KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, June 29, 2010

Mauaji ya Rugambage washukiwa wakamatwa


Watu wawili wamekamatwa na polisi nchini Rwanda kwa shutma za mauaji ya mwandishi wa habari wiki iliyopita. Polisi wanasema lilikuwa shambulizi la kulipiza kisasi.

Watu walioshuhudia wanasema Jean Leonard Rugambage, ambaye alikuwa mhariri wa gazeti za Umuvugizi ,alipigwa risasi na watu wawili na kisha wakaingia ndani ya gari na kukimbia.

Serikali ya Rwanda imesema madai kuwa ilihusika katika mauaji hayo hayana msingi.

Taarifa ya polisi inasema mmoja wa washukiwa ni kutoka familia ya mtu ambaye aliuawa na Bw Rugambage wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Rugambage, aliondolewa mashtaka ya kuhusika katika mauji hayo na mahakama ya Gacaca mwaka 2006.

Mashirika ya kutetea haki za bianadam yamemshtumu Rais Paul Kagame kwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na upinzani ,kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Agosti.

Hivi karibuni serikali ilisimamisha gazeti la Umuvugizi na likalazimika kuchapisha habari kwenye tovuti pekee. Aliyekuwa mhariri Jean Bosco Gasasira, ambaye alikimbilia Uganda mwezi Aprili amesema serikali ilihusika katika mauaji ya Rugambage ambaye alikufa akiwa hospitalini baada ya kupigwa risasi.

"Nina uhakika idara ya usalama wa kitaifa ndiyo ilimpiga risasi,'' amelimbia shirika la habari la Marekani VOA.

Bw Gasasira, amesema mauaji hayo yalifanywa baada ya taarifa iliyochapishwa katika gazeti la Umuvugizi kuhusu jaribio la mauaji dhidi ya aliyekuwa mkuu wa jeshi Generali Faustin Kayumba Nyamwasa nchini Afrika Kusini.

Lakini waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amekanusha madai hayo.

''Kwa hakika sio ya kweli na hayana msingi,''ameliambia shirika la habari la AFP.

Serikali pia imekanusha shutma za kuhusika katika shambulizi shidi ya Generali Nyamwasa.

Alihamia Afrika Kusini mapema mwaka huu baada ya kutofautiana na Rais Kagame

No comments:

Post a Comment