KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 26, 2010

Mtikila kizimbani tena kwa uchochezi


MCHUNGAJI Christopher Mtikila amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la uchochezi kwa mara nyingine kwa kusambaza walaka wa maneno ya uchochezi mitaani
Mtikila alifikishwa katika mahakama hiyo jana mbele ya Hakimu Michael Mteite wa mahakama hiyo.

Akisoma hati ya mashitaka, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Francis Mboya alidai mahakamani hapo kuwa, mshitakiwa huyo alifanya kosa hilo kati ya Novemba Mosi, 2009 na Aprili 17, mwaka huu katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Mboya alidai kuwa, Mtikila alisambaza walaka wenye maneno ya uchochezi kwa wananchi a jiji hilo.

Mboya alidai kuwa walaka aliosambaza Mtikila ulikuwa maneno yanayosema: “Rais Kikwete kaangamiza kabisa ukristo kutokana na imani yake, na kuongezea kuwa Kikwete yuko Ikulu kwa kuusambaratisha ukristo, hivyo aliwataka wakristo waungana upesi kupeleka ukristo Ikulu”.

Ilidaiwa kuwa katika shtaka la pili Mchungaji huyo alikutwa akimiliki pasipo halali waraka huo wa uchochezi Aprili 16, mwaka huu huko Mikocheni Dar es Salaam.

Hivyo kutokana na mashitaka hayo mtikila kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti, Sura ya 229, kifungu cha 32(i) (c) mshitakiwa huyo alitoa uchochezi ndani ya nchi kinyume na sheria.


Alipotakiwa kujibu mashitaka hayo Mtikila alikana kuhusika na matukio hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo mshitakwia huyo aliachiwa huru bada ya kukamilisha masharti ya dhamana alipotakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika wenye uwezo wa kusaini laki tano kila mmoja pamoja na hati yenye thamani hiyo.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 6, mwaka huu itakapokuja tena ka kutajwa

No comments:

Post a Comment