KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 8, 2009

Wafungwa Burundi wafanya ghasia


Wafungwa Burundi wafanya ghasia

Wafungwa katika gereza kubwa zaidi la Burundi wamefanya ghasia wakilalamikia walichotaja kama hali mbaya ya maisha na msongamano, huku wakitaka kundi fulani la wafungwa waachiliwe.
Baadhi ya wafungwa walivunja na kuondoka katika gereza la Mpimba nje ya mji mkuu wa Bujumbura kabla ya maafisa wa polisi kuwathibiti.

Mapema moto uliowashwa na wafungwa hao uliteketeza mafaili ya wafungwa.

Mkereketwa wa haki za kibinadamu, Pierre Mbonimpa, alisema wafungwa walikuwa wakilalamikia hali mbaya zinazokiuka haki za kibinadamu na walitaka kuachiliwa mapema wa wafungwa wakisiasa, wazee na watoto.Gereza la Mpimba lilijengewa wafungwa 800 lakini kwa sasa lina wafungwa 3,500

No comments:

Post a Comment