KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, June 26, 2010

KATIKA hali iliyowashangaza wengi na kufanya wakinamama waogope kijana Beatus Alex (29) aliingia kwenye wodi ya wanawake


KATIKA hali iliyowashangaza wengi na kufanya wakinamama waogope kijana Beatus Alex (29) aliingia kwenye wodi ya wanawake ya kujifungulia kwa madai kuwa alikuwa akimfata mchumba wake aliyekuja kujifungua hospitalini hapo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi huko katika hospitali ya KKKT Machame wakati kijana huyo alipobuni vazi na kujifunika mithili ya mwanamke na kufanikiwa kupenya wodini humo hali iliyofanya baadhi ya akina mama kumshtukia na kuanza kupiga mayowe ya kuomba msaada.

Uongozi wa hospitali hiyo ulifanikiwa kumkamata kijana huyo na baada ya kukamata na kufunuliwa mavazi hayo aligundulika kuwa aliwahi kuwa mtumishi hospitalini hapo kwa cheo cha Afisa tabibu wa hospitali hiyo na alishafukuzwa kazi Februari mwaka huu kwa kosa la kujidunga sindano za usingizi ambazo alikuwa akitumia kama dawa ya kulevya.

Hata hivyo katika mahojiano ya kina alipoulizwa ni kwanini aliingia wodini humo ambapo haruhusiwi mtu kuingia zaidi ya mama mjamzito na wakunga alijieleza kuwa kuna mchumba wake aliyemtaja kwa jina la Josiphine alikuja kujifungua na yalipoangaliwa mafaili hakukuwa na mwanamke mwenye jina kama hilo.

Hata hivyo iligundulika kuwa mtuhumiwa huyo alifanya mbinu hiyo ya kujifunga ushungi kuingia wodini humo ili aweze kuiba dawa za usingizi zinazotambulika kitaalam kama DDA zinazotumika kuwachoma wagonjwa na alikuwa akijichoma mwenyewe akizitumia kama dawa za kulevya

No comments:

Post a Comment