KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 29, 2010

Milipuko Burundi wakati wa kuhesabiwa kura za urais


Hali ya wasiwasi imetanda mjini Bujumbura,Burundi baada ya mabomu ya guruneti kulipuka katika eneo moja lenye watu wengi jana usiku.

Hakuna aliyekufa kwenye tukio hilo lililotokea wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais inaendelea katika sehemu zengine nchini humo.

Kumekuwa na matukio ya mashambulio ya maguruneti katika siku za hivi karibuni.

Wakati huo huo vyama vya upinzani nchini Burundi vimesema kwamba havitatambua matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu wa jana ambapo rais Pierre Nkurunziza alikuwa mgombea wa pekee.

Wapinzani wa rais Nkurunziza walijiondoa mchuano wa urais wakidai udanganyifu kwenye uchaguzi wa mabaraza.

Muungano wa vyama 12 vya upinzani umesema ni asili mia 30 pekee ya wapiga kura waliojitokeza kwenye zoezi la jana na kuapongeza raia waliosusia uchaguzi huo.

Uchaguzi wa jana ndiyo wa kwanza tangu kundi la mwisho la waasi kujiunga na mpango wa amani na kuitikia kushiriki katika mchakato wa kisiasa

No comments:

Post a Comment