KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 29, 2010

Luanda, Angola mji ghali zaidi duniani


Utafiti wa kimataifa umebaini kuwa Luanda,mji mkuu wa Aangola ndiyo mji wenye gharama ya juu kwa wataalamu wanaotoka nje na kwenda kufanya kazi huko.

Ripoti iliyonadiwa na kampuni ya masuala ya kifedha ya - Mecer imesema gharama za kupanga nyumba mjini Luanda ni mara dufu ikilinganishwa na jiji la London.

Mji wa Luanda umetajwa kuwa ghali zaidi, ukifuatwa na Tokyo, Ndjamena na Moscow. Bara Afrika lina miji mitatu miongoni mwa miji kumi ambayo ni ghali duniani.

Jiji la Libreville, Gabon likishikilia nafasi ya saba. Uchunguzi ulifanyiwa katika miji 214 katika mabaraza yote matano. Mambo yaliyoangaziwa ni pamoja na gharama za maisha ikiwemo usafiri, chakula, mavazi na starehe.

Tiketi moja ya kutazama filamu mjini Luanda inauzwa dola 13.

Licha ya raia wengi wa Angola na Gabon kuishi katika lindi la umasikini, hali ni tofauti kwa wageni ambapo gharama za maisha miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni za mafuta zinaambatana na usalama wao pamoja na ada ya kuagiza bidhaa kutoka nchi zao.

Gharama za juu zimawalazimu wenyeji wengi kuondoka mijini kwani hawawezi kukimu maisha.

No comments:

Post a Comment