KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, April 15, 2011

Niqab na Burka


Mavazi yanayofunika uso gubigubi-NIQAB au kuacha macho tu BURKA yamepigwa marufuku kuvaliwa hadharani nchini Ufaransa. Sheria inayozuia uvaaji huo ilianza kutumika rasmi wiki hii nchini humo. Wanawake wawili walitiwa nguvuni na baadaye kuachiliwa baada ya kuhusishwa na maandamano yasiyo rasmi yanayopinga sheria kuzuia mavazi hayo.

Ufaransa inakuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kupitisha sheria hiyo. Anayekamatwa analipishwa faini ya dola 133 au pound 217. Wanaowalazimisha wanawake kuvaa mavazi hayo kufunika uso gubigubi au kubakisha macho tu wanakabiliwa na faini kubwa zaidi au kufungwa jela miaka miwili.

Sheria hiyo haijagusia mavazi mengine kama hijab -linalofunika kichwa tu na kuacha uso. Hijab ni neno la kiarab na vazi hili huvaliwa na wanawake wa kiislam na wengine kama ishara ya heshima kwa mwanamke kutoacha viungo vyake wazi.

Mjadala huu unazungumzia iwapo mavazi haya ya gubigubi -niqab au Burka inayoacha macho tu yazuiwe? Je ni utamaduni au yanahusihwa na masuala ya dini. Wachangiaji ni pamoja na :

Bi Mzuri Issa aliyeko Zanzibar, Tanzania, yeye ni mwandishi wa habari na mwanaharakati wa masuala ya wanawake

Bi Halima Shwaib aliyeko Dar es Salaam, Tanzania ni mwalimu , na anavaa Niqab

Sheikh Jongo, Imam wa msikiti wa Manyema - Dar es Salaam, Tanzania

Na pia

Adam Khamis Mwamburi, mwanafunzi wa Udaktari wa falsafa Ph.D -kutoka Taasisi ya Kimataifa ya masomo kuhusu mtazamo na ustaarabu katika Uislam nchini Malaysia

Haijat Habiba- anavaa niqab na anaishi Burundi












Papandreou awasilisha hatua za kiuchumi hadi 2015




Waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou anasema kuwa nchi yake inaweza kufanikiwa katika matatizo yake ya kiuchumi kwa kufanya mageuzi zaidi, badala ya kuchelewesha ulipaji wa madeni. Papandreou amesema hayo katika mkutano wa baraza la mawaziri leo, ambapo aliwasilisha hatua kadha za kubana matumizi zenye thamani ya euro bilioni 23, zitakazotumika kuanzia mwaka 2012 hadi 2015. Mageuzi hayo yana lengo la kupunguza nakisi katika bajeti ya Ugiriki na kuimarisha hamasa kwa wawekezaji. Ugiriki ililazimika kutoa ahadi ya kurejesha kiasi kikubwa cha asilimia 13 katika dhamana za serikali zinazopevuka katika kipindi cha miaka 10 siku ya Alhamis ili kuvutia wawekezaji. Mkopo wa kunusuru uchumi wa kiasi cha euro bilioni 110 kutoka umoja wa Ulaya na shirika la fedha la kimataifa IMF mwaka jana umesaidia Ugiriki kuepuka kufilisika.












Polisi wa Hispania wathibitisha kukamata silaha za kundi la ETA






Polisi wa Hispania wamethibitisha kuwa kiasi cha silaha zilizokamatwa kutoka kundi la ETA wiki hii kilikuwa kikubwa kuliko wakati mwingine wowote katika tukio moja la operesheni dhidi ya kundi hilo linalotaka kujitenga kwa jimbo la Basque. Polisi siku ya Jumanne walikamata tani 1.6 za milipuko katika msako uliofanyika majira ya alfajiri katika maeneo matano tofauti. Watu watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na kundi la ETA. ETA inashutumiwa kwa kuhusika na vifo vya watu 829 katika kampeni yake ya miongo minne sasa ya mashambulio ya mabomu na vita katika azma ya kuunda taifa huru katika jimbo la Basque. Mwezi Januari , mwaka huu kundi hilo lilitangaza hatua ya kusitisha kabisa mapigano, ambayo haraka ilikataliwa na wanasiasa wa Hispania. Waziri wa mambo ya ndani wa Hispania Alfredo Perez Rubalcaba amesema kuwa kukamatwa kwa silaha hizo kunathibitisha kuwa kundi hilo la ETA bado halijaacha matumizi ya nguvu.











Gotovina ahukumiwa miaka 24 jela




Mahakama ya umoja wa mataifa ya uhalifu wa kivita imemhukumu jenerali wa zamani wa jeshi la Croatia Ante Gotovina kwa mauaji, kuwatendea vibaya na kuwarejesha makwao Waserb katika hatua ya kijeshi mwaka 1995. Operesheni iliyopewa jina la kimbunga, ilikuwa ni shambulio lililofanikisha kudhibitiwa tena kwa ardhi iliyochukuliwa na waasi wa Serbia mwishoni mwa mzozo wa eneo la Balkan. Waendesha mashtaka wamesema kuwa zaidi ya Waserb 300 wameuwawa na karibu wengine 90,000 wamekimbia makaazi yao wakiwa chini ya uongozi wa Gotovina. Alihukumiwa kwenda jela miaka 24, wakati mshtakiwa mwenzake Mladen Markac amepewa kifungo cha miaka 18. Mtuhumiwa wa tatu katika kesi hiyo, Ivan Cermak, ameachiwa huru. Kesi hiyo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu nchini Croatia, na televisheni kubwa ziliwekwa nchi nzima kuweza kutangaza hukumu hiyo. Serikali ya Croatia, ambako watu hao wanaonekana kuwa ni mashujaa, imeishutumu hukumu hiyo na kusema haikubaliki.










Mawaziri wakuu wa majimbo ya Ujerumani wahudhuria mkutano wa nishati Berlin

Viongozi wa majimbo 16 ya Ujerumani wanakutana na kansela Angela Merkel mjini Berlin kujadili sera ya serikali yake kuhusu nishati. Ikiwa katika mbinyo mkubwa kutoka kwa wanaharakati wanaopinga nishati ya nyuklia pamoja na upande wa upinzani, serikali imekuwa ikiangalia njia za kuharakisha kuondoa vinu vya nyuklia nchini Ujerumani na nafasi yake kuchukuliwa na vyanzo vya nishati inayoweza kutumika tena. Waziri wa uchumi Rainer BrĂ¼derle amesema leo kuwa kipindi cha haraka cha mpito kitagharimu kiasi cha euro bilioni moja hadi mbili kwa mwaka. Wakati huo huo chama cha upinzani cha Social Democratic, SPD, kimewasilisha hoja katika bunge la wawakilishi wa majimbo la Ujerumani , Bundesrat kutaka kufungwa kabisa kwa vinu saba vikongwe vya nyuklia nchini Ujerumani. Matthais Platzek, waziri mkuu wa jimbo la Brandenburg, amesema kuwa binadamu hana uwezo wa kupambana na teknolojia ya kinuklia.
















Mwendesha mashataka amhamishia Mubarak katika hospitali ya jeshi





Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali nchini Misri ameamua kumhamishia rais wa zamani wa nchi hiyo Hosnu Mubarak katika hospitali ya jeshi, ambako atahamishiwa jela wakati hali yake itakapokuwa nzuri. Mubarak alipelekwa hospitali katika mji wa kitalii wa Sharm el-Sheikh baada ya kupata matatizo ya moyo wakati akihojiwa na waendesha mashtaka kuhusiana na madai ya kuhusika katika vifo vya waandamanaji waliokuwa wakipinga utawala wake pamoja na madai ya ulaji rushwa.












Kiongozi wa vijana wa utawala wa Gbagbo akamatwa




Radio ya kimataifa ya Ufaransa imetangaza leo kuwa kiongozi maarufu wa vijana na muungaji mkono mkuu wa kiongozi wa zamani wa Cote D'Ivoire Laurent Gbagbo amekamatwa. Charles Ble Goude, kiongozi mkakamavu wa kundi la harakati za vijana wazalendo, anatuhumiwa kwa kuchochea mashambulizi dhidi ya raia, wageni na vikosi vya jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani nchini humo. Haikuwezekana mara moja kuthibitisha taarifa hizo juu ya Goude, ambaye alikuwa pia waziri wa vijana wa uongozi wa Gbagbo na ambaye amelengwa katika vikwazo vya umoja wa mataifa na umoja wa Ulaya. Gbagbo alikamatwa siku ya Jumatatu wiki hii baada ya wiki kadha za mapambano katika taifa hilo linalozalisha kwa wingi zao la kakao duniani. Taarifa pia zinasema kuwa msemaji wa rais wa zamani wa Cote D'Ivoire amejiuzulu wadhifa huo.













Binti Gaddafi amtetea baba yake





Binti wa kiongozi wa Libya

Aisha Gaddafi amesema muungano wa kijeshi wa nchi za magharibi unaotaka baba yake aondoke madarakani ni kuwatukana wa Libya wote.


Akitoa hotuba yake mjini Tripoli, katika maadhimisho ya miaka 25, ya Libya kushambuliwa kwa mabomu, wakati Marekani ilipofanya mashambulio ya anga katika mji huo mkuu mwaka 1986,


Aisha Gaddafi amesema watoto kadhaa waliuawa wakati huo na sasa baada ya miaka kadhaa mashambulio kama hayo tena yanafanywa kwao na watoto wao.





Huku akishangiliwa na wafuasi wa baba yake katika viwanja vya Bab al Aziziyah, Aisha alisema wanajeshi hao wanataka kumuua baba yake, wakijifanya kuwalinda raia.




Katika taarifa yao ya pamoja ambayo imechapishwa leo, Rais Barack Obama wa Marekani, Waziri Mkuu wa Uingereza

na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa, wamesema kumuacha Gaddafi aendelee kuiongoza Libya kutakuwa ni usaliti wa kupita kiasi.

Wakati huo huo, majeshi ya Libya yanadaiwa kuwaua watu wanane baada ya kushambulia kwa roketi mji wa Misrata.

Kwa mujibu wa daktari katika eneo hilo watu wengine saba akiwemo mtoto na mzee walijeruhiwa katika mashambulio hayo.

Wakaazi wa eneo hilo walikiambia kutuo cha teklevisheni cha al Jazeera

kwamba takriban roketi 120 zilivurumishwa katika mji huo leo asubuhi.

Katika hatua nyingine, mtandao wa kigaidi wa al Qaeda umeyataka majeshi ya nchi za kiarabu kuingilia kati mzozo wa kisiasa nchini Libya na kumuondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo Muammar Ghadafi.



Katika taarifa yake aliyoitoa kupitia mkanda wa video, kiongozi nambari mbili wa al Qaeda Ayman al Zawahiri,

ameyatolea wito majeshi ya nchi za kiarabu kumuondoa kanali Gaddafi, ili hatua ya kuingilia kati kusaidia waasi inayofanywa na majeshi ya nchi za magharibi isije kuwa uvamizi.

Msaidizi huyo wa Osama bin Laden amepongeza pia kuangushwa kwa aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak.



Al Zawahiri, ambaye ni Mmisri alikuwa ni mpinzani mkubwa wa utawala wa nchini mwake na kwamba alishawahi kutumikia kifungo gerezani kwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Anwar Sadat katika miaka ya 80.




Wakati mapigano yakizidi kuendelea nchini humo,

Malawi imekata uhusiano wake wa muda mrefu wa kibalozi na Libya kutokana na mzozo huo wa kisiasa unaoendelea na idadi kubwa ya raia wanaouawa.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya Nchi za nje ya nchi hiyo imesema Malawi itabadili msimamo wake kuhusiana na uhusiano wao baada ya hali kuimarika na maisha kurudi katika hali yake ya kawaida.






Supporters of Libyan leader Muammar Gaddafi gesture as they chants slogans during a pro-government rally at the heavily fortified Bab al-Aziziya compound in Tripoli April 14, 2011. Muammar Gaddafi's daughter said the West's demand that her father leave power was an "insult" to all Libyans in a defiant appearance before a crowd of his chanting supporters in Tripoli early on Friday.













Wanajeshi wa Rais waasi Burkina Faso



Rais Blaise Compaore
Wanajeshi katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou wameasi, huku milio ya risasi ikisikika usiku kucha.


Uasi huo umeanza wakati baadhi ya walinzi wa rais walipoanza kupiga risasi hewani wakipinga kutolipwa posho za nyumba.

Rais Blaise Compaore alitarajiwa kukutana na mjumbe wa Umoja wa Mataifa mjini humo, maafisa wamesema, baada ya kukimbia usiku mzima.

Mapema, Bwana Compaore, ambaye yuko madarakani tangu 1987, alijaribu kupata namna ya kuwatuliza askari hao baada ya kutokea malalamiko kama hayo mwezi uliopita.

Mwandishi wa BBC Mathieu Bonkoungou akiwa Ouagadougou anasema ghasia hizo zilisambaa katika kambi nyingine za jeshi na upigaji risasi hewani ukaendelea mpaka karibia na alafajiri.

Hata hivyo inaripotiwa kuwa mji huo mkuu umetulia sasa.
Maandamano yalifanyika siku ya alhamis katika mji huo mkuu na kwenye miji mingine kupinga kupanda bei ya vyakula na shutuma nyingine za kuvunjwa kwa haki za binadamu, shirika la habari la Ufaransa-AFP limeripoti

No comments:

Post a Comment