KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, April 18, 2011

Amtetea Mike Tyson, Amuua Mgeni Wake

Mwanaume mmoja toka Urusi ambaye alikuwa akibishana na wageni wake kuwa bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu Mike Tyson ni mkali zaidi kuliko wababe wa sasa duniani katika ngumi hizo ndugu wawili wa familia ya Klitscho toka Ukraine, ubishi huo umepelekea mwanaume huyo amuue rafiki yake.


Ubishi uliozuka kwenye nyumba ya mwalimu Nikolai Makayev wa mji wa Tyumen nchini Urusi ulipelekea mwalimu huyo awacharange kwa kisu wageni wake wawili.

Katika ubishi huo, Nikolai alikuwa akibishana na wageni wake juu ya nani mkali kati ya Mike Tyson na ndugu wawili toka Ukraine wa familia ya Klitschko ambao hivi sasa ndio wanaotamba duniani katika anga ya ngumi za uzito wa juu.Nikolai ambaye alikuwa akipata ulabu pamoja na wageni wake hao wawili, alitamba kuwa Tyson ndio mkali zaidi kuliko Vitali Klitschko na ndugu yake Wladimir Klitschko.

Wageni wake walimshutumu Nikolai kuwa hana uzalendo kwa kumshabikia Tyson ambaye ni bondia wa Marekani na kuwaacha akina Klitchko ambao wao ni Warusi.


Nikolai alikasirika kuambiwa hivyo na ghafla alichukua kisu na kuanza kumshambulia mgongoni mmoja wa wageni wake.

Mgeni mwingine ambaye naye alikuwa ni rafiki wa karibu wa Nikolai, aliamua kukimbilia nyumbani kwake kunusuru maisha yake ingawa naye alikuwa tayari ameishajeruhiwa kwa kuchomwa na kisu na Nikolai.

Polisi waliitwa lakini hadi wanafika tayari Nikolai alikuwa ameishamuua mmoja wa wageni wake.

Vifo vinavyosababishwa na pombe vimekuwa vikiongezeka nchini Urusi ambapo watu 500,000 huuliwa au hufariki kutokana na ulevi.

Hali hiyo imewaathiri zaidi wanaume nchini Urusi ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki kutokana na ulevi au matatizo yanayotokana na pombe, hali hiyo imesababisha kuwe na idadi kubwa ya wanawake kuliko idadi ya wanaume nchini Urusi
Akodisha Wapelelezi Kumpeleleza Obama


Ili kuuthibitishia uma kuwa rais wa Marekani, Barack Obama hakuzaliwa nchini Marekani hivyo hafai kuwa rais, bilionea mmoja wa nchini Marekani amekodisha wapelelezi ili kupeleleza maisha ya rais Obama.


Bilionea wa nchini Marekani, Donald Trump ametenga jumla ya dola milioni mbili ili kuweza kupeleleza sehemu aliyozaliwa rais wa Marekani, Barack Obama.

Trump anadai kuwa rais Obama si mzaliwa wa mji wa Hawaii nchini Marekani kama anavyodai hivyo haruhusiwi kisheria kuwa rais wa Marekani.

Kwa mujibu wa sheria za Marekani, mtu yoyote ambaye hajazaliwa ndani ya ardhi ya Marekani, haruhusiwi kuwa rais wa Marekani.

Akiongea kwenye televisheni ya NBC, Trump alisema kuwa amewakodisha wapelelezi maalumu kwaajili ya kupeleleza sehemu halisi aliyozaliwa rais Obama.

Trump alidai kuwa matokeo ya upelelezi wake yatawathibitishia watu kuwa Obama hafai kuwa rais wa Marekani.

Hata hivyo kura ya maoni iliyopigwa hivi karibuni ilionyesha kuwa asilimia 72 ya raia wa Marekani wanaamini kuwa Obama ni mzaliwa wa Marekani
Watu wakanyagana kumshuhudia aliyefumaniwa na shemeji yakeKATIKA hali ya kuonyesha mmomonyoka wa adabu unazidi kushika kasi kwa baadhi ya watu, mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Rabia [32] amejikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mume wa mdogo wake.
Hali hiyo ilijitokeza jana huko maeneo ya Yombo Vituka, majira ya saa moja usiku baada ya mdogo wa mwanamke huyo kupiga kelele za mayowe baada ya kuwakuta mumewe na dada yake wakiwa ndani wakifanya mapenzi.

Tukio hilo lilisisimua watu na watu walimiminika eneo hilo kumshuhudia mwanamke huyo aliyekosa hata chembe ya huruma kuiba mume wa mdogo wake.

Nifahamishe ilishuhudia tukio hilo wakati ilipokuwa katika harakati za kusuka habari na ilipofika eneo hilo ilikuta watu wakimshambilia huku wengine wakitoa maneno machafu kwa mwanamke huyo huku mdogo wake akilia kwa uchungu kuhusiana na tukio hilo.

Na huku akijaribu kuwasiliana na kuwajuza wazazi wake kuhusiana na tukio hilo huku wengine wakimtia moyo kuhusiana na tukio hilo.

Imedaiwa kuwa, Fatuma [28] ambaye ni mke wa mume aliyefahamika kwa jina la Fred, asubuhi ya jana aliwaaga majirani zake kuwa anakwenda mkoani Pwani kwa mama yake mzazi akamsalimie.
Ilipofika majira ya saa 5 asubuhi walimuona dada yake alifika hapo na majirani walimjuza kuwa mdogo wake hayupo lakini cha kushangaza alionekana akifungua mlango na kuingia ndani.

Majira ya mchana waliweza kumuona mume wa Fatuma alirudi hali ambayo hawakuielewa kwa kuwa hawakuzoea mume huyo kurudi majira hayo lakini walidhani huenda alirudi mara moja

Majirani waliendelea na shughuli zao na kumuona dada huyo akijishughulisha na shuhguli za nyumbani kwa mdogo wake huyo na watu hawakupata na wasiwasi kwa kuwa walishamzoea kufika hapo mara kwa mara

Mpashaji wa habari hii ambaye anaishi chumba cha pili kutoka chumba cha Fatuma alidai majria ya saa 10 jioni walisikia sauti ya redio imefunguliwa kwa sauti ya juu lakini waliendelea na shughuli zao.

Imedaiwa Fatuma aliweza kufika nyumbani hapo majira ya saa 12:47 na aliingia ndani na ghafla alipiga kelele za mayowe na ghafla hakusikika tena akipiga kelele hizo

Ndipo majirani walipokimbilia na kumkuta ameanguka chini kwa hofu na mume wa dada huyo akiwa amevaa upande wa kitenge na kumuona tena dada yake akiwa na amevaa upande wa khangaHata hivyo waliachana na wawili walichofanya wamshuhulikie kwanza afya ya Fatuma na dakika chache baadae hali yake ikawa sawa ndipo alipoelezea hali aliyoikuta ndani kwake na kueleza kuwa alimkuta dada yake na mumewe wakiwa katika hali ya kufanya mapenzi na majirani walianza kumshambulia mwanamke huyo na kwa makelele na watu waliposikia tukio hilo walimiminika kushuhudia tukio hilo

Imedaiwa mwanamke huyo alitaka kuchomoka mlangoni na kukimbia lakini kuna baadhi ya watu walimzuia na walimzuia pia asivae nguo na abaki hivyo hivyo

Nifahamishe ilishuhudia mdogo wa mwanamke huyo akishikwa na majirani zake na aliomba majirani hao wampeleka kwa shangazi yake anayeishi karibu nae ili akapumnike huko na asingeweza kulala hapo

Hadi nifahamishe inaondoka eneo hilo iliacha Fatuma anaondoka nyumbani kwake hapo kuelekea kwa shangazi yake huyo akajipumnzishe na dada yake akilia kwa kujilaumu kwa aliyoyafanya huku mume huyo nae akibaki ameinama kwa aibu aliyoipata kwa majirani zake9 papohapo kwa ajali- Arusha


WATU wanaokadiriwa kuwa ni tisa wamefariki dunia asubuhi ya juzi, katika ajali iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Ngorika huko mkoani Arusha
Ajali hiyo imehusisha basi la Ngorika kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Hiace na kusababisha vifo hivyo na majeruhi ambao idadi yake haijaweza kupatikana mara moja

Ajali hiyo imetokea eneo la kijiji cha Makumila asubuhi ya saa 2 na nusu leo, ambapo basi la Ngorika lilikuwa likitokea mkoani Arusha kuelekea Dar es Salaam na Hiace ilikuwa inaelekea Arusha

Habari za haraka ilizoifikia nifahamishe imefahamika kuwa chanzo ni katika eneo la ajali kulikuwa na daraja na palikuwa na dereva wa baiskeli akiendesha njia hiyo na dereva wa Hiace alikuiwa ikijaribu kuikwepa asimgonge na wakati ikijaribu asimgonge nakuja upande wa kulia ndipo imegongana uso kwa uso na basi la Ngorika

Hivyo magari hayo yaliweza kuburuzana umbali wa mita 7 na watu waliopatikana kwa haraka haraka kufa papohapo ni tisa na majeruhi bado hawajafahamikaMahakama yanafuta chama cha Mubarak
Mahakama ya Misri yameamrisha kuwa chama cha rais wa zamani, Hosni Mubarak, kifutwe

kifutwe.
Mahakama ya Utawala yalisema kuwa mali ya chama cha National Democratic,

pamoja na fedha na nyumba zake, zinafaa kutaifishwa na kukabidhiwa kwa serikali.


Hatua hiyo inaonekana kama inaridhia sana vugu vugu la waandamanaji, ambalo lilimlazimisha Rais Mubarak ajiuzulu.

Chama cha Bwana Mubarak, kilitawala Misri kwa zaidi ya miaka 40, baada ya kuundwa miaka ya '70, na Marehemu Anwar Sadat, aliyemtangulia Mubarak.

Bwana Mubarak na watoto wake wa kiume sasa wako kifungoni, na wanakabili mashtaka ya ulaji rushwa.


Vimini vyapigwa marufuku bungeni
KATIBU Mkuu wa Bunge,

Bw. Job Ndugai ametoa tamko kwa wabunge wanawake kuacha mara moja mavazi yasiyo na heshima wanapohudhuria vikao vya bunge linaloendelea mjini bungeni kwani mavazi hayo yameonekana kukera bunge hilo

Amewataka wabunge hao wanawake kuachana na mavazi hayo yakiwemo sketi fupi kupita kiasi “vimin” kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania


Hivyo amewataka wabunge hao wanaopendela mavazi hayo kupitia upya vifungu vya sheria bungeni ili wasikumbwe na adha ya kufukuzwa bungeni na kujiondolea sifa zao katika vikao hivyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuonekana kumekwua na mmomonyoko wa mavazi zikiwemo na zile nguo zinazoonyesha maungo kwa wabunge na ametaka tabia hiyo ikome bungeni humo.

MBali na vimini pia vazi la kilemba viendavyo hewani mithili ya waniigeria

umepigwa marufuku kwani husababisha usumbufu kwa badhi ya wabunge endapo ukikaliwa mbele na aliyevaa kilemba hicho husababisha usumbufu wa kutoona mbele wakati mbunge anaongea

Wibmi la uvaaji wa vimini ulishamiir katika bunge hikli jipya linaloitwa la vijana kutiokana na bunge hili kuwa na wabungeg wengi vijana na awali wabunge hao walisimamishwa uvaaji wa vikuu vya miguu kwa upande wa wabunge wanawakeAkutwa ajinyonga gestiAUGUSTINO Nicholous (35), mkazi wa Majengo Moshi,mkoani Kilimanjaro, amekutwa amekufa kwa kujinyonga jijini Dar es Salaam katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Jitegemee.
Kamanda wa Polisi Mkoani Temeke, David Missime, amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 asubuhi huko Keko Magurumbasi katika nyumba hiyo .

Amesema mwanaume huyo alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka ambalo alilifunga kwenye feni katika chumba namba 10 alipokuwa amepanga.


Chanzo cha kujinyonga hakijafahamika na maiti ilichukuliwa kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya TemekeKumetokea fujo nyengine nchini Burkina Faso.


Fujo zimezuka tena Burkina Faso
Inaarifiwa kuwa wanajeshi wanaolalamika juu ya malipo na mafao wamepora maduka na vibanda vya sokoni katika mji mkuu, Ouagadougo.


Mamia ya wenye maduka waliokuwa na hasira walijibu kwa kushambulia ofisi ya baraza la jiji na kuchoma moto makao makuu ya chama tawala.

Inasemekana ghasia hizo zinaendelea.


Siku ya Ijumaa, Rais Blaise Compaore, alifuta baraza lake la mawaziri na kumteua mkuu mpya wa jeshi, ili kurejesha udhibiti wa serikali yake.

No comments:

Post a Comment