KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, April 29, 2011
'Mtume' Kupigwa Faini Kwa Kutabiri Tetemeko la Ardhi
Mwanaume mmoja wa nchini Taiwan ambaye alijitangaza kuwa yeye ni mtume amesababisha mtafaruku nchini humo baada ya kutabiri litatokea tetemeko kubwa la ardhi nchini humo mwezi mei na kusababisha watu waanze kuzikimbia nyumba zao.
Serikali ya Taiwan imetishia kumpiga faini mwanaume mmoja wa nchini humo anayejiita yeye ni mtume kwa kusababisha mtafaruku nchini humo.
Mamlaka za Taiwan zimesema kuwa Mtume huyo anayejulikana pia kwa jina la “Teacher Wang” aliandika kwenye blogu yake utabiri wa kutokea tetemeko kubwa la ardhi litakaloambatana na Tsunami.
Mtume huyo feki pia aliwataka watu wazikimbie nyumba zao kwani hazitaweza kuhimili tetemeko hilo la ardhi na kuwashauri waishi kwenye nyumba zilizotengenezwa kwa makontena ya mizigo.
Wataiwan wengi wamekuwa wakizikimbia nyumba zao na kuuhama mji na kwenda kuishi kwenye nyumba zilizotengenezwa kwa makontena kwenye miji ya ukanda wa kati wa Taiwan.
Jumla ya makontena 170 ya mizigo yameishageuzwa nyumba huku watu wengi zaidi wakitarajiwa kufuata utabiri huo wa Mtume Wang.
Serikali ya Taiwan imemtaka Wang aondoe utabiri wake kwenye blogu yake au la atapigwa faini ya dola milioni moja za Taiwan ambazo ni sawa na takribani Tsh. Milioni 50
Wanaotuhumiwa kutaka kumuua Chageni wapewa dhamana
HAKIMU Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Agelous Rumisha, jana amewaachia kwa dhamana, watu wanne wanaotuhumiwa kula njama za kutaka kumuua alikuwa mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni.
Washtakiwa katika kesi hiyo namba 113 ya mwaka 2011,ni Dismas Zacharia (47), Erasto Kazimiri (48), Queen Bogohe (37) na mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ya Mkoa wa Mwanza, Ellen Bogohe (54).
Akitoa maamuzi kuhusu hoja kama kesi inapaswa kusikilizwa ama katika Mahakama ya Mkoa au Mahakama Kuu, hakimu huyo alisema kulingana na sheria za jinai kesi hiyo inapaswa kusikilizwa Mahakama na Kuu.
Msimamo huo ulisababisha mjadala wa kisheria baina ya mawakili wa utetezi na wa serikali.
Katika maelezp yake, hakimu huyo alisema dhamana kwa watuhumiwa ni haki yao na kwamba hilo limo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkali kuhusu katiba ya nchi, wapo wanaosema kuwa katiba iliyopo haifai kwa sababu ina viraka vingi, lakini Ibara ya 13 Kifungu kidogo cha (b) fasihi ya 6 ya mwaka 1979 inatoa haki ya mtu ambaye hajathibitika kuwa na hatia kupewa dhamana," alieleza hakimu huyo.
Alisisita kuwa katika ibara hiyo mshtakiwa yeyote anayo haki ya kupewa dhamana isipokuwa pale Jamhuri itakapothibitisha vinginevyo.
"Huo ndiyo uzuri wa katiba hii kwa upande mwingine, hivyo natoa dhamana kwa watuhumiwa hawa lakini, kwa masharti yafuatayo," alisema.
Alitaja masharti hayo kuwa ni kila mshtakiwa kuwa na wadhamini kwa hati ya dhamana ya Sh3 milioni kila mmoja.
Alisema ingawa juzi kuliwasilishwa ombi la kutotolewa ka dhamana kwa watuhumiwa, lakini wakili wa serikali hakuwasilisha mahakamani, hati ya kupinga dhamana.
Ingawa dhamana sasa iko wazi kwa washtakiwa, lakini mshtakiwa wa kwanza Dismas Zacharia alishindwa kuachia baada ya mmoja wa wadhamini wake, kushindwa kutoa uthibitisho wa barua.
Watuhumiwa wengine walidhaminiwa na kuachiwa kwa dhamana.
Kesi hiyo itatajwa tena Mei 5 mwaka huu.
Wakati huo huo,kesi inayomkabili aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza, Leonard Bihondo na wenzake watatu, pia imeahirishwa hadi Mei 6 mwaka huu.
Awali akizungumzia kesi hiyo wakili wa serikali Paschal Marungu, alisema waliiomba mahakama isigoze mbele shauri hilo ili waweze kukamilisha upelelezi ambao alidai uko katika hatua za
Amuua Bibi Yake Kwasababu ya Dola 1
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani anashikiliwa na polisi baada ya kumuua bibi yake kwakuwa alimpa dola 1 badala ya dola 175 alizokuwa akizihitaji, aliificha maiti ya bibi yake kwenye kabati na kula uroda na kahaba kwa siku mbili kwenye kitanda cha bibi yake.
Larry Davis mwenye umri wa miaka 22 amekiri mbele ya polisi kuwa alimuua bibi yake mwenye umri wa miaka 76 Cora Davis.
Larry amewaambia polisi wa mjini Manhattan kuwa alimuomba bibi yake dola 175 lakini badala yake bibi yake huyo alimpa dola moja tu hali iliyomfanya akasirike na kuamua kumshushia kipigo cha nguvu bibi yake.
Bibi Cora alidondoka chini kwenye sakafu na kuvunjika shingo yake na baadae kupoteza maisha yake.
Ili kuficha mauaji aliyoyafanya, Larry aliificha maiti ya bibi yake kwenye kabati.
Kesi ya Larry ilichukua nafasi kubwa sana kwenye vyombo vya habari mwezi uliopita baada ya kugundulika kuwa Larry kwa kutumia pesa za bibi yake alikula uroda kwa siku mbili mfululizo na kahaba kwenye kitanda cha bibi yake huku maiti ya bibi yake akiwa ameificha kwenye kabati la nguo.
Larry bado anaendelea kushikiliwa na polisi ambapo kesi yake imepangwa kusikilizwa juni 1.
Larry amenyimwa dhamana na ataendelea kunyea debe jela mpaka hukumu ya kesi yake itakapotolewa
Mbunge ataka kuwalipia faini wafungwa 50
MBUNGE wa Morogoro Mjini, Azizi Abood, ameahidi kuwalipia faini wafungwa 50 wanaotumikia vifungo vya kati ya mwezi na mwaka mmoja, baada ya kushindwa kulipa faini.
Abood alitoa ahadi hiyo juzi baada ya kutembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Morogoro na kuzungumza na mahabusi na wafungwa wanaotumikia adhabu za vifungo vya muda tofauti, katika gereza hilo.
Katika mazungumzo hayo, Abood alielezeav kushangazwa kwake na hatua ya msichana aliyejitambulisha kuwa Nasra Ramadhan (13), kutumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja, baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh70,000, kwa kosa la kutoa lugha chafu.
Kufuatia maelezo ya Nasra, mbunge huyo aliomba orodheshewe idadi ya wafungwa waliohukumiwa kutumia adhabu za vifungo vya kati ya mwezi na mwaka mmoja, ambao walitakiwa kulipa faini, lakini na wakashindwa kuzilipa.
"Nimemwomba mkuu wa gereza aniorodheshe majina ya wafungwa 50 walioshindwa kulipa faini kwa makosa waliyokutwa nayo na hivyo kusababisha watumikie vifungo. Nataka kuwalipia, wameniomba na wameahadi kujirekebisha," alisema Abood.
Alisema wafungwa hao ni wale waliopaswa kulipa faini ya kati ya Sh10, 000 na Sh120,000 na kwamba lengo ni kuwafanya watoke jela na kuungana na familia zao katika katika ujenzi wa taifa.
Katika hatua nyingine, mbunge huyo ameahidi kutoa vifaa vya kupikia vyakula vya wafungwa wa gereza hilo.
Kwa mujibu wa Aboodi ahadi hiyo inatokana na kuharibika kwa baadhi ya vifaa zikiwemo sufuria zinazotumika katika kupikia vyakula.
Mbunge huyo pia alielezea kusikitizwa kwake kuhusu msongamano wa mahabusi na wafungwa katika gereza hilo na kwamba hali hiyo ni tishio kwa afya za watu hao.
Alisema kwa sasa gereza hilo lina wafungwa na mahabusi 565 wakati uwezo wake ni kuhifadhi watu 144 tu.
Alisema msongamano huo unachangiwa na ucheleweshaji wa kesi mahakamani
Rumande kwa mauaj
MKAZI wa Keko Dar es Salaam, Noel Mwapula (24), anayedaiwa kuwa mlinzi, amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akikabiliwa na mashiatka yapatayo matano likiwemo la mauaji ya watu wawili katika maeneo tofauti.
Amesomekwa mashitaka yake na mahakimu wanne tofauti na awali alisomewa mashitaka Mbele ya Hakimu Karim Mushi, na Wakili wa Serikali , Alice Mtulo na kudaiwa kuwa, Agosti 21 mwaka jana, majira ya saa 3 usiku, katika eneo la Mchikichini, Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua Omary Juma kwa makusudi
Pia imedaiwa kumuua Yassini Ramadhan Februari 23 mwaka huu, majira ya saa 2 asubuhi, katika eneo la Sharrif Shamba,jijini Dar es Salaam.
Pia Mbele Hakimu Janeth Kaluyenda imedaiwa kuwa, Machi 13 mwaka huu saa 12 jioni, katika eneo la Mchikichini, mshitakiwa alipanga njama ya kuiba kiasi cha shilingi 300,000na kabla ya alitumia vitisho ili apewe fedha hizo.
Ilidai kuwa kabla ya kuiba fedha hizo, mshitakiwa ambaye alirudishwa rumande alitumia kisu kumtishia Bena Kimaro ili ampe fedha hizo.
Kutokana dna sheria za Jamuhuri waMuungano wa Tanzania mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kuendesha kesi za mauaji na mshitakiwa alirudishwa rumande hadi Mei12
Wahabeshi,Wasomali 56 wafungwa jela
MAHAKAMA ya Wilaya ya Handeni, imewahukumu kifungo cha miaka miwili jela, wahamiaji haramu 56 kutoka za Ethiopia na Somalia, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia na kuishi nchini isivyo halali.
Mapema, Mwanasheria wa Idara ya Uhamiaji wilayani Handeni, Charles Kasambula, alisema watu hao walikamatwa Aprili 13 mwaka huu katika shamba la katani la Kwaraguru, lililoko katika Kata ya Kwedizinga.
Alisema hatuan hiyo ilikuja baada ya taarifa zilizotolewa na raia wema kuhusu kuwapo kwa kundi la watu, lililokuwa limejificha katika shamba hilo.
"Baada ya kupata taarifa hizo, tulikwenda katika eneo hilo na kukuta kundi la Wahabeshi na Wasomali wakiwa wamejificha. Walikuwa wanasubiri usiku uingie ili waendelee na safari yao," alisema Kasambula.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, wahamiaji haramu sita miongoni mwa waliokamatwa ni wanawake na 50 wengine ni wanaume. Alisema wapowahoji, walidai kuwa walikuwa walikuwa wanatoka Kenya na kwenda Afrika Kusini.
"Wahamiaji hao haramu walidai kuwa wamekimbia kutoka nchini mwo ili kusalimisha maisha yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe," alisema ofisa huyo. Kufuatia kitendo cha wahamiaji hao kukiri hilo la kuingia na kuishi nchini isivyo halali, hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Jonathan Mgongolo, alisema kuwa ameridhika na maelezo ya pande zote mbili.
"Hivyo kutokana na kifungu cha sheria za uhamiaji namba 31 (1)(i) mahakama inawahukumu kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh20,000 kwa kila mmoja kwa kosa la kuvunja sheria hiyo," alisema.
Hata hivyo, wahamiaji hao walishindwa kulipa faini, jambo lililosababishwa kupelekwa jela kutumikia adhabu ya kifungo. Wimbi la wahamiaji haramu kuingia wilayani Handeni linazidi kuwa kubwa kwa kadri siku zinavyodi kwenda mbele.
Machi mwaka huu,wahamiaji haramu 11 kutoka Somalia, waliongia Handeni na baadaye, walikamatwa
Babu amaliza mazishi ya mwanae arudi Samunge
MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, amerejea kijijini Samunge jana baada ya kwenda safari ya kwenda kumzika mtoto wake Jackson Masapile [43] huko mkoani Manyara.
Mchungaji MWasapile aliondoka kijijini Samunge Jumatatu ya wiki hii, majira ya saa 12 jioni na gari la Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro akielekea Wilayani Babati mkoani Manyara kwa ajili ya mazishi ya mwanae huyo na aliondoka kijijini Samunge na maofisa usalama kwa ajili ya ulinzi kuelekea huko.
Hivyo leo anatarajiwa kuanza kutoa dawa baada kurudi safari yake hiyo ya kumalizia mazishi ya mwanae.
Kijijini hapo wagonjwa waliweza kumsubiria mchungajihuyo kwa takribani siku atatu wakingojea arudikutoka Manyaaraili waweze kupata kikombe cha tiba
Jamhuri yagoma kujibu rufaa
JAMHURI imegoma kujibu hoja za rufaa za muomba rufaa, Danford Anthorny katika kesi ya maombi ya rufaa namba 94/2010 kwa kile ilichoelezwa kuwa mahakama iliyosikiliza kesi ya msingi haikuwa na uwezo wa kisheria.
Mrufani huyo alitiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Kilosa na kuhukumiwa adhabu ya kifungo mwaka 2009 baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za serikali.
Hata hivyo hakukubaliana na hukumu hiyo, hivyo akakata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akitoa sababu nane za kupinga hukumu na adhabu hiyo.
Lakini wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, mwishoni mwa wiki serikali ambayo ni mjibu rufaa hiyo ilikataa kujibu sababu hizo za rufani ikidai kuwa mahakama iliyosikiliza kesi ya msingi haikuwa halali.
Wakili wa serikali aliyejitambulisha kwa jina moja la Katuga alidai kuwa kwa kuwa haina uwezo wa kisheria kusikiliza kesi ya namna hiyo na kwamba kwa hali hiyo shauri hilo halikuwa halali kisheria.
“Mheshimiwa Jaji, mrufani alishitakiwa kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali kinyume cha kifungu cha 70(1) (2) cha Sheria ya Hifadhi ya Wanyama sura ya 283 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambalo limo katika makosa ya uhujumu uchumi,” alisema wakili Katuga.
Alisema mahakama za chini ya Mahakama Kuu, hazina uwezo wa kisheria wa kusikiliza shauri la uhujumu uchumi isipokuwa tu kama zimepata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kwa mujibu wa kifungu cha 12(3).
“Lakini mahakama ya Wilaya ya Kilosa ilisikiliza kesi hii bila kuwa na kibali hicho.Kwa hiyo ilisikiliza kesi ambayo haikuwa na mamlaka nayo, hivyo shauri halikuwa halali kisheria. Kwa sababu hizo Jamhuri haina sababu ya kujibu hoja za mrufani kwa sababu si halali mbele ya sheria,” alidai Wakili Katuga.
Baada ya kusikiliza hoja za upande wa mjibu rufaa (Jamhuri) Jaji Fatuma Masengi alimuuliza mrufani iwapo alikuwa na jambo lolote la nyongeza, lakini mrufani huyo akajibu kuwa hana hivyo Jaji Masengi aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 4 kwa ajili ya uamuzi.
Akitoa maoni yake juu ya msimamo huo wa Jamhuri nje ya mahakama, Wakili wa kujitegemea Makaki Masatu baada ya Wakili wa serikali kubainisha kasoro hizo za kisheria zilizofanywa na mahakama ya chini, alisema jaji alipaswa kumwachilia palepale muomba rufaa.
“Wakili wa serikali anapokwenda kwenye kesi haendi kutetea tu upande wa serikali hata kama kuna makosa ya kisheria bali ni lazima asimame katika sheria;
Hivyo baada ya wakili wa serikali kubainisha kasoro hizo mahakama ingeweza kumwachilia mpaka pale serikali kama ingetaka ingeweza kujipanga tena na kumshtaki upya ”, alisema. Wakili Masatu.
Matokeo kidato cha sita shule za serikali zang’ara
MATOKEO ya Kidato cha sita yaliyotangazwa yameonyesha shule za serikali kushika nafasi za juu kufaulisha wanafunzi huku wavulana waking’ara katika matokeo hayo kwa kushika 10 bora .
Matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu yalitangazwa jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako.
Ndalichako amesema, unaonesha kuwa daraja la kwanza waliofaulu ni asilimia 7.25, daraja la pili ni asilimia 20.23 , daraja la tatu 51 , daraja la nne 13.51 na waliopata sifuri ni asilimia 7.97 ya wanafunzi wote.
Amesema shule 10 bora zilizofaulisha wanafunzi ni za serikali zikifuatiwa na za seminari.
Pia Somo lililoongoza kwa kufaulisha wanafunzi wengi ni Uchumi ambalo limeweza kufaulisha asilimia 93 ya watahiniwa na kufuatiwa na Biashara klimefaulisha asilimia 88.7, Advanced Mathematics limefaulisha aslimia 81.5, Kemia limefaulisha asilimia 80.3, Fizikia 67.03, Basic Applied Mathematics limefaulisha asilimia 50.69 na Jiografia limefaulisha asilimia 9.65.
Baraza limefuta mitihani ya watahiniwa 12 kutokana na udanganyifu kati yao watano ni wa shule na saba wa kujitegemea ambapo pia watahiniwa 218 matokeo yao yamesitishwa hadi watakapolipa ada ya mitihani
Viongozi wa ushirika kortini wa uhujumu uchumi
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani Kilimanjaro, imemburuta
mahakamani, Diwani wa Machame, wilayani Hai Rajabu Nkya (CCM) na watu wengine wawili kwa tuhuma za
uhujumu uchumi.
Desemba 6 mwaka jana, Mwananchi lilifichua tuhuma za kuwapo kwa vitendo vya ufisadi wa Sh52 milioni, katika Chama cha Msingi cha Ushirika cha Nkuu-Machame, ukimhusisha Nkya ambaye ni Mwenyekiti wa
chama hicho.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alikanusha vikali tuhuma hizo na kwamba ni chokochoko zinazochochewa na baadhi ya waliokuwa viongozi wa chama hicho walioondolewa madarakani.
Lakini jana Takukuru ilimfikisha Nkya mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Hai,Denis Mpelembwa na kumsomea mashtaka mawili likiwamo la uhujumu uchumi na kushindwa kutimiza masharti ya
dhamana.
Washtakiwa wengine katika waliosomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Maghela Ndimbo, ni Katibu wa chama hicho, Esther Shoo na mfanyabiashara Awadhi Lema.
Katika shtaka la kwanza linalowahusu Nkya na Shoo, mwendesha mashtaka alidai kuwa kati ya Machi na Oktoba mwakan 2007, washtakiwa walikisababishia chama hicho hasara ya Sh38 milioni, kwa kununua trekta kuukuu (mtumba).Ilidaiwa kuwa trekta hilo lilinunuliwa kutoka kwa mshtakiwa Lema.
Ilidaiwa kuwa kitendo kilichofanywa na washtakiwa hao ni matumizi mabaya ya ofisi ya chama hicho, kosa ambalo ni kinyume cha kifungu namba 31 cha sheria namba 11 ya kuzuia na kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho hicho, washtakiwa wote watatu kwa makusudi wanadaiwa kukisababishia chama hicho hasara ya Sh21,176,725 kosa linaloangukia kwenye uhujumu uchumi.
Washtakiwa Nkya na Lema walikanusha mashtaka yanayowakabili lakini mshtakiwa Shoo, akakiri kutenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi.
Aprili 28 upande wa mashtaka utamsomea maelezo ya kosa.
Kwa kuwa kosa linaloangukia chini ya sheria ya uhujumu uchumi linamtaka mshtakiwa kuweka mahakamani fedha taslimu ambayo ni nusu ya kiasi alichosababisha hasara au hati za mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.
Kutokana na sharti hilo, ni mshtakiwa Nkya aliwasilisha hati ya nyumba ambayo ilikataliwa na mahakama kwa kuwa ilikuwa haijaambatanishwa na ripoti ya mthamini na washitakiwa wengine waliobaki kushindwa
kutimiza sharti hilo.
Wanafunzi 1000 UDOM wafukuzwa
KUFUATIA MGOMO unaoendelea kati ya wanafunzi na uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma imepelekea wanafunzi wapatao 1000 kusimamishwa masomo na kutakiwa kuondoka chuoni hapo.
Wanafunzi hao ni wale wa Sayansi ya Habari (Informatics) kutoka chuoni hapo wamesimamsishwa kwa muda usiojulikana kufuatia mgogoro yao na Menejimenti toka wiki iliyopita.
Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho anayehusika na masuala ya Taaluma, Utafiti na Ushauri, Profesa Ludovick Kinabo, amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na hali ya usalama kutokuwa shwari chuoni hapo.
“Chuo kinafungwa kwa muda usiojulikana, Kamati ya Baraza la Chuo itakaa Jumatatu ndipo itaamriwa hatima ya wanafunzi hao na hatua zitakazochukuliwa baada ya kuondoka chuoni.” Alisema
Amesema vurugu hizo zimesababisha msongo wa mawazo kwa wanafunzi wengine wasiohusika chuoni hapo
Tangu wiki iliyopita chuoni hapo hali ilikuwa tete kutokana na badhi ya wanafunzi kuchochea migomona maandamano yaliyopelekea kusababisha usumbufu chuoni hapo
KUFUATIA MGOMO unaoendelea kati ya wanafunzi na uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma imepelekea wanafunzi wapatao 1000 kusimamishwa masomo na kutakiwa kuondoka chuoni hapo.
Wanafunzi hao ni wale wa Sayansi ya Habari (Informatics) kutoka chuoni hapo wamesimamsishwa kwa muda usiojulikana kufuatia mgogoro yao na Menejimenti toka wiki iliyopita.
Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho anayehusika na masuala ya Taaluma, Utafiti na Ushauri, Profesa Ludovick Kinabo, amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na hali ya usalama kutokuwa shwari chuoni hapo.
“Chuo kinafungwa kwa muda usiojulikana, Kamati ya Baraza la Chuo itakaa Jumatatu ndipo itaamriwa hatima ya wanafunzi hao na hatua zitakazochukuliwa baada ya kuondoka chuoni.” Alisema
Amesema vurugu hizo zimesababisha msongo wa mawazo kwa wanafunzi wengine wasiohusika chuoni hapo
Tangu wiki iliyopita chuoni hapo hali ilikuwa tete kutokana na badhi ya wanafunzi kuchochea migomona maandamano yaliyopelekea kusababisha usumbufu chuoni hapo
Wakimbizi 700,000 warudishwa Rwanda, DRC
ZAIDI ya wakimbizi 700,000 kutoka Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) wamerudishwa kwao kuanzia mwaka 2000, huku wengine takriban 100,000 wakitafutiwa makazi ya kudumu nchini.
Wakimbizi hao ni wale ambao walikuwa wamepewa hifadhi nchini kwenye kambi za Nyarugusi na Ntaboba, Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Takwimu hizo ni kuanzia mwaka 2000 hadi sasa.
Akizungumza kwenye warsha ya waandishi wa habari, Ofisa Msaidizi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) nchini, William Ngeze, alisema wakimbizi hao waliorudishwa wengi wao walikuwa mikoa ya Tabora, Kigoma na Tanga.
“Wakimbizi wengi waliorudishwa ni waimbaji wanakwaya wa Bulyanhulu na wengine kutoka kwenye kambi za Nyarugusi na Ntaboba,” alisema Ngeze.
Ngeze alisema idadi ya wakimbizi hao waliorudishwa inaonyesha jitihada kubwa zilizofanywa na UNHCR na kwamba, waliosalia ambao ni chini ya 100,000 wanatafutiwa eneo la makazi ya kudumu.
Alisema suala la kuwahamisha wakimbizi hao kutoka kwenye kambi hizo na kuwapeleka nyingine, limekuwa gumu kutokana na kukosekana kwa fedha na nchi ambayo iko tayari kuwapokea.
“Ili mtu aweze kuitwa mkimbizi lazima awe na sababu ya msingi iliyomuondoa nchini kwake, ambayo inaweza ikampelekea kukosekana kwa usalama wa maisha yake,” alisema.
Ofisa Mipango Mwandamizi wa UNHCR, Mbogozi Andrew, alisema shirika hilo linatumia dola 22 bilioni za Marekani kila mwaka kuhudumia wakimbizi hao nchini.
Pia, Andrew alisema miongoni mwa huduma wanazozitoa kwa wakimbizi, ni zile za jamii ikiwamo elimu, matibabu, chakula, makazi na malazi.
Alisema wakimbizi wanapokuwa nchini wanatakiwa kufuata sheria kama wananchi wengine na kwamba, iwapo atavunja sheria anahukumiwa kama raia mwingine.
Anywa sumu baada ya dada yake kumtamkia kuwa ana mimba ya mumewe
MWANAMKE anayetambulika kwa jina moja la Fatuma amelazimika kunywa sumu kwa aibu baada ya dada yake kumtamkia kuwa anaujauzito aliopewa na mume wake.
Mwanamke huyo ni ili habari iliyochapishwa wiki mbili zilizopita katika mtandao huu aliyeweza kumfumania mume wake na dada yake chumbani kwake.
Nifahamishe ilipata habari y a kunywa sumu kwa mwanamke huyo jana majira ya usiku na asubuhi hii ilifika nyumbani kwa mwanamke huyo na kukuta tayari alishakimbizwa zahanati kwa msaada zaidi
Imedaiwa kuwa mwanamke huyo juzi katika sikukuu ya Muungano dada yake ambaye alimfumania na mume wake wakati alipokwenda safari ya kumsalimia mama yake alimfata mdogo wake na kumuambia kuwa amsaidie kutafuta daktari ili aweze kutoa ujauzito aliokuwa nao
Imedaiwa kuwa mdogo wake huyo alijaribu kumuuliza ni kwanini autoa ndipo dada huyo alipoanza kulia na kumuomba radhi kwa mara nyingine na kumueleza alipewa na shemeji yake ambaye ni mume wa mwanamke huyo
Ndipo mwanamke huyo alianza kilio kwa mara nyingine na kwenda kwa shangazi yake aishio karibu naye kumueleza tukio hilo na kudaiwa majira ya saa moja usiku Aprili 26 alitafuta sumu ya kuulia panya bila wana familia kujua na alikoroga na kunywa
Hata hivyo imedaiwa kuwa dakika chache baadae alikutwa kitandani akiwa hoi na hatua za awali za kutoa povu zilianza kujitokeza na kudaiwa kukimbizwa hospitali
Hadi leo asubuhi mwanamke huyo anaendelea na matibabu katika zahanati moja ya karibu na maeneno hayo
Awali mwanamke huyo alimfumani mume wake na dada yake na aliweza kuacha nyumba hiyo na kwenda kwa shangazi yake lakini baadae maongezi ya kifamilia yalifanyika na kumalizika na kusameheana kwa pande zote mbili ana alirudi nyumban I kwake bila wanafamilia kutotambua kwamba alipewa ujauzito na yeye mwenye alikuwa hafahamu
Ndipo juzi jambo hilo lilijitokeza baada ya dada yake kujigundua kuwa mjamzito na kumfata mdogo wake wasaidiane kutoa ujauzito huo bila wanandugu kujua
Nifahamishe itaendelea kuwajuza kitakachoendelea kuhusiana na mtafaruku huu wa kifamilia
Ban Ki Moon ampongeza JK, wananchi
WAKATI Watanzania leo wakiadhimisha miaka 47 ya Muungano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemtumia salamu za pongezi, Rais Jakaya Kikwete, serikali na wananchi wote.
Katika salamu zake ambazo nakala yake ilitumwa katika Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, alisema, kuliko ilivyokuwa wakati mwingine wowote, dunia sasa inakabiliwa na changamoto nyingi.
Alisema changamoto hizo zilizovaa sura na uzito tofauti, zinavuka mipaka kutoka katika taifa moja hadi lingine na kwamba ufumbuzi wake unahitaji utulivu, umakini, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa.
Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, alimweleza Rais Kikwete kuwa yeye binafsi, amedhamiria kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa, unakwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea sasa duniani.
"Nakuhakikisha (Kikwete) kwamba Umoja wa Mataifa, unasimamia na kutoa matarajio yenye kuridhisha na halisi katika kazi zake tatu kuu za msingi ambazo ni maendeleo, amani na usalama na haki za binadamu," alisema Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.
Pia alielezea kufarijika kwake na kupata moyo kuhusu namna uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unavyojituma.
Alisema anaihesabu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mshirika mkubwa katika kuifanya dunia, kuwa endelevu na salama kwa watu wote
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment