KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, April 19, 2011

Maelfu wakimbia machafuko Nigeria

Maelfu ya watu wamekimbia nyumba zao kaskazini mwa Nigeria baada ya ghasia kuzuka kufuatia kuchaguliwa kwa Rais Goodluck Jonathan


Ghasia katika eneo la Kaduna


Shirika la Msalaba Mwekundu limeiambia BBC kuwa watu wapatao 16,000 wamekimbia makazi yao katika majimbo sita upande wa kaskazini, ambapo pia baadhi ya raia walilala katika kituo cha polisi kwa ajili ya usalama wao.

Bw Jonathan ametoa wito wa kumalizika kwa ghasia, na kutangaza hali ya kutotembea usiku



Ghasia katika eneo la Kano


Mpinzani wake mkuu, Jenerali Muhammadu Buhari, ambaye anatokea upande wa kaskazini, ameiambia BBC kuwa ghasia hizo zinasikitisha, hazina msingi na ni uhalifu.

Baadhi ya wanaofanya ghasia wanadai ulifanyika wizi wa kura, lakini kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi amesema anataka kutojihusisha yeye na chama chake katika ghasia.

"Katika saa 24 zilizopita, kumekuwa na ghasia nchini: hii imehusisha kuchoma moto kanisa na inasikitisha, na pia haikuwa na ulazima," amesema katika taarifa yake.

"Lazima nisisitize kuwa kinachotokea sio suala la kikabila au la kidini."

Machafuko Kano, Kaskazini mwa Nigeria


Bw Jonathan, anayetokea upande wa kusini, alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Jumamosi, huku tume ya uchaguzi ikisema alipata takriban 57% ya kura milioni 22.5 zilizopigwa, na Jenerali Buhari akipata kura milioni 12.2.

Waangalizi wa kimataifa wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki











Wajane wa India wapigwa mpaka kufa






Ramani ya India
Wajane wawili wa kike wamepigwa mpaka kufa na mtu mmoja katika jimbo la Haryana lililopo kaskazini mwa India.

Polisi ilimkamata mtu mmoja mwenye umri wa miaka 23, mpwa wa mmoja wa wanawake hao. Alikuwa katika kifungo cha nje baada ya kutumikia kifungo cha gerezani kwa makosa ya ubakaji.

Walioshuhudia waliwaambia polisi alimwuua shangazi yake na mwanamke mwengine huku wanakijiji wote wakishuhudia, baada ya kuwashutumu kuwa katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.

Haryana ni eneo lenye msimamo mkali sana na lenye mfumo dume.

Waandishi walisema kile kinachoitwa "kujiua kwa heshima" ni jambo la kawaida eneo hilo.

Walisema kumekuwa na matukio kadhaa kwenye eneo hilo la kijiji la Haryana ambapo wanawake na wanaume wanaokana mila na heshima za kifamilia hutengwa, huuliwa au hata kuuliwa kiholela hadharani.

Mauaji ya hivi karibuni yalifanyika siku ya Jumapili katika kijiji cha Ranila.

Iliripotiwa kuwa anayeshutumiwa alianza kumpiga mwanamke mojawapo, aliyetambulika kwa jina la Suman mwenye umri wa miaka 35, na rungu la mbao baada ya kumshutumu kuwa na "uhusiano usio wa kawaida" na shangazi yake Shakuntala.

Dakika chache baadae, alimburuta shangazi yake kwenye mitaa ya kijiji hicho na kumpiga mpaka kufa mbele ya wanakijiji wote waliokuwa wakiogopa kuingilia, waandishi walisema.

Wawili hao walitoka damu mpaka kufa huku wanakijiji wakiangalia.

Afisa wa polisi alisema, "Aliwatishia wanavijiji wengine kutowasaidia wajane hao na hata kuita madaktari."

Alisema aliwaua wanawake hao kulinda "heshima ya familia."









Wafanyakazi wa kutoa misaada ruhsa Libya



Mtoto aliyejeruhiwa Misrata
Kulingana na Umoja wa Mataifa, serikali ya Libya imeahidi kutoa ruhusa kwa wafanyakazi wa kutoa misaada katika maeneo inayodhibiti.

Maafisa wa umoja huo wamesema makubaliano hayo yanawaruhusu wafanyakazi wanaotoa huduma za kibinadamu kuwepo kwenye mji mkuu, Tripoli, na kuingia na kutoka wakati wowote nchini humo.

Wakati huo huo, takriban watu 1,000 walioondolewa kutoka Misrata wamewasili katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Benghazi.

Majeshi yanayomwuunga mkono Gaddafi yamekuwa yakishambulia Misrata kwa siku kadhaa sasa na mamia ya watu wanadhaniwa kufariki dunia.

Walioondolewa wamesafirishwa kwa kutumia meli iliyoandaliwa na shirika la kimataifa la kutoa misaada la IOM, linalosema wengine kwa maelfu bado wanasubiri kuokolewa.











Aliyeichoma Moto Quran Atupwa Jela Siku 70



Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ambaye aliiba msahafu toka maktaba na kisha kuuchoma moto msahafu huo mbele ya mamia ya watu amehukumiwa kwenda jela siku 70.
Andrew Ryan mwenye umri wa miaka 32 aliiba msahafu toka kwenye maktaba ya mji wa Cumbria na kisha kwenda katikati ya mji na kuuchoma moto msahafu huo kwenye eneo ambalo kulikuwa na maduka mengi.

Andrew alilifanya tukio hilo mwezi januari mwaka huu akidai analipiza kisasi kwa vitendo wanavyofanyiwa wanajeshi wa Uingereza nchini Afghanistan.

Andrew ambaye ana historia ya kufikishwa mahakamani mara sita kwa makosa tofauti tofauti likiwemo kosa la kutoa kauli za ubaguzi wa rangi kwenye mechi ya soka, alihukumiwa kwenda jela siku 70.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo, jaji Gerald Chalk alimwabia Andrew: "Wewe ni mtu mwenye historia ya kufanya matukio ya uhalifu na kuvunja sheria".

"Uliamua kufanya kosa hili kubwa na kuwavunjia heshima waislamu", alisema jaji Chalk.

Andrew aliambiwa kuwa anaruhusiwa kuonyesha hisia zake hadharani lakini si kwa kufanya kitendo ambacho kitasababisha ukosefu wa amani kwenye jamii.

Andrew alikiri kosa la kufanya kitendo cha kueneza chuki za dini na pia alikiri kufanya wizi kwa kuiba msahafu toka kwenye maktaba ya manispaa










Kenya waandamana kupinga kupanda kwa bei




Wanachama wa mashirika ya kijamii pamoja na raia waliandamana katika miji mbali mbali nchini Kenya,kupinga kupanda kwa gharama za maisha


mmoja wa waandamanaji


Hali hii imejiri baada ya bei ya mafuta kupanda wiki iliopita jambo ambalo limeathiri bei za bidhaa zengine muhimu.

Mjini Nairobi waandamanaji waliandamana kutoka uwanja maarufu wa Uhuru wakibeba mabango yenye ujumbe tofauti kusisitiza kilio chao.

''Tumeamua leo ni leo,njaa inauma hapa huku wakubwa wakiendelea kunona, sisi tumejitokeza kwa wakenya wote lazima watimize haki yetu, wakenya wanaumwa njaa hadi wanafariki dunia", alisema mmoja wa waandamaji.

Salama

Katika maeneo mengi maandamano yalikuwa ya amani huku polisi wakiongoza wale waliokuwa wakiandamana.

Mji wa Nairobi ambao kwa kawaida una matatizo ya foleni ndefu za magari,foleni ilikuwa ndefu zaidi wakati waandamanaji walipokuwa wanapita barabarani na mara nyingi polisi walisaidia kuweka barabara kuwa salama.

Ugumu wa maisha

Kwa zaidi ya saa moja walipita katika barabara za Nairobi hadi katika ofisi za waziri wa fedha,waziri mkuu,ofisi ya rais na kufikisha ujumbe wao bunge.

Mmoja wa wabunge aliahidi kuwasilisha malalamiko bungeni,''Nawahakikishia kwamba tuko pamoja naomba nipokee hayo malalamiko yenu na niwasilishe bungeni kwa niaba yenu'', Mbunge Ababu Namwamba aliahidi.

Raia hao pia walitaka waziri wa fedha Uhuru Kenyatta na mwenzake wa kawi Kiraitu Murungi kujiuzulu kwa kile walichokiita kushindwa kuwalinda wakenya na ugumu wa maisha







Museveni aonya mataifa ya Magharibi


Rais Museveni wa Uganda amelaani hatua ya nchi za magharibi kuingilia kati masuala ya Afrika na kuonya kuwa jambo hilo watalivalia njuga.
Rais Yoweri Museveni



Bw Museveni pia amekanusha madai kuwa Muungano wa Afrika umeshindwa kushughulikia migogoro ya Afrika hususan suala la Libya.

Bw Museveni ameyasema hayo mwishoni mwa juma alipokutana na waandishi habari nyumbani kwake Rwakitura, magharibi mwa Uganda, ambapo amezungumzia masuala mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Mashambulizi

Hii ni mara ya kwanza kwa rais Museveni kukutana na waandishi wa habari wa Uganda na wa kimataifa, tangu achaguliwe tena kuliongoza. Amezungumzia masuala mbalimbali.

Alizungumzia suala la Libya - ambapo yeye ni rafiki wa Kanali Muammar Gaddafi - inayokabiliwa na upuinzani sio tu kutoka kwa raia wa mashariki mwa nchi lakini pia na mashambulizi ya anga ya Nato.

Bw Myuseveni alisema mashambulizi hayo ni hatua ya mataifa ya Ulaya kujiingiza katika masuala ya Afrika.

Ukoloni mamboleo

Alisema kuwa hii ni hatua mpya wakati huu japo walikuwa wanafanya hivyo wakati wa nyuma.

Ameongeza kuwa Afrika itaweza kushinda watu wanaotaka kuleta alichosema "ukoloni mamboleo kama ilivyofanya kupambana na ukoloni siku za nyuma".

Bw Museveni amesema mataifa ya magharibi yalifanya vibaya kutohusisha Muungano wa Afrika.

Ameonya

Mwandishi mmoja alipendekeza kuwa huenda uingiliaji huo wa mataifa ya magharibi ulichochewa na kujivuta kwa muungano wa Afrika.

Museveni alipinga hoja hiyo, akisema muungano wa Afrika umefanya mengi, kama vile kuipatia uhuru Afrika kusini, kumfukuza Idi Amin kutoka Uganda na pia suala la Libya na Ivory Coast.

Alisema muungano huo ungeweza kutatua suala la Libya.

Aidha ameonya kuwa ikiwa nchi za Ulaya hazitakoma kuingilia kati masula ya Afrika wajitayarishe kwa kile alichoita "Vietnam nyingine".










Mkurugenzi Sunrise Hotel kizimbani kwa mauaji



MKURUGENZI wa Hoteli ya Kitalii ya Sunrise Beach ya jijini Dar es Salaam,

Bw. Salim Nathoo (53), amepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa kosa la mauaji.


Nathoo ambaye ni mkazi wa Mikocheni ‘A’ alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Khasim Mkwawa wa mahakama hiyo.
Mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo alitambulika kwa jina la John Mwangiombo (32).

Upande wa Mashitaka uliongozwa na Mwendesha Mashtaka, Inspekta wa Polisi Dastan Kombe na kudai kuwa, washitakiwa hao walitenda kosa hilo Aprili 10 mwaka huu majira ya saa 6.30 usiku eneo la Mjimwema Kigamboni.

Washitakiwa hao walishirikiana kwa pamoja kumpiga na kumchoma moto kijana Lila Hussen (34) na kumsababishia kifo kwa kumuhisi mwizi mara alipoingia hotelini hapo

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kusikiliza na kesi hiyo.
Kesi iliahirishwa hadi Mei 2, mwaka huu kwa kutajwa tena na washitakwia watakwenda kujibu shtaka hilo mahakama kuu.

Awali imedaiwa kuwa marehemu Lila alichomwa moto na washtakiwa hao baada ya kuingia hotelini hapo kwa ajili ya kuwatafuta wageni wake raia wa kigeni aliowasindikiza hotelini hapo jana yake na mara alipoingia hotelini hapo kwa kuwa hakuwa na muonekano mzuri wa hadhi ya kua hotelini hapo mmiliki huyo alitoa agizo la kukamatwa kijana huyo kwa kudai ni mwizi na baadae walimmwagia mafuta na kumvisha tairi na kumchoma moto na alianza kuungua huku wageni wake wakiwa hawajui kinachoendelea.

Taarifa ziliwafikia jamaa zake anaofanya nao kazi maeneo ya feri na walifika hapo na kumuokoa kijana huyo na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Na muda machache baadae mkurugenzi huyo alipogundua kuwa si mwizi na kuona alifanya makosa alianza hatua za kukimbia nchini na aliwezwa kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere na kufikishwa kituo cha polisi









Mwalimu Achinja Watoto na Mama Yao Dar



UPEPO wa mauaji unazidi kushika kasi siku hadi siku na kutishia amani, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mondo, Wilayani Kondoa, Bw.Kassim Bindo (25), anatuhumiwa kuua watoto wawili na kujeruhi mama wa watoto hao kwa kuwachoma kisu tumboni.
Tukio hilo la kikatili lilitokea jijini Dar es Salaam eneo la Kipunguni ‘B’ majira ya saa 5 usiku wa kuamkia jana, baada ya mwalimu huyo kuwachoma kisu tumboni watoto hao na kisha kumchoma kifuani mama yao.

Watoto waliokufa katika tukio hilo walitambulika kwa majina ya Mwanamkasi Shabani (4), Asha Shabani na mama yao Kuruthum Shabani [28].

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema mtuhumiwa hajapatikana kwa kuwa alitoroka baada ya dakika chache baadae mara baada ya kufanya mauaji hayo.

Kamanda Shilogile alisema kuwa baba mzazi wa mtuhumiwa aliithibitishia polisi kuwa mwanae huyo miaka ya nyuma aliwahi kulazwa hospitali ya Muhimbili kwa muda unaozidi wiki tatu kutokana na matatizo ya afya ya akili.

Mtuhumiwa huyo alifanya mauaji hayo Kipunguni nyumbani kwa baba yake mzazi majira ya usiku. Watoto waliouliwa walikuwa ni wa kaka yake na mtuhumiwa.

Mtuhumiwa huyo inadaiwa ni mwalimu huko mkoani Dodoma.

Babu wa watoto hao amedai kuwa mazishi ya watoto hao yanatarajiwa kufanyika leo.










Dr Besigye wa Uganda akamatwa tena





Dr Kiiza Besigye
Kiongozi wa upinzani wa Uganda Kiiza Besigye amekamatwa karibu na nyumba yake baada ya kudhamiria kujiunga na maandamano mapya kupinga kupanda kwa gharama za maisha.

Wiki iliyopita pia alikamatwa kutokana na kampeni ya "kutembea kazini" kwa makundi na kupigwa risasi mkononi baada ya kuibuka ghasia baina ya polisi na wafuasi wake.

Viongozi wengine wa upinzani nao wamekamatwa kutokana na maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika kila Jumatatu na Alhamis.

Mwishoni mwa juma, Rais alielezea mpango huo kuwa wa "kipumbavu" na kinyume cha sheria.

Dr Besigye alishindwa na matokeo yake Rais Yoweri Museveni aliibuka mshindi katika uchaguzi wa mwezi Februari huku akidai uchaguzi huo ulifanyiwa hila.

Ameshindwa mara tatu na Bw Museveni katika uchaguzi wa rais, akiwa ameongeza asilimia 26 zaidi ya asilimia 68 za rais huyo mwezi Februari







Babu wa Loliondo Asistisha Kugawa Vikombe Pasaka



Babu wa Loliondo akigawa vikombe Tuesday, April 19, 2011 12:09 PM
MCHUNGAJI mstaafu Ambilikile Mwaisapile [78] awataka wale wanaoshughulikia vibali kwa wageni kuingia kijijini Samunge kwa ajili ya huduma usitishwe kwa muda ili aweze kuadhimisha kumbukumbu ya mateso ya Bwana Yesu Kristu
Mchungaji huyo amesema hataweza kutoa huduma ya uponyaji kuanzia siku ya Ijumaa Kuu na Pasaka yenyewe ili kupisha kumubukumbu hiyo.

Hivyo aliwataka watu wafuate na kuheshimu utaratibu unaotolewa katika vituo hasa kwa wale wa Kanda ya Ziwa kwa kuwa kumeonekana kuwa na watu wengi toka ukanda huo.

Kutokana na hilo viongozi wa wilaya zinazoingiza watu kwenda Samunge wamesitisha kutoa vibali vya kuelekea huko ili kupisha watu waliopo huko kupungua na wagonjwa wametakiwa kuheshimu amri hiyo ya babu.









Uasi Burkina Faso wasambaa


Jeshi la waasi lililoibuka wiki iliyopita Burkina Faso, taifa lililopo magharibi mwa Afrika limeenea mpaka mji mwengine wa nne.





Basi limechomwa moto Burkina Faso


Maandamano yameanza katika mji wa Kaya kaskazini mwa nchi hiyo, kufuatia ghasia mjini Po na Tenkodogo.

Ghasia hizo zimeanza Alhamis iliyopita wakati maaskari na walinzi wa rais kwenye mji mkuu wa Ouagadougou walipopinga kutopewa posho ya nyumba.

Saa chache kabla vurugu hazikuibuka, maelfu ya watu waliandamana kupinga gharama kubwa za bei ya vyakula.

'Polisi wajiunga na uasi'
Rais Blaise Compaore, aliyewahi kuongoza mapinduzi tangu mwaka 1987, ameifukuza serikali na kumteua kiongozi mpya kuwa mkuu wa majeshi kujaribu kutuliza ghasia.

Serikali yake ilitoa onyo siku ya Jumapili kuwa walioasi watakabiliwa na "sheria kali".

Mwandishi wa BBC mjini Ouagadougou Mathieu Bonkongou alithibitisha ghasia hizo kufika mpaka mjini Kaya.

Iliripotiwa kuwa maaskari na polisi waliingia mitaani siku ya Jumapili jioni na kuanza kufyatua risasi angani mpaka muda wa asubuhi wa Jumatatu.

Vurugu hizo kwenye mji mkuu zimesababisha takriban watu 45 kujeruhiwa na kulazwa hospitali.

Mwezi Machi, baadhi ya askari walighadhibika na kufanikiwa kuwaachia huru wenzao wengi ambao walifungwa kutokana na ubakaji










Jeshi linashambulia Ajdabiya na Misrata




Taarifa kutoka Libya zinaeleza kuwa jeshi la Kanali Gaddafi, limekuwa likishambulia kwa mizinga mji wa Ajdabiya unaodhibitiwa na wapiganaji.



Walioshuhudia mashambulio hayo wanasema makombora zaidi ya 10 yalipiga karibu na mitaa ya magharibi ya mji huo, na kufanya wapiganaji wakimbie.

Baadhi ya taarifa zinasema jeshi la Kanali Gaddafi linakaribia Ajdabiya. Piya kulikuwa na ripoti kwamba jeshi hilo limeanza tena kushambulia kwa mabomu, mji wa Misrata, ulioko magharibi mwa nchi.

Msemaji wa upinzani alieleza kuwa watu 6 waliuwawa huko mapema hii leo.











Mutai ashinda London Marathon




Emmanuel Mutai amevunja rekodi na kuibuka mshindi wa London Marathon huku mwenzake Mary Keitani pia akishika nafasi ya kwanza katika mashindano ya wanawake
Emmmanuel Mutai


Mutai alivunja rekodi kwa kukimbia kwa saa 2:04:39 na Keitany alichukua ushindi kwa saa mbili, dakika 19 na sekunde 17.

Katika mashindano ya wanaume, Martin Lel alichukua nafasi ya pili, huku mwenzake kutoka Kenya, Patrick Makau, akimaliza katika nafasi ya tatu.

Wakenya walitwaa ubingwa kwa kuchukua nafasi zote tatu za kwanza katika mashindano hayo.

Bingwa mtetezi katika mashindano ya wanawake, Liliya Shobukhova kutoka Urusi, alichukua nafasi ya pili.


Ketiany, wa tatu kushoto


Keitany ambaye anashiriki katika mashindano haya kwa mara ya pili alionekana kudhibiti mkondo wa mwisho wa mbio hizo na kumshinda Shobukhova kwa karibu dakika moja.

Shobukhova alionekana kushabikiwa sana kuwa atashikilia ubingwa wake wa London Marathon na alikuwa akiongoza mwanzoni mwa mashindano hayo, lakini Keitany aliongeza kasi alipofika maili 15 na kuendelea hivyo hadi tamati.

Edna Kiplagat mwenye umri wa miaka 31 alichukua nafasi ya tatu na hii ni mara yake ya kwanza kushiriki katika mashindano haya ya riadha ya London Marathon.

Keitany alianza riadha mwaka 2007 kama mchochea kasi na aliibuka mwanamke wa 10 kukimbia kwa muda wa saa mbili na dakika 20.

Mwanariadha huyo sasa ana nafasi nzuri ya kushiriki katika Olympic Marathon mwaka 2012.










Slaa ataja mafisadi, Nape naye acharuka





KATIBU Mkuu wa Chadema,

Dk Willibrod Slaa na safu ya uongozi wa juu
wameorodhrsha ya majina ya wanaodai kuwa ni mafisadi katika mkutano wake aliofanya mkoani Tabora mwishoni mwa wiki iliyopita.
Dk. Slaa aliwataja mafisadi hao kwa majina ambayo (yamehifadhiwa) na kati ya majina hayo yumo Waziri Mkuu mstaafu ambaye amedai kuhusika na wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Pia yumo Rais mstaafu na waziri mmoja aliyekuwa akitumikia Serikali ya awamu ya tatu na anaendelea na awamu hii kwa amemtuhumu kuuza nyumba za Serikali .

Wengine ambao wametajwa na Dk Slaa ni Katibu Mkuu wa zamani wa CCM ambaye amewahi kushika nyadhifa nyingine serikalini kwa tuhuma za kuhusika na EPA.

Wamo wafanyakazi wawili wa kampuni moja inayomilikiwa na kada mkongwe wa CCM ambao wanatuhumiwa kuchota mabilioni ya fedha kupitia Kampuni ya Kagoda.

Hivyo aliwataka wafisadi hao wajitokeze na serikali iwachukulie hatua za kisheria na kama Serikali imeshindwa kuwachukulia hatua yeye ataisaidia kwa kuwa ana ushahidi wa kutosha.


Wakati huohuo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM),ametangaza vita ya kuwataja mafisadi ambao wanataka kukichafua chama.

Nnauye ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Bahresa jijini Dar es Salaam na kusema chama hicho kimegundua mbinu za mafisadi za kutaka kumchafua Mwenyekiti Taifa wa chama hicho Rais Kikwete na familia yake kupitia vyombo vya habari.


Ametangaza vita hiyo kwa kuwataka mafisadi kuondoka kwenye Kamati Kuu ya chama hicho.


“Tutahakikisha mafisadi hao wataondoka ndani ya chama na tutahakikisha watang’oka kwani wana lengo la kuharibu chama cha CCM” alisema Nnauye

Aliwataka mafisadi waondoke kwa amani ndani ya chama hicho, na kuwaonya kuwa wasianzishe vita ambavyo hawataviweza na wakiendelea kunga’nga;ania atawataja hadharani

Nape ni Katibu wa Itikadi na Uenezi aliyechaguliwa na Halmashauri Kuu,, hivi karibuni mjini Dodoma nafasi ambayo alikuwa ikishikiliwa na John chiligati









Mawaziri wa zamani wa Misri watashtakiwa



Mkuu wa mashtaka wa Misri amesema kuwa waziri mkuu wa zamani, Ahmed Nazif, na mawaziri wengina wawili, watafikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kutumia vibaya mali ya umma.




Afisa mmoja amesema mashtaka hayo yanahusu manufaa ya dola milioni 15, waliyopata Bwana Nazif, Youssef Boutrous Ghali, waziri wa fedha wa zamani; na Habib al-Adli, waziri wa zamani wa mambo ya ndani ya nchi.

Mwezi uliopita, ofisi ya mashtaka yalitoa idhini kuwa Bwana Adli achukuliwe hatua za kisheria, kwa sababu ya mauaji ya waandamanaji mjini Cairo, mwezi Januari.

No comments:

Post a Comment