KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, April 25, 2011

Pasaka ya Kikristo
Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulibiwa kwake. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika Ukristo.

Jina la Pasaka


Jina la "Pasaka" limetokana na sherehe ya Pasaka ya Kiyahudi linaloitwa "פסח" (tamka: pasakh) kwa lugha ya Kiebrania. Kwa Kiswahili majina ya sherehe za Kikristo na Kiyahudi hazitofautiani. Asili yake ni ya kwamba kusulibiwa na kufufuka kwa Yesu Kristo kumetokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi mnamo mwaka 30 BK. Wakristo wa kwanza ambao wote walikuwa Wayahudi walisheherekea sikukuu ya kiyahudi pamoja na kumbukumbu kwa ufufuo wa Yesu. Baadaye sherehe na pia tarehe zikawa tofauti.

Tarehe ya PasakaTarehe ya Pasaka inafuata mwezi kwa hiyo sikukuu hiyo haina tarehe imara katika kalenda ya kawaida. Inapatikana katika Machi au Aprili. Mtaguso au Sinodi Kuu ya Nikea mwaka 325 BK iliamua ya kwamba Pasaka itasheherekewa Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya Machi 21 (tarehe ya sikusare machipuo ambayo ni siku ya usawa wa mchana na usiku hivyo mwanzo wa majira ya kuchipua katika kaskazini ya dunia). Kwa sababu mwezi mpevu baada ya Machi 21 inaweza kutokea kati ya Machi 22 na Aprili 19 tarehe ya Pasaka ambayo ni Jumapili inayofuata hutokea kati ya Machi 22 na Aprili 25.

Katika Ukristo kuna kalenda mbili zinazotumika hivyo pia tarehe mbili za Pasaka. Makanisa ya magharibi yaani Wakatoliki na Waprotestant hufuata Kalenda ya Gregori (ambayo imekuwa kalenda ya kawaida ya kimataifa), lakini Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda iliyotangulia yaani Kalenda ya Juliasi.
Makombora yabomoa makaazi ya Gaddafi


Mapigano makali yanaendelea mjini Misrata licha ya serikali kutangaza kusitisha mashambulio dhidi ya waasi


Ndege za kijeshi za shirika la Nato zimeangusha makombra kwenye mkaazi ya Kanali Muammar Gaddafi mjini Tripoli.

Walioshuhudia wanasema makombora hayo yamesababisha uharibifu mkubwa kwenye eneo Bab al Azizia.

Milipuko hiyo inasemekana kuwa mikubwa zaidi kusikika mjini Tripoli na ilisababisha vituo viwili vya kitaifa vya televesheni kukatiza matangazo yao kwa muda wa nusu saa.

Matangazo ya vituo hivyo Jamahiriya na Shababiya yalikatizwa muda mfupi baada ya saa sita usiku baada ya shambulio hilo la Nato mjini Tripoli.


Majeshi ya Nato yamekuwa yakishambulia majeshi na kambi za jeshi za Kanali Gaddafi baada ya kuidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Nia ikiwa kuwalinda raia wa Libya waliokuwa wakilengwa na majeshi.Awali, Kiongozi wa Upinzani, Mustafa Abdel Jalil amesema Kuwait imekubali kuwapa dola milioni 180 kama msaada, huku wakiendelea na mikakati ya kupambana na majeshi ya serikali ya kanali Gaddafi.

Bw Jalili ambaye pia ni Mkuu wa baraza la kitaifa la serikali ya mpito nchini Libya, amesema wanahitaji msaada huo wa kifedha kwa wakati huu.

Kwengineko mapigano makali zaidi yameendelea mjini Misrata licha ya serikali kutangaza kuwa inasitisha mapigano.

Lakini msemaji wa serikali Moussa Ibrahim amesema jeshi linajibu mashambulizi kutoka kwa waasi.

No comments:

Post a Comment