KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 29, 2010

Wakamatwa na kilo 31 za Cocaine


RAIA wawili wa kigeni wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine wakiwa wameweka kwenye makasha maalum ya kimataifa yenye nembo ya ubalozi.

Watuhumiwa hao ni Diaka Kaba (52) raia wa Guinea na Abubakar Ndijane (50), raia wa Liberia, walikuwa wamehifadhi dawa hizo mabazo wakaguzi hawakugundua mapema na hata mashine zisingeaini uihaliofu huo.

Mkuu wa Kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa alisema watuhumiwa hao walikamatwa Juni 23 majira ya saa 1.30 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema watuhumiwa hao walitumia ujanja wa kupaka kahawa mifuko hiyo na hata mbwa wanaotumika kukagua mizigo uanjani hapo hawakugundua waliponusa na kutokana na karatasi hizo walizotumia kufunga hazikuonyesha kwenye mashine ya ugunduzi.

Alisema katika ukaguzi wa kina katika mabegi yao waliwapekua na kuwakuta na pakiti zenye kilo 31 za dawa za Cocaine ambazo walipaki kwenye mifuko na kuweka nembo ya ubalozi wa Guinea na mihuri mbalimbali.

Alisema walipofanya mawasiliano na ubalozi husika kama wanahusika na watu hao walidai hawawatambui na kuwa chini ya ulinzi wa polisi.

Nzowa alisema katika mahojiano ya kina na kibano watuhumiwa hao walipohojiwa walibainisha kuwa walianza safari yao nchini Trinidad and Tobago kupitia Panama, Brazil na Johanesburg Afrika Kusini na hatimaye kuingia nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment