutokana na shambulio la Septemba 4 eneo la Kunduz.
Uamuzi wake umetokana na ripoti kuwa taarifa kuhusu shambulio hilo-liloamrishwa na kamanda wa Ujerumani - hazikuwekwa wazi, waziri wa ulinzi alisema.
Inasemakana kuwa shambulio hilo liliwauwa raia wengi waliokuwa wakichota mafuta.
Wapiganaji wa Taliban waliteka magari mawili ya mafuta yakitoka Tajikistan kuelekea Kabul yakiwa na bidhaa za vikosi vya Nato.
Idadi ya raia waliouawa haijulikani.
Uchaguzi Namibia mashakani
Kampeni za uchaguzi nchini Namibia zimekumbwa na mizozo ya kisheria kabla ya kura za hapo kesho ijumaa.
Chama cha National Society for Human Rights kimewasilisha kesi kortini baada ya tume ya uchaguzi kuondoa hadhi yake ya msimamizi kwa madai kuwa na upendeleo.
Wakati huo huo chama kilichojitenga kutoka chama kikuu cha Swapo kimeiambia BBC kuwa kiongozi wake anadaiwa dollar za Marekani milioni kumi na tatu kwa kudai kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa na dosari.
Mgombea wa chama cha Swapo akiwa ni Rais Hifipekunye Pohamba anawania muhula wa pili baada ya ushindi wqa kishindo katika uchaguzi wa mwaka 2004.
Kiongozi wa upinzani, Hidipo Hamutenya, aliyejitenga kutoka Swapo mnamo mwaka 2004 anatarajiwa kumsumbuwa Bw.Pohamba katika uchaguzi utakaofanyika kwa siku mbili
Mahujaji leo waingia katika bonde la Arafa
Zaidi ya mahujaji millioni mbili wamewasili katika nyanda za Arafat katika siku ya pili ya ibada ya Hijjah.
Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na dhoruba kali ilinyesha mwanzoni mwa ibada hii takatifu siku ya Jumanne na kusababisha uharibifu katika maeneo matakatifu na vifo vya takriban watu 44.
Lakini hali ya hewa inaonekana kutulia na mamilioni ya mahujaji wamekusanyika katika nyanda za Arafat. Kwa mahujaji wengi huu ni wakati wa msisimko mkubwa unaozingatiwa kuwa ni kilele cha hijjah takatifu.
Hapa ndipo mtume Muhammad(SAW) alisimama karne 14 zilizopita na kutoa hotuba yake ya mwisho.Tangu wakati huo kila mwaka waislamu wamekuwa wakikusanyika hapo kusali na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu
Man United yapoteza nyumbani
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson hakusikitishwa na kichapo cha 1-0 katika mchuano wa Ligi ya mabingwa na Besiktas.
Kipigo hicho kinatokea baada ya mechi 23 za Ulaya bila kupoteza kwenye uwanja wa Old Trafford na bado Man.united inahitaji pointi moja kuongoza kundi la B.
Lakini Ferguson, aliyefanya mabadiliko nane tafauti ya timu iliyochuana na Everton siku nne kabla alisema baada ya mechi kwamba nadhani tulipuuza kwa kiasi na ni makosa. Hata hivyo hawa ni vijana wadogo.
Besktas ilipata bao lake kupitia Rodrigo Tello ingawa lilimgusa beki wa United Rafael da Silva.
Avram Grant ateuliwa kuifunza Portsmouth
Aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea hapo zamani, Avram Grant, ametangazwa kuwa meneja wa Portsmouth baada ya Paul Hart kutimuliwa kufuatia kiwango cha timu hiyo kuzidi kuzorota.
Hii ni mara ya pili kwa Grant kufanya kazi kwenye klabu hiyo, mara ya kwanza alitumika chini ya Harry Redknap ambaye sasa yuko na Tottenham.
Raia huyo wa Israili aliwahi kushika wadhifa kama huo wa mkurugenzi mtendaji wa soka wa klabu ya Chelsea kabla ya Mourinho kutimuliwa na yeye kuteuliwa kama kocha.
Grant ataanza kwa mchuano utakaotangazwa na ''Ulimwengu wa Sokar'' Jumamosi hii kati ya Portsmouth na Manchester United.
Panga kumkosakosa Benitez
Mkurugenzi mkuu wa Liverpool Christian Purslow amesisitiza nafasi ya Rafael Benitez ni madhubuti, licha ya kutolewa ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Liverpool imeshindwa kusonga mbele hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita, licha ya ushindi kuifunga Debrecen bao 1-0.
Lakini Purslow amesema Benitez ataendelea kufundisha na akaongeza: "Hayupo hatarini.
Amesisitiza kwamba Benitez amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na ndio kwanza amemaliza miezi minne chini ya mkataba huo, kwa hiyo kuujadili mkataba wake sio sahihi.
Wednesday, November 25, 2009
Al Shabab lashutumu shirika la WFP
Moja ya makundi ya wapiganaji nchini Somalia limesema kwamba msaada wa chakula unaotolewa na Umoja wa Mataifa umezorotesha kilimo nchini humo.
Katika taarifa wapiganaji wa Al Shabab ambao sasa wanadhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia wanalishutumu shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP kwa kuhujumu juhudi za wasomali za kuzalisha chakula chao wenyewe.
Kundi hilo la Al Shabab linataka Umoja wa Mataifa kuacha kuagiza chakula kutoka nje na badala yake kununua chakula kutoka wakulima wa Somalia. Shirika hilo la mpango wa chakula halijasema lolote kuhusu taarifa hiyo ya Al Shabab
Subscribe to:
Posts (Atom)