KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 29, 2010

Wanaowania kiti cha urais Zanzibar wafika 10


MBALI ya saba waliotangaza nia kwa muda mrefu na kuchukua fomu visiwani Zanzibar kuwania kiti cha uraisi wengine watatu wamejitokeza kuwania kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi [CCM]
Walioanza kuchukua fomu hiyo juzi makao makuu ya chama hicho zilizopo Kisiwandui ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Balozi Ali Abeid Karume, Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna.

Wengine ni Hamadi Bakari Mshindo, Waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohammed Gharib Billal na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud.

Wengine watatu waliotangaza nia na kupangiwa kuchukua fomu hizo kesho ni pamoja na Mohammed Raza, aliyewahi kuwa mshauri wa Michezo wa Rais wa Awamu ya Tano wa Zanzibar.

Wengine ni Waziri wa Elimu Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman na Mohammed Yusuph, ambaye wadhifa wake haufafanuliwa.

Wanachama hao kila mmoja anatakiwa kutafuta wadhamini 250 katika mikoa mitatu ya Zanzibar na kati ya mikoa hiyo mmoja lazima uwe wa Pemba na watatakiwa kurudisha fomu hizo Julai mosi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment