KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, June 29, 2010

Ndugu wawili wa familia moja wajinyonga


VIJANA wawili ndugu wa familia moja wamejinyonga kwa nyakati tofauti kwa sababu ambayo bado haijafahamika mara moja
Ndugu hao ni Joachim Luciani (27) na Dominic Lucian [33] walijinyonga kati ya Juni 17 na 19 mwaka huu ambao walikuwa wakazi wa Kata ya Kaloleni, Moshi.

Aliyeanza kujinyonga ni Joachim kwa sababu ambayo bado haijafahamika na ndugu yake huyo alishiriki katika zoezi la uchimbaji kaburi na kuwaaga wengine kuwa alikuwa anakwenda kunywa maji kwa kuwa alikuwa na kiu.

Wakati wa maziko ya mdogo wake Dominic hakuonekana makaburini na watu kudhani labda ni uchungu aliokuwa nao amekaa mahali na watu wengine kuendelea na mazishi.

Ilidaiwa hadi mazishi hayo yanamalizika ndugu huyo hakuonekana kuja kumzika mdogo wake, na kesho yake alionekana akining’inia kwenye mti katika msitu wa Njoro akiwa amejinyonga na kuinua msiba mpya wa waombolezaji waliokuwa katika matanga ya ndugu yake.

Mwili huo ulikuja kuchukuliwa na polisi mkoani humo na umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi na uchunguzi wa kina unaendelea kuhusiana tukio hilo.

No comments:

Post a Comment