KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, April 28, 2011

Wafungwa 480 Watoroka Kupitia Kwenye Kishimo Hiki




Wafungwa 480 wa Taliban nchini Afghanistan wametoroka kupitia kwenye kishimo hichi kilichochimbwa na wanamgambo wa Taliban kwaajili ya kuwatorosha wanamgambo wao waliotupwa jela na serikali ya Afghanistan.
Wafungwa hao wa jela ya mji wa Kandahar walitoroka kupitia shimo lilichimbwa kwenye sakafu ya jela hiyo na kutokezea kwenye eneo jingine lililopo umbali wa kilomita moja.

Wanamgambo wa Taliban ndio waliochimba shimo hilo ambapo walidai iliwachukua miezi mitano kulichimba handaki hilo kwaajili ya kuwatorosha wanamgambo wao waliotupwa jela na serikali ya Afghanistan.

Wafungwa hao 480 walitoroshwa usiku wa siku ya jumapili na asubuhi yake maafisa wa gereza walishangaa kukuta jela ikiwa nyeupe wafungwa wametoroka.

Msako mkali umeanzishwa kuwasaka wafungwa hao ambapo Taliban walitamba kuwa miongoni mwa wafungwa waliotoroshwa kulikuwa na makomando wao 100






Mlokole apewa notisi kwa kukera wapangaji wenzake





MWANAMKE mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mkristo anayeabudu katika dhehebu la Makanisa ya Kilokole amelazimika kupewa notisi na mwenye nyumba wake baada ya kuonekana kuwa kero kwa wapangaji wenzake.
Mwanamke huyo [jina linahifadhiwa] amekutwa na kadhia hiyo, Aprili 25 mwaka huu, huko maeneo ya Uwanja wa Ndege alipokuwa amepanga nyumba hiyo

Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 28 amedaiwa kuwa kero kwa wapangaji wenzake kwa kusababisha kelele usiku wa manane wakati akiwa katika maombi ya kumuomba Mungu.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo ambaye alipanga chumba kimoja imedaiwa chumba chake kilikuwa kikitumika na waumini wenzake kama kituo cha kufanyia maombezi mara kwa mara na siku za awali walijaribu kumvumilia lakini miezi mitatu baadae baadhi ya wapangaji walishindwa kuvumilia na kuripoti tukio hilo kwa mmiliki wa nyumba hiyo ili aweze kutatua tatizo hilo

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo amefikisha muda wa miezi mitatu na wiki mbili katika nyumba hiyo toka alipie pango lake

Imedaiwa mwanamke huyo siku za mwishoni mwa juma huwa na kawaida ya kuja na waumini wenzake na kufanya maombi chumbani kwake na kusababisha kelele mithili ya kuwa na msiba jambo ambalo lilikuwa likileta usumbufu kwa baadhi ya majirani wa nyumba hiyo hata na baadhi ya majirani wa nyumba za karibu kwa kuwa mara kwa mara walikuwa wakidhani alikuwa amefiwa na kukimbilia chumbani humo hadi walipozoea kuwa huwa anasali

Mbali na kusali na waumini wenzake majira ya mchana ama jioni, pia maombi ambayo yalikuwa yakikera watu zaidi ni yale ya usiku wa manane na kusababisha usumbufu kwa watoto na hata watu wazima kwa kuwa husababisha kelele za hali ya juu.

Kufuatia hali hiyo wapangaji waliitisha vikao na kukubaliana kuwa wafikishe ripoti hiyo kwa mwenye nyumba na hatimaye mmiliki huyo alifika hapo na kumsihi kuwa awe anafanya maombi hayo bila kusababisha usumbufu kwa wenzie

Kwa kuwa alishazoea hali hiyo ilimuia vigumu kuacha maombi hayo na baadae mmiliki huyo kuchukua uamuzi wa kumpa taarifa ya kumsimamisha mkataba ama aweze kumrudishia kodi yake iliyobaki aweze akapange nyumba nyingine

Hata hivyo mwanamke huyo hajaafiki hayo na kumtaka radhi mmiliki wa nyumba hiyo na kumwambia alikuwa ameipenda nyumba hiyo hata hivyo mwenye nyumba alimtaka amalizie mkataba ahame








Wafungwa zaidi ya 3000 wasamehewa




RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 3000 katika maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano yaliyofanyika juzi visiwani Zanzibar
Rais Kikwete ametoa msamaha huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu hizo ambazo huadhimishwa kila mwaka nchini

Msahamaha alioutoa uliwahusu wafungwa waliokuwa waneakaribia kumaliza vigungo vyao, na haukuwahusu wale waliokuwa wamehukumiwa vifungo vya maisha.

Wengine waliohusika katika msamaha huo ni wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ambao umri wao utathibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au wilaya.

Pia wafungwa wanawake waliofungwa gerezani wakiwa na mimba, pamoja na wale walioingia na watoto wachanga wanaonyonyesha na wasionyonya.

Waliobahatika pia ni wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili








Anywa sumu baada ya dada yake kumtamkia kuwa ana mimba ya mumewe






MWANAMKE anayetambulika kwa jina moja la Fatuma amelazimika kunywa sumu kwa aibu baada ya dada yake kumtamkia kuwa anaujauzito aliopewa na mume wake.
Mwanamke huyo ni ili habari iliyochapishwa wiki mbili zilizopita katika mtandao huu aliyeweza kumfumania mume wake na dada yake chumbani kwake.

Nifahamishe ilipata habari y a kunywa sumu kwa mwanamke huyo jana majira ya usiku na asubuhi hii ilifika nyumbani kwa mwanamke huyo na kukuta tayari alishakimbizwa zahanati kwa msaada zaidi

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo juzi katika sikukuu ya Muungano dada yake ambaye alimfumania na mume wake wakati alipokwenda safari ya kumsalimia mama yake alimfata mdogo wake na kumuambia kuwa amsaidie kutafuta daktari ili aweze kutoa ujauzito aliokuwa nao

Imedaiwa kuwa mdogo wake huyo alijaribu kumuuliza ni kwanini autoa ndipo dada huyo alipoanza kulia na kumuomba radhi kwa mara nyingine na kumueleza alipewa na shemeji yake ambaye ni mume wa mwanamke huyo

Ndipo mwanamke huyo alianza kilio kwa mara nyingine na kwenda kwa shangazi yake aishio karibu naye kumueleza tukio hilo na kudaiwa majira ya saa moja usiku Aprili 26 alitafuta sumu ya kuulia panya bila wana familia kujua na alikoroga na kunywa
Hata hivyo imedaiwa kuwa dakika chache baadae alikutwa kitandani akiwa hoi na hatua za awali za kutoa povu zilianza kujitokeza na kudaiwa kukimbizwa hospitali

Hadi leo asubuhi mwanamke huyo anaendelea na matibabu katika zahanati moja ya karibu na maeneno hayo
Awali mwanamke huyo alimfumani mume wake na dada yake na aliweza kuacha nyumba hiyo na kwenda kwa shangazi yake lakini baadae maongezi ya kifamilia yalifanyika na kumalizika na kusameheana kwa pande zote mbili ana alirudi nyumban I kwake bila wanafamilia kutotambua kwamba alipewa ujauzito na yeye mwenye alikuwa hafahamu

Ndipo juzi jambo hilo lilijitokeza baada ya dada yake kujigundua kuwa mjamzito na kumfata mdogo wake wasaidiane kutoa ujauzito huo bila wanandugu kujua

Nifahamishe itaendelea kuwajuza kitakachoendelea kuhusiana na mtafaruku huu wa kifamilia








Konda Nae Kaoteshwa na Mungu -Mbagala


MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.

Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.

Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.

Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.

Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe






Muhogo mbichi wapoteza maisha ya mtoto



MTOTO Lawrence Gervas [4] amefariki dunia baada ya kumaliza kutafuna muhugo mbichi unaosadikiwa kuwa na sumu na watu wengine wawili kuugua kutokana na kutafuna mihogo hiyo.
Akitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba, alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Aprili 19, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni huko Kata ya Igoma, Wilayani Nyamagana.

Kamanda huyo amesema kuwa mtoto huyo alifariki, baada ya kutafuna mihogo mibichi waliyokuwa wakitafuta na wenzake.

Katika tukio hilo wengine wamenusurika na kifo hicho na wanaendelea na matibabu hospitali ya Bugando kutokana na kutafuna mihogo hiyo.

Gervas alifariki dunia wakati akikimbizwa katika hospitali ya Bugando.

Taarifa hiyo imendelea kusema kuwa, “Tayari mihogo hiyo tumeipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mwanza kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili pia kujua kiasi cha sumu iliyomo katika chakula hicho,” alisema Kamanda Komba







Maadhimisho miaka 47 Muungano








MAADHIMISHO miaka 47 ya Sikukuu ya Muungano wa Tanzania yanatarajiwa kufanyika kesho huko visiwani Zanzibar
Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa, maadhimisho hayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar

Maadhimisho hayo ni kumbukumbu ya kukumbuka kuungana kwa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar na kupatikana Tanzania nchi zilizoungana April 26, mwaka 1964 kwa kuchanganya udongo wa pande zote mbili na waasisi wa nchi hizo.

Hivyo kila mwaka ifikapo Aprili 26 ni siku ya mapumnziko kupisha sikukuu ya kumbukumbu hizo.

Hivyo watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo kusherehekea kwa pamoja sikukuu hizo na milango ya uwanja huo ityafunguliwa kuanzia majira ya 12 asubuhi kuruhusu wananchi kujumuika katika sherehe hizo









Shule ya awali Nia yafungwa





KAIMU Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick ametoa agizo kufungwa kwa shule ya Awali Nia iliyopoteza maisha ya watoto wanne walioangukiwa na ukuta iliyopo Kimara Matosa jijini Dar es Salaam
Hatua hiyo imekuja baada ya kugunduklika kuwa shule hiyo ilikuwa ikiendeshwa isivyo halali na mmiliki kuendesha shule hiyo bila kibali na Jacqueline Sarungi [42]

Sadick amesema kufuatia hatua hiyo shule hiyo ifungwe na kutoa onyo kali kwa shule zote zinazoendeshwa isivyo halali zigungwe haraka iwezekanavyo

“Shule zote za awali ambazo hazina usajili wala kibali za kuendesha shule hizo zifungwe, na ikigundulika sheria itafata mkondo wake

Watoto wanne walipoteza maisha katika shule wakati wakiwa wanabembea ndani ya shule hiyo na ukuta wa jirani wa nyumba iliyokuwa karibu na shule hiyo ukaanguka na kuwafikia watoto hao na kupoteza maisha papohapo

Watoto waliopoteza maisha ni Isaack Ndosi [5], Gladness Shimwela (5), Devotha Living (5)na Ludacris Lawrence (3) wote walikuwa wakazi wa Kimara B Matosa






Siogopi vitisho, mapambano yapo palepale- Nape






KATIBU wa Halmashuri Kuu, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema atapambana vilivyo kuwang’oa mafisadi waliopo ndani ya chama hicho na kudai katika hilo haogopi mtu na kutotishika na vitisho vinavyoendelea dhidi yake.
Nape alitoa siku 90 kutaka mafisadi kujiondoa wenyewe ndani ya chama hicho na kinyume na hapo watatajwa hadhrani kwani kuwepo kwao wanakiharibu chama hicho na kukiondolea sifa.

Hata hivyo alisema hayo si maamuzi yake binafsi na kudai kuwa ni maazimi ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Kamati Kuu ya CCM yaliyoazimiwa katika vikao vyake.

Hivyo kufuatia vitisho kwa mafisadi hao amesema katika maisha yake hamwogopi mtu anapotekeleza majukumu yake ya kikazi na kuwataka wafanye wanayoyataka na kusisitiza kuwa amezaliwa katika jiji la Dar es Salaam, hivyo mapambano kwake ni mambo ya kawaida na kamwe hawezi kuogopa watu wanaomtisha.

“Mimi natimiza majukumu yangu nashangaa wanaosema kwamba nafanya mashambulizi yangu kwa ajili ya kuwalenga wanachama fulani”.

“Kwanza mimi namuamini sana Mungu na si kawaida yangu kumuogopa mtu, kwani Mungu akiamua kuniita sitaweza kupinga najua siku yangu ndio imefika’ sitaweza kukwepa” alisema Nnauye

“Sitavunjika moyo, sitakata tamaa na chochote wanachofanya mafisadi ni sawa na kumwagia petroli kwenye moto, matokeo yake ni kuendelea kuulipua na kukoleza mapambano ya vita dhidi yao,”

Hayo yamekuja baada ya kudaiwa kuna baadhi ya wanachama hawataki kujiondoa ndani ya chama hicho na kuleta vikwazo kutokana na hivi karibuni, CCM kuweka mikakati mipya ya kukijenga Chama na kuwataka watuhumiwa wa ufisadi walioko ndani ya CCM kutafakari na kuachia madaraka ndani ya siku 90, vinginevyo watalazimishwa.

Tangu kutangazwa kwa mkakati huo, kuna taarifa kuwa baadhi yao hawataki kuondoka na wamepanga kuanza kutekeleza njama za kuwachafua viongozi waandamizi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa CCM , Rais Jakaya Kikwete na familia yake.








Mfanyabiashara Rumande kwa Kuvunja Nyumba ya Mwandishi




Mfanyabiashara mmoja maarufu wa mjini Kasulu mkoani Kigoma amefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo akituhumiwa kuvunja na kubomoa nyumba ya mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kigoma ndugu Prosper Kwigize iliyopo mjini Kasulu.
Katika mahakama hiyo mwendesha mashtaka wa polisi Baraka Hongoli ameieleza mahakama hiyo juzi kuwa, Bw. Jared Bugeraha maarufu kama Bwato aliivunja nyumba hiyo yenye thamani ya shilingi milioni kumi na mbili siku ya jumanne asubuhi akishirikiana na vijana watano walioajiliwa kwa kazi hiyo.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, mfanyabiashara huyo alifanya kitendo hicho baada ya kufanikiwa kuwafukuza mafundi na familia ya mwanahabari huyo akitishia kuwaua endapo wangezuia kutekelezwa kwa uharibifu huo.

Aidha imetajwa kuwa, Bw. Bwato alifanya hivyo kama sehemu ya kutekeleza azima yake ya kujichukulia sheria mkoanoni kwa kile alichotaja katika maelezo yake kwa jeshi la polisi kuwa Bw. Kwigize na wengine watatu walikuwa wamejenga nyumba zao katika viwanja vyake vilivyoko mtaa wa mwilamvya kitalu T.

Katika mahakama hiyo mshtakiwa alisomewa mashtaka mawili moja la kuvunja nyumba na kosa la pili likitajwa kuwa alitishia kumuua Bw. Masoud Kitowe mkazi wa mjini Kasulu ambaye naye amejenga nyumba yake katika eneo hilo.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alikusudia kuvunja nyumba tatu ikiwemo ya Bw. Japhet Jonas ambapo kabla ya kutimiza azima yake jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa mamlaka ya idara ya ardhi, maliasili na mazingira na kufanikisha kuzuia uharifu huo.

Hata hivyo polisi waliokwenda eneo la tukio walikuta nyumba ya Bw. Kwigize ikiwa chini na kufanikisha kuzua kipande kimoja tu cha ukuta wa nyumba hiyo yenye ukumbwa wa mita 13.5 urefu na upana mita 8 ikiwa na vyumba vinne self container, sebule moja pamoja na jiko la kupikia.

Pamoja na mhakama ya wilaya ya Kasulu kutoa mwanya wa dhamana kwa mshatakiwa ndugu zake hawakukidhi masharti na hivyo mshtakiwa akapelewa rumande hadi Mei 5, kesi yake itakapotajwa tena katika mahakama hiyo.

Hii ni mara ya nne kwa mfanya biashara huyo kuvunja nyumba za wananchi wenzake kwa visingizio mbalimbali kwa madai ya kuwepo kwa migogoro ya ardhi na amekuwa hana desturi ya kufuata sheria akitamba kuwa pesa anazomiliki zinaweza kumaliza tatizo au kesi yoyote katika maisha yake, aidha amekuwa akiwanyima mishahara watumishi wake na kuwazushia kesi za wizi ili kuwahujumu na kuwatishia kutodai madai ya posho zao







Masikini watoto hawa!




SIMANZI imetawala kwa wazazi na uongozi wa Shule ya Awali iitwayo Nia baada ya kupoteza watoto wanne kufa papohapo baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wakiwa michezoni
Shule hiyo ya awali ‘chekechea’ ipo Kimara Matosa jijini Dar es salaam wilayani Kinondoni inamilikiwa na Jacqueline Sarungi [42] mkazi wa Kimara Matosa.

Juzi majira ya saa 6:30 mchana katika shule hiyo watoto wane walipoteza maisha papohapo na wengine watatu walijeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba uliokuwa karibu na shule hiyo.


Watoto hao walipoteza maisha wakati walipokuwa wakibembea na ghafla waliangukiwa na ukuta wa nyumba iliyo karibu na shule hiyo

Watoto waliopoteza maisha ni Isaack Ndosi [5], Gladness Shimwela (5), Devotha Living (5)na Ludacris Lawrence (3) wote walikuwa wakazi wa Kimara B







Waislamu waliombea Taifa




WAUMINI WA KIISLAMU wamefanya maombi maalumu ya amani kuliombea Taifa la Tanzania liendelee kuwa katika amani.
Maombi hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Waislamu ya Taibah Tanzania kwa lengo la kuliombea Taifa lisiende pabaya kwa kugawa watanzania kwa matabaka.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Shehe Hassani Kiburwa, alisema wameamua kufanya Maulid hayo ya kuombea amani ya nchi, baada ya kuona kuna dalili za kutoweka kwa utulivu na amani nchini.

Katika maombi hayo waislamu walitoa wito kwa serikali kuwashughulikia wale wote wanaoonekana kutaka kulipeleka taifa pabaya

Waliitaka serikali kuwashughulikia watu hao wanaoonekana kutaka kuligawa taifa hili kwa ukabila, udini na hata wanaotaka kulifanya taifa hilo kama lao binafsi na kusahau wananchi

“Nchi hii ni ya wote na waliomo pia wanatoka kumoja, Watanzania sote tunasafiri katika jahazi moja, hivyo kama kuna mmoja






Mahakama yaamuru kufungwa kwa ukumbi



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mwanza, imeamuru kufungwa kwa ukumbi wa Palm Inn ulioko Kata ya Nyakato kwa kuwa ulikuwa ukisabasisha usumbufu kwa wakazi eneo hilo
Amri hiyo imetolewa na Mahakama hiyo kumtaka mmiliki wa ukumbi huo kusimamisha shughuli zake kwa kuwa ukumbi huo una shitaka mahakamani.

Mmiliki wa ukumbi huo Bw. Paulo Mushi anashitakiwa na watu wawili waliotambulika kwa majina ya Kapeji Donald na Gbral N. Mong’osyson kwa kuathirika na kelele za usiku kutoka ukumbini humo na kuwanyima usingizi nyakati za usiku.

Hivyo Mahakama hiyo imeamuru kufungwa kwa NightPub hiyo ili kupisha kumalizika kwa kesi hiyo ya madai hadi itakapomalizika

Walalamikaji hao wamefungua kesi hiyo ya madai kutaka walipwe kiasi cha shilingi million 85 kama fidia ya usumbufu huo








Askari auawa wakati akisaka walima bangi-Tabora


ASKARI Polisi Joseph mwenye namba E 9530, PC wa Kituo Kidogo cha Puge Wilayani Nzega mkoani Tabora, ameuawa kwa kupigwa mawe na kukatwa mapanga na wananchi wakati akiwa katika msako wa kukamata watu wanaolima zao aina ya bangi wilayani humo.
Akitoa taarifa hiyo jana kupitia Televisheni ya Taifa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Bw. Liberatus Barlaw aliseman kuwa, tukio hilo lilitokea jana saa 4 asubuhi katika kata hiyo.

Wananchi hao pia waliweza kumjeruhi askari mwingine na wengine wawili walifanikiwa kukimbia.

Tarifa ya awali kutoka wilayani humo imedai kwua askari hao hawakuwa na silaha na ndo mana wananchi walipata nguvu ya kuwadhibiri kirahisi na kusababisha kifo hicho














Mwanamke mbaroni kwa kutupa mtoto chooni






HAPPY Freddy (28), mkazi wa Mikocheni, anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kusababisha kifo cha mtoto wa kiume wa siku moja kwa kumtupa chooni.
Kamanda wa mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Kenyela amesema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8 mchana huko maeneo ya Mikocheni 'A'.

Kenyela amesema kuwa, taarifa hiyo iliifikia polisi baada ya wifi wa mtuhumiwa aitwae Shadya Ally (18) kupeleka taarifa kituo cha polisi Osterbay.

Amesema mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake Mikocheni alianza kusikia uchungu wa kuashiria kutaka kujifungua na alimuomba wifi yake huyo amsindikize hospitali .

Kamanda akiendelea kutoa taarifa hiyo alisema kuwa, walianza safari ya kumpeleka hospitali lakini wakiwa njiani ghafla mtuhumiwa ambae ni ‘Happy’ alimwambia wifi yake huyo kuwa anajisikia haja na alishuka eneo hilo kwenda chooni kujisaidia na Shadya alimsubiri nje.

Amesema ghafla Shadya akiwa nje alisikia sauti ya mtoto ikilia kutoka chooni humo na aliamua kuingia na kukuta kichanga cha jinsia ya kiume kikiwa kimeegeshwa pembezoni mwa tundu la choo na kutoelewa ilikuwaje.

Kenyela alisema” wifi mtu aliamua kuwasha tochi ya simu yake ya mkononi na alimwona vizuri mtoto huyo na ghafla mtuhumiwa alikisukumiza kichanga hicho ndani ya tundu la choo kwa mguu wake na kwa madai kuwa alikuwa ameharibika.

Hivyo kufuatia tukio hilo Shadya aliomba msaada kwa majirani na kutoa taarifa kituo cha polisi kuomba kuopolewa kwa kichanga hicho na walifanikiwa kuokoa mwili huo kwa kushirikiana na polisi ukiwa tayari mfu.

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na polisi kufuatiwa tukio hilo







Daladala yauwa wawili asubuhi hii




DALADALA

WATU wawili wamefariki dunia na wengine zaidi ya 21 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Kigogo jijini Dar es Salaam.
Basi aina ya Toyota DCM linalofanya safari zake kati ya Kigogo Mburahati na Kivukoni limepinduka lilipofika eneo la Kigogo Festini na kusababisha ajali hiyo.

Kufuatia ajali hiyo watu wawili wameweza kupoteza maisha papohapo na kupatikana majeruhi hao










Hausigeli Jela miaka 7 Kwa Kumuiba Mtoto wa Muajiri Wake





MSICHANA wa kazi za ndani, Khadija Athumani (27), mkazi wa Kimara amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kuiba mtoto wa mwajiri wake Victory Charles (4).
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani na huku upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mtani Magoma.

Mtani alidai kuwa, Februari 18, mwaka 2009 mshitakiwa alimuiba mtoto wa mwajiri wake aitwae Charles Aloyce.

Alidai kuwa aliiba mtoto huyo wakati alipokwenda kumfata mtoto huyo kumrudisha nyumbani kutoka shuleni.

Mshitakiwa huyo wakati wa ushahidi alidai kuwa alipokuwa kituoni akisubiri basi la mwanafunzi kufika kituoni hapo walitokea vijana wawili ambao alidai hawaelewi na kukaa hapo

Aliendelea kusema kuwa wakati basi hilo lilipofika kituoni hapo mtoto huyo alishuka garini na alimchukua na vijana hao walimueleza kuwa wampe hela na awape mtoto huyo na kudai alikataa

Wakati vijana hao wakiendelea kumsemesha mtoto huyo alimwambia dada huyo kuwa anahitaji kujisaidia na alimruhusu akajisaidie pembezoni na vijana hao walitoweka na mtoto huyo hakurudi.

Hata hivyo shahidi wa pili wa kesi hiyo ambae ni dereva wa basi la wanafunzi hao aliileza mahakama kuwa wakati alipofika katika kituo hicho walimkuta msichana huyo akiwa na vijana hao na walimshusha mwanafunzi huyo na basi lilisubiri kwa muda kidogo kumsubiri mzazi mwingine afike kituoni hapo kumchukua mtoto wake

Hakimu aliposikiliza ushahidi huo alitoa adhabu hiyo kali ili iwe fundisho kwa wengine na baada ya Mwendesha Mashitaka kumwambia hakimu huyo hakuwa na shtaka lingine zaidi ya hilo

Hata hivyo ndugu wa mtoto huyo hawakuridhika na hukumu hiyo kwa kuwa mtoto huyo hafahamiki yuko wapi mpaka sasa na kama yu hai ama la.








Wataka Hoteli ifungwe kwa kusababisha mauaji



WAKAZI wa Kigamboni jijini Dar es Salaam Wilayani Temeke wameipa Serikali siku zipatazo saba Hoteli ya Kitalii ya South Beach iwe imefungwa vinginevyo wataitisha maandamano kuichoma hoteli hiyo.
Pia wametaka kuondolewa kwa mwekezaji huyo nchini kwa kusababisha kifo cha Lila Hussein (34) kwa kumhisi mwizi alipoingia hotelini humo.

Imedaiwa kuwa, mwekezaji huyo amekuwa na vitendo vya kikatili vinavyoenda kinyume na haki za binadamu kwa kuwa mara kwa mara wamekuwa wakiokota maiti jirani na hoteli hiyo.

Jana kiliitishwa kikao kilichohudhuriwa na wananchi na kushirikisha maofisa wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) cha jijini Dra es Salaam.

Katika kikao hicho wananchi hao wametoa mapendekezo ya kufungwa kwa hoteli hiyo na kuona ni suluhisho la kukomesha vitendo hivyo.

Pia walitaka hoteli hiyo itaifishwe na kupewa mtu mwingine ambaye atakuwa na moyo wa kibinadamu anayeweza kushirikiana na wananchi wanaolizunguka eneo hilo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Mohamed Athumani (75), akizungumza katika kikao hicho alisema lazima walipize kisasi kwa kuwa ndugu yao ameuawa kikatili kwa kuchomwa moto na mwekezaji huyo bila hatia.

Hivyo waliitaka serikali kufuata maagizo hayo vinginevyo wananchi watashirikiana kwa pamoja na kuichoma moto hoteli hiyo.

Hivi sasa hoteli hiyo inalindwa na askari polisi wenye silaha baada ya mmiliki wake kushikiliwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za kusababisha kifo hicho










Mvua zazua tafrani-Dar



MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimeonekana kuwa kero kwa wakazi wa jiji hilo.
Kufuatia mvua hizo imesababisha uharibifu wa miundombinu na kubwa imeweza kuvunja daraja linalounganisha barabara ya Bahama Mama ya Ubungo na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Kufuatia hali hiyo mawasiliano kwa wakazi watumiao barabara hiyo.

Manispaa ya Kinondoni imesema kuwa inafanya tathimini ili iweze kujenga daraja hilo na kurudisha mawasiliano.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesabasisha mafuriko katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es salaam.

Mvua hizo kubwa bado zinaendelea kunyesha na uharibifu zaidi unaotokana na mvua hizo unatarajiwa kutokea







Muuaji apatikana ashikiliwa na polisi







MWALIMU Kassim Bindo (25), anayedaiwa kuuwa watoto wawili wa kaka yake amepatikana na anashikliwa na polisi



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema mtuhumiwa huyo yuko chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa katika msako mkali uliofanywa na polisi.

Amesema mtuhumiwa huyo amekiri kuhusika na ukatili huo na uchunguzi wa kina zaidi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.

Hivyo Kamanda huyo amesema muda wowote mtuhumiwa huyo anaweza kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kuwaua watoto wawili ambao ni Mwanamkasi Shaban (4) na Asha Shabani mwenye umri wa siku 40 na kumjeruhi mama wa watoto hao Kuruthum Shabani [28] kwa kuwachoma na visu wakati walipokuwa wamelala nyumbani kwa babu yao huko maeneo ya Kipunguni.

Watoto hao wamezikwa jana

Awali mama wa watoto hao alikwenda nyumbani kwa wakwe zake akitokea nyumbani kwake maeneo ya Buguruni
kwa lengo la kwenda kupumzika akisubiriri kujifungua baada ya kutakiwa kwenda huko ili apate uangalizi wa karibu.

Alijifungua salama na alikuwa katika hatua za mwisho za kurudi nyumbani kwake Buguruni baada ya kukaa hapo takribani siku 40 na kabla hajarudi amekutwa na msiba huo wa kuuliwa mtoto wake mkubwa wa miaka minne na mtoto aliyejifungua akiwa hapo.

Hata hivyo imedaiwa kuwa mtuhumiwa ameonekana huenda alikuwa amechanganyikiwa na tukio hilo halikufikiriwa hata na familia.

Jana kijana huyo alikamatwa akiwa amerudi nyumbani hapo na hakutambua alichokuwa amefanya na kukuta watu wamekaa nyumbani hapo kwenye msiba na yeye kukaa na kujichanganya na watu waliofika katika msiba huo.

Ndipo alichukuliwa na kukamatwa na kufikishwa kituo cha polisi








Barcelona 2 Real Madrid 0



Nyota wa Barcelona Lionel Messi alifunga mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za mwisho, na kuipa nafasi kubwa Barca kucheza fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.


Messi


Kulikuwa na mvutano mkali kati ya timu hizo mbili, katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, hadi pale Pepe wa Real alipopewa kadi nyekundu katika dakika ya 61.

Baada ya kadi hiyo, Barca walianza kutawala, na kupata magoli hayo mawili.







Makundi hasimu ya Palestina yaafikiana





Israel inapinga muafaka huu kati ya Fatah na Hamas
Makundi mawili yanayozozana ya Fatah na Hamas yamesema yamekubaliana kuunda serikali ya mpito ya muungano huko Palestina.

Habari hii muhimu ilitangazwa nchini Misri, nchi ambayo imekuwa inajaribu kupatanisha makundi haya.

Mapigano ya makundi hayo mawili yalianza miaka minne iliopita yakiacha kundi la Fatah likidhibiti eneo la West Bank na Hamas eneo la Gaza.

Lakini hatua hii ya kuafikiana imepingwa na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye anasema kundi la Fatah linaloongozwa na Rais Mahmoud Abbas haliwezi kufanya amani na Israel na Hamas.

Bw Netanyahu anasema lengo la Hamas ni kuangamiza Israel na kuwa hatua hii inaonyesha ulegevu wa utawala wa Rais Abbas.

Mgawanyiko kati ya Hamas na Fatah ni mkubwa na wakati mwengine kumekuwepo na maafa.

Vyombo vya usalama kutoka pande zote vimekuwa vikizozana na kuna hofu ikiwa vitaweza kuweka tofauti zao kando na kutii amri kwa utawala mmoja.

Kulingana na makubaliano hayo, Hamas watasimamia usalama wa Gaza na Fatah watadhibiti eneo la West Bank.

Ni wazi kuwa Rais Abbas amekerwa na kukwama kwa mazungumzo ya amani kati yao na Israel ndio maana ameamua kukubaliana na Hamas.

Serikali ya Marekani na Umoja wa nchi za Uropa wanalitambua kundi la Hamas kama magaidi, na haijulikani ikiwa wataendelea kufadhili utawala wa Rais Abbas baada ya muafaka huu.







Palestina yajibu kuhusu 'nyaraka za siri'




Wakimbizi wa Kipalestina, Lebanon
Maafisa wa Palestina wameishutumu al-Jazeera kwa kupotosha, baada ya kutoa taarifa za siri zilizokusudia kuonyesha nchi hiyo kuwa na maridhiano makubwa na Israel.

Rais Mahmoud Abbas alisema siri hizo zimechanganya kwa makusudi misimamo ya Palestina na Israel.

Nyaraka hizo zinasema kuwa Palestina iliikubalia Israel kubaki na eneo kubwa la mashariki mwa Israel wanalomiliki kinyume cha sheria- jambo ambalo Israel imelikataa.

BBC imeshindwa kuthibitisha binafsi nyaraka hizo.

Al-Jazeera ilisema ina rekodi 16,076 za siri za mikutano, barua pepe, na mawasiliano baina ya Palestina, Israeli na viongozi wa Marekani, baina ya mwaka 2000-2010.

Inaripotiwa Wapalestina wamependekeza kuundwa kwa kamati ya kimataifa ili kuhodhi maeneo matakatifu ya Kiislamu Jerusalem, na kupunguza idadi ya wakimbizi wanaotaka kurejea kufikia 100,000 kwa kipindi cha miaka 10.

Nyaraka hizo zinaaminiwa kutolewa kwa upande wa Palestina.

Bw Abbas, anayetarajiwa kufanya mazungumzo ya amani ya Mashariki ya kati siku ya Jumatatu na Rais wa Misri Hosni Mubarak, alisema mazungumzo ya amani yamefanyika kwa uwazi, na viongozi wenzake wa kiarabu walikuwa wakijua kila kilichoendelea.







Gaza
Akinukuliwa na shirika la habari la Reuters, alisema akiwa Cairo, " Kinachokusudiwa ni kutuchanganya. Nilishuhudia jana wakiwasilisha taarifa kama Palestina lakini walikuwa Israel...kwa maana hiyo hilo limefanywa kusudi."

Wakati huo huo, msemaji wa serikali ya Palestina, Yasser Abed Rabbo, alikataa kusema iwapo nyaraka hizo ni za kweli au la.

Alisema " Leo al-Jazeera imechapisha kwa kile kinachoita nyaraka zilizotolewa na wakurugenzi wa mapatano wa PLO."

" Hatutajadili uhalali au kutokuwa na uhalali wa nyaraka hizo."

Mhariri wa BBC wa Mashariki ya Kati Jeremy Bowen alisema kauli ya Palestina inaashiria mtikisiko mkubwa ambao nyaraka hizo za siri zinaweza kusababisha kwa Bw Abbas na wenzake.

Serikali ya Palestina kwa sasa itabidi kuwashawishi raia wa Palestina kwamba uamuzi huo ulifanyika kwa faida yao, hasa ambapo wengine wataona nyaraka hizo kama namna nyingine ya kuwadhalilisha.

Msemaji wa kundi la Hamas, ambalo linadhibiti ukanda wa Gaza na ni mpinzani wa chama cha Fatah cha Bw Abbas, alisema nyaraka hizo zilidhihirisha "ubaya wa serikali ya Palestina, na kiwango cha ushirikiano wao na umiliki wa Israel."









Vikosi vya Outtara vyauwa mshirika wake




Kiongozi wa kundi lijulikanalo kama ''Invisible Commandos'' Ibrahim Coulibaly, aliuawa katika shambulio la jumatano



Mmojapo wa viongozi maarufu wa makundi ya waasi nchini Ivory Coast ameuawa na vikosi vya Rais mpya wa nchi Alassane Ouattara.

Kiongozi wa kundi lijulikanalo kama ''Invisible Commandos'' Ibrahim Coulibaly, aliuawa katika shambulio la jumatano kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Ulinzi.

Vikosi vya Bw.Coulibaly vilimsaidia Bw.Outtara katika juhudi za kudhibiti sehemu za mji mkuu Abidjan wakati wa mgogoro wa hivi karibuni.

Coulibaly ameshiriki majaribio kadhaa ya kuipindua serikali katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Mwaka 2002 alikuwa chachu katika mgogoro ulioigawa nchi mapande mawili hadi vikosi vya Bw.Outtara vilipompindua aliyekuwa Rais Laurent Gbagbo majuma mawili yaliyopita.

Akiwa mwenye umri wa miaka 47 na maarufu kama ''IB'' alikua mlinzi mkuu wa Bw.Outtara lakini hakutaka kusalimisha silaha zake akitaka kama wadadisi wengi walivyodhani akisubiri mchango wake katika vita vya kumuondoa Gbagbo ukubalike.

Mwandishi wa BBC mjini Abidjan, John James anasema kuwa kifo cha Bw.Coulibaly kitaondoa uwezekano wa kutokea kwa ghasia na kuikosesha utulivu serikali mpya.

Hata hivyo mwandishi wetu anasema kuwa mvutano wa ndani miongoni mwa washirika kutoka makundi ya wababe wa vita uliomuweka Rais Outtara madarakani bado unaleta wasiwasi.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi Capt Leon Alla Kouakou alielezea shirika la habari AFP kuwa aliiteka familia moja kufuatia hatua ya vikosi vya Bw.Outtara kumtaka asalimishe silaha zake.

Vikosi vya Ouattara vilipofyatua risasi za kumuonya alijibu kwa kutumia silaha nzito na walipojibizana kwa moto ndipo akauawa pamoja na wapambe wake.

Serikali ilipoteza askari wawili na Bw.Coulibaly kuuawa na wapiganaji wake sita katika mapigano yaliyofanyika katika kitongoji cha mji mkuu Abidjan kijulikanacho kama PK18 katika wilaya ya Abobo






Upinzani wapanga maandamano Uganda




Kisa Besigyge
Kundi la wanaharakati wa kisiasa nchini Uganda maarufu kama "Activists for Change" wanatarajiwa kurejelea tena maandamano ya kutembea hadi kazini kupinga kupanda kwa bei ya mafuta na chakula.

Naye Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye ambaye aliachiwa huru jana baada ya wiki moja rumande ameapa kuunga mkono juhudi za kundi hilo.

Ikiwa hatashiriki, hii itakuwa mara ya kwanza yanafanyika bila viongozi wa ngazi ya juu kutoka upinzani ikizingatiwa pia kuwa mwenzake, Norbert Mao wa chama cha DP yupo chini ya ulinzi.








Maafisa wa polisi wapya wasajiliwa Kenya




Mkuu a Polisi nchini Kenya
Usajili wa makurutu watakao jiunga na kikosi polisi nchini Kenya umekamilika huku mabadiliko makubwa yakishuhudiwa ili kuhakikisha kuwepo na uwazi katika utekelezaji wa mchakato mzima.

Makurutu elfu saba walitarajiwa kusajiliwa kutoka wilaya 47 kote nchini na kujiunga na vikosi vya polisi tawala na polisi wa kawaida.

Ili kuhakisha kuwepo kwa uwazi na usawa katika usajili huo, wasajili waliweka mikakati kadhaa ili kupunguza visa vya ufisadi au ukiukaji wa sheria katika usajili wa makuruti.







Malawi na Uingereza 'zatunishiana misuli'


Uingereza imetoa amri kwa balozi wa Malawi kuondoka nchini humo kufuatia kufukuzwa "kusiko sawa" kwa balozi wa Uingereza nchini Malawi.



Rais Mutharika


Balozi wa Uingereza Fergus Cochrane-Dyet alitakiwa kuondoka Malawi baada wa kukaririwa katika waraka uliovuja akisema rais havumilii kukosolewa.

Mjumbe mmoja wa UIngereza ameonya kuwepo kwa "madhara makubwa", kwa mujibu wa waraka wa siri ambao BBC imeuona.

Asilimia 40 ya bajeti ya serikali ya Malawi inatoka nchi za nje. Uingereza ndio mhisani mkubwa zaidi.

Mualiko wa serikali ya Malawi katika haruzi ya Kifalme umefutwa pia.

Kwa mujibu wa waraka wa kibalozi uliochapishwa katika gazeti moja wiki iliyopita, Bw Cochrane-Dyet alimuelezea rais wa Malawi Bingu wa Mutharika kuwa anazidi kuwa "dikteta na kutovumilia kukosolewa".

Alisema wanaharakati wa vyama vya kiraia wamekuwa waoga baada ya kupata simu za vitisho na kusema serikali ilikuwa inazuia uhuru wa vyombo vya habari na watu wa makabila madogo.

Mwaka jana, kutokana na shinikizo kutoka kwa nchi wahisani, aliwapa msamaha wapenzi wawili wa jinsia moja waliofungwa gerezani kutokana na uhusiano wao wa kimapenzi, jambao ambalo ni kosa nchini Malawi








Kanisa latakiwa kuwashitaki makisisi wake


Nchini Rwanda kanisa katoliki bado linalaumiwa kwa kushindwa kuwafungulia mashtaka makasisi wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 94.

kawadia kanisa katoliki linakuwa na mahakama zake zenye mamlaka ya kufuatilia na kuadhibu makasisi wanaofanya makosa mbali mbali.


rais Rais wa Rwanda
Lakini wakuu wa kanisa katoliki nchini Rwanda wanasema hakuna aliyefanya mauaji kwa niaba ya kanisa hilo. Na Makasisi binafsi waliohusika walitoweka kwa hivyo wasilaumiwe







Obama aonyesha cheti chake cha kuzaliwa


Ikulu ya White House huko Marekani imeonyesha cheti cha kuzaliwa cha Rais Barack Obama, kukabili uvumi wa muda mrefu kwamba kiongozi huyo hakuzaliwa Marekani.

Awali Bw Obama alikuwa ameonyesha tu cheti kinachothibitisha "alizaliwa akiwa hai" kikibainisha alizaliwa Hawaii.





Sehemu ya nakala ya cheti cha kuzaliwa Bw Obama.


Lakini wapinzani wake wamekuwa wakisisitiza kuwa Bw Obama alizaliwa Kenya, nchi alikozaliwa baba yake, na hivyo kumfanya asikidhi mojawapo ya vigezo vya kuchaguliwa kuwa rais.

Katika siku za karibuni Donald Trump anayedhaniwa kuwa na nia ya kugombea kupitia chama cha Republican alifufua uvumi huo. White House ikahisi kuna haja ya kulikabili swala hilo na kuumaliza uvumi.

Kuachana na upuuzi

Siku ya Jumatano, Bw Obama alielezea hatua hiyo isiyo ya kawaida inalenga kukomesha siasa zisizokuwa na maana, na kusema kwa miaka kadhaa amekuwa akitizama na kuchekeshwa na fitna za kuwa hakuzaliwa Marekani.

"Hatuna muda wa upuuzi wa aina hii," Bw Obama alisema. "Tuna mambo ya muhimu zaidi kufanya. Nina mambo ya maana zaidi kufanya. Tuna matatizo ya kutatua lakini tutayashughulikia, siyo swala hili."

Kutolewa kwa nakala hiyo ya cheti halisi cha Bw Obama, ambacho kilikuwa kimehifadhiwa kwenye chumba maalum chenye usalama huko Hawaii tangu kuzaliwa kwake Agosti 1961, kumetokea baada ya miaka mingi ya uzushi kutoka kwa watu wa Marekani wanaoegemea siasa za mrengo wa kulia







Dhulma nchini Libya kufanyiwa uchunguzi




Jopo hilo litachunguza dhulma zilizofanywa na majeshi ya serikali na waasi tangu Februari
Kundi la maafisa kutoka Umoja wa Mataifa limetumwa mjini Tripoli kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Libya.

Jopo hilo liliteuliwa na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa punde tu utawala wa Libya ulipoanza kushambulia waandamanaji wanaompinga kanali Muammar Gaddafi.

Serikali ya Libya imesema itashirikiana na jopo hilo la wachunguzi ambalo pia litachunguza madai ya dhulma zilizotekelezwa na waasi na majeshi ya Nato.

Kuna taarifa kuwa tangu maandamano ya kumpinga Kanali Gaddafi yaanze watu wametoweka, wengine wameteswa na hata kuuawa.

Kamishna wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay alisema kuwa huenda uhalifu dhidi ya binadamu unafanyika nchini Libya tangu mzozo huo uanze.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu elfu moja wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Meli zimekuwa zikiwasafirisha watu waliojeruhiwa hadi mjini Benghazi kupata huduma za matibabu.








Bunge kujadili ongezeko la bei ya chakula-Kenya




Raia wa Kenya wakiandamana kupinga bei ya Petroli
Nchini Kenya, Waziri mkuu Raila Odinga, leo anatarajiwa kufafanua bungeni hatua serikali inachukua kudhibiti hali.

Wiki iliopita shirika linalotetea haki za wanunuzi liliandaa maandamano katika sehemu kadhaa nchini, kulaani ongezeko hilo.

Chama cha wafanyikazi kimetisha kuongoza mgomo tarehe mosi mwezi Mei mwaka huu, ikiwa mishahara ya wafanyikazi haitaongezwa, suala linalozua wasi wasi serikalini na miongoni mwa wawekezaji.







Nigeria yachagua magavana




Upigaji kura Nigeria


Raia wa Nigeria wanapiga kura katika duru ya mwisho katika mchakato mrefu wa uchaguzi uliojaa vurugu.

Uchaguzi wa magavana 36 wenye ushawishi mkubwa umecheleweshwa katika majimbo mawili yaliyoathirika zaidi na ghasia.

Mabomu mengi zaidi yamelipuka kwenye mji wa Maiduguri kaskazini-mashariki mwa mji huo, ambapo takriban watu watatu waliuawa tangu siku ya Jumapili.

Shirika la kutetea haki za bindamu la Nigeria limesema zaidi ya watu 500 walikufa kufuatia ghasia ziliozibuka baada ya uchaguzi wa rais.

Ghasia ziliibuka upande wa kaskazini baada ya Bw Goodluck Jonathan, mkristo kutoka kusini, alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Aprili 16.

Makanisa yalichomwa moto na Waislamu walilengwa katika mashambulio ya kulipiza kisasi.

Wakristo wengi walisherehekea sikukuu ya Pasaka kwenye kambi za jeshi ambapo walijihifadhi kutokana na vurugu hizo.

Licha ya kuwepo ghasia, waangalizi wengi walisema uchaguzi umekuwa bora zaidi tangu kurejeshwa kwa uongozi wa kiraia mwaka 1999.

No comments:

Post a Comment